BIKRA YANGU (60)

0
Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA SITINI
ILIPOISHIA...
“Naomi,nina maswali machache tu wala sio mengi, ulisema kuwa ulipewa chupa yenye maji ukaambiwa kuwa ukampe Marehemu Heather wodi ya

SASA ENDELEA...
vichaa,kwanini haukuhoji kuwa chupa ina nini?”

“kwa sababu Enock ni mwanaume ambaye hapendi kuulizwa maswali, pia nilivyomuhoji aliniambia kuwa ataniambia baadaye nikishampa”

“Well…una habari kuwa nawewe unakesi ya mauaji,alivyokwambia kuwa umfichie siri yake nawewe ukafanya ivyo hilo ni kosa kifungu namba tatu,umemficha muhalifu,nina uwezo pia wa kukufungulia kesi, una kataa unakubali?”

“Muheshimiwa Nolan hapo unakuwa kama unamfosi mteja wangu kukubali kosa na unakuwa kama unamtisha”

Alikatisha maongezi wakili Faaris alivyoona swali hilo litakua na utata sana.

“naomba aendelee kunijibu maswali yangu,ni kosa la mauaji vile vile kumficha muhalifu kifungu kitam-bana”

Waliendelea kulumbana mpaka Wakili Faaris alipotulizwa ili amuachie uwanja Nolan Mkwiche aulize maswali.

“kwanini polisi walivyokuhoji kuhusu hayo maji yenye sumu ukawajibu kuwa ni kwa ajili ya panya na marehemu Heather alikunywa kwa bahati mbaya ulivyotoka,nani aliyenunua hiyo sumu wewe au Enock?”

“Ni Enock ndiye aliyenunua na kuiweka ndani ya maji kisha kunipa”

“Huoni kuwa unasema uwongo,asubuhi ya siku hiyo hiyo uliamka na kwenda dukani kwa kimario pale jirani na kununua sumu hiyo ya panya na siku hiyo hiyo habari za msiba zika letwa,unaweza ukalizungumzia hilo,?”

Wakili Nolan Mkwiche kila alilosema alikua na uhakika nalo, ni kweli alikua na ushahidi wa kila kitu kuhusiana na kifo cha Heather, aliamini kesi hiyo ataenda kushinda alijiamini sana.

Jaji Patrick Ndilito aligonga nyundo mezani na kesi kuhairishwa mpaka mwezi ujao tarehe kumi na saba mwezi wa kumi!.

Watu wote walitawanyika na Enock kurudishwa maabusu ili kusubiri siku nyingine ya kesi yake.
Wakili Nolan Mkwiche alimuhakikishia kuwa ataenda kushinda na kuwa huru, maana kila vithibitisho anavyo lakini alichomsistizia ni kuwa azidi kukanusha juu ya sumu iliyokua imewekwa ndani ya maji.

“Nakuhakikishia utashinda utakuwa huru,Naomi hawezi kutoka hata kidogo Yule wakili anayemtetea hawezi kitu,cha kufanya endelea kukataa kata kata, kama nilivyokwambia kama ukiulizwa swali liki kuchanganya usitoe jibu lolote!”

Ivyo ndivyo alivyoambiwa na wakili wake ambaye alimtafuta kwa pesa nyingi sana.Kway,Mtoto wa Becker pamoja na Anderson Peter, nao walimfata na kumpa pole , wote walimtia moyo kuwa atashinda kesi hiyo, kwani waliamini kuwa Enock hana hatia hata kidogo.

Ndugu wa Marehemu Heather waliungana na Naomi na kuzidi kumkandamiza sana wakimtuhumu kuwa ndiye yeye aliyefanya mauaji hayo.

“Mambo Naomi”

“safi tu”

“Naona umeamua kumshtaki mpenzi wako lakini ni safi sana”

“ndiyo alivyokutuma Enock uje kunilaghai?”

“Hana jeuri hiyo hata kidogo,tuachane na mambo ya kesi, mimi nimekuja na mambo yangu binafsi”
“nakusikiliza”

“hapa sio pa kuyaongelea,mimi nataka nikusaidie”

Nolan Mkwiche wakili wa Enock alimtafuta Naomi na kuanza kujenga naye mazoea ya karibu sana,ndani ya siku tatu tu walikua ni marafiki wa karibu sana.

wakiwa wanaenda wote sehemu mbali mbali pamoja tena wakiongozana, jambo hilo walifanya siri sana bila ya Enock kujua lolote lile,

Ni kweli Nolan aliamua kuwa upande wa Naomi na kuwa naye bega kwa bega na ndiyo ivyo alivyomwambia na wote walikubaliana kumkandamiza Enock, kwa mara ya kwanza Naomi aliona ni njama tu ila baadaye alikubali sana na kufurahi.

“nataka nikufanye hii kesi ushinde,kama ukinilipa pesa nazotaka mimi naona Enock ni m-babaishaji tu ananiletea longolongo”

Alisema Wakili Nolan Mkwiche siku hiyo wakiwa ndani ya mgahawa wa samaki samaki.

“unataka bei gani kwani?”

“Laki tisa tu,Enock atanyea debe segerea”

“ina maana Enock kashindwa kukulipa izo pesa?”

“anadai haniamini hata ivyo siku izi kafulia hana pesa kachoka sana,ukinipa hiyo pesa mimi naondoka zangu namuachia hiyo kesi najua ni lazima atawekwa ndani kifungo cha maisha,”

“umenifurahisha sana Nolan,sawa nitafanya ivyo kesho jioni nitakupa hiyo pesa,naomba usinilitee za kuleta”

“niamini nayokwambia, hii kazi sijaanza leo unajua”

Habari izo zilimfanya Naomi afurahi kupita kiasi, hakutaka kumwambia mtu wa aina yoyote ile, siri hiyo walibaki nayo yeye pamoja na Nolan wakili wa Enock, hakutegemea kama mambo yangemnyookea kiasi hiko laki tisa haikuwa pesa kubwa kwake.

Hata ivyo kwa gharama yoyotebile ilikua ni lazima amuweke Enock ndani au waende wote Gerezani, lakini dalili zilionesha kuwa yeye atakua huru na Enock kufungwa kifungo cha Maisha na ndiyo ivyo alivyohaidiwa na wakili Nolan Mkwiche.

Bila kujifikiria alichukua kiasi cha laki tisa kisha kumtafuta Nolan hewani, kesho yake aliwasha gari mpaka Salasala nyumbani kwa Nolan mkononi akiwa na bahasha ya kaki iliyojaa Noti nyekundu.

Alivyofika tu alimkabidhi pesa izo.

“kwaiyo niambie cha kufanya,kabla ya kuondoka au ikitokea nimepanda kukuhoji nataka nijue ni kweli uliweka sumu ya panya na Heather kufariki?”

“Ndio mimi ndiye niliyeweka sumu ile kwenye maji,nilitaka anioe mimi Naomi”

“Ha!Ha!Ha!, sasa ilikuwaje akaghairi?”

“Alikuja sijui Demu gani sijui from no where akadai sijui alidhani amekufa,nilikasirika sana nikaamuua kufanya ivyo ana bahati sana nayeye ningemuuwa shenzi zake”

“Duu pole sana, sasa mimi ndio naondoka ivyo sasa hivi, nakutakia kila la kheri, usimwambie mtu yoyote kuwa tulionana, sawa?”

“sawa,mimi naenda”

Naomi aliondoka akiwa mwenye furaha ndani ya moyo wake,

shukrani aliyompa Nolan haikuelezeka hata kidogo, aliwasha gari mpaka kwake na kujitupa kitandani akiwa mwenye furaha alijiona mshindi sana.

“lazima afie jela, shenzi zake”

Aliwaza Naomi.

Siku zilikatika na majuma kusonga hatimaye mwezi kuisha na tarehe ya kesi ya Enock kufika.
Watu walikusanyika mahakamani umati wa watu ulifurika kila mtu alitega sikio, Bado Enock aliendelea kukanusha kuhusu mauaji ya marehemu Heather aliyoshutumiwa kuwa yeye ndiye aliweka sumu hiyo kali ndani ya chupa ya maji na kumtuma Naomi, alikataa kata kata.

Alivyopanda Naomi alizidi kumkandia akiongeza chumvi dalili zilionesha kuwa anaenda kushinda kesi hiyo.

Kilichomchanganya Enock na kila mtu ni baada ya kutokumuoana wakili Nolan,
hawakuelewa nini kimetokea isipokua kwa Naomi yeye alijua kila kilichotokea,alitabasamu na kuona mambo yanaenda kama yalivyopangwa.

Picha ilionesha kuwa anaenda gerezani

kilimchomjia kichwani ni milango ya gereza inafunguka nayeye kutupwa ndani gerezani akihukumiwa kifungo cha Maisha, machozi yalianza kumlenga, Dunia aliona ipo chini juu,juu chini alimtizama Naomi kwa macho ya huruma, alishaelewa kuwa yeye ndiye mkandarasi wa matatizo yake yote yanayomtokea mpaka yeye kufungwa, alitamani muda urudi nyuma ili aweke mambo sawa lakini ilishindikana!.

Ghafla kila mtu aligeuza shingo yake nyuma na kushangazwa baada ya kumuona Mwanaume mnene kiasi aliyekua amevalia suti nyeusi kutokeza,

Enock alitabasamu na kujipa tena moyo baada ya kumuona Mkombozi wake amefika Wakili Nolan Mkwiche.

Naomi alishindwa kuelewa ni kitu gani kimetokea moyo ulimwenda kasi.

Nolan Mkwiche aliweka begi lake dogo mezani kisha kupita mbele na kumkazia macho Naomi aliyekua akitokwa na jasho mwilini mwake anatetemeka.

Bila kuongea chochote alitoa kamera na kinasa sauti kisha kukiweka mezani,kila mtu alitega sikio lake kusikiliza.

“NDIO MIMI NDIYE NILIYEWEKA SUMU KWENYE MAJI,NILITAKA ANIOE MIMI NAOMI,…”

Sauti ya Naomi ndiyo iliyosikika kutoka kwenye kinasa sauti.

Watu wote walikuwa katika hali ya utulivu wa hali ya juu,wakitaka kujua hukumu ya Enock ambaye leo hii ana shtakiwa kwa kosa la mauaji ya kumuwekea sumu ya panya Mke Wake Heather akiwa wodi ya vichaa Muhimbili,

Mchumba wake Naomi ndiye aliyefungua kesi hiyo akishirikiana na Ndugu wa marehemu Heather, kila mtu alimchukia Enock wanawake walimuwekea vigenge na kumteta wakitaka afungwe kifungo cha maisha au anyongwe kabisa,kilichowauma zaidi ni kitendo cha kusikia alimpiga mke wake enzi za uhai wake alivyokuwa mjamzito akidai kuwa alimuendea kwa waganga.

“Huyu kaka afungwe ningekuwa mimi ni jaji nisingesikiliza hiyo kesi,ni kufungwa tu”

“wamlete hapa tumpige ata viboko,huyu angekuwa kule Mexico angenyongwa yaani nashaangaa hii nchi yetu ya Tanzania mtu kama huyu anapumua bado”

“Mimi kaniudhi kwa kweli”

Hayo ndiyo maneno yaliyosikika mitaani kutoka kwa baadhi ya watu waliosikia habari izo.

Kila mtu alitega sikio lake kusubiri hukumu ya Enock, wengi waliomba afungwe kifungo cha maisha.
Wakili Nolan Mkwiche ndiye alikuwa akisubiriwa kama mtetezi wa Enock dakika kumi sasa zilipita bila kutokeza mahakamani, hawakuelewa nini kimempata,ndugu wa upande wa Enock walizidi kuingiwa na Mashaka walishajua maana yake kuwa ni lazima Enock afungwe kifungo cha maisha kutokana na kukosa kithibitisho na utetezi wa aina yoyote ile.

Ghafla Wakili Mkwiche aliingia akiwa ana tabasamu sana kisha kuweka kinasa sauti pamoja na mkanda wa video uliowachukua yeye na Naomi wakiwa katika maongezi. Alitumia njama hiyo ili kumkamata Naomi kirahisi na kweli alifanikiwa kabisa, hakukuwa na haja yoyote ile ya kuzidi kumuweka Enock kizuizini.

Jaji aligonga Nyundo mezani na Naomi kuhukumiwa kifungo cha Maisha jela kwa kosa la kuuwa kwa kukusudia huku Enock akiachiwa huru aende, machozi ya furaha yalimtoka Enock hakuamini hata yeye kile anachosikia kutoka kwa JAJI aliyekuwa kushoto kwake kwa juu, alishaamini kuwa anaenda kutumikia maisha yake yote Gerezani,hapo ndipo Askari magereza walimuendea NAOMI na kumfunga pingu kisha kuondoka nae huku akiwa analia machozi mengi mfululizo.

Tayari waandishi wa habari walikuwa nje na kamera zao walitaka kujua ni kitu gani kimetokea, Catherine muda wote alikua ni mwenye furaha kupita maelezo yaliyojitosheleza.

“Enock Mpenzi”

“Naaam Catherine”

“nakupenda sana”

“Hata Mimi”

Muda wote walikumbatiana kwa furaha wakiwa na amani ndani ya mioyo yao. Mtoto wa Becker, Kway, Mama Catherine pamoja na Anderson Peter muda wote walikuwa wenye furaha wamemzunguka wanampongeza sana, hata wao aliwashukuru kwakuwa naye bega kwa bega.

“Namshukuru Mungu sana kwa kuuonyesha ukweli, Nolan nashukuru sana kaka najua umefanya kazi kubwa sana,jioni la leo naomba uungane kwenye sherehe nitakayo fanya kwenye ukumbi wa Meeda pale sinza, tafadhali usikose”

Enock aliongea akiwa mwenye furaha muda wote anatabasamu alijiona ni Mshindi sana, ndani ya akili yake aliwaza ndoa atakayo funga na Catherine na ndiko hiko kitu kilichobaki na wala sio kitu kingine,

Karandinga la magereza lilifika mahakama ya kisutu kisha Naomi kutupwa akiwa na wafungwa wengine,walitizamana na Enock na kuingizwa ndani ya gari hilo maalumu linalobeba watu waliohukumiwa vifungo kisha kuwapeleka magerezani.

Enock na ndugu zake huku Catherine akiwa pembeni Waliingia ndani ya magari yao kisha kuondoka,moja kwa moja walifika nyumbani kwa Anderson Peter ili abadili nguo, Siku hiyo ilikuwa ni siku ya furaha sana ndani ya moyo wake,hakuweza kufurahi mwenyewe siku hiyo, aliwapigia simu wafanya kazi wake wote pamoja na ndugu jamaa na marafiki zake ili waweze kuungana katika ukumbi wa Meeda uliopo sinza.

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)