BIKRA YANGU (52)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Mwanaume mcheza kick boxa mfupi aliyekua mbele yake amejazia misuli mikononi, nusu saa nzima alikua akipokea mateso, aligoma kabisa kumpigia simu Catherine, alijua kufanya ivyo alikua anamuweka kwenye matatizo makubwa ilikua ni bora afe. Uso wake tayari ulishaharibika lakini hakuonesha ushirikiano wa aina yoyote ile.
SASA ENDELEA...
“nii…..pige mpaka n..iiife”

Alizungumza Enock kwa tabu sana akiwa mwenye maumivu mwili mzima.

“sawa, wacha tuone kama wewe kweli ni kidume cha mbegu!”

Kitendo cha kutoa jibu hilo tu na hapo ndipo kipondo kilizidi na mateso makali sana kwa Enock kufuata, ili aweze kumumleta Catherine mahali hapo kama wajibu wa kazi yake iliyo mfanya afunge safari yake kutoka kisiwani Zanzibar mpaka Dar es salaam akiwa tayari kasha pewa pesa taslimu ili kazi hiyo ndogo kwake aliyo ifananisha kama kuua mbu ndani ya neti ifanyike,

Hata yeye alikerwa kwa kitendo cha Enock kuifanya kazi yake iwe ngumu, damu zilichuluzika chini juu ya makochi na kutapakaa kila mahali, alikua hajiwezi tena hata kuongea, hakika alikua katika mateso yasiyoweza kuelezeka, licha ya kuteseka sana hakutaka kuongea lolote lile.

Hapo ndipo Rodgers mwanaume katili asiyekua na utu kutoa kisu chake mfukoni na kuanza kumkata nyama za mikononi taratibu.

“nitaendelea kukukata kila mahali”

Bado aliendelea kumkata kata, kitendo cha simu ya Enock kuita ndiyo ili fanya zoezi hilo alisitishe, Simu ilitolewa na kuwekwa mezani aliyekua akipiga simu sio mtu mwingine bali ni Catherine alielewa kabisa Enock atakua ana tatizo sababu kila asubuhi ilikua ni lazima wajuliane hali na mpenzi wake kisha mengine yafuate.

“Halloo”

Rodgers jambazi katili ndiye aliyepokea simu akitoka nje.

“naomba niongee na mwenye simu”

“amedondoka ghafla hapa nyumbani kwake”

“una sema?”

“Amedondoka ghafla nyumbani kwake, ana hali mbaya sana tuna msubiri daktari aje”

“naweza nikaja?”

“sawa njoo”

Catherine Alisha ingiwa na wasiwasi mwingi moyoni mwake hakuelewa ni kitu gani kili mpata mpenzi wake mpaka akadondoka, hakuwahi kusikia taarifa kama izo tangu amjue,haraka haraka alimlaza Christopher kitandani na kumuaga mama yake,

“huu ugonjwa umemuanza lini, sijawahi kusikia”

Aliwaza Catherine akiwa njiani anaendesha gari, njia nzima alikua akiwaza kisha kuweka gari nje ya geti la nyumba ya Enock nayeye kushuka haraka haraka, kitendo cha kuingia getini tu alishikwa mkono kwa nguvu sana bila kufanya lolote na kubebwa begani moja kwa moja mpaka sablen na kutupwa chali juu ya sofa, hakuamini alivyomuona Enock anavuja damu nyingi mwilini mwake, alishindwa kuelewa nini kimetokea kwa wakati huo.

“Mpigie Mama yako simu mwambie aje sasa hivi”

Aliongea Rodgers akimtizama Catherine, hakua na haja ya kumfunga kamba alijua kuwa ni mwanamke, hawezi kufanya lolote, hakujua kuwa anafanya kosa kubwa la jinai kumwacha mwanamke huyo huru bila kumuwekea ulinzi mkali.
“nimpigie wa nini?”

“acha maswali binti, piga simu kama una hitaji kuishi,usinipotezee muda wangu nina shughuli nyingi za kufanya aroo”

Alizidi kuzungumza jambazi huyo katili akiwa bado na kisu chake mkononi kakishika,hapo ndipo Catherine aliporuka haraka kama umeme na kumvaa na kumtwanga kichwa kizito puani, alivuta kichwa chake na kukipigiza juu ya stuli ya kioo, hakuishia hapo alirusha teke lingine hewani lakini Rodgers aliliona na kuhepa kushoto nayeye kurusha ngumi iliyotua usoni mwa Catherine puani na kumfanya ayumbe,

Rodgers alitabasamau na wote kukunja ngumi tayari kwa mpambano ambao ulikua hauna refalii, katika watu hao wawili mmoja wao alikua akimdharau mwezake, ngumi zilianza kurushwa na kuanza kutupana huku na kule Catherine alivyotaka kukiwahi kisu kilichokua chini alipigwa teke na kutupwa upande wa pili, tayari alikua amezidiwa ameumia amepigwa sehemu mbaya kwenye mbavu zake.

Ilibidi atulie anyamaze hakua na ujanja mwingine wa aina yoyote ile wa kujitetea alitembea akijiburuza mpaka juu ya kochi alilolala Enock anavuja damu mwilini na kumkumbatia, wote walikua kwenye maumivu makali, bado walikua na safari ndefu ambayo iliyo jaa maadui wengi walio wazunguka kila sehemu na walisha lielewa jambo hilo, Walishaelewa kuwa ni Mzee Mwasha ndiye anawawinda na wala sio mtu mwingine yoyote Yule.

“Bosi, ninao Enock na demu wake tayari”

Aliongea na Simu Rodgers

“vipi kuhusu Sabrina?”

“sipo nae”

“upo nao wapi?”

“hapa kwa Enock wote wawili, nasubiri nisikie kauli yako tu”

“wachomee ndani na moto kisha maliza kwa Sabrina nataka hiyo kazi iishe leoleo”

Kauli ya Mzee Mwasha akiwa kisiwani Zanzibar wakiongea na simu ilieleweka kabisa kwa Rodgers, hakua na chaguo lingine zaidi ya kuwazungushia kamba wote wawili kwa pamoja tayari kwa kuwateketeza na moto, alitoka mpaka nje na kununua mafuta makali aina ya Petroli lita kumi na kuanza kumimina nje kisha kuingia ndani akimimina kila sehemu, walijihesabia hiyo ndiyo ilikua siku yao ya mwisho kuishi duniani hawakua na ujanja wa aina yoyote,

“Ca…their..ne nakupenda sana”

Alisema Enock kama ishara ya kumuaga mpenzi wake.

“hata mimi Enock,buliani tuta kutana mbinguni tuendeleze mapenzi yetu upya”

Wote walisemezana na kuibananisha mikono yao, wakiwa ndani walihisi harufu kali ya Moshi wa petrol dalili zilionesha kuwa moto mkubwa ulikua ukiwaka nje, haikuchukua hata dakika mbili moto ulikua mkubwa sana ndani uliofanya moshi mwingi sana na mzito, ujaze mapafu yao, walianza 
kukohoa baada ya kupaliwa na moshi, hewa ya oxygen ilianza kuisha taratibu kisha kukatika kabisa,moto ulikua karibu yao taratibu macho yao yalianza kujifumba kutokana na uzito wa moshi mkali sana uliokua ukiteketea, wote walilaliana ili kusubiri kifo chao muda mfupi ujao, fikra za miili yao ikiwa katika hali ya majivu vilianza kujijenga ndani ya vichwa vyao,
ilikua ni picha mbaya ya kutisha sana,

“Cat..theer…ine mp…penz…i wa..ngu nime..ishiwa pumz….i tayari.. mi..mi natangu…liia”

“ha..ta mimi mp.e.nzi ni..po nyuma yako.. na…kufua…ta, nak..upend..a p..ia”

Waliagana tayari kwa safari ya kwenda Mbinguni walishaelewa roho zao zilikua ni lazima ziache mwili. Moto tayari ulikua ukiteketeza nyumba kubwa ya kifahari ya Enock ambayo aliijenga kwa gharama nyingi sana punde tu alivyorejea masomoni Marekani,leo hii ilikua ikiungua na moto uliosababishwa na baba yake mzazi Mzee Mwasha,

Hata angebahatika kupona na kuokolewa katika moto huo asingeweza kumsamehe hata mara moja, japo aliamini swala hilo halitoweza kutokea labda itokee miujiza, wote na mpenzi wake Catherine walikua ndani ya nyumba inayowaka moto mkali wa petroli na kutoa moshi mkubwa juu.

Hawana msaada wowote ule wala njia ya kujinusuru na kuziokoa roho zao, walishakata tamaa ya kutaka kuzipigania nafsi zao,walisha pitia mengi sana na kunusurika kufa sasa waliona huo ndio mwisho wa maisha yao kuishi duniani waliamini kuwa kuna maisha mengine huko waendapo ahera………..

USO WAKE ULIKUA NA DAMU nyingi,mdomo umemvimba, macho yake yameumuka sana, alihisi maumivu mwilini mwake, alishapigwa vya kutosha na kulia bila kupata msaada wa aina yoyote ile, aliona bora afe ili apumzike na kuepukana na mateso anayopata kuliko kuendelea kuteseka, hata kama ungebahatika kumuona alivyokua hapo na ukapewa picha yake usingeweza kudhani kuwa ndiye Kway,
alishateseka sasa siku mbili nzima akiwa ametekwa nyara hajui alipo, njaa kali ndio ilitafuna tumbo lake, na kuishiwa nguvu mwilini kabisa, alikumbuka mara ya mwisho alikua Goma nchini 

Kongo,akishughulikia maswala ya tiketi za ndege ili waweze kurejea Tanzania yeye na mke wake julia waka anze maisha mapya na mtoto wao Natu ambae walidhani amekufa, furaha yake ilikatishwa na wema wake baada ya kusimamishwa na omba omba akimuomba pesa hapo ndipo alipohisi kitu kimetua kichwani mwake juu utosi na kilichotokea hapo hakuelewa.

Alikua hana shati la juu amefungwa kati kati ya miti mingi msituni, hapo ndipo kilikua kitanda chake hata haja ndogo alitolea hapo hapo,kila siku alikuja kuchapwa na mkia wa taa ambao ulifanya nyama zake zitoke mwilini na kufanya vidonda vidonda vilivyoanza kuliwa na nzi, hakika yalikua mateso yasiyo stahili kwa kiumbe hai wa aina yoyote ile, aliikumbuka sana familia yake,bado hakuelewa ni nani aliyesababisha mpaka kufika ndani ya msitu huo, hakuelewa ni nani alimkosea ila alijua ametekwa nyara teyari na kuna mambo mawili tu kufa au kupona ndiyo yatakayo tokea hapo baadaye!.

“Mfungueni”

Kauli hiyo ilitoka kwa mtu mwenye misuli mingi mrefu sana kwenda juu kama Goliati, kisha Kway alifunguliwa na kudondoka kama gunia la mchele puu! chini hana nguvu hata za kuinuka anatetemeka kwa njaa na maumivu.

“Kway!”

Liliita jitu hilo, Kway alishtuka alijua vizuri kuwa watu waliomteka wanamfahamu vizuri tena waliongea Kiswahili cha kitanzania lakini bado hakujua ni kipi wanachotaka kutoka kwake.alivyotaka kuitikia alishindwa na kuinua kichwa chake juu.

“Najua,hutaki kurudi hapo na kuendelea na mateso, naomba unijibu swali moja tu ili uwe huru uende zako kwa amani,Catherine yuko wapi?”

Swali aliloulizwa ndilo lilimshtua sana na kuelewa kwanini ametekwa, alichojua yeye Catherine alisha fariki dunia.

“Ametaja?”

Mwanamke mrefu wa wastani alitokea huku akiwa na mti wa chuma uliomsaidia kutembea, Kway alimtizama mwanamke aliyekua mbele yake Joyla, alikumbuka risasi aliyopigwa na Enock siku waliyokua wanawakomboa Catherine na Natu nchini Uganda,hata yeye hakuamini kama bado mwanamke huyo mpenzi wake wa zamani alikua akimtafuta, alijua teyari yasha kwisha kumbe ilikua ni kama kamwaga Petroli kwenye moto,.

Joyla na Mume wake Don Mullosi walimtafuta Kway kwa kipindi kirefu sana walishakula pesa nyingi za Carl Martin raia wa Germany baada ya kukubaliana kumuuza Catherine lakini hawakufanikiwa baada ya Kway na Enock kuingilia zoezi lao,

Bado walisumbuliwa na Carl Martin na kuwalazimu wamsake Kway kwa wudi na uvumba na kupata habari kuwa yupo nchini Kongo sehemu iliyoitwa Goma na ndo hapo walipo mkamata na kumteka na kuanza kumsulubu vya kutosha kutokana na hasira walizokua nazo.

“bado hajataja,ndio”

“mrudishe kwenye mti”

Kway alirudishwa kwenye mti na kuanza kuchapwa tena na mkia wa taa mwilini mwake, kila alipokua akichapwa ulitoka na nyama na kumchana, kelele za maumivu alizopiga hazikuweza kumzuia mtu anaye mchapa, vidonda alivyokua navyo vilianza tena kutoa damu, alilia sana kwa maumivu kama mtoto

“aaaaaah aaaaaaaaah”

Kway alilia machozi mpaka kumkauka kabisa, hakuweza tena kutoa sauti na kutulia kwenye mti hasemi tena.

“leteni maji mummwagie, zoezi liendelee tena”

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)