SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Jicho la kway lilitua kwa mtoto aliyekua ame mbeba Sabrina ambaye bila kuuliza mtu yoyote Yule usingebisha ukiambiwa kuwa ni mtoto wa Kway sababuSASA ENDELEA...
walifanana kwa kila kitu, aligeuza shingo yake na kumtizama Mke wake Julia aliyekua amembeba Natu wakiwa wenye furaha kisha kushusha pumzi!.
“Sabrina”
Aliita Kway kwa ujasiri ilikua ni lazima waweke mambo sawa siku hiyo hiyo kabla haijapita.
“Abee”
“naomba nimuone Mtoto”
Hakukua na mtu yoyote mwenye kipingamizi cha aina yoyote ile kila mtu alikua kimnya, hata kwa Julia pia, alionyesha furaha pia na kumchukua Mtoto huyo
Christopher aliyekua teyari keshaanza kuota Meno alikua mweupe Mzuri na mwenye afya.Kwa pamoja walikombatiana wakiwa wenye furaha sana.
“Sasa Baba Mkwe, kabla ya kufika kwako,najua umechoka naomba tutafute sehemu nzuri tufurahi sote kwa pamoja”
Alishauri Enock na wote kumuunga Mkono. Kway na familia yake waliingia kwenye gari ya Hussein Molito huku Catherine pamoja na Mama yake kuingia
Kwenye gari ya Enock na wote kuanza kuongozana Marcedez Benz mbele nyuma Landcruiser vx.
Safari yao ilikomea Kwenye Bar ya Mtoto wa BECKER iliyokua Kimara Suka.
Tajiri aliyesifika kwa kumiliki vituo mbali mbali vya redio na t,v ndani na nje ya nchi, japo alikua kijana mdogo lakini alikuwa mwenye mafanikio kutokana na juhudi zake za kazi, hapo ndipo walipojenga urafiki na Enock Mwasha siku chache wakipeana ushauri kuhusiana na Maisha, habari zilizo mchanganya Mtoto wa
BECKER ni kitendo cha Enock kuunguliwa kwa nyumba yake kubwa, aliguswa sana na kumuhaidi kuwa atakuwa naye bega kwa bega mpaka mambo yatakapo kuwa sawa!.
Siku hiyo ilikuwa ni furaha sana kwao walikunywa na kula walivyoridhika kila mtu aliwasha gari na kuondoka sababu usiku ulikua tayari umeingia.
“Enock mpenzi pole na matatizo uliyopata”
Alisema Naomi siku hiyo akiwa ofisini kwa Enock baada ya kuzuga kuwa amefika kutokea mkoani Mwanza, ukweli ni kwamba hakua safarini,ndani ya moyo wake alikua na visasi vikichanganyika na hasira.
“nilisikia bado Baba yako anakuwinda?”
“ndio Naomi, hapa nashindwa cha kufanya sijui nifanye nini?”
“kwani yuko wapi?”
“yupo kisiwani unguja navyosikia”
“ulishaenda polisi kutoa mashtaka?”
“hapa navyokwambia ndiyo nimetoka kituoni”
“wamesemaje?”
“ndio wameenda huko wiki iliyopita kumkamata”
“sawa..!sasa akishakamatwa itakuaje?”
“Nitaacha sheria ifate mkondo wake”
“vipi kuhusu swala la ndoa yetu?”
Hilo ndilo swali lililomfanya Enock asitishe kubonyeza bonyeza kompyuta iliyokuwa mbele mezani kwake na kumkazia Macho Naomi.
“Lakini Naomi, huoni bado nina matatizo,wacha tulimalize hili la kwanza mambo ya ndoa yatafuata”
“usijifanye mjanja sawa, usiniletee longolongo na usanii, na uache uwongo najua kila kitu kinachoendelea kuhusu wewe na kahaba wako Catherine,sasa basi utaozea jela hapa napokwambia namimi pia nimetoka polisi kutoa maelezo ya kifo cha Heather”
“Unasema?”
“Ndo ivyo, unatafutwa na polisi, wewe si ulimwaga ugali mimi namwaga mboga hapaliki”
Aliongea Naomi akipayuka akimaanisha kwa aliyokuwa anaongea tena akiwa mwenye hasira huku akiwa amesimama ameukunja uso wake.
Na ni kweli haikuchukua hata dakika thelathini Askari walifika ofisi za Nissan wakimuhitaji Enock, hawakumpa hata nafasi ya kuongea na kujitetea, hapo hapo walimpiga pingu kwa nyuma baada ya kauli iliyotoka kwa Kamanda Amata mkuu wa kituo kikubwa cha Oysterbay.
Kila mtu alishindwa kuelewa ni nini kimetokea, wafanya kazi wake walizidi kunong’ona wasielewe ni kitu gani kilifanya mpaka bosi wao afungwe pingu kwa nyuma kama muhalifu au jambazi sugu.
Hakukua na masihala hata kidogo dhidi ya polisi hawa, walimsukuma mpaka nyuma ya difenda kisha kuondoka naye mpaka kituo cha polisi Oysterbay, maelezo aliyotoa Naomi pamoja na ushahidi wote ulitosha kabisa kufanya kesi ya Enock izidi kupamba moto na kupandishwa ngazi za juu na kisha kufunguliwa kesi ya mauaji kumaanisha kuwa anaenda kufungwa kifungo cha Maisha gerezani.
Ndugu wa Heather tayari walipata taarifa hizo na kuzidi kumlaani Enock kwa kitendo cha kumuwekea ndugu yao Heather sumu kali ya panya akiwa wodi ya vichaa na kufa, na ndiyo ivyo Naomi alivyowaambia ndugu hao waliofunga safari kutoka Morogoro Matombo, mpaka Dar es salaam ili kusikiliza kesi hiyo itakayo anza baada ya wiki tatu.
Jiji la Dar es salaam lilikua katika hali ya utulivu na ukimnya wa hali ya juu kila mtu alitega sikio lake,kesi ya Enock David Mwasha iliunguruma sana, historia yake fupi iliyosimuliwa na kila mtu ilifanya ijaze mamia ya watu ndani ya mahakama ya kisutu, kila mtu alitega sikio ili kusikia kitakacho zungumzwa na mwanaume huyu aliyekua mtoto wa tajiri mkubwa jijini Dar es salaam aliyefahamika kisha kupata kashfa ya ujambazi na uharamia vile vile.
Wengine walichukizwa sana kwa kitendo chake cha kumuuwa mke wake Heather aliyekuwa mwenda wazimu katika wodi ya vichaa Muhimbili ili awe na mwanamke mwingine na ndiyo ivyo alivyotangaza Naomi kwa kila mtu hata katika vyombo vya habari mbali mbali vya redio, magazeti mpaka t,v.
Wanawake wengi walimchukia na kutamani hata anyongwe, walimuona Enock ni mnyama sana hana roho ya kibinadamu na hastaili kuishi Duniani.
Mnamo tarehe nane mwezi wa tisa ndiyo siku ya kesi yake kusomwa kwa mara ya kwanza hapo kisutu akisomewa mashtaka ya mauaji, Umati wa watu ulizidi kufurika ili kusikia hukumu ya Enock Mwasha, wengi walitaka ahukumiwe kifungo cha maisha, ila wachache ndiyo walioamini kuwa kijana huyu Mdogo hana hatia, licha ya hayo walisubiri sheria ifate mkondo wake sababu siku zote ukweli hujitenga na uwongo.
Catherine muda wote alikua akilia machozi haamini kile anachokiona na kukisikia hata yeye alishajua kuwa Enock mchumba wake hawezi kuwa huru tena ni kifungo cha maisha ndiko anachostaili!.
Kway na Mtoto wa Becker walifika mapema siku hiyo asubuhi ya saa mbili wakiwa viti vya mbele upande wa watu wachache ambao waliamini kuwa Enock hakuwa na hatia ya aina yoyote ile.
Ukimya ulitawala baada ya majaji kuingia, kesi hiyo iliongozwa na jaji Patrick NDILITO aliyesifika kwa roho mbaya, kila aliyemuona alishtuka hakuonesha hali yoyote ya kucheka, nyuma yake walifuata mawakili wake waliovalia majoho meusi wakiwa na vitabu mikononi mwao tayari kwa kusikiliza kesi hiyo iliyokua
Ngumu, hasa walipomuona wakili Nolan Mkwiche aliyekuwa upande wa Enock amevalia suti nyeusi,
walimfahamu sana wakili huyo aliyesomea kazi yake ya sheria nje ya nchi, alipata umaarufu sana kutokana na kufanya kazi yake vizuri, hakuwahi kushindwa kesi hata siku moja na ndo hapo Anderson Peter alipomshauri Enock wamtafute kwa gharama yoyote ile na kufanikiwa kumpata.
Upande wa mashtaka waliruhusiwa kupanda, Naomi ndiye wa kwanza kupanda kizimbani na kuweka mkono wake juu ya Biblia kama kiapo asiongee uwongo.
“Kwa majina naitwa Naomi Cosmas Masunga, mnamo tarehe tatu mwezi wa pili mwaka huu ndipo nilianza kujuana na Enock,tukawa wapenzi lakini hakuwahi kuniambia kuwa ana mke ili mradi anipate, ni kweli nilimpenda na alitaka kunioa, nilivyofanya uchunguzi nikagundua kuwa ana mke nilivyo muuliza akadai kuwa nimuachie yeye kwa kuwa ananipenda sana na hayupo tayari kuniacha,ni kweli sikua na roho mbaya yoyote nikawa naenda hospitali kumuona marehemu
Heather na ndiye yeye aliniambia niwe nafanya ivyo ili nizoeleke, hapo mwanzo sikujua ana maana gani mpaka siku aliponipa chupa ya maji na kuniambia kuwa nikampe Heather wodi ya vichaa,nilivyompa tu nikaona Heather anatoa mapovu na umauti kumkuta hapo hapo nikagundua yale maji yana sumu ya panya,nilipomuuliza akasema ni kweli nimfichie hiyo siri nikafanya ivyo, ila baadaye nikaona siwezi kukaa na kitu hiko moyoni!”
Kila aliloongea Naomi kizimbani kiliandikwa vizuri, wakili Nolan Mkwiche alimsikiliza kwa umakini sana na kukariri yote anayosema.
Baadaye alisimamishwa Enock akiwa na pingu mpaka kizimabani, alikuwa amekonda sana ana vipelevipele usoni alitia huruma, Catherine alilia tena macho yao yalivyogongana,hata yeye alionekana kushangazwa na umati wa watu.
Alipewa Biblia na yeye kuweka mkono wake kama alivyofanya Naomi kisha kufuatisha maneno aliyoambiwa aseme!.
“Kwa majina naitwa Enock David Mwasha mbele ya mahakama tukufu napenda kukanusha haya yote aliyoongea Naomi”
Hapo ndipo Enock alipoanza kuongea ukweli jinsi alivyompata Naomi na kudhani kuwa Catherine amefariki kwenye vita vya kongo!.
“Nilimpenda sana Naomi,kwa kujua kuwa Mpenzi wangu Catherine alifariki dunia,yeye ndiye aliyekua akinisisitiza kuhusu ndoa tutafunga lini,kabla ya hapo nilimwambia nina Mke ila yupo wodi ya vichaa na nina mpenda, sikuwahi kumwambia aweke sumu kwenye maji kama anavyodai,kifo cha Marehemu mke wangu kilinishtua baada ya kuambiwa kuwa amekufa kwa sumu ya panya iliyokuwa kwenye chupa ya maji nilivyomuuliza aliniambia kuwa alinunua sumu ya
panya kwa ajili ya kuwatega panya na ndo ivyo alivyowaambia polisi pindi walivyomuhoji”
Maneno aliyopewa na Wakili Nolan Mkwiche kuwa akatae na kukanusha kuhusu sumu ya panya ili kesi isiwe ngumu na ndivyo alivyofanya,ilibidi akatae kata kata kuwa hakuwa anaelewa mipango yoyote ile juu ya sumu hiyo iliyomuuwa Marehemu Heather, baada ya kuongea hayo alipanda wakili wa upande wa kumtetea Naomi na ndugu zake Heather ambao walionyesha kumkandamiza Enock!.
“Bwana Enock,ulisema kuwa ulimpenda sana Marehemu mke wako,katika historia ya hapo nyuma inaonesha kuwa mlishawahi kuwa na ugomvi mkubwa
ukimsingizia kuwa alienda kwa waganga kukuwekea dawa, ukampiga wakati alikua na mimba, huoni hiyo inatufaya tuzidi kukuwekea mashaka kuwa wewe ndiye ulifanya hayo mauaji?”
Wakili Faaris aliuliza kwa kujiamini sana huku akishika shika tai yake iliyokua kooni akitembea tembea.
“Ndio sikatai tulikuwa na ugomvi wa kifamilia,lakini baada ya hapo tulielewana vizuri baada ya kurudi kutoka nchini Brazil nikakuta yupo wodi ya vichaa,sikuelewa ni kitu gani kilimpata”
“Najua kuwa unajitetea ili umkandamize mteja wangu ambaye hana hatia yoyote ile,swali lingine ulitambua kabisa kuwa una mke, kama ulivyosema mwenyewe katika maelezo yako, ni kipi kilikufanya uwende kwa Naomi, kama mkristo navyojua mimi ni kuwa kitakacho watenganisha wanandoa ni kifo peke yake,unaiambia nini mahakama tukufu juu ya hilo?”
Ni kweli swali hilo lilionekana kuichanganya akili ya Enock na kushindwa ni kitu gani akijibu, alivyomuangalia wakili wake alimtingishia kichwa kuwa asijibu kitu chochote kile!.
“Ni hayo tu muheshimiwa hakimu”
Wakili Faaris alikaa kwenye kiti kisha upande wa utetezi alisimama Wakili Nolan Mkwiche akitabasamu na kumuendea Naomi.
“Naomi,nina maswali machache tu wala sio mengi, ulisema kuwa ulipewa chupa yenye maji ukaambiwa kuwa ukampe Marehemu Heather wodi ya
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA