BIKRA YANGU (55)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Jasho liliaza kumtoka mwilini mwake na kulowanisha shati alilokua amelivaa japo alikua ametoka kuoga muda mchache uliopita, alikua katika wakati mgumu sana, ilibidi tu achukue maamuzi ya kuuwa ili kuepukana na fedhea atakayoipata siku chache zijazo, bila kuongea chochote Dokta Simon aliingia ndani ya gari mpaka hospitalini, hakua na chaguo lingine zaidi ya kuandaa chupa yenye sumu kali sana na kuiweka ndani ya droo lake akisubiri usiku uingie ili amalize kazi yake.

SASA ENDELEA...
“dokta simon kuna kitu nataka nikwambie samahani lakini”

Muuguzi wa kike aliingia ofisini mwake.

“sipo sawa sasa hivi njoo baadae au kesho”

“hapana ni muhimu,”

“sipo sawa kuruthumu,niache kidogo”

Kweli alikua amechanganyikiwa, alimaini kuwa baadae ataenda kubeba dhambi kubwa sana ya kuuwa mtu asiyekua na hatia, alijutia sana ni kwanini alifanya mapenzi,alimlaumu sana shetani alitamani muda urudi nyuma angalau amkatae Naomi, lakini hilo halikuwezekana alikua kesha chelewa tayari, na ana masaa machache tu atimize aliyoambiwa,bado jasho lilizidi kumtoka mwilini mwake, masaa yalienda haraka haraka siku iyo mpaka giza linaingia bado alikua juu ya kiti chake ndani ofisini akitafakari,

Alivuta droo na kutoa kichupa cha sumu na kuweka pamoja na bomba la sindano ndani ya koti lake kubwa jeupe, baadhi ya wauguzi walishaanza kuaga na kuondoka ili baadae waingie wenye zamu za usiku, alitembea mpaka wodi alilolazwa Catherine, alikijua sana kitanda alicholazwa, na kuona alivyojifunika shuka gubi gubi mpaka usoni kama afanyavyo kila siku, bila kuuliza kitu chochote 

Alimchoma sindano ya sumu hiyo kali shingoni huku akizikandamiza pua zake, miguu ilivyokua ikitupwa tupwa juu ya kitanda ilimaanisha kuwa pumzi imekosekana ivyo baada ya muda mfupi angetulia, alizidi kukandamiza mikono yake puani mwa catherine, baada ya sekunde chache sumu ilikua teyari isha sambaa mwilini na kufanya ukimnya utawale,kazi aliyokua ametumwa aifanye tayari alikua ameikamilisha.

Alichomshukuru Mungu wake binti yake hakua na maambukizi ya virusi vya ukimwi bali ni magonjwa ya zinaa ndiyo yalikua yakimtesa kupindukia, kutokana na uhaba wa dawa hospitalini hapo ilibidi kitendo cha haraka kifanyike cha Catherine kuhamishwa hospitali.

“Kuruthumu, muandikie huyu mgonjwa transafer”

“lakini si mpaka Dokta Simon afike?”

“hayupo sasa, na simpati kwenye simu yake, itabidi umwambie kesho asubuhi akifika, hatuwezi kumuacha huyu binti afe”

“sawa hakuna tabu”

“andika na dawa zote alizokua akitumia hapa”

“sawa dokta”

Utaratibu wa Catherine kuhamishwa hospitali ulianza dakika hiyo hiyo na kupelekwa hospitali nyingine, hawakujua kuwa ni kama Mungu alikua akiipigania roho yake bado,hawakuelewa kuwa isingekuwa kumuhamisha hospitali wenda angeuwawa mara moja,

Matibabu yalianza haraka sana akiwa hospitali nyingine, hapo alipata ahueni na hali yake taratibu kurudi kama awali, miezi ilizidi kukatika tayari na siku kuyoyoma siku hiyo asubuhi na mapema Mama yake alivyo fika hospitalini hakumkuta alishtuka sana na kuanza kuwauliza madaktari.

“Alitoka na mwenzake hapa Yule Jenipher”

Alijibu daktari

“tangu saa ngapi?”

“Asubuhi sana”

“mbona hakuniambia lakini, ngoja nimtafute kwenye simu”

Kilichomchanganya tena simu ilikua haipo hewani. Lakini hakuweka mashaka ya aina yoyote, sababu alishamzoea Jenipher tangu wanamuuguza Catherine hapo hospitalini akimletea chakula pamoja na baadhi ya pesa za matibabu, hakujua kuwa yupo ndani ya kiza kinene hakuelewa kuwa mwanamke huyo Jenipher ni zaidi ya chui….

Moyo wa Sabrina ulizidi kumwenda mbio lakini bado alijipa matumaini kuwa mwanae Catherine yupo salama huko alipo japokuwa alikua hapatikani hewani, hakutaka kubanduka hospitalini ili kumsubiri Jenipha kitu alichojilaumu ni kutokua na namba ya mwanamke huyo ambaye madaktari walidai aliondoka na binti yake.Alizidi kukaa juu ya benchi bila kuona dalili yoyote ile ya Catherine kutokea, na ndo hapo alipoinuka mpaka mapokezi kwenda kumuulizia tena.

“kwani alivyoondoka hakuaga?”

“hapana, hakuaga”

“inakuaje mnaruhusu mgonjwa kiholela aondoke na mtu ambaye hana uhusiano nae?”

“alidai kuwa wanaenda kufanya mazoezi na Yule ndugu yake,lakini watarudi sasa hivi”

Hata wauguzi nao walishaanza kuingiwa na mashaka mioyoni mwao, picha ilionesha kuwa kuna kitu kibaya kimetokea kwa mgonjwa wao, hio ilimaanisha vibarua vyao vitaota nyasi endapo Catherine atapata matatizo ya aina yoyote yale huko alipo,

Ghafla walimuona Jenipha amefika hospitalini lakini bila ya Catherine pembeni wala nyuma yake, Sabrina Alisimama wima na kumuendea kwa haraka.

“Catherine yuko wapi?”

“yupo hapo nje samahani Mama kulikua kuna foleni ndio maana tumechelewa nilimpeleka kidogo akafanye mazoezi”

Alijibu Jenipha kwa upole Mama Catherine hakuelewa kuwa anaongea na mwanamke hatari mno,Jenipher hakutaka kupeleka mambo harakaharaka ilibidi ayafanye mambo taratibu sana ili ampeleke Catherine Kongo akiwa salama Salmin kwa Don Mullosi,alishapewa hundi ya milioni tano teyari kama malipo na kubaki na salio la shilingi milioni mbili endapo atafanikiwa kumkabidhisha Catherine kwa watu wabaya ambao bado walitaka kumpeleka nchini Germany na hapo ndipo kazi yake hiyo ndogo kuisha.

Catherine alitokea akiwa mwenye furaha sana na kumsalimia Mama yake, wote walikumbatiana kwa furaha baada ya kuonana tena, baada ya siku mbili kupita Catherine aliruhusiwa kutoka hospitalini kutokana na hali yake kuwa nzuri kiafya, alipatiwa dawa za kutumia akiwa nyumbani kwao, ilikua furaha sana kwake, Kwa upande wa Enock aliruhusiwa siku tatu kabla, alisikitika sana kuona nyumba yake kubwa imetekea na moto na kuwa kama gofu,alinyoosha mpaka kituo cha polisi baada ya kupigiwa simu na mkuu wa kituo ili kutoa maelezo ya ziada kabla ya nyumba yake kuungua na moto.

“Ndio, kuna mtu alikuja akatufunga kamba mimi na mpenzi wangu, kisha baadae akamimina mafuta ya petroli”

“huyo mtu unamfahamu?”

“hapana simfahamu”

“kuna mtu yoyote una ugomvi nae?”

“ndio”

“nani?”

“baba yangu mzazi”

Polisi walizidi kuandika maelezo ya Enock kwenye karatasi.

“unajua alipo kwa sasa hivi?”

“hapana, lakini mimi mwenyewe nita mkamata kwa mikono yangu, lazima nimuuwe nifungwe. Lazima nimuuwe mwenyewe, nitamtafuta kwa gharama yoyote ile, hawezi kunifanya niishi kwa wasi wasi, hastaili kuishi huyu mzee!”

Aliongea Enock kwa hasira sana akiwa anapigapiga kifua chake kwa Uchungu sana huku pumzi zikiwa zimemjaa kifuani mwake na kufanya kifua chake kipande juu na kushuka.

“punguza jazba Enock ili tuongee kwa utaratibu, wewe nenda tutakupigia simu tukikuhitaji tena, tupe siku nne tutakua tumemtia nguvuni, hiyo ndiyo kazi yetu jeshi la polisi”

Aliongea mmoja wa polisi akiwa na uhakika kwa kile anachokisema, Enock aliondoka akiwa na Amani japo sio sana, sababu hata yeye alielewa ni jinsi gani baba yake mzee Mwasha alivyokua katili na asiye kubali kushindwa kitu,

“Dad, lazima nikutafute”

Alisema mwenyewe kwa jazba akiwa ndani ya gari akielekea Goigi kwa rafiki yake Anderson Peter na ndo hapo alipokua akiishi tangu alipo ruhusiwa hospitalini, hakua na mahali pa kulala tena, Anderson peter ndiye aliyempa hifadhi kwa kila kitu alichohitaji, kama rafiki yake hakuweza kumuacha ateseke au akodi hotel na kupoteza pesa.

Mwanamke aliyeitwa Jenipha alizidi kuzoeleka nyumbani kwa akina Catherine hata wakati mwingine kudiriki kulala kabisa, Mama Catherine hakua na tatizo kabisa juu ya mwanamke huyo, sababu alimuamini na wakati mwingine kuwaruhusu waende popote akiwapa gari yake wakatembee sehemu tofauti, alishamuamini kabisa asilimia zote mia moja bila kufanya utafiti wowote juu ya mwanamke huyu.

Hata kwa Catherine naye ilikuwa ivyo ivyo kwa upande wake, alipata faraja sana na kumuamini Jenipha kwa muda mchache sana, sababu ya kuonesha kuwa nae karibu mno tangu alipokua hospitalini anapatiwa matibabu baada ya kunusurika kifo cha moto, hakuelewa hata yeye kuwa muda mchache baadaye ataingia tena kwenye matatizo makubwa kama asipokuwa makini.

“Catherine”

Aliita Jenipher siku hiyo wakiwa wanaelekea sokoni kununua vyakula vya kupika mchana nyumbani.

“Nambie Jenifa” “Mama yangu anaumwa sana”

“Jamani nini tatizo anaumwa nini?”

“Ana presha, alafu mimi ndiye mtoto wake wa pekee baba yangu alifariki tangu nipo mdogo sana, nampenda sana Mama yangu kuliko kitu kingine chochote kile”

Aliongea Jenipher kwa simanzi sana huku machozi yakimlega,

“pole sana, inabidi uwende ukamuone”

Catherine aliguswa na historia hiyo.

“sina mtu wa kunisindikiza naomba twende wote”

“sawa mimi nipo tayari, lakini tuwahi kurudi ili tupike,tukishatoka kumuona”

“hapana Catherine hayupo hapa nchini”

“sijakuelewa”

“yupo India, naomba unisindikize”

“Mhh… Wacha niongee na Mama kwanza ili tujue tutafanya nini, yeye ndiye atakae toa ruksa”

“sawa ahsante sana Catherine”

Moyo wa Jenipha ulijawa na furaha sana ni baada ya kuona njama alizopanga zina mnyookea za kumkabidhisha Catherine mikononi mwa Don Mullosi tena bila kutumia nguvu yoyote ile wala silaha, aliwasiliana na Mullosi pamoja na Joyla kwa kila hatua aliyopiga na wao walifurahishwa sana na utendaji kazi wa mwanamke huyo Jenipha na kumsubiri sana Catherine nchini Uganda na baada ya hapo wamkabidhi kwa Carl Martin wamalize biashara yao kwani alishawasumbua sana.

Mama Catherine hakuwa na tatizo lolote lile juu ya Catherine kuondoka na Jenipha alitokea kumuamini sana na kumchukulia kama mwanae wa kumzaa alichokosea ni kutokumchunguza ni wapi anaishi, wema wake tu ndio aliyochukulia kuwa hakua mtu mbaya kwao hata kidogo, hata alivyosikia habari za Mama yake kuwa yupo India Anaumwa alishtuka sana,na kuwaongezea kiasi cha pesa kidogo kiwasaidie mbele ya safari sababu kuanzia nauli mpaka makazi Jenipha ndiye alisema atagharamia.

“Mimi nawatakia safari njema wanangu, Mama yako atapona sawa, Mungu atampigania”

“Ahsante Mama”

Mama Catherine aliwapa Baraka zote na kuwaombea wafike salama na Mungu awatangulie, mipango ya tikeki ya ndege ilikua teyari imekamilika mpaka visa ndani ya wiki moja baadaye. Ni siku mbili tu zilibaki ili safari yao ianze. Catherine hakutaka kuondoka bila ya kumuaga Enock kupitia simu, kwa kuwa alikua bize siku hiyo hawakubahatika kuonana, Catherine hakua na neno juu yake.

Wote waliamka saa kumi na mbili ya asubuhi siku hiyo kwa ajiiri ya safari, Jenipha alilala kwa akina Catherine ili asichelewe na kuachwa na ndege, siku hiyo asubuhi ya saa mbili walijiaanda na kupata kifungua kinywa kisha baadaye kupakia mabegi yao ndani ya gari, kila kitu kilivyo kaa sawa tu Mama Catherine aliondosha gari mpaka uwanja wa ndege Mwalimu Nyerere ili kuwahi shirika la Ndege la RwandAir.

Walifika uwanja wa ndege na kushusha mizigo yao nyuma ya buti kisha kuanza kuburuza mabegi yao.
“wanangu nawatakieni safari njema”

“sawa Mama hata wewe ubaki salama”

“kuweni makini sana, Catherine ukirudi tu inakubidi uje umalizie chuo Mama sawa?”
“sawa Mama”

Wote walikumbatiana kisha kuagana kwa mara ya mwisho, walifika mlangoni na kuweka mabegi yao juu ya mashine maalumu inayopeleka mabegi upande wa pili na wao kupita mlangoni mpaka ndani ya ndege.

Sauti nyororo kutokea kwenye spika za pembeni ziliwataka wafunge mikanda sababu ndege ilikua tayari inaondoka, baada ya dakika mbili taratibu ilianza kutembea kisha kuchanganya kasi na baadaye matairi ya mbele kuinuka na ya nyuma kufuata ikipaa angani.

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)