SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Kway alilia machozi mpaka kumkauka kabisa, hakuweza tena kutoa sauti na kutulia kwenye mti hasemi tena.
“leteni maji mummwagie, zoezi liendelee tena”
SASA ENDELEA...
Maji ya baridi yaliletwa na Kway kumwagiwa mwilini mwake,pale pale alizinduka na mateso kuendelea kama kawaida,hakutegemea kama Joyla angekua na roho mbaya zaidi ya shetani, maumivu aliyokua akisikia mwilini mwake hayakuweza kuelezeka, kimoyo moyo alimuomba Mungu eweze kuichukua roho yake japo alielewa kuwa anakufukuru.
“EEEH Mu…..ngu na….omba uichu..kue ro…ho yangu”
Aliwaza Kway! Na mateso kuzidi.kesho yake asubuhi sana walimfungua na kumlaza chali chini ya matope.
“Catherine yuko wapi bwana mdogo?”
Liliuliza jitu hilo katili
“am..eku.fa tayari”
“Ha ha ha ha ha unajifanya giniasi sio?”
“ukwe..li tena au mna muuli..zia cath..rine yupi?”
“Catherine uliyekuja wewe na fala mwenzako kumchukua”
“ame fariki tayari mi..mi sijui lolo..te mnanitesa tu bure, Catherine amekufa tayari siwezi kuwadanganya”
“ushawahi kushuhudia mtu ana kufa?, nitamleta mke wako nimuuwe mbele yako unashuhudia na sitoshindwa”
Hakuelewa ni kitu gani aongee,familia ya Rafiki yake marehemu Ramsey ndiyo iliyo mtia kwenye matatizo alijilaumu sana kujiingiza kwenye matatizo lakini alishaingia ilimbidi tu akubali matokeo,
“labdaaa niwape namb….a za simu za MAMA ya..ke ndiye atawapa jibu kamili tafadhali naomba maji ya kunywa ja…apo tone moja nina ki..u sana”
Alizidi kuongea maneno ya uchungu akiwa mwenye maumivu, na kuletewa maji taratibu alianza kuyanywa ila ghafla aliya tema kwa maumivu makali sana, ndani yalikua yana pilipili mtama iliyo mfanya awashwe sana, hapo ndipo ndoo ya maji ililetwa na kumiminiwa pili pili ya unga kisha Kway kumwagiwa mwilini mwake na kumuingia mpaka machoni hapo ndipo alipoangua kilio cha uchungu.
Kila alivyotaka kujikuna alihisi maumivu makali sana mwilini mwake na kuzidi kukwangua vidonda vilivyo sababishwa na mijeredi aliyopigwa.
Siku hiyo nzima ilipita akiwa mwenye maumivu mengi sana mwilini mwake.
“Namb…a za ma…ma yake zip..o kwen…y simu yangu”
“sasa tuta mpata vipi?”
“Siii…ju.i si…elew….i kwa kwe….l….i”
“okay, wacha tujaribu kumtafuta”
Mchakato wa kumtafuta Sabrina ulianza mara moja haikuwa rahisi kwa watu hao wanaomuhitaji kuamini kuwa catherine amefariki Dunia, ilikua ni lazima hata wapate mwili wake ili wamuoneshe Carl Martin kama ushahidi sababu ndiye yeye aliyemuhitaji kwa wudi na uvumba akizidi kumpa vitisho Don Mullosi na Mke wake Joyla hata wao walihaha.
“sasa twende Tanzania au?”
“Noo..nina watu wangu Tanzania watanisaidia kumpata huyo binti, nipe namba za huyo Mama, nifanye mawasiliano”
“utawasiliana na nani?”
“subiri uone”
Kikao kizima walizungumzia jinsi ya kumpata Catherine awe mzima au amekufa. Mawasiliano yalianza mara moja na kuruka nchini Tanzania, akiwasiliana na watu tofauti wa vitengo maalumu, alituma namba kwa mkuu wa mitandao ya simu ili aweze kuinasa namba iyo kisha kazi ya kumtafuta Catherine ifuate, haikupita hata siku nne tayari alishajua wapi alipo na kupewa taarifa, lakini taarifa zilizo mchanganya sana ni kusikia kuwa yupo ndani ya nyumba inayo teketea moto.
“nataka akiwa hai, fanya juu chini”
“sawa usijali”
Kila hatua aliyopiga Catherine mwanamke aliyeitwa Jenipher alikua nyuma yake akimfuatilia kila hatua anayopiga ni agizo hilo alilopewa na Don Mulosi aliyekua Demokrasia ya Kongo kwa wakati huo, alishapewa agizo kuwa Catherine awe hai kwa gharama yoyote ile,
Na ndo hapo hapo alipoamua kupiga simu gari la zima moto asubuhi alipoona nyumba aliyoingia Catherine ikiungua moto, baada ya dakika mbili gari tatu kubwa kikosi cha zima moto zilifika na kuanza kutoa mabomba ya maji makubwa ili kuuzima moto mkubwa ambao ulianza kuteketea.
Moto ulikua bado mkubwa sana ilibidi simu ipigwe na gari nyingine zenye maji kuja mbili,watu waliobobea kwenye kazi hiyo ya uzimaji moto walishika mabomba ya maji wawili wawili na kuzidi kuushambulia moto huo kwa maji.
“kuna watu ndani?”
Aliuliza mmoja kati ya watu hao zima moto
“ndio,nimeambiwa kuna watu wawili nadhani, lakini sina uhakika”
“wengie waingie kuwatoa moto ushapungua sasa”
Haraka haraka wasamalia wawili waliingia mbio mbio mpaka ndani kila mtu alisikitika sana kuona nyumba hiyo kubwa ya Enock ya kifahari ikiwa inateketea moto,
“hawa hapa”
Mmoja wao alishtuka baada ya kuwaona Enock na Catherine wapo juu ya kochi wame kakamaa.
“embu tuwatoe nje kwanza”
“sawa lakini wameungua upande mmoja kuwa makini”
“aya twende moja, mbili ta..”
Walisaidiana kuwa beba Enock na Catherine ivyo ivyo wakiwa kwenye kamba zao, maswali mengi walijiuliza lakini hawakuwa na majibu juu ya kamba walizofungwa walichotakiwa ni kuwawaisha hospitalini na wala sio kitu kingine, gari maalumu la wagonjwa lilikuja hapo hapo na safari ya kuelekea hospitalini kuanza. Jenipher hakucheza mbali nayeye alikua nyuma nyuma mpaka hospitalini, hakua na shida na Enock, shida yake ilikua ni kumchukua Catherine lakini ili mbidi afanye mambo taratibu sana na baadaye amteke, na ndo hayo yalikua mahesabu yake.
Enock na Catherine mpaka wanafikishwa hospitali walikua hawana fahamu zao kabisa ila mmoja kati ya hao wawili alikua na hali mbaya kuliko mwingine. Enock aliungua mgongoni na kufanya nyama zake zote zionekane, dalili ya kupona ilikua ni asilimia mbili, Waliingizwa ndani ya vyumba vya matibabu ili matibabu ya haraka yaanze mara moja.
“huyu ameshafariki”
Alisema Dokta Ibrahim baada ya kuchukua vipimo vya mapigo ya moyo kutoka kwa Enock,. Walimfunika na shuka jeupe na kusukumiza kitanda mpaka chumba maalumu cha kuhifadhia maiti yaani Monchwari ili kusubiri taratibu za ndugu zake waje kuchukua mwili wa Enock ili wafanye mazishi...
Hali ya ubaridi ndiyo iliyomfanya fahamu zimrudie hakuelewa ni wapi alipo zaidi ya kufumbua macho yake na kukuta yupo ndani ya giza nene,fikra zake zilirudi nyuma haraka kama umeme na kukumbuka mara ya mwisho alikua katika mateso na Catherine, kisha baadaye moto mkubwa ulikua ukiteketea,
lipapasa upande wa kushoto ili kumtafuta Catherine na kugusa chuma kingine, wakati mwingine alidhani keshafika Mbinguni kwa Mungu baba, sababu mara ya mwisho waliagana na Mpenzi wake tayari kwa safari ya ahera, alijipapasa mwilini mwake na kujikuta yupo kama aliyetoka tumboni mwa mama yake hana nguo hata moja!
Haikuchukua hata dakika mbili aligundua kuwa yupo ndani ya friji tena monchwari ili kuhakikisha hilo alijisukuma kwa nguvu zake zote na Friji kufunguka na kudondoka chini.
“Mtumeeeee!”
Sauti ya mlinzi mlinda maiti alidondosha sigara yake na kuanza kutetemeka sana baada ya kuona maiti imefumbua macho yake imedondoka chini, hapo hapo alimwaga kojo kwenye suruali yake akiwa anatetemeka sana sababu mambo hayo huona kwenye sinema za Nigeria,alirudi kinyume nyume kwa uwoga na kuteleza hapo hapo mpaka chini mzima mzima, kitendo cha kusimama alikimbia kama
‘kipepe’ huku akipiga kelele. Kitu kimoja kilichokuwa kinagonga katika akili ya Enock ni Catherine na ndiye aliyetaka kujua ni wapi alipo,aliona shuka pembeni yake na kujifunga na kuanza kutoka nje,
hapo ndipo watu walianza kukimbia baada ya kumuona anatoka ndani ya monchwari chumba cha kuhifadhia maiti!.
Watu walishaanza kukimbia huku na kule na habari kuanza kutapakaa hospitalini, za Enock kuzinduka monchwari wakidhani ni uchawi, dokta Ibrahim aliyempima mapigo ya moyo alifuatwa na jopo la madaktari na kumnusa mdomo wake, waligundua kuwa alikua amelewa ananuka pombe hapo hapo alifukuzwa kazi kwa kitendo cha kufanya mambo ya ajabu yatokee hospitalini,walielewa pombe ndiyo iliyomfanya atoe majibu hayo.
Taratibu walimfuata Enock ambaye anatembea kila wodi anamtafuta Catherine wake huku akiwa ana majeraha ya moto mgongoni mwake.
“kijanaa”
Aliita mmoja wa madaktari.
“Naam, Catherine yupo wapi?”
“yupo, yupo usijali yupo salama nachokuomba uje naomba upunguze jazba, mkeo yupo salama yupo kwenye matibabu”
“sawa yuko wapi? Nahitaji kumuona sasa hivi”
Madaktari walimtuliza na kumsogelea karibu ili wampe mavazi ya kuvaa kisha baada ya muda mfupi waliingia nae mpaka ndani ya chumba alichokua Catherine, alikua teyari keyafumbua macho yake lakini anaongea kwa shida.
“Mun..gu yupo pa..moja na.sisi Enock tumepona”
“Ni kweli mpenzi wangu tumekishinda kifo, unajisikiaje?”
“Nitapona usijali,naaa.omba umpigie simu MAMA yangu mwambie nipo mahali hapa,”
“sawa Cathe nakupenda sana”
Enock tayari aliridhika na kulazimika apatiwe matibabu sababu bado alikua na majeraha yanatoa damu mwilini mwake, hata yeye hakuamini yupo hai mpaka dakika hiyo, alishajihesabia yeye ni maiti baada ya moto mkubwa kuzuka nyumbani kwake uliosababishwa na jambazi aliyetumwa na baba yake Mzazi Mzee Mwasha.
“Mimi naitwa jenipher unajisikiaje Catherine?”
“sasa hivi nina hali nzuri sana”
“Utapona sawa mamii”
“Ahsante”
Pembeni alisimama Mama yake catherine na Mwanamke aliyeitwa Jenipher, japo hakumjua ni nani lakini alijua kuwa ni msamalia mwema aliyeokoa maisha yake sababu alijielezea hapo awali, alijikuta anazoeana sana na Jenipher kutokana na kila siku kuwepo hospitalini hapo, hakuelewa kuwa
Mwanamke huyo hatari sana laiti angejua wenda angekaa nae mbali sana, alikua ndani ya giza nene sasa, hakujua ukweli uliojificha nyuma ya pazia, hakuelewa kuwa alikua ni mtu wa Don Mullosi na siku chache baadaye angerudi mikononi mwao, Jenipher ilibidi afanye mambo taratibu sana hata ingemchukua mwezi mzima, ilikua ni lazima afanikishe zoezi hilo na kupewa pesa nyingi walizomuhaidi.
Kwa upande wa Naomi bado alikua na kinyongo sana juu ya watu hao wawili haswa kwa Catherine habari zilisha mfikia tayari kuwa wapo hospitali na waliponea chup chup kufa kutokana na itlfau ya moto mkubwa, hata yeye alikua katika harakati za kuwauwa watu hao wawili, alishapata jina la Dokta Simon kuwa ndiye anayehusika na matibabu yote ya Catherine,
Taratibu sana alianza kumzoea na kuanza kuwa nae karibu mara kwa mara.
“hapa ni kumpa mapenzi tu, nishajua huyu mwanaume ni dhaifu sana mimi ni mwanamke lazima atafanya kazi yangu kirahisi sana bila kumpa hata senti tano”
Aliwaza Naomi na kumpigia simu dokta Simon usiku huo huo wa saa mbili.
“Dokta mambo”
“safi tu”
“tunaweza tuka onana?”
“ndio itawezekana, inategemea na muda”
“sasa hivi”
“aaaah well, labda baada ya lisaa”
“sawa”
“sasa wapi?”
“ni mambo ya siri tukutane Rombo Hotel shekilango”
“sawa nitakuja”
“okay”
Naomi alishajiona mshindi tayari alitafuta chumba haraka haraka, na baada ya masaa mawili alikua na daktari huyo chumbani, taratibu alitoa nguo yake ya juu na kubaki na sidiria Dokta Simon alishindwa kuelewa.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA