BIKRA YANGU (65)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Alikumbuka vikwazo vingi walivyopitia mpaka kugombana na Baba yake mzazi Mzee Mwasha na kupigana mpaka risasi kisa mwanamke huyo mremboSASA ENDELEA...
Catherine.
Alikumbuka mpaka watu aliowauwa na kuwadhuru. Ni kweli katika mapenzi yao walipitia mengi.
“Kaka tayari tumefika”
Sauti ya kike nyororo ya dada wa kipemba ndiyo iliyomshtua kutoka katika dimbwi la mawazo,
“okay ahsante!”
Boti tayari ilishatia nanga na Enock taratibu kuanza kushuka hakuwa na mizigo ya aina yoyote ile alienda yeye kama yeye,baada ya kufika kituo cha basi alipiga simu ili apatiwe maelekezo,
Hapo hakukaa sana watu watatu walimfuata kisha kufanya kama walivyo mfanyia Catherine,
Gari liliondoka akiwa na kitambaa cheusi machoni ili asijue ni wapi anapelekwa.
Mpaka wanafika hakuelewa ni wapi alipo zaidi ya kuona yupo nje ya nyumba kubwa baada ya kitambaa kutolewa usoni mwake.
“Catherine yuko wapi?”
“hauna mamlaka ya kuuliza maswali”
“mnataka nini?”
“msubiri baba yako ndiyo umuulize hayo maswali yako”
Bado Enock hakuwa anaelewa ni wapi Catherine ameweka, ila katika hali ya ghafla ulisikika mlipuko wa ajabu na kulipua nyumba,
Kwa mbali walianza kusikia mlio wa helikopta, kwa mara ya kwanza hawakuelewa ni kitu gani kinaendelea.
Hapo ndipo waliposhuhudia mtu aliyekua juu ya helkopta mlangoni ameshika mtutu aina ya AK 47 anamwaga risasi, kila mtu aliruka upande wake ili kuokoa maisha yao.
Bomu lingine aina ya granade la mkono lilirushwa getini na kufanya mlipuko mwingine utokee,
Helkopta ilizidi kuzunguka angani huku ikizidi kuwasambaratisha walinzi wa mzee Mwasha ambao hata wao walionekana kujitetea wakirusha risasi lakini walizidiwa nguvu,
Baada ya ukimnya kutawala Helikopta ilianza kushuka chini taratibu huku ikizidi kuzungusha mapanga boi yake na kufanya vumbi jingi kuruka.
Walishuka watu watano ndani ya Helkopta na kuingia mpaka ndani moto ulipokua unawaka kisha baadaye kutoka na Catherine aliyekua hana nguvu zake,alipuliziwa dawa kali za usingizi na kuzirai hapo hapo kisha kuingia naye ndani ya Helkopta,walivyo hakikisha kila kitu kimeenda sawa, taratibu Helkopta ilianza kuzungusha mapanga boi na kupaa angani huku ikizidi kutokomea.
Kifusi cha mchanga kilichodondoka kutokana na bomu lililorushwa kilimfanya Enock apoteze fahamu zake,
Taratibu aliyafumbua macho yake, cha kwanza kuona ni nyumba iliyokua ndani inateketea na moto,bila kuuliza haraka haraka aliinuka bila kujiuliza mara mbili,mawazo yake yote yalimtuma kwa Catherine mchumba wake.
“Catheriiineeeee”
Aliita na kujitosa ndani ya moto bila kujali kitu chochote kile,moshi ulikua mkali alijitahidi sana kuyatoa macho yake,alikohoa sana kutokana na kupaliwa na Moshi uliokua mweusi sana,
Alitafuta huku akimuita Catherine lakini ghafla alimuona Mama Catherine amelala chali kabanwa na mbao,kwa haraka alimfuata na kutoa mbao iliyokua imem-bana kisha kuuzungusha mkono wake juu ya mabega yake, ilibidi awahi kumuweka Mama catherine nje kisha yeye arudi ndani ya moto ili kumuokoa Mchumba wake.
Zoezi hilo lilifanikiwa alimuweka mama Catherine nje na yeye kurudi tena ndani ila kabla ya kufika mbali, moto ulizidi kuwa mkali na kufanya mbao za moto zidondoke,alivyojaribu kutoka nje alishindwa mbao zilikua teyari zimeregea na kumdondokea kichwani.
Kway na mke wake Julia aliyekuwa mjamzito sasa wapo njiani wakiwa na jeshi la polisi, hakutaka kumuacha Mume wake aende peke yake, wapo ndani ya boti za polisi ziendazo kasi, alishatoa taarifa polisi juu ya Enock kuwa yupo visiwa vya Zanzibar na mchumba wake ametekwa nyara,Jina la Enock halikuwa Ngeni masikioni mwao walijua sana historia yake ivyo waliungana na kuanza safari, walishajua tayari makazi ya Mzee Mwasha na eneo aliloweka kambi yake,
Na alipokua anajificha, saa tisa ya Alasiri waliwasili Visiwa vya Zanzibar kimnya kimnya bila ya kufanya mawasiliano yoyote yale na jeshi la Zanzibar kama wafanyavyo siku zote.
Wote walivalia nguo za kiraia, walivyofika tu walitafuta usafiri wa kukodi mpaka ndani ya msitu aliokuwa anajificha Mzee Mwasha wakiwa na mitutu yao mkononi, lakini ghafla waliona kwa mbali Helkopta ina mwaga risasi, ilibidi wasitishe kwanza zoezi lao,
Hali ilitulia baada ya nusu saa kufika kisha wote kuingia kwa pamoja, wakiwa kwenye miti miti walimuona Enock anaingia ndani ya moto kisha kukaa huko dakika mbili nzima bila kutoka, hapo ndipo askari wawili shupavu walijitosa ndani ya moto huo mkali ili kumuokoa kijana huyo,
Ni kweli walifanikiwa kumuokoa, alikua amebanwa na Mbao mgongoni, walimuinua na kutoka naye nje ili kumpa huduma ya kwanza,
Baada ya kusikia nafuu jina la kwanza kulitaja lilikuwa ni Catherine.
“Catherine mmempata?”
“hapana hatukufanikiwa”
“wacha nijaribu kuingia tena kumtafuta”
“hapana Enock hatuwezi kukuruhusu”
“haya ni MAISHA yangu hamuwezi kunizuia kwenda kumuokoa mchumba wangu,niacheni niende”
Haikuwa kazi rahisi kumzuia Enock kutaka kuingia ndani ya Moto,
Moyo ulimuuma sana kidonda kilichokua kinaanza kupona moyoni sasa kilitoneshwa na kuanza kutoa damu,
Mikono ilimtetemeka, bado alikua akibishana na polisi mpaka walipomfunga pingu ili asifanye kile anachotaka kukifanya.
Msako wa polisi ulizidi kufanyika wakizunguka nyuma ya nyumba huku wakianza kufanya mawasiliano na jeshi la Zanzibar, kilichotokea wakati huo bado kilikua Gumzo, Mwanamke waliyeenda kumfuata ili kumuokoa hawakumkuta.
“Afande, nakuomba huku nyuma mara moja ova”
“sawa ova”
Koplo Kato alitoa taarifa kupitia redio upepo baada ya kuona miili mitatu ipo chini.
Haraka haraka walifika, mwili mmoja ulikua wa Inspector Mkumbo huku pembeni yake akiwa amelala na mtoto mdogo akiwa amemlalia huku akiwa anavuja damu mkononi lakini walikua wanapumua kwa shida sana,
Mwili mwingine walishindwa kuutambua vizuri.
“Huyu ndiye Mwasha tuliyekua tunamtafuta”
Alisema Askari mwingine baada ya kufika eneo hilo la tukio aliloitwa, hawakuelewa ni kitu gani kimetokea.
Haraka haraka walibebwa mpaka kwenye magari ya polisi, huku Mzee Mwasha akiwa amefungwa pingu kwa nyuma,
Enock alipomuona Baba yake hasira zilimkaba na kuyabana meno yake, mapafu yake yalijaa hewa na kufanya kifua chake kipande juu na kushuka kwa hasira, midomo ilimtetemeka kwa hasira na uchungu.kama angepewa bastola basi pale pale angemmaliza.
“Afande naomba nifungue pingu mimi sio muhalifu”
“subiri kwanza, zitafunguliwa”
“sasa kwanini umenifunga pingu?”
“Afande Juma, Enock yupo sahihi sio muhalifu embu mfungulie”
Hapo ndipo Enock aligeuka kwa nyuma na kufunguliwa pingu.
Ghafla kama umeme alichomoa bastola iliyokua kiunoni mwa askari mmoja wapo kisha kuikoki na kumuelekezea baba yake mzazi huku akiyabana meno yake.
Kila askari aliganda baada ya kumuona Enock kashika bastola,walijua ni lazima atafyatua risasi na kumuondosha Mzee Mwasha Duniani na hawakutaka hilo
litokee.
“Enock weka silaha chini tafadhali”
Aliamuru Polisi.
“hapana siwezi huyu Mzee Lazima nimuuwe siwezi kukubali aishi”
“Weka silaha chini Enock sheria itafuata mkondo wake,huyo atatusaidia kutuambia ni wapi Catherine alipo”
“hapana siwezi Afande”
“Enooooock”
Aliita Kway.
“Weka silaha chini tafadhali wacha jeshi la polisi lifanye kazi yake,punguza jazba”
Taratibu Enock alianza kushusha silaha chini lakini bado alikua mwenye hasira sana,polisi walimfuata na kumnyang’anya bastola aliyoshika.
Mzee Mwasha alipakizwa ndani ya diffenda ya polisi iliyokuwa teyari imefika kisha kuondoka naye. Bado Enock alikua akilitaja jina la Catherine kila dakika moja ikipita, hakuelewa ni wapi mchumba wake alipo,aliona maisha ni bure kabisa bila ya kuwa na Catherine karibu yake.
“Enock”
Aliita mama Catherine.
“Naam Mama”
“Catherine amechukuliwa na watu ambao walikuja na helkopta”
“ilikuaje?”
“nashindwa kuelewa maana Mara ya mwisho nilikua naye Mimi na Christopher kisha tukasikia mlipuko mkubwa hapo ndipo sikujua kinachoendelea”
“zitakuwa ni njama za huyu mzee atataja tu”
Siku hiyo hiyo usiku walimsafirisha Mzee Mwasha mpaka mkoani Dar es salaam, baada ya kufika kivukoni walipanda magari mengine ya polisi yaliyokuwa teyari yamefika.
Kila polisi alikuwa ni mwenye furaha sana baada ya kumtia nguvuni Mzee huyo hatari sana.
Ni kweli alisumbua sana jeshi la polisi hawakulala usiku kucha,Wenzao wengi walipoteza maisha,kila mtu alikuwa na hasira sana na mzee huyu.
Walimfikisha kituo kikubwa cha polisi oysterbay ili kusubiri sheria ifate mkondo wake.
Enock alizidi kuwa sumbua polisi akitaka kumuhoji baba yake ni wapi Catherine alipo, kila kukicha ilikua ni lazima aripoti oysterbay polisi.
“Dad mimi ni mwanao, naomba nirudi katika hali ya furaha,nini kilikupata lakini,haukuwa hivi, naomba nitajie ni wapi mchumba wangu alipo, sawa sikatai unamchukia,hata kama amekufa niambie ili nione japo mwili wake”
Mzee Mwasha hakujibu kitu chochote na kugeukia upande wa pili hakutaka kusema lolote lile,
Enock alitafsiri hiyo kama dharau lakini hakuwa na namna nyingine ya kufanya, kwa upole alisimama na kutoka nje alishindwa ni wapi aanzie.
Hakuelewa ni njia gani atumie ili aweze kujua ni wapi mchumba wake alipo, habari za kuchukuliwa na Helkopta ndizo zilimuumiza sana mtima wake.
Ki ukweli alijiona ni mwanaume mwenye mkosi katika mapenzi, tangu alipoanza kuwa na mapenzi na mwanamke huyo miaka iliyopita,vitu vingi sana walipitia na mateso mengi,lakini hiyo haikumfanya akate tamaa ya kuwa naye na alishaapia ndiye atakaye kuja kumzalia watoto wawe mke na mume hapo baadaye.
Mama Catherine,Enock,Anderson Peter pamoja na Mtoto wa Becker wote waliunganisha nguvu zao ili kumtafuta Catherine kila kona ya jiji,wakibandika picha zake kila mkoa na kutoa taarifa mbali mbali vituo vya Redio na tv.
Becker t.v kituo kikubwa kinachovuma ndani na nje ya Africa kwa ujumla kilichomilikiwa na Rafiki yake ndiko kilikuwa kinarusha matangazo juu ya upotevu wa Mwanamke Catherine kila kukicha.
“Habari kwa ufupi,Mwanamke mwenye umri wa miaka ishirini na nne anatafutwa, anaitwa Catherine Ramsey Kidhirwa kwa yoyote atakaye muona basi atoe taarifa kituo cha polisi kilichokua karibu yako”
Habari hizo zilidumu wiki nzima bila mafanikio yoyote yale,
Enock alitumia pesa nyingi sana kusafiri mikoa mbali mbali kumtafuta Mchumba wake.
Alipigiwa simu tofauti nyingi za pole lakini hazikuwa na maana kwake, akili yake ilishachoka sasa kuzunguka, lakini hiyo haikumfanya akate tamaa, siku hiyo hiyo aliingia mpaka ofisi za Becker fm Msasani,na kuomba aongee machache studio!.
“Catherine mpenzi wangu, ni wiki tatu sasa zimepita nakutafuta kila mkoa, sijui ulipo mchumba wangu,nimesha hangaika sana, bila wewe siwezi, kama unanisikia tafadhali naomba urudi nyumbani,..nakup…”
Enock alishindwa kumalizia maneno anayoongea na kuanza kububujikwa na machozi hapo hapo, moyo ulimuuma sana hakujali kuwa yupo hewani na
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni