SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Kujua ni kipi kilicho msibu Enock mchumba wake na kufanya hata kutokushiriki nae tendo la ndoa kama zamani, alijua fika Mwanamke Aliyeitwa Catherine ndiye chanzo cha yote licha ya kudhani hayo yote ilibidi afanye uchunguzi wa kina ili apate ushahidi wa kutosha.
SASA ENDELEA...
“nitaua mtu namimi nife hawa wanacheza na Akili zangu”
Aliwaza Naomi siku hiyo akiwa anaendesha gari anarudi nyumbani kwa Enock walishaamua tayari kuishi wote kama mume na mke wakilala chumba kimoja lakini kulikua hakuna maelewano ya aina yoyote.
“Mume wangu”
Aliita Naomi siku hiyo mezani wakiwa wote wanakula chakula cha usiku.
“Naam”
“nikuombe kitu”
“niombe tu”
“kesho nasafiri naenda Mwanza”
“kuna nini?”
“naenda kikazi”
“sawa sina shida, safari njema”
Enock hakuweka kipingamizi chochote kile zaidi tu alifurahi sana ndani ya mtima wake, alijua mambo yake angeyafanya chap chap na Catherine na kujiachia,Alisha mchukia sana Naomi aliona ndiye kikwazo cha mapenzi yake na Catherine kukwama, kitu kimoja ndicho alichoogopa endapo akimfukuza mwanamke huyo ghafla ilimaanisha yeye kwenda jela kutokana na mauaji ya Heather yaliyo tokea hospitalini. Alitamani afunge ndoa na Catherine hata kesho yake asubuhi ili waishi kwa amani.
“sasa tiketi ulishakata?”
“ndio”
“unaondoka na basi au ndege?”
“basi”
“aya safari njema Mama”
Baada ya kumaliza kula chakula cha usiku vyombo vilitolewa na Naomi kwa kuwa hawakua na mfanya kazi wa ndani waliiishi wenyewe ndani ya nyumba hiyo kubwa.
Saa kumi na moja ya asubuhi ilifika na Naomi kudamka, alijiandaa haraka haraka na kumuamsha Enock ili ampeleke Ubungo terminal, waliwasha gari mpaka ubungo Terminal tayari kwa safari, walikuta basi lina karibia kuondoka, hapo ndipo Naomi alipoingia ndani ya basi kubwa baada ya kutoka kuagana,
Enock alisubiri ili kuhakikisha kama Kweli Naomi anasafiri, alishuhudia basi lina ondoka nayeye kuondoka zake akiwa na furaha tele moyoni mwake, hapo hapo alimpigia simu Catherine na kupanga waonane siku hiyo jioni yake!.
“Konda kimara shusha!”
Alisema Naomi akiwandani ya basi, ki ukweli hakua na safari yoyote ile ilikua ni lazima akamilishe swala lake la uchunguzi juu yanayo fanyika, ikiwezekana auwe hata mtu. Aliteremka hapo hapo Kimara mwisho na kutafuta taxi iliyompeleka mpaka Mwenge na kutafuta hotel ili apumzike na kupanga kitu cha kufanya,
jioni ya saa kumi na moja ilipofika alijua ndiyo mida ya Enock kutoka kazini ivyo alitafuta taxi iliyompeleka mpaka posta kimnya kimnya kama mpelelezi,
Kwamacho yake alimuona Enock anaagana na kuingia ndani ya gari lake BMW.
“unaona hio BM?”
“ndio dada”
“ifate nyuma nyuma”
“sawa hakuna tabu”
Walizidi kuifata nyuma nyuma gari ya Enock mpaka alipo fika nyumbani kwake kisha baadae kumuona anatoka na gari nyingine hapo ndipo umakini ulipo hitajika,
walizidi kumfuatilia taratibu sana.
“Nani Catherine mpenzi wangu nipo njiani nakuja, si umesema nikukute nyumbani?”
“ndio Enock nipo nyumbani, Mama hayupo nipo na mtoto siwezi kutoka”
“sawa basi nakuja”
Bilakujua nyuma yake anafuataliwa na mchumba wake Naomi aliyekua na hasira hata ya kuuwa mtu,alitembeza gari mpaka tabata Bima na kuliweka upande wa kushoto kisha kushuka na kuingia kwa Catherine, yote yaliyokua yana tokea Naomi aliyashuhudia kwa macho yake yote mawili.
Alishuka na kumlipa Pesa dereva taxi na yeye kusimama upande wa pili, alipiga mahesabu mengi sana bila kujua nini chakufanya,ghafla mawazo yalimjia pale pale na kuelekea dukani kununua kisu kidogo na kuliendea gari la Enock lililokua upande wa pili, aliingia uvunguni na kutafuta paipu ya mafuta ya breki na kuikata alijua nini maana yake,
Alisha taka kumuuwa Enock kisha baadaye Catherine afuate na hakuna hata mmoja angewahi kumshtukia,
Alitembea mpaka kwenye baa ya jirani na kukaa ili kuwashuhudia,
kweli hakukaa sana aliwaona Catherine na Enock wanatoka huku wameshikana viuno mpaka ndani ya gari na kutabasamu sana sababu aliona ni kifo kitakacho wapata…
“Enock nisubiri kidogo nimesahau simu yangu”
Hiyo ndiyo ilikua ponea yake,na kushuka ndani ya gari na kumuacha Enock, ni simu tu peke yake ndiyo ilimuepusha na kifo cha ajali iliyotaka kutokea muda mfupi ujao, aliyetaka kusababisha yote hayo alikua ni Naomi yupo pembeni mbali kidogo kwenye moja ya grosari anawatizama, hata yeye alivyoona tukio hilo la Catherine kuteremka ndani ya gari alikasirika sana lakini alisubiri ili ajue nini kitaendelea, alikata paipu za breki ya gari la Enock tayari akitaka kumuua kutokana na wivu alio kua nao ndani ya moyo wake, kitendo cha Enock kurudiana na Catherine kilizidi kumsumbua usiku na
Mchana mpaka akadanganya ana safari kumbe haikuwa ivyo alitaka afanye mauaji hayo kimnya kimnya bila mtu yoyote kujua, hata kama wasinge kufa kwa ajali ilikua ni lazima awaangamize watu hao wawili hata kwa kuwapiga risasi za utosini, sana sana Catherine mwanamke aliye sababisha mpaka yeye asiolewe kabisa.
Enock Alisha subiri sana bila kuona dalili ya Catherine kutokea alishuka ndani ya gari na yeye kumfuata, kilichomshtua zilikua ni kelele za mtoto mdogo Christopher akilia kwa sauti yaa juu akipaza sauti yake sana, alivyo fungua mlango alimuona Catherine kambeba akiangaika nae mgongoni mwake,
Ilimbidi ajumuike nae na kughairi safari yao, masaa matatu yalipita bado mtoto alikua akilia ila baadae alinyamaza na kulala.
“Enock nimechoka naomba iyo safari tughairi tu”
Alisema Catherine
“sawa, hakuna tabu lakini sitoweza kukuacha hapa peke yako, nitabaki nawewe mpaka mama yako atakapo rudi”
“hakuna tabu mpenzi”
Hawakutaka kulala badala yake walipiga stori mpaka usiku mzito kuingia.
“mtapigwaje na Mwanamke?”
“lakini…..”
“nyamaza usiongee upuuzi, usinitie kichefu chefu, sikutegemea kama mtaniangusha yaani mnakuja na makende yenu, mpaka huku Zanzibar mnakuja kuniambia huo ujinga ujinga”
“bosi tusamehe”
“mimi nitaenda mwenyewe na vijana wangu wengine nyie hamnifai, lazima Enock,Sabrina na Catherine wafe tu, ndiyo nitaishi kwa amani sana”
Alifoka mzee Mwasha kitendo cha vijana wake aliowatuma wakamchukue Catherine,Enock na Sabrina kupigwa kili mkera sana hakutegemea kupokea habari kama izo siku hiyo, siku hiyo hiyo alinyoosha mpaka Forodhani kukitafuta kikundi kilichoitwa NO MITEGO kilichosifika kwa wapiganaji mahiri na wafanya mazoezi kilichoongozwa na Rodgers Mbita aliye fahamika Zanzibar nzima kwa upambanaji
Kwenye ndondi za ulingoni katika michezo ya kick boxa, hakuwahi kushindwa ulingoni hata siku moja, kipindi alicho kaa Zanzibar aliweza kuzisikia habari zake hata mara nyingi humuona kwenye t,v akiwa ana pambana na watu wengi wenye misuli na kuwapiga vibaya sana. Aliona huyo ndiye atakae mfaa katika kazi zake chafu atakazo zifanya popote pale.
“habari zenu vijana?”
Alisalimia Mzee Mwasha baada ya kufika maskani waliyokua wakikaa kikundi hiko cha No Mitego jioni ya siku hiyo.
“salamaa atiiii”
Alijibu mpemba mmoja wao kwa rafudhi yao
“Namuulizia Rodgers Mbita kuna kazi nataka nimpe,nime mkuta?”
“Alikuwepo sasa hivi hapa, ngoja kidogo”
walimtafuta dakika hiyo hiyo kupitia simu yake ya mkononi, haikuchukua muda mwingi mtu mfupi mwenye misuli alikua amesimama mbele yao,
“Njoo tuongee Rodgers,”
Alisema Mzee Mwasha kisha wote kutoka pembeni ili kuteta, hapo hapo alianza kumpa kazi hiyo ya kwenda barani Dar es salaam ili kuwatafuta Catherine, Enock na Sabrina, kazi hiyo ilikua ndogo sana kwa mtu mafia kama huyo, ilikua ni kama kuweka tonge la ugali nyama mdomoni.
“Andaa pesa tu,nauli makazi na chakula itakua juu yako, kazi yako nitaianza ukishanipa nusu ya malipo yangu”
“mimi sina shida nitakupa pesa yote, ingia kwenye gari twende”
Walinyoosha mpaka kwenye moja ya benki. Hapo mzee Mwasha alichukua kiasi cha shilingi milioni mbili taslim na kumkabidhi Rodgers ili kazi yake ianze, muda wote alitabasamu sana alijua kazi yake sasa inaenda kuwa rahisi.
Jiioni ya siku hiyo hiyo Rodgers alikua kwenye boti ya Azam akielekea Dar es salaam huku mikononi mwake akiwa na picha za watu hao watatu,.
Bado alishindwa kuelewa ni nani aliyekata paipu za breki ya gari lake, alielewa maana yake kuwa kitendo cha kuliwasha gari angepata ajali, bila kushtuliwa na wasamalia wema kuwa mafuta yana vuja chini angesha kufa usiku wa jana yake,na angeitwa marehemu siku hiyo hiyo,alishajua kuwa bado kuna watu wabaya wanamuwinda na vita bado havijaisha, hisia zilimpeleka ni lazima atakua ni baba yake Mzazi Mzee Mwasha sababu Naomi aliamini alikua amesafiri na yupo Mwanza alishindwa kumuhisi mchumba wake huyo!.
“itabidi nipeleke gari sevisi kesho”
Aliwaza Enock na kujitupa kitandani kulala, fikra zake zilimtuma kwa mwanamke Catherine mwanamke wa maisha yake, bado aliamini kuwa anaota na atashtuka na kukuta kuwa Catherine alifariki dunia,alitamani isiwe ivyo hata siku moja, Mchumba wake Naomi ndiye aliyekua kikwazo tu cha harusi yake yeye na Catherine hakuelewa ni kitu gani akifanye kwa wakati huo,
Kutokana na msongo wa mawazo alipitiwa na usingizi na kushtuka asubuhi na mapema, alivaa haraka haraka na kujiandaa ili awahi ofisini kwake, baada ya kumaliza alichukua funguo zake za gari na kushusha ngazi, ila alivyotoka nje alimuona mwanaume mfupi mwenye misuli ametanda huku baadhi ya walinzi wake wakiwa chini, hakuelewa ni kitu gani kimetokea.
“wewe ni nani?”
Aliuliza Enock
“Mafia, mimi naitwa mafia ninja”
Alijibu Rodgers kwa majigambo huku akimsogelea karibu, alimfuata na kumtandika ngumi moja nzito ya mdomoni iliyompeleka mpaka chini mzima mzima chali na suti yake, kisha kumkaba ili amzimishe baada ya zoezi hilo kufanyika alimpigia simu mzee Mwasha.
“Tayari Enock mwanao ninae,”
“Nataka wote watatu, ukisha wapata nitakwambia cha kufanya”
“okay”
Rodgers alikata simu na kumbeba Enock begani mpaka ndani kisha kumuweka juu ya kochi, fahamu zilimrudia huku akiwa na maumivu mengi sana kichwani mwake kutokana na ngumi aliyopigwa muda mchache uliopita.
“kijana, mpigie simu Catherine mwambie aje mara moja”
“Sii…wezi”
Neno moja tu lilimfanya Enock apigwe ngumi nyingine ya pua iliyofanya damu nyingi zimvuje puani, hapo ndipo alipoanza kusha mbuliwa akipigwa ngumi usoni mpaka kuzirai tena kwa mara ya pili.
Hata angepigwa nusu kufa asingethubutu kufungua kinywa chake kusema ni wapi Mpenzi wake Catherine alipo, aligoma kumpigia simu, hapo ndipo kipondo kilizidi kuendelea kutoka kwa
Mwanaume mcheza kick boxa mfupi aliyekua mbele yake amejazia misuli mikononi, nusu saa nzima alikua akipokea mateso, aligoma kabisa kumpigia simu Catherine, alijua kufanya ivyo alikua anamuweka kwenye matatizo makubwa ilikua ni bora afe. Uso wake tayari ulishaharibika lakini hakuonesha ushirikiano wa aina yoyote ile.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA