BIKRA YANGU (64)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Waliingia ndani ya gari kisha hapo hapo kumfunika Catherine na kitambaa cheusi usoni ili asiweze kuona njia yoyote ile.SASA ENDELEA...
Baada ya nusu saa alifunguliwa kitambaa cheusi, mbele yake aliona ngome kubwa na walinzi wanaolinda huku wakiwa na mitutu mikononi mwao, walimtoa ndani ya gari kisha kupita naye mpaka kwa Mzee Mrefu aliyekua amekaa juu ya sofa anatabasamu kwa dharau.
“Huyu hapa bosi”
“sawa nendeni”
Hasira zilimkaba tena baada ya kumuona Mzee Mwasha mbele yake tena anacheka kwa dharau huku mkononi mwake akiwa na glasi ya pombe kali.
“Mama yangu yuko wapi?”
“yupo salama usijali hata kidogo, nimefurahi kukuona tena mpenzi wangu Catherine Ramsey Ha ha ha ha ha ha ha ha ha,pole na misukosuko ya maisha ningekuwa mimi ndiye wewe ningemtafuta mwandishi wa vitabu Bwagayo aniandikie simulizi ingeuza sana,maana tangu Baba yako kifo chake wewe kuteseka kutuchanganya mimi na Mwanangu Enock,hiyo ingetosha kuandika simulizi na kuuzika na ukapata pesa za kutosha”
Alizungumza Mwasha na kusimama kisha kumsogelea Catherine.
“lakini umechelewa sababu muda mfupi unaenda kuwa historia,Ha ha ha ha ha”
Mzee Mwasha alizidi kuongea kwa dharau sana tena kwa Majigambo, katika maisha yake tangu alivyoanza kuwa jambazi na kulindwa kama mfalme hakuwahi kuwaza kuwa atakuja kukamatwa siku moja hata kidogo, alishaweka ulinzi wa kutosha hasa aliposikia siku hiyo kuna jeshi la polisi linakuja kumkamata.
Hapo hapo wanaume Wawili walioshiba walimkamata Catherine na kupandisha naye ngazi mpaka juu na kumtupa ndani ya chumba kikubwa,
Alipomuona Mama yake alimkumbatia na wote kuanza kulia kwa sauti za kwikwi mfululizo!.
“Ma..ma”
Aliita Catherine kisha kutoa bastola kiunoni baada ya kupangusa machozi yake.
“Catherine usifanye ivyo”
“No Mama, lazima tutoke humu nimekuja kukukomboa wewe na Christopher niamini Mama”
“Cate hata ukifanya ivyo ni kazi bure tazama nje kuna walinzi wa kutosha unadhani tutawezakutoka?”
“Mama usiwe na wasiwasi kuhusu hilo, Mimi nitafanya kila kitu, cha kufanya jiweke tayari kwa kuwa huru”
“Lakini sawa…..”
Mama Catherine bado alikua na mashaka hakuweka matumaini juu ya mpango wa Catherine aliokua anaupanga wa kutoroka ndani ya ngome hiyo inayolindwa, wote walishtuka baada ya usiku kuingia, walisikia milio ya risasi inarindima mfululizo, waliogopa sana na hofu kuwatanda mioyoni mwao, milio ya risasi sasa ilizidi kusogea karibu, walivyochungulia nje waliwaona polisi wakiwa wanarusha risasi na kupambana na jeshi la Mzee Mwasha, lakini polisi walionekana kuzidiwa na wote kuuwawa.
“Inpector Mkumbo”
Alisema Mwasha huku akimtizama Polisi huyo kwa macho makali, ni kweli watu hawa wawili walikua na historia, walikua wakiwindana kama paka na panya.
Mawazo ya Mzee Mwasha yalirudi nyuma kama mkanda kisha kukumbuka alivyoteswa na polisi huyo mpaka akatolewa baadhi ya meno yake mdomoni.
Hapo hapo alikunja ngumi na kumtandika nayo usoni iliyomfanya polisi huyo aende chini mzima mzima.
“Subiri siku zako za kuishi leo upo kwenye himaya yangu nimefanya kusudi kukuacha hai nataka ufe huku unateseka,Rodgers mshughulikie”
Kauli hiyo ilivyotoka kwa Mwasha tu Rodgers alianza kumpiga polisi huyo ngumi zisizo kua na idadi kamili mpaka alipopoteza fahamu zake, walimuacha hapo hapo mpaka siku inayo fuata kisha Catherine na Mama yake kutolewa nje ili wateswe kisha baadaye wauliwe,
Catherine hakutaka jambo hilo litokee hapo ndipo alipotoa bastola yake, lakini kabla ya kufanya lolote Rodgers alimrukia na kumpiga kichwa cha puani huku bastola ikidondoka upande wa pili na Mzee Mwasha kuiwahi!.
“Nasikia siku izi unapigana ngumi,nataka nione leo”
Alizungumza Mzee Mwasha kisha kuketi kwenye kiti akiwatizama Rodgers na Catherine waanze kupigana.
Catherine alikunja ngumi vizuri alishaelewa mtu huyo Rodgers ana mafunzo ya kutosha sababu walishawahi kupambana na kupigwa sana ivyo umakini wa hali ya juu ndiyo ulihitajika,aliiona ngumi inakuja na kuhepa kushoto kisha kukaa sawa, alitisha kama anarusha ngumi ya kushoto na kurusha ya kulia iyo ilizaa matunda na kumfikia
Rodgers puani hapo hapo aliruka juu na kujizungusha hewani na teke aina ya round kick lililomfanya Rodgers aende chini chali…
Mama catherine ametekwa nyara na Mzee Mwasha yupo huko visiwa vya Zanzibar,huku nyuma akimuacha Mwanae Catherine asipate hata lepe la usingizi akimtafuta usiku kucha bila mafanikio ya aina yoyote yale, alisharipoti mpaka vituo vya polisi lakini hawakumpa majibu yaliyomridhisha kabisa.
Baadaye anapigiwa simu na Mzee Mwasha kuwa yupo na mama yake, hapo ndipo anaamua kuiba silaha na kuamua kwenda visiwa vya Zanzibar kimnya kimnya ili akafanye ukombozi akijiita jeshi la mtu mmoja, alijiamini sana sababu ya mafunzo mengi ya kupigana aliyofunzwa huko Demokrasia ya kongo.
Ni kweli anafika Zanzibar na kujaribu kila aliwezalo amuweke mama yake huru lakini kwa mara nyingine anakutana na Rodgers mpiganaji wa kick boxer na wote kukunja ngumi,
Ngumi aliyorusha Rodgers baada ya kusimama ilipita hewani baada ya Catherine kuinama chini kidogo, akiwa ameinama hakufanya makosa hata kidogo alitupa ngumi mbili zilizomfikia Rodgers kwenye chembe ya moyo, hapo aliinuka kidogo na kuzungusha teke lililompeleka chini,hakuwa Catherine lelemama Yule wa miaka iliyopita nyuma alikuwa ni mwanamke jasiri,ilikua ni lazima amalize alichokianza alimuinua Rodgers na kumtwanga kichwa cha puani,
Rodgers alionesha kuzidiwa, damu zilianza kumvuja puani na midomoni mwake hana nguvu tena yupo chini amelala.
Mzee Mwasha aliyekua juu ya sofa hata yeye alishangazwa na upiganaji wa Catherine hakuamini kama mwanaume anayemuamini yupo chini kachakazwa yupo hoi bin taaban!
Majambazi wengine wawili walifungua mlango na kumzunguka Catherine, Mzee Mwasha alitabasamu sana na kuona huo ndiyo mwisho wa catherine.
“Mshughulikieni huyo”
Tamko hilo alitoa Mzee Mwasha na kukaa sawa sawia.
Catherine hakukata tamaa aliwatizama watu wawili mwingine mbele yake kisha mwingine akiwa nyuma yake akiwa na kisu,alishusha pumzi ndefu sana na kukunja ngumi upya kwa ajili ya mpambano mwingine.
Mama yake muda wote alikua pembeni analia hakuwa na mategemeo kuwa kama kuna uhai tena au wangekua huru kutokana na jumba hilo kubwa kulindwa na watu wengi,hakuwa na uhakika kuwa Catherine angeweza kuwamaliza watu wote wa jumba hilo kubwa na kisha baadaye kuwa huru.
Bado mapambano makali yaliendelea, Catherine ilibidi aweke umakini sana kwa jambazi aliyeshika kisu mkononi mwake, huyo ndiye aliyemuwekea umakini wa hali ya juu sana kuliko mwingine,alikiona kisu kinakuja usawa wa tumbo lake,alichofanya ni kurudi nyuma lakini alijikuta yupo chini baada ya mwingine kumpiga mtama,hapo ndipo alipoanza kushambuliwa tena upya.
Akiwa yupo chini hakutaka kukata tamaa baada ya kukumbuka kile kilichomleta Mama yake na Christopher ilikua ni lazima wawe huru,alivyokumbuka hayo tu nguvu zilimrudia hapo hapo na kupata nguvu upya,
Ni kweli haikuchukua hata dakika kumi majambazi wote walikua chini wameuwawa baada ya mwanamke huyu jasiri kuvunja shingo zao.
“Hongera sana siku tegemea kama ni mwanamke jasiri kiasi hiko”
Alisema Mzee Mwasha akiwa na bastola mkononi.
“Any way,hiyo haimaanishi mimi kukuacha hai,lazima nikuuwe tu,kachakacha”
Mzee Mwasha alikoki bastola yake na kusimama wima,hakuwa na masihala hata kidogo kwa maneno aliyokuwa anazungumza, aliukunja uso wake kwa ghadhabu sana,dalili zilionesha kuwa ni lazima awaondoshe duniani watu waliosimama mbele yake, alimuendea mama yake na Catherine kisha kumpiga na kitako cha bastola kilichompeleka mpaka chini puuh! Catherine alipotaka kusogea alitulizwa na risasi ya bega.
“Paaaaaa”
Nayeye kudondoka chini akiwa mwenye maumivu mengi sana,taratibu alianza kukata tamaa ya kuishi na kufanya ukombozi.
Alitambaa na kumsogelea Mama yake ili waagane, walikombatiana kama familia kisha kufumba macho yao na milio ya risasi kusikika.
“Mama Natu”
“Abee”
“ile kitu yangu iko wapi?”
“kitu ipi hiyo?”
“silaha yangu niliiweka hapa chini ya mto”
“hapana mimi siyuwe iko wapi”
“isiwe ikawa anayo Natu”
Usiku kucha Kway alikua na kazi ya kutafuta bastola yake bila mafanikio, hakuelewa ni wapi ameiacha aliingia makabatini bila mafanikio ya aina yoyote yale na kushindwa kukumbuka ni wapi aliiweka, japo alikumbuka kuwa mara ya mwisho aliiweka chini ya mto hapo seblen lakini hakuwa na uhakika wa kutosha,usiku huo huo alienda mpaka ofisini kwake na kuanza kuitafuta kila mahali, alielewa nini maana yake alielewa kivyovyote vile ni lazima ingemuweka kwenye matatizo makubwa endapo itatumika kufanyia uhalifu wa aina yoyote ile.
Walipojaribu kumdadisi Mtoto wao Natu kuhusu hilo hawakuweza kupata jibu kamili.
“Natu mwanangu ile kitu nayoweka hapa kiunoni iko wapi?”
“Ulinikataza nisiguse Dad,itakuwa pale unapoweka”
Natu alijibu.
Hawakulala usingizi wa raha mpaka kunakucha.
“bado haijaonekana?”
Kway alimuuliza mke wake asubuhi kulivyokucha.
“hapana,lakini….”
“nini?”
“namuhisi Yule Catherine pengine atakuwa nayo”
Ni kweli hisia zake zilimtuma kuwa silaha yake anayo Catherine alikumbuka jinsi aliketi pembeni yake, alikumbuka kuwa Mama yake alitekwa nyara ivyo kivyovyote vile alitaka silaha akafanyie ukombozi,kabla ya kufanya lolote simu yake ya mkononi iliita.
Alivyoangalia kioo cha simu aligundua kuwa ni Enock.
“Mzee Shikamoo”
“Marahaba habari yako Enock”
“sio nzuri”
“kwanini?”
“Catherine na Mama yake wametekwa nyara”
“unasema?”
“mchumba wangu Catherine ametekwa nyara nimepigiwa simu na Baba yangu ndio yupo nao na ananihitaji niende Zanzibar”
“yaani baba yako ndiyo kawateka?”
“ndio,naomba unisaidie kitu kimoja”
“kitu gani?”
“siwezi kufanya hili jambo mwenyewe tafadhali naomba msaada wako”
“msaada gani?”
“naomba utoe taarifa polisi mimi natangulia”
“sawa lakini…tititi”
Enock tayari alikuwa amechanganyikiwa baada ya kupigiwa simu na Baba yake mzazi aliyekuwa huko kisiwani Zanzibar amejificha, anasifika hivi sasa kwa ujambazi na uharamia,alikua ni mtu hatari ambaye hashindwi kufanya kitu na hakuna mtu wa aina yoyote ile aliyeweza kumzuia,
Jasho jembamba lilimtoka Enock alishaelewa kuwa mchumba wake huko alipo anateseka na ameshapigwa risasi,ivyo kama mwanaume ni lazima aende ikiwezekana akamuokoe japo hakua na uhakika kama angefanikiwa,ilikua ni bora wafe na mchumba wake kwani aliamini kila nafsi itaonja umauti.
“hata nikifa najua nilikua namtetea mchumba wangu,lakini hata ivyo mwisho wa siku tutakufa tu”
Hayo ndiyo aliyowaza Enock akiwa ndani ya boti akielekea huko visiwa vya Zanzibar,aliwaza juu ya maisha yao waliyopitia na mpenzi wake Catherine tangu mara ya kwanza alipomuona hospitalini miaka mingi iliyopita,kisha kuanza kumwambia juu ya hisia zake.
Alikumbuka vikwazo vingi walivyopitia mpaka kugombana na Baba yake mzazi Mzee Mwasha na kupigana mpaka risasi kisa mwanamke huyo mrembo
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni