SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Hata wao walivyowaona hawakuwa na haja tena ya kuweka kizuizi cha aina yoyote ile kama hapo awali,ili mradi mtoto wao Julia karudi katika furaha.SASA ENDELEA...
“Mimi sina cha zaidi, napenda tu kumshukuru Mungu maana pasipo yeye wenda tungekua tunaongea mengine,naamini mambo tuliyopitia mimi na Mama Natu ni mitihani tu ya hapa Duniani”
Alizungumza Kway akiwa katikati ya wazee wa kikongo.
“hakuna njoo mushida yoyote ile,ako nataka kumuomba Mungu aliye yuu Mbiguni atende Miuyiza,Mimi nawatakia Mupate Baraka zote wanangu, pia utusamehe sisi kwa kukuondoshea Mukeo Tanzania”
Baba Mzazi wa Julia alitoa Baraka zote na siku hiyo hiyo walichinja Ng’ombe mzima kama kuwapa Baraka na ndio ivyo walivyoamini.baadhi ya wazee walikaa kikao kidogo wakiteta kwa lugha ya kikongo na kuwapa kila baraka wakiamini kuwa wameshawaondolea Nuksi.
Wote walirudi wakiwa wenye furaha sana,siku hiyo hiyo walitafuta tiketi tatu za Ndege itakayo ondoka kesho yake jioni.kweli walipata ndege, muda huo ulitosha kabisa kujiandaa na kupanga kila kitu kuanzia nguo zao na vingine kadhalika.
Hata kwa Catherine vile vile alitamani hata kesho ifike mapema ili aweze kurudi nchini Tanzania, alimkumbuka sana Enock mpenzi wake.walimaliza kula chakula cha usiku na kila mtu kuelekea chumbani kwake kulala kwa ajili ya kesho yake safarini.
“Darling nimekumisi sana”
Alisema Julia akimwambia Mume wake usiku mnene baada ya kumaliza kupanga nguo kwa ajili ya safari.
“hata mimi mke wangu”
Na ndo hapo walipoanza kunyonyana midomo yao kisha kuvuana nguo na kubaki kama walivyotoka tumboni mwa Mama zao, ni kweli ilionekana kila mtu alikua na hamu na mwenzake kutokana na fujo za mabusu walizokua wanapeana. Hakika ilikua ni kama siku yao mpya.miguno ya mahaba ndiyo peke yake iliyosikika na kelele za chaga kwa mbali!.
Asubuhi kulichuka tayari. Catherine ndiye aliye kuwa wa kwanza kuamka kutoka kitandani na kuanza kufanya usafi wa mwisho, baada ya hapo alitenga chai jikoni kisha kwenda chumbani kuwaamsha wazazi wake Kway na Julia.
Hata wao ilionekana walikua macho, hawakuchukua muda mwingi walikua wameshajindaa na wote kujumuika mezani kwa ajili ya kula chakula cha asubuhi.
walipanga panga vitu na kuweka sawa. Majira ya saa nane mchana waliweka mabegi yao nje ili kuwahi ndege inayoondoka Saa kumi jioni ya siku hiyo hiyo.
Dereva taxi kutoka uwanja wa ndege ambaye walifanya naye mawasiliano jana yake alishafika tayari na kuanza kuingiza mizigo ndani ya boneti kisha wote kuingia ndani ya taxi.
Haikuchukua hata dakika sitini walikua teyari wapo uwanja wa ndege na kushusha mabegi yao.
Wote walikua wenye nyuso zenye furaha muda wote wakitabasamu, kila mtu alitamani kufika Tanzania wakati huo huo.Wakati Catherine ana muwaza Enock, Kway na mke wake muda wote walimuwaza mtoto wao mdogo Natu waliyemkabidhi Kwa Husssein Molito wakiwasiliana naye kwa njia ya simu, ni kipindi kirefu sana.
Waliweka mizigo yao juu ya mashine maalumu kisha kuvua vitu vyote vya chuma chuma kama utaratibu.
Macho ya Catherine yalitua juu ya sura ya mwanaume mrefu aliyevalia kanzu mwenye ndevu nyingi kama za Osama bin Laden aliyekuwa na asili ya kiarabu.
Hakika sura hiyo haikuwa ngeni machoni mwake lakini hakukumbuka ni wapi aliiona. Hofu na mashaka ndivyo vilimtanda moyoni mwake.Ni kweli alivyojaribu kumuangalia mwanaume huyo machoni aliinamisha kichwa chake chini!.
“Huyu Mzee nilimuona wapi Mungu wangu”
Aliwaza Catherine baada ya kuingia ndani ya ndege akiweka begi lake dogo juu ya sehemu maalumu ya kuwekea mizigo midogo, alimtizama mwarabu huyo mpaka alipoenda kuketi siti za nyuma. Sauti nyororo ndiyo iliyowashtua waweze kufunga mikanda kwani ndege inaanza kupaa angani. Kila abiria alifunga mkanda wake,bado Catherine aligeuza geuza shingo yake akimtizama mwarabu huyo, lakini ghafla hakumuona siti za nyuma na ndo hapo alipoamua kusimama nayeye.
“Dada samahani naomba ukae kwenye siti yako na ufunge mkanda, ndege ikiwa hewani ndiyo tutawaruhusu muweze kutembea”
Sauti ya muhudumu wa Ndege ndiyo iliyomfanya asitishe zoezi la kutaka kusimama,
Moyo wake bado ulimwenda mbio na kutulia kwenye kiti, fikra zake zilimtuma kuwa hakukua na usalama ndani ya ndege hiyo,alijaribu kuvuta kumbu kumbu ni wapi mwanaume huyo alipomuona na kushindwa kupata jibu la haraka haraka.
“Allah Akbar!, Allah Akbar!”
Ni sauti nzito ndani ya ndege ndiyo iliyowashtua abiria wote baada ya ndege kuwa hewani tayari. Kati kati alisimama mwarabu mwenye ndevu nyingi huku mkononi mwake akiwa na bastola.hiyo ilimaanisha kuwa ndege tayari imetekwa nyara.
Catherine aliyekua amekaa kwenye kiti chake hata yeye alishtuka na kupata jibu la swali lake.
Alishindwa kuelewa ni kivipi mwarabu huyo kaingia na silaha ndani ya ndege jibu lilikuja hakua peke yake alishirikiana na muhudumu wa ndege sababu hata alivyomuangalia nayeye alitoa bastola huku wakiongea lugha ya kiarabu.
“silence (kimnya)”
Aliamuru mwanamke huyo muhudumu huku akiwa na bastola mkononi mwake, yaliyokua yanaendelea hakuna hata rubani mmoja aliyejua, ndege ilizidi kusonga mbele.
Hakuna hata abiria mmoja aliyejua ni kitu gani wanachotaka mpaka wakaamua kuiteka ndege hiyo, kila mtu alimkombatia ampendae. Kway alimkombatia Mke wake Julia na kuwa tayari kwa lolote litakalo tokea huku baadhi ya abiria wengine wakianza kusali sala zao za mwisho.
“Captain Karunji Johnson,tuna mateka, ndege yako ipo chini ya ulinzi, unachotakiwa kufanya ni kupeleka ndege uwanja wa ndege wa Entebbe mara moja una sekunde tano,”
Alisema mwanamke gaidi aliyevalia nguo kama za wahudumu wa ndege akiwa na kipaza sauti mkononi mwake na kufanya sauti hiyo kupenya mpaka ndani ya chumba cha marubani.
“moja, mbili, tatu.. paa paaaa”
Tayari abiria mmoja alipoteza maisha yake hapo hapo baada ya kupigwa risasi ya kichwa, hiyo ilimaanisha kuwa watu hao hawana masihala hata kidogo, na ndo ivyo walivyofanya kwa abiria mwingine!.
“Captain Abeid, sasa tunafanyaje hapa?”
Ndani ya chumba kidogo cha marubani kelele za bastola zilisikika hata wao walitandwa na hofu, hawakuelewa ni kitu gani wakifanye.
“we unahisi tutafanya nini zaidi ya kutii wanachotaka”
“unadhani hilo ni wazo zuri?”
“sasa tukiendelea kusonga mbele abiria wote watauwawa alafu hawana hatia”
Hawakua na chaguo lingine zaidi ya kugusa gusa mitambo yao kisha kugeuza ndege, na hayo ndiyo maamuzi waliyoamua kuyafanya kuliko kuzidi kufanya abiria wasiokua na hatia wauwawe.
“tuna muhitaji Catherine Ramsey Kidhirwa hapa mbele”
Aliongea Mwarabu huyo huku akimuwekea mmoja wa abiria bastola. Catherine Alishaelewa tayari nia ya kutekwa ndege hiyo walikua wakimuhitaji yeye, japo hakujua kwanini, akiwa ana tetemeka alisimama huku mikono yake ikiwa juu akisalimu amri, mpaka kuwasogelea walipo.
“piga magoti”
Alitii amri huku akiwa chini ya ulinzi baadaye kidogo yaliletwa mabegi matatu moja alivaa mwarabu kisha jingine kuvalishwa Catherine na lingine kupewa Mwanamke aliyevalia sare za waudumu.
Mwarabu mwenye ndevu nyingi alitembea mpaka chooni kisha kutoa bomu kubwa na kuliseti dakika thelathini, baada ya hapo aliliachia na dakika zake kuanza kujihesabu zikirudi nyuma. Mlango ulifunguliwa na kufanya upepo mkali sana kuingia ndani ya ndege, kilichofuata hapo ni catherine kusukumizwa nje kisha Mwanamke muhudumu na Mwarabu kufuata wakiruka nje huku nyuma wakiacha dakika kumi tu bomu lilipuke.
Catherine akiwa anaelea hewani alishuhudia mlipuko mkubwa wa Ndege na kufanya vipande vipande viruke dalili zilionesha kuwa hakuna hata mmoja aliyepona ndani ya ndege hiyo.
“Noo!”
Catherine alishtuka kutoka usingizini akiwa ndani ya ndege hakuelewa ni wakati gani usingizi ulimpitia na kulala fofofo! ndoto aliyokua akiota ilimshtua sana ni kweli alivyogeuka kuangalia siti za nyuma Mwarabu hakuwa bado amerudi kwenye siti yake.
Alifungua mkanda wake wa kiti na kuanza kutembea taratibu mpaka chooni!…
“Noo!”
Catherine alishtuka kutoka usingizini akiwa ndani ya ndege hakuelewa ni wakati gani usingizi ulimpitia na kulala fofofo! ndoto aliyokua akiota ilimshtua sana ni kweli alivyogeuka kuangalia siti za nyuma Mwarabu hakuwa bado amerudi kwenye siti yake. Alifungua mkanda wake wa kiti na kuanza kutembea taratibu
mpaka chooni!…
Ndani ya moyo wake bado alimuwekea mashaka mwarabu aliyeingia ndani ya ndege ni kweli alimuona mahali, lakini hakuweza kukumbuka ni wapi na ni lini,alichotakiwa kufanya ni kumuangalia kila hatua anayopiga.
Ndoto aliyotoka kuiota kuwa ndege imelipuka baada ya kutekwa nyara kisha bomu kutegwa, ndiyo iliyomfaya azidi kuingiwa na hofu sana dhidi ya mtu
huyo,hapo ndipo alipoamua kusimama na kutembea mpaka msalani kumfuatilia, macho yao yaligongana!.
“Asalam aelekuy”
Alisalimia Mwarabu huyo alivyoonana na Catherine baada ya kutoka msalani.
“samahani sijui tunafahamiana?”
“Hapana wenda umenifananisha”
“okay”
Bado Catherine alizidi kumuwekea mashaka mwanaume huyo mpaka ndege inakanyaga Ardhi ya Kigali nchini Rwanda na kubadilishiwa ndege nyingine.
Walivyopanda ndege nyingine hakumuona tena na kushusha pumzi ndefu. Baada ya masaa matatu kipaza sauti kilisikika sauti ikitokea pembeni mwa spika ndogo
kutoka kwa msichana mrembo kikiwataka abiria wote wafunge mikanda yao kwani ndege inaenda kutua Tanzania Dar es salaam, uwanja wa Mwalimu Nyerere,
Catherine alitabasamu sana kusikia habari izo, abiria wote walifunga mikanda kisha kichwa cha ndege kwa mbele kuinama kidogo baada ya kutoa matairi yake,
ilivyotua ilitingishika kidogo kisha kukaa sawa ikiwa katika mwendo wa kasi sana kisha baadaye taratibu ikipunguza mwendo kasi na kusimama na ndo hapo
baadhi ya abiria waliofika kuanza kutoa mizigo yao sehemu ya juu maalumu.
Catherine ndiye aliyekua wa kwanza kutoka mlangoni akifuatiwa na Kway pamoja na mke wake Julia kushoto kwake, wote walikua wenye nyuso zenye furaha
sana. Walitembea mpaka kwenye vidirisha maalumu na kugonga passpot zao mihuri immigration kisha kupita mpaka sehemu ya mizigo, Kway alitembea mpaka
ndani ya chumba maalumu alipoacha bastola yake kipindi anaondoka kisha baada ya kukagua kama kila kitu kipo sawa aliiweka kiunoni na kuifunika na shati iliisionekane. Yalivyokamilika hayo yote walianza kutoka nje wakiwa na abiria wenzao!.
“Daaaaa…diiiiii!”
Kelele zilisikika kutoka kwa Natu akitoka mikononi mwa Hussein Molito kisha kumkimbilia Baba yake na kumrukia kwa nguvu, furaha ilirudi tena katika
familia hiyo iliyokua imetengana kwa kipindi kirefu sana, Catherine alivyopiga jicho pembeni alimuona Enock akiwa na MAMA yake mzazi wakiwa wenye
nyuso zenye furaha wote walirukiana na kukombatiana. Kila mtu alikua na furaha sana ndani ya moyo wake baada ya kukutana tena.
“Catherine mpenzi wangu pole na matatizo”
“Ahsante mpenzi”
Baada ya kuachiana na Catherine alimsogelea Kway kisha kukombatiana, huku wakipigana pigana migongoni, ni muda mchache tu walifahamiana lakini kwa
matatizo waliyopitia wakiwa nchini Uganda ilibidi wajipongeze sababu waliyashinda.
“sasa sijui nikuiteje, Mkwe au?”
Aliuliza Enock huku akicheka.
“vyovyote vile sawa Enock”
Jicho la kway lilitua kwa mtoto aliyekua ame mbeba Sabrina ambaye bila kuuliza mtu yoyote Yule usingebisha ukiambiwa kuwa ni mtoto wa Kway sababu
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA