BIKRA YANGU (66)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Enock alishindwa kumalizia maneno anayoongea na kuanza kububujikwa na machozi hapo hapo, moyo ulimuuma sana hakujali kuwa yupo hewani naSASA ENDELEA...
Watanzania wanamsikiliza kupitia redioni.
Becker ilibidi amuinue rafiki yake kisha waende nje, Leo hii Enock analia kisa mapenzi kitu ambacho hakutegemea kuja kukifanya katika maisha yake.
“Kaka usilie,Catherine tutampata nitakuwa nawewe bega kwa bega mpaka atakapo patikana”
“Becker, siweziii.. siweezii”
Alizidi kulia huku akifikicha pua zake.
Picha mbali mbali zilipita ndani ya ubongo wake wakiwa na Catherine na kumfanya azidi kulia kila kukicha,
Mawazo yalikula kabisa mwili wake wote kutokana na Mawazo aliyokuwa nayo.
“tuku tuku tuku tuku”
Helkopta ilizidi kusonga mbele ikizidi kukata mawingu, Catherine hakuwa na fahamu zake baada ya kupuliziwa madawa makali sana puani na kuchukuliwa na usingizi mkali.
Baada ya Helkopta kubwa kutoka visiwa vya Zanzibar ilitua visiwa vya chakechake hapo walimshusha Catherine na kumuingiza ndani ya boti ndogo.
Baada ya zoezi hilo kukamilika boti ilitoka kasi mpaka ilivyofika kati kati ya bahari hiyo ya Hindi na kusimama,walivyo fanya mawasiliano ulisikika mlio wa ndege ndogo ya majini kisha kutua juu ya maji, hapo walimpakia Catherine ndani ya ndege, ilionekana mipango hiyo ilipangwa na watu makini sana.
Kwa mbali sana Catherine alihisi kelele za Ndege alivyoyafumbua macho yake alikutana na sura aliyoifahamu na mara ya mwisho alipanda naye ndege walivyokua wakitoka nchini Kongo.
Sura ya mwarabu huyu mwenye ndevu nyingi kama Osama bin Laden aliikumbuka sana na kukumbuka ndoto aliyoota.
Alishapata jibu tayari la swali lake kuwa ametekwa nyara.
Alivuta kumbu kumbu nyuma kuwa mara ya mwisho alikuwa yupo ndani ya jumba la Mzee Mwasha na Mama yake pamoja na mdogo wake Christopher,
Bado alishindwa kuelewa watu hao ni akina nani mpaka alipoiona ngozi nyeupe ya kizungu,hakuweza kumsahahu Carl Martin.
“Well well well well Catherine nice to meet you again,I am amprest(Catherine nimefurahi kukutana nawewe tena,nimevutiwa)”
Aliongea Carl Martin kwa nyodo huku akimshika shika Catherine mashavu yake.
Hata angewekewa kisu shingoni asingekubali kwenda nchini Germany ili akachezeshwe filamu za ngono.
Alishaelewa nini maana ya Carl Martin kumtafuta,ubongo wake ulikusanya vitu haraka haraka na kukumbuka kuwa ana kisu cha kukunja kwenye kiatu chake,alichotakiwa kufanya ni kutumia akili nyingi na umakini ili ajinusuru na watu hawa, na hayo ndiyo yalikua mahesabu yake kichwani.
Hapo hapo alianza kuwahesabu walinzi waliopo ndani ya ndege,baada ya kujua idadi yao alianza kufikiria jinsi ya kutoka na kujitupa ndani ya maji.
Ndege ilianza kutoa kasi sana kisha taratibu kuanza kupaa angani baada ya kila mmoja kukaa kwenye kiti chake, kama umeme Catherine aliruka mlangoni akiwa na kisu mkononi mwake na kumchoma nacho mlinzi aliyekua amezubaa anavuta sigara,
Kisha kufungua mlango haraka haraka na kujitupa nje 'chubwi' ndani ya maji….
“Halloo”
“Yes Halloo”
“Naongea na Mr.Enock?”
“ndiyo mimi,sijui nani Mwenzangu?”
“Naitwa Rama!,niilichukua namba yako jana Becker t.v nina habari nzuri,nimemuona Catherine sehemu”
“Unasema, upo wapi sasa hivi,niambie ulipo, ulimuona wapi?”
“Huku Dodoma Chamwino”
“Naweza nikaja huko?”
“sawa njoo”
Moyo wa Enock ulilia pah asubuhi hiyo.
Baada ya kusikia habari hizo kutoka kwa msamalia mwema aliyedai kuwa kamuona Mchumba wake Catherine huko Dodoma Chamwino,hakutaka kujifikiria mara mbili hata kidogo, alichungulia gari yake kama ina mafuta ya kutosha na kuipiga funguo kwa safari moja tu kuelekea Dodoma kijiji cha Chamwino kwenda kumchukua Mchumba wake ambaye alimtafuta kwa takribani miezi minne bila
Dalili na mafanikio ya aina yoyote ile,hakukata tamaa hata kidogo na sasa alikua yupo njiani anakimbiza gari kwa spidi sana kama mwendawazimu akitamani afike haraka ili akamuone tena mchumba wake,wakati mwingine alitamani gari yake ipae ili aweze kufika dakika hiyo hiyo lakini hilo halikuwezekana hata kidogo,njiani aliwaza mengi sana,hususani swala la yeye kufunga ndoa kubwa na Catherine hata kesho yake akimpata.
Jioni ya saa kumi na moja aliwasili Mkoani Dodoma kisha kupiga simu kwa Ramadhani aliyedai kuwa alimuona Mchumba wake,hakutaka kupoteza muda wowote ule,maelekezo aliyopewa yalimfikisha mpaka kijiji cha Chamwino na kuonana na Ramadhani!.
“Jana nili muona maeneo ya huku twende nikupeleke”
“sawa”
Wote waliongozana mguu kwa mguu mpaka kwenye nyumba ndogo ya udongo iliyotengenezwa kwa mfumo wa nyasi zilizokauka.
Mwanamke aliyetoka ndani ya kijumba hiko ni kweli alifanana na Catherine lakini hakuwa yeye,
hapo hapo alinyong’onyea na kukaa chini akiwa amechoka.
“Kaka nipatie basi ile pesa uliyosema, Catherine huyo hapo”
Alisema Ramadhani.
Enock hakuwa na kitu chochote cha kuongea zaidi ya kutoa noti mbili za shilingi elfu kumi na kumkabidhi kisha kuondoka zake taratibu.
Alikaa Dodoma takribani wiki nzima akizidi kumuulizia Mchumba wake bila kuona dalili yoyote ya kumpata alimtafuta kwa hali na Mali,wiki ya pili nayo ilikuwa ivyo ivyo mpaka inafika wiki ya tatu alikuwa yupo hoi bin taaban! Amechoka sana.
Siku hiyo akiwa ametoka bafuni kuoga anajiandaa ili kurudi mkoani Dar es salaam alikuta ujumbe wa video kwenye simu yake kupitia mtandao wa Watsap kisha kuufungua, hakuamini alichokiona, hakuamini baada ya kumuona Catherine yupo uchi wa mnyama tena anafanya mapenzi na wanaume wawili kwa mpigo,wakati mwingine alidhani anaota yupo Ndotoni na angeshtuka,mambo aliyoyaona yalikua yana ukweli,alijikuta anakaa juu ya kitanda na kuitizama tena video hiyo kwa mara nyingi.
Alivyojaribu kuipiga namba iliyotuma video ya ngono haikuwa hewani, Moyo ulimwenda mbio sana, wakati mwingine alidhani wenda sio Catherine sababu Duniani watu wawili wawili,
Lakini alivyoivuta picha karibu sana kiunoni aliona kidoti cheusi hiyo ilimaanisha ni kweli alikuwa Catherine mchumba wake.
“Griii Griiiiiiii grriiiiiii”
Risasi zilirushwa kutokea juu ya ndege ndogo zikipigwa chini ya maji alipokuwa ametumbukia Catherine anaogelea kisha baadaye kuzamisha kichwa chake ndani ya maji, bado waliendelea kurusha risasi zao.
“Do not shoot,I said do not shoot, I need her alive, she is an asset”(msipige risasi,nasema msipige risasi,namuhitaji akiwa mzima,huyo ni mali”).
Kauli hiyo ilitoka kinywani mwa Carl Martins akifoka.
Ni kweli alimuhitaji Catherine ili kutengeneza pesa nyingi sana alishaini mikataba juu ya kumchezesha mwanamke huyo filamu za ngono,kumuuwa Catherine ilikuwa ni sawa na kutumbukiza gunia la dhahabu ndani ya chemba la choo, na hakutaka hilo litokee.
Hapo ndipo alipoamuru ndege igeuzwe na kurudi nyuma,wazungu wawili walijitosa kutokea juu ya ndege mpaka ndani ya maji ili kumchukua Catherine,kwani walipewa maagizo kuwa anahitajika akiwa mzima kabisa.
Maumivu ya Bega yaliyosababishwa na risasi aliyopigwa na Mzee Mwasha wakiwa huko visiwa vya Zanzibar akitaka kumuokoa mama yake ndiyo iliyomfanya ashindwe kuogelea vizuri,
Maji ya bahari yaliyokua na chumvi ndiyo yaliyomfanya asikie maumivu mengi sana,licha ya yote hayo kutokea hakutaka kukata tamaa alizidi kupiga mbizi akiyakata maji huku akitingisha miguu yake, aliibua kichwa chake juu ili kuvuta pumzi kisha kukizamisha tena ndani ya maji ili asonge mbele.
Ilikuwa bora afe kuliko kupelekwa Nchini Germany akachezeshwe filamu za ngono na kuuzwa Dunia nzima,hakutaka hiko kitu kitokee tena kwa mara nyingine hata kama angepewa kiasi cha bilioni mia mbili, aliuthamini sana mwili wake.
Kitendo cha kuibua kichwa chake juu aliona watu wawili wanaogelea tena wanakuja kwa kasi nyuma yake huku juu yake bado ndege ya Carl Martins ikiwa inamfuatilia,hakufika mbali tayari alikuwa amekamatwa, alivyotaka kurusha ngumi alishindwa.
Alipojaribu kujitetea hakuweza baada ya kichwa chake kuchukuliwa na kuingizwa ndani ya maji, aliinuliwa na kutumbukizwa tena, zoezi hilo lilidumu mpaka alipoishiwa pumzi zake na kulegea kabisa na ndiyo hayo yalikua mahesabu yao.
Baadaye kidogo ndege ilishuka kisha kuchukuliwa na kuingizwa ndani,walimfunga kamba mikononi na kumkalisha juu ya kiti.
Ndege ilitembea kwa kasi sana juu ya bahari ya Hindi kisha kupaa angani wakiwa tayari wapo na catherine mikononi mwao!.
Ndege ilizidi kusonga mbele ikiwa angani inakata mawingu,kwa mbali sana Catherine fahamu zake zilianza kumrudia taratibu,
Iakini hakutaka kuyafumbua macho yake kwa haraka,bado hakutaka kukubali kushindwa hata kidogo,
alifumbua taratibu jicho lake moja la kulia na kumuona Carl Martins amelala na baadhi ya walinzi wanakunywa pombe kali, aliwahesabu na kugundua wapo watano kujumuisha na rubani wa ndege,
usiku ulikua teyari umeingia,mahesabu yake yalikua moja kwa moja kwa rubani wa ndege, ilikua ni lazima afanye kitu ili kuikwamisha safari hiyo ya Germany,
Taratibu sana alianza kucheza na kamba za katani alizofungwa mkononi kwa umakini sana, hazikupita hata dakika tano alikuwa keshazifungua na mikono yake kuwa huru na kuanza kuhesabu kimoyo moyo.
“Moja, Mbili, ta…”
Kama umeme alichomoka kwenye kiti mpaka kwa rubani aliyekua yupo bize haelewi chochote kisha kumvaa mpaka kwenye mitambo, alikamata kitu kilichofanana na gia na kuanza kukizungusha, kila alipokizungusha ndipo ndege ilipokua inapoteza muelekeo wake,
Kila mtu alichanganyikiwa baada ya kuona ndege inaenda kombo, Catherine alizidi kubonyeza bonyeza vitu asivyovijua na ndege kuanza kurudi chini kwa kasi sana, hapo ndipo aliposali sala yake ya mwisho kwani chini kulikua kuna msitu uliokuwa na miti mingi sana,
Walipojaribu kumtoa walishindwa haikuchukua hata dakika saba ndege ilianza kujipiga juu ya miti mingi, kila mtu alijigonga gonga lakini kwa Catherine alijishika kwenye kiti kwa nguvu zake zote mpaka ndege ilipogota juu ya tawi la mti mkubwa,
Damu alizokua akivuja mkononi ndizo zilifanya ilegeze mikono yake na kuifanya iteleze,alishindwa tena kujishikilia na kuanza taratibu kwenda chini, alijigonga kwenye kioo na kutoka nje, hapo alijipiga piga na miti na kuporomoka mpaka kwenye matawi puu chini,
Alihisi maumivu mengi sana kwenye paja lake na mgongoni,alivyojiangalia vizuri aliona mti mkubwa umezama kwenye nyama,damu nyingi zilimtoka alihisi maumivu makali mno,
Taratibu alianza kujiburuza kama nyoka mpaka chini ya mti na kukaa huku akilia machozi ya uchungu,
hakuelewa ni wapi alipo zaidi ya kusikia sauti za wanyama pori tena wakali kama simba na Chui.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni