SEHEMU YA HAMSINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Kway akiwa amelala sakafuni amelowa damu nyingi, hakutaka kupoteza wakati, mzima mzima aliingia na kumtwanga Don Mullosi na kitako cha bastola kichwani aliyekua juu anampiga denda Joyla na kujisahau kuwa yupo seblen.SASA ENDELEA...
“kaeni chini sasa hivi”
Alifoka Catherine akiwa kaishika bastola vizuri tena na mikono yake yote miwili tayari kwa kufyatua endapo wataenda kinyume.
“Catherine!”
“kaa kimnya, nenda kamfungue Kway kahaba wewe”
Kwa hofu nyingi Joyla alitembea Mpaka kwa Kway aliyekua chini na kumfungua kamba zote walizomfunga.
“aya mfunge huyo baasha ako pia na kamba, FANYA UPESI kabla sija weka ubongo wako sakafuni”
Joyla alitii kila kitu alichoambiwa na mwanamke jasiri Catherine aliyekua mbele yake na bastola tayari kwa kuuwa, alienda na kumfunga Don Mullosi kamba mikononi na miguuni kisha kusimama huku mikono yake ikiwa juu, na kuhamriwa mpaka ndani ya chumba kikubwa kilichokua kina wanawake wengi waliotekwa nyara, wote walifunguliwa na kuwa huru kabisa, Joyla akiwa Mbele Catherine nyuma yake akiwa amemuwekea bastola nyuma ya kisogo chake bado, ghafla alivyofika seblen
Alimuona Kway amesimamishwa huku nyuma yake akiwa amesimama Don Mullosi na bastola ambayo amemuwekea Kway Kichwani, alishaelewa maana yake kuwa asalimu amri vinginevyo risasi ingepenya na kumwaga ubongo wa Kway chini aliyemchukulia kuwa ni Baba yake, bado alikua katika wakati mgumu sana, hakutaka kukubali kirahisi, nayeye alimvuta Joyla na kumkaba shingoni na kumuwekea bastola kichwani.
“Binti weka bastola yako chini,”
“hapana”
“WEka moja,”
“Hapana weka wewe nitamuuwa mkeo”
“weka mbili,”
Don Mulosi hakuwa na masihala, alishaanza kuhesabu tayari huku taratibu kidole chake kikisogea kwenye triga,kumaanisha kuwa kitendo cha kuvuta Triga risasi ingetoka na kumuondosha Kway Duniani hapo hapo.
“WEka ta…. Paaaaaaaaaa”
Kilichosikika hapo ulikua ni mlio wa bastola na kufanya risasi kufumuka kutoka ndani ya chemba.
Moto ulioteketeza nyumba ya Enock kwa nia ya kumuuwa akiwa na Mpenzi wake Catherine haukuweza kuzaa matunda kwani waliokolewa na sasa wapo salama Salmin!
Ilikua kazi rahisi sana kwa taarifa izo kumfikia Mzee Mwasha aliyekua huko kisiwani Unguja ameweka kambi yake amejificha na kulindwa sana, alishaamua kuwa Gaidi sasa, bado alikua ana kisasi na watu watatu Catherine, Enock na Sabrina, aliapia ni lazima awamalize tena kwa mikono yake miwili ndipo apumzike au ajisalimishe polisi!.
Tetesi zilifika mpaka makao makuu ya polisi kituo kikuu cha staki shari kuwa Mzee Mwasha ambaye anatishia na kuogopeka anaishi Kisiwani Unguja, waliandaa majeshi yao na kubeba silaha za kutosha, haraka haraka askari shupavu walipewa taarifa hizo na kuweka kikao kidogo cha siri,kilichofanywa na maaskari kumi na sita.
“sasa tunaenda kufanya ambushi”
“sawa mkuu”
“kuna cha ziada?”
“hapana mkuu”
“Mpigie kamishna Brighton MANDA mwambie sisi tunaanza safari sasa hivi, baada ya masaa mawili tutakuwa tumefika,mwambie tushawasiliana na jeshi la Zanzibar”
“sawa mkuu”
“sawa mkuu”
Wote waliitikia kwa pamoja.
Kila Askari alikua teyari kajipanga kwa ajili ya msako mkali waliokua wameupanga Muda mrefu sana dhidi ya Mzee Mwasha aliyekua tishio sasa jijini Dar es salaam,kwa ujambazi na uharamia, kikao kilifungwa saa tisa ya alasiri na wote kuingia ndani ya defender mpaka bandarini posta, hapo walichukua boti za polisi zilizokua tayari zimeandaliwa na wote kuingia,
Boti za spidi zilizidi kwenda mwendokasi zikikata mawimbi huku polisi wakizidi kufanya mawasiliano kupitia redio upepo na jeshi la Zanzibar ambao hata wao walikua wanajua ugeni huo, kutokana na kasi za boti hizo zilizokua na injini mbili nyuma, lisaa limoja na nusu waliwasili na kupokelewa na Jeshi la polisi Zanzibar.
Risasi ilipenya moja kwa moja na kuzama ndani ya ubongo wa Don Mullosi ni kitendo cha umakini wa hali ya juu sana ndio uliofanyika,kitendo cha Catherine kupima kwa jicho moja na kuona kichwa cha Mulosi kimejitokeza akiwa nyuma ya Kway ndiko kilichofanya avute triga bila kujifikiria na kufanya umauti umkute Don Mullosi hapo hapo.
Kama asingekua na shabaha basi Kway ndiye angekua chini na ubongo wake kutapakaa sakafuni, hakua yule Catherine ambaye anamjua miaka mingi iliyopita, sasa alikua ni mwanamke anayejiamini mwenye mengi mafunzo ya kupigana hata ujuzi wa kutumia bastola vile vile na ndiye yeye aliyefanya ukombozi na kumuweka Kway huru pamoja na wanawake waliokuwa wakiteseka na kuchezeshwa filamu za Ngono!.
Bastola aliyoshika ilikua bado inafuka moshi na ndo hapo alipomsukumiza Joyla mpaka juu ya sofa, akitetemeka na kufanya ajikojolee ndani ya jinsi aliyovaa baada ya kuona Ubongo wa Mume wake upo chini na damu kutapakaa, lilikua ni tukio la kutisha ambalo hakuliamini mbele ya macho yake.
“sasa mbona umejikojolea mtu mzima?”
“Ninininini samehe Catherine Mwanangu”
“haustaili kuishi hata kidogo, mshahara wa dhambi ni mauti we….”
“paaa paaa paaaaa”
Catherine alishtuka sana baada ya kusikia mlio wa bastola sababu hakuwa yeye amefyatua risasi alivyogeuza shingo yake nyuma Alimuona Kway ndiye kashika bastola akiwa anayabana meno yake, dalili zilionesha kuwa alikua na hasira sana na mwanamke huyo, alisimama kwa shida na kumpiga risasi nyingine Joyla ya kichwani papo hapo.
Mateso aliyokua anayapata hakika hakuweza kuyasahau, alimgeukia Catherine na kumshukuru sana kwa alicho mfanyia.
“wapigieni simu wazazi wenu mpo huru sasa”
Agizo hilo alitoa Catherine,kwa wanawake waliokuwa mateka.
Hakuweza kwenda popote pale isipokuwa kurudi nchini Kongo ili ahakikishe usalama wa mke wake Mama Natu, Moyo wake ulitulia baada ya kuongea naye kupitia simu ya mkononi kisha safari ya kwenda kongo kuanza, kwa kuwa Catherine alikua na pesa bank. walitafuta usafiri wa basi ili waanze safari usiku huo huo, ni kweli walipata basi na kukata tiketi kisha kuingia na kusubiri safari.
“Najua kinachoendelea,najua wewe ni baba yangu sasa hivi”
Aliongea Catherine wakiwa ndani ya basi safarini.
“Naomba niruhusu nikuite Baba, mimi sina Baba.. Baba yangu alikufa kipindi nipo mdogo, nilitamani siku moja namimi niite Baba kama wanafunzi wenzangu lakini sikuweza, sikutaka kumkufuru Mungu sababu najua ni mipango yake,Christopher ni mdogo wangu, najua wewe ndiye Baba yake najua unamchukia Mama yangu, lakini naomba umsamehe na tuishi kama familia”
Catherine alitia huruma aliongea huku machozi yakimlenga na kutamani kulia, Kway aliyekua pembeni yake alinyamaza kimnya bila kusema lolote, hata yeye aliingiwa na huruma alimkumbuka sana rafiki yake marehemu Ramsey walivyokuwa wakiishi miaka mingi iliyopita, mpaka alivyokufa kifo kibaya cha kansa ya ubongo, alivuta fikra zake nyuma jinsi kipindi Catherine ana miaka miwili alivyompoteza baba yake huyo, ni yeye Loyda pamoja na Sabrina ndiyo waliokua wakipigania kuokoa uhai wa Ramsey na kufia uwanja wa ndege wakijaribu kumsafirisha India kwa ajili ya matibabu, na kugundua kuwa ni miaka mingi sana ilipita, lakini alijiona ni mwenye dhambi sana kumsaliti rafiki yake na kutembea na Sabrina.
Licha ya kuwaza hayo yote aliamini kuwa yashatokea na hana jinsi tena ya kurudisha mambo nyuma na kuyabadilisha.
Ni kweli alimzalisha Sabrina Mtoto, ilibidi tu awe kama mwanafamilia achukue jukumu la kuwatunza,
“Catherine”
Aliita Kway.
“Abee”
“Kwanzia leo mimi nitakua baba yako,nitahakikisha nakulea na kukusomesha pia, Nakupenda mwanangu”
Maneno hayo yalimfariji sana Catherine na wote kukombatiana wakiwa wenye furaha sana mioyoni mwao. Basi kubwa la kusafiria lilizidi kusonga mbele,Siku nzima walikua njiani bado hawajawasili nchini Kongo.
Asubuhi ya saa mbili walikua wamefika nchini kongo na kutafuta usafiri mwingine uliowapeleka mpaka Bukavu, hapo walinyoosha mpaka nyumbani alipokua anaishi na Julia mke wake na kutamani afike mapema ili aonane nae!.
Moyo wa Kway ulizidi kumlipuka na kumwenda mbio, alitoa macho yake baada ya kuangalia chini na kuona michirizi ya damu, dalili zilionesha kuwa hakukua na usalama hata kidogo alizidi kufuata damu zilizopita mpaka seblen kisha kuelekea chumbani, hata kwa Catherine alikua na hofu lakini sio sana. Alisogea Kwa hatua za taratibu, picha iliyomjia kway ilikua ni lazima mke wake atakua amejeruhiwa na risasi na kufa, alimuomba Mungu sana ndani ya moyo wake yasiwe kweli kwa anayofikiria.
Mikono yake ilikua na jasho sana baada ya kufungua mlango wa chumba alipoona kuna michirizi ya damu ilipoelekea……
Kway na Wanawake wengine waliokuwa mateka sasa wapo huru wamekombolewa kutoka ndani ya nyumba kubwa iliyokua na ulinzi wa kutosha huko nchini Uganda na Mwanamke Catherine huku nyuma akiwaachia jeshi la polisi lifanye kazi yake,
lilikua ni jambo la kushangaza kwa mwanamke huyu tena mmoja kufanya kitendo ambacho hata kwa jeshi la polisi lilishindwa kutekeleza.
Hakuwa Yule Catherine aliyemeza sumu na kutaka kujiua kisa mapenzi miaka ya nyuma iliyopita, hakua Catherine aliyekua lelemama na dhaifu, sasa ni mwanamke mwingine shupavu aliyekua na mafunzo mengi ya kujitetea na kujiamini pia, hata wewe ungemuona na kupewa historia yake ungekataa katakata kuwa ndiye aliyewatoa watu mateka!.
Alishamuokoa Kway tayari na kuanza safari ya kuelekea nchini kongo Kwa Mama Natu kisha baadaye waweze kuondoka na kurejea nchini Kwao Tanzania, njiani waliongea mengi sana hususani juu ya mambo yaliyopita.
Kway alikubali kumlea Catherine kama mwanae wa kumzaa, ni Mwanamke aliyeitwa Sabrina ndiye aliyawaunganisha. wote wawili walikua wenye furaha sana lakini furaha yao ilikatika ghafla baada ya kufika tu nchini kongo. Michirizi ya damu ndiyo iliyowashtua na kuingiwa na hofu mioyoni mwao. Walizidi kufuata michirizi mpaka chumbani.
“Mama Natu!”
Aliita Kway baada ya kumuona Mke wake anajifunga na bandeji mkononi mwake.
“nimeyikata na kisu nilikua napika”
Wote walikumbatiana kwa furaha zote baada ya kuonana tena wakiwa wazima. Mama Natu muda wote alijawa na furaha kumuona Mume wake akiwa salama Salmin! hakutegemea kama angekuwa hai.
Hakuwa na kinyongo cha aina yoyote alivyomuona Catherine mbele yake,ilibidi Kway aweke mambo wazi wakimjumuisha Catherine awe kama mtoto wao wa kumzaa, Julia hakua na haja ya kuweka kipingamizi na kuonesha hali ya chuki badala yake alimshukuru sana alivyosikia kuwa ndiye yeye aliyemkomboa Mume wake Kway.
Siku mbili nzima walishinda vizuri, Kway akiwa anapatiwa matibabu ya majeraha yaliyotokana na kuteswa. Baada ya wiki kukatika walichukua usafiri mpaka kwa wazazi wake na Julia ili kuomba tena baraka zao.
Hata wao walivyowaona hawakuwa na haja tena ya kuweka kizuizi cha aina yoyote ile kama hapo awali,ili mradi mtoto wao Julia karudi katika furaha.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA