BIKRA YANGU (62)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Walizidi kusonga mbele wakipita ndani ya miti hiyo ya mikoko.Ilikua ni lazima wamkamate Mzee Huyu Hatari sana, kabla hawajafika mbali walisikia milio yaSASA ENDELEA...
risasi inarindima upande wa magharibi, hofu ilizidi kuwatanda.
“Afande afande unanisoma kiiisshhh,Afande ova Afande Ngussa Kishhhhh Afande Mbaruku ovaa”
Hofu ilizidi kuwatanda baada ya kukosa jibu upande mwingine wa redio upepo,
Ghafla lilitokea kundi la watu wengi wakiwa wenye silaha za moto na kuwazunguka, polisi wote waliwekwa chini ya ulinzi.
“Pigeni magoti”
“yakhee tafadhali usitutoe uhaiiii, tuoneee hurumaaa hatutorudia tenaaa atiiiiii”
“Kaa kimnya”
“Nani kawatuma?”
“huyuuu hapaaaa ndiyo katoka huko baraaa sisi hatuna shidaa na nyieee hataaa kidogoooo”
“Paaa paaa paaaaa”
Pale pale kamishna Kobello aliuliwa kwa kupigwa risasi za kichwa, ni kweli watu hawa hawakuwa na masihala hata punje, walikua na roho za kinyama, kuuwa mtu kwao ilikua ni kawaida sana na ndiyo hiyo amri waliyopewa kutoka kwa tajiri yao Mzee mwasha,baadhi ya polisi waliinuliwa na kuwekwa mateka mpaka ndani ya nyumba kubwa ya Mwasha kwa ajili ya kuhojiwa kisha baadaye wauwawe.
“nani kawapa hiyo amri huko Dar es salaam?”
Aliuliza Mzee Mwasha.
“Mimi mimi mimi alikuja kijana mmoja kufungua kesi hiyo ni mwanao anadai anaitwa Eno Enock alafu tukapewa Amri na na Mkumbo”
“Ha ha ha ha ha,Mkumbo namfahamu nitajua cha kumfanya”
“okay, huu utakuwa kama ujumbe”
Hapo hapo baada ya kauli iyo alichukua SMG na kuwamininia risasi askari waliokuwa mbele yake, hapo ndipo ukawa mwisho wa maisha yao Na maiti zao kutupwa barabarani,
Askari waliopewa habari izo za wenzao kuuliwa waliogopa sana. Ilibidi wasitishe kwanza zoezi lao na kumsaka Mzee Mwasha.
Kilichobaki ni kitu kimoja tu kumtafuta Enock popote alipo alishaamua kumchukia mtoto wake ki ujumla, alishaelewa kuwa akimfumbia macho atamletea matatizo hapo baadaye,haikupita hata siku mbili alishajua tayari ni wapi Enock anaishi na kujua kuwa alishamvalisha pete ya uchumba Catherine na ndoa ndiyo inasubiriwa,hakutaka hilo litokee hata siku moja, ivyo ilibaki yeye kutuma watu wake wakamuuwe kabisa!.
“Sasa Thomasi,nenda kibaha,huyu ni mtoto wangu mpige risasi muuwe nadhani iyo ni kazi ndogo kwako usifanye makosa hata kidogo”
“sawa nitafanya ivyo”
“Lakini subiri kidogo…”
“Naam bosi”
“nitafutie Sabarina uniletee hapa Zanzibar hii hapa picha yake pia,huyu anaishi Tabata Bima ana duka Kariakoo pale nitakupa maelekezo ukifika Kivukoni nataka
kazi hiyo ifanyike leo hii hii,achana kwanza na Enock najua atajileta mwenyewe”
“sawa Bosi, sitokuangusha niamini, Leo hii hii mzigo wako nitakuletea”
“Nakuaminia Thomasi utaenda na Ngulumbalyo”
“sawa”
Siku hiyo hiyo asubuhi na mapema Thomasi na Ngulumbalyo walitafuta usafiri wa Boti za Azam iliyowavusha bahari ya Hindi na kufika upande wa pili kivukoni Dar es salaam kwa kazi moja tu kumteka nyara Sabrina na kumpeleka huko Zanzibar kama walivyoagizwa na bosi Wao Mzee Mwasha, ilikua ni lazima wafanye ivyo,baada ya kufika walitafuta sehemu nzuri na kupiga simu kwa Bosi wao Mzee Mwasha ili wapewe maelekezo ya ziada.
“Sasa fikeni kariakoo nendeni mtaa wa siku kuu ulizieni duka linaloitwa RASA Classic,hilo duka hamuwezi kupotea hapo hapo mtajua cha kufanya”
“sawa Bosi”
“kuweni makini”
“sawa bosi tuamini uko na majeshi”
“okay”
Baada ya kukata simu zao, walitafuta piki piki zilizowapeleka mpaka Kariakoo mtaa wa siku kuu kisha kuwalipa madereva hao, haikuwa chukua dakika hata mbili walishafika duka la Sabrina na kumkuta ana wateja wengi, pembeni yake kulikuwa kuna mtoto mdogo anatambaa hapo hapo walimtumia ujumbe mfupi
Mzee Mwasha kwa njia ya simu.
“Na mtoto pia mleteni”
“sawa Bosi”
Hayo ndiyo maagizo waliyopewa.
Mpaka usiku unaingia Catherine hakumuona Mama yake, alisubiri na kujua wenda itakuwa foleni za magari,furaha yake taratibu ilianza kuisha baada ya kufika saa nne ya usiku bila kuona dalili ya gari la Mama yake,wala simu yoyote kutoka kwa Mama yake kama afanyavyo endapo ana dharura ya aina yoyote ile,hapo ndipo alipochukua simu na kumtafuta hewani lakini haikupatikana, alizidi kuingiwa na wasi wasi mpaka inafika usiku bado hakumpata hewani, ilibidi ampigie simu Enock amueleze kinachoendelea na kumuulizia kama aliongea na mama yake siku hiyo, Jibu la hapana lilimchanganya akili yake,
Mpaka kunakucha hakuweza kulala alitafuta daladala mpaka kariakoo kwenye duka la Mama yake lakini alishindwa kuelewa alivyokuta limefungwa alijafunguliwa nje kuna makufuli makubwa,alikaa hapo mpaka saa saba mchana ili kumsubiri lakini hakutokea!.
“Samahani,Jana Mama alifunga duka saa ngapi?”
Catherine aliuliza Duka la jirani.
“Mhh Catherine hujambo lakini?”
“samahani shikamoo nimechanganyikiwa hapa,mpaka nimesahau kukusalimia”
“Marahaba, Mama yako alifunga duka hapa mapema sana aliondoka na wakaka wawili alisema anaenda benki kwani vipi?”
“tangu jana hajarudi”
“unasema kweli?”
“kwanini nidanganye Anti”
“ulimtafuta kwenye simu yake?”
“hapatikani”
“Embu tusubiri tuone itakuaje”
Siku hiyo ilipita bila kufanikiwa kumuona Mama yake,kesho yake tena ivyo ivyo, hapo ndipo alipoamua kunyoosha mpaka kituo cha polisi kushtaki.
Wakiwa na Enock wote walisaidiana kumtafuta Mama yake mzazi wakizunguka kila sehemu mpaka hospitali zote,wiki nzima ilikatika bila mafanikio ya aina yoyote yale na kumfanya Catherine azidi kuingiwa na hofu nyingi sababu hakuelewa ni wapi Mama yake alipo….
Sabrina Mama yake na Catherine kapotea haonekani, Enock na Catherine wanamtafuta jiji zima la Dar es salaam,walishazunguka mpaka mahospitalini na vituo mbali mbali vya polisi bila mafanikio ya aina yoyote yale,wasiwasi unazidi kuwaingia, hakuna hata mmoja wao aliyepata hata lepe la usingizi, usiku kucha walikesha wakiwasumbua polisi ni wapi walipofikia.
Taarifa zilizowasikitisha kutoka kwa koplo Jovan ni kuwa kuna ajali mbaya imetokea huko Segera mkoani Tanga, ambapo basi kubwa lililokuwa limetoka Dar es salaam kuelekea Tanga lilipinduka na kuuwa abiria wote usiku huo huo.
“ndiyo habari iliyo tufikia sasa hivi”
Alizungumza Koplo Jovan.
“sasa mnafanyaje?”
“ngoja tusubirri kukuche ili tujue tutaanzia wapi”
“hapana mimi siwezi kusubiri nitaenda hata sasa hivi”
“sasa huo ni uamuzi wako,nimekwambia subiri kukuche tutaenda sote na eskoti ya polisi”
“mimi siwezi”
“kwaiyo?”
“nitaenda”
“utajijua,shauri yako”
Catherine hakukubali haikuwa kazi rahisi kubadilisha uamuzi ambao ameamua kuufanya, hata polisi ilionekana walishachoshwa na usumbufu wa Catherine
sababu kila siku alikua akifika kituo cha polisi kumuulizia mama yake.
Alimgeukia Enock aliyekuwa pembeni.
“Lakini Catherine”
“Abee”
“Kwanini usiwasikilize polisi”
“kuhusu?”
“usubiri kukuche Mpenzi”
“kama wewe utabaki baki, ila mimi nitaenda mwenyewe hata nikifa najua nilikua namtafuta Mama yangu isitoshe huko alipo yupo na mdogo wangu Christopher”
“siwezi kukuruhusu uwende mwenyewe mpenzi”
Waliingiya ndani ya gari na Enock kutoa gari mbio mpaka Segera ambapo iliwachukua masaa matatu kufika.
Ni kweli walikuta watu wengi wamelizunguka basi kubwa la abiria ilikua ni ajali ya kutisha sana, baadhi ya ndugu jamaa na marafiki walishafika ili kuangalia wapendwa wao.
Catherine na Enock waliungana nao baada ya magari ya wagonjwa kufika na kuchukua maiti za wagonjwa ili kuzipeleka hospitali ya wilaya ya Segera hapo mkoani Tanga.
Catherine alikua na moyo mgumu pengine kupita mwanamke wa aina yoyote ile. ni kitendo cha kuingia Monchwari bila kuogopa na kuanza kuutafuta mwili wa Mama yake pamoja na mdogo wake christopher, alizidi kufungua fungua mafriji na kuona ni kiasi gani maiti zilivyoharibika usoni.
“Daktari naomba uvute friji nione vizuri”
“sawa lakini binti huogopi?”
“Tafadhali naomba uvute friji”
Maisha aliyopitia nyuma hakupaswa kuogopa, alishauwa watu wengi sana alishaona maiti nyingi tofauti za kutisha hakuwa muoga tena katika maisha yake kama hapo awali, sasa alikua ni mwanamke jasiri asiyeogopa kitu cha aina yoyote ile.
Mpaka kunakucha alishapitia maiti zote kisha kuelekea kwenye vyumba vya wagonjwa maututi bila ya kumuona Mama yake mzazi hakujua ni wapi alipo,alichanganyikiwa sana walirudi ndani ya gari wakiwa na Enock wote wakiwa wamechoka sana.
“Kivipi?”
“tumekuta maiti zao kwenye hii njia ya kwenda hospitali ya kwenda mnazi mmoja Mkuu”
“hakuna aliyepona?”
“nina wasiwasi huo”
“okay! Fanya utaratibu wa kuchukua maiti zao zikahifadhiwe kisha urudi ili tuandae jeshi lingine namimi itanibidi nisimamie”
“sawa Mkuu nitafanya ivyo”
Mkuu wa polisi Nchini Tanzania Inspector Mkumbo alikasirishwa sana kupita maelezo, alimtambua sana Mzee David Mwasha kuwa ni mtu aliyeogopeka na ni katili sana, ni kweli Mzee huyo alitokea kusumbua sana polisi alishauwa kikosi kizima, licha ya hayo alishawahi kumuweka mikononi mwake miaka mingi iliyopita,siku hiyo hiyo aliita kikosi cha polisi kituo kikubwa cha posta akiwa mwenye ghadhabu sana, ilikua ni lazima aende Zanzibar siku hiyo hiyo,
“nasikitishwa sana na wenzetu waliouwawa huko Zanzibar.Mungu azilaze roho zao pema peponi,hii haimaanishi kuwa tusiendelee kumsaka Mzee huyu hatari,Jeshi la Tanzania tumekula kiapo kulitumikia taifa letu na kuwalinda wananchi wetu kiujumla,nahii ndiyo kazi yetu”
Alizungumza Inspector Mkumbo kwenye kikao hiko kisha kuendelea.
“sasa basi leo tutaenda kimnya kimnya kumkamata mzee huyu na kikundi chake kwa ujumla, awe hai au amekufa mimi mwenyewe nitaongoza kikosi,Mjuni anza kufanya mawasiliano na jeshi la Zanzibar sasa hivi, Haruna piga simu jeshi la majini waambie tunahitaji spidi boti”
“sawa Mkuu”
Mawasiliano yalianza mara moja hapo hapo, huku baadhi ya polisi wakikusanya silaha za moto tayari kwa safari ya kwenda kisiwani Zanzibar,
Saa saba ya mchana walikua teyari, difenda ziliwashwa mpaka bandarini kisha wote kuingia kwenye boti za polisi zinazoenda kasi sana, baada ya dakika hamsini walifika Zanzibar na kupokelewa na jeshi la Zanzibar!.
Mzee Mwasha tayari Alisha pokea taarifa za ujio wa jeshi hilo kutoka Tanzania siku hiyo asubuhi na mapema kutoka kwa mkuu wa polisi jeshi la Zanzibar, nayeye ilibidi ajihami kama alivyofanya Mara ya kwanza aliweka watu wake na kuwapanga vizuri.
“Rodgers utapanga watu wako kule mbele kabisa mwanzoni,najua watatokea kule juu,wewe Mick utakaa huku nyuma mwanzoni mtawasubiri wote waingie
ndani kisha muwazunguke”
“sawa Bosi usijali kwa hilo hiyo ni kazi ndogo sana kwetu sisi”
“sawa kuweni makini”
Hayo ndiyo maagizo waliyopewa na mzee huyu katili mwenye roho mbaya kumzidi Shetani huko kuzimu,alishaamua kumwaga damu kwa yoyote atakae ingia katika himaya yake, Ni kweli mzee huyu alitisha sana kuliko ugonjwa wa ukoma.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni