Notifications
  • MY DIARY (36)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA SITATULIPOISHIA...Sasa wewe fikiria mimi niliyeletewa zawadi sikujua ni zawadi gani lakini yeye tayari alishafungua na kuchungulia na kujua nini kilifungwa huko ndani.Basi nikaendelea kumuhudumia yule mama huku na yeye akiniambia kuwa itabidi nikimmaliza hizo zawadi tusifungue hapo hapo na waniimbie wimbo wa happybirthday.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Tuliendelea na stori mbili…
  • MY DIARY (35)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TANOTULIPOISHIA...Tatu niliambiwa kuwa ndugu zake na wazazi wake walihusika kwenye mipango hiyo hivyo walibariki kabisa huyo binti kuniacha mimi mumewe wa ndoa na kuamua mtoto wao aolewe upya. Nne ni kwamba huyo mzungu amewaamishia wazazi wake mjini na amewajengea nyumba ya kifahari.Kwa hiyo mimi ninavyowapigiana simu na kuwajulia hali kumbe wenzangu huwa wananichora tu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (34)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA NANETULIPOISHIA...Hapo nikakumbuka kuwa zile zana zangu za kazi nilikuwa nazo ni vile vifaaa vya kupimia ukimwi ambavyo huwa navitumia kabla ya kukutana na mwanaume yeyote nisiyemfahamu. Nikaamua kumkubalia huku nikiamini kuwa hiyo ndo kinga yangu pekee iliyobaki kama mwanaume huyo atataka kuzini na mimi usiku huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi tuliondoka na kwenda sehemu…
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…

BIKRA YANGU (67)

Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA SITINI NA SABA
ILIPOISHIA...
Taratibu alianza kujiburuza kama nyoka mpaka chini ya mti na kukaa huku akilia machozi ya uchungu,
hakuelewa ni wapi alipo zaidi ya kusikia sauti za wanyama pori tena wakali kama simba na Chui.
SASA ENDELEA...
Mambo yanayomtokea katika maisha yake hakuelewa mkosi huo alipewa na mtu gani,aliuangalia mguu wake jinsi mti ulivyoingia na nyama zake kutokeza nje,licha ya yote maumivu ilibidi asonge mbele na kuiokoa nafsi yake na siyo kukaa chini ya mti na pengine kuwa kitowewo cha wanyama.

Alivua shati lake la juu kisha kulichana kidogo,

Alichukua kipande cha mti na kukiweka mdomoni ili asiweze kuung’ata ulimi wake kwa jambo analoenda kulifanya.

Alivuta pumzi ndefu na kuzishusha kisha kuushika mti mkubwa uliozama juu ya paja lake, kwa nguvu zake zote aliuvuta mpaka ulipotoka na kufanya damu ziruke mfululizo.

“Aaaah!Mungu weeee”

Maumivu aliyoyasikia hakika hayakuweza kuelezeka hata kidogo, lakini ilibidi ajikaze, alichukua kipande cha shati na kukifunga kidonda kilichokuwa kinavuja damu nyingi ili kuzuia isiendelee kuvuja.

Alisimama kwa tabu sana na kuanza kutembea,hakuelewa ni wapi anaelekea Magharibi au Mashariki,kaskazini au Kusini.

Ghafla alihisi parakacha za mtu zinakuja nyuma yake, alivyogeuka alimuona mtu anavuja damu kichwani huku mkononi akiwa na bastola, alikua ni mmoja wa watu wa Carl Martins.

“Stay where you are bitch,you make a step I shoot you(hapo hapo ulipo Malaya,ukipiga hatua yoyote nakupiga risasi”)

Catherine alishakua tena chini ya ulinzi akiwa amewekewa bastola,ilibidi asalimu amri na kuanza kuongozana wote huku wakisonga mbele akiwa anachechemea,bado vita ilikua haijaisha,lakini alipofika mbele baada ya kupiga hatua chache alisimama na kumgeukia Mwanaume aliyeshika bastola.

“Do you want to kill me?”(unahitaji kuniua)

“if you wont cooperate, I will kill you”(kama hautoonesha ushirikiano,nitakuua)

“No!,you are lying if you wanted to kill me, I would be dead already,go ahead and pull the trigga, I said go ahead and pull the trigga(Hapana,sio kweli,kama ungehitaji kuniua,ningekuwa nishakufa tayari,fanya ivyo nipige risasi,nasema nipige risasi”)

“Move,”(songa)

“No I can’.t(hapana siwezi).

Catherine alishachezwa na machale kuwa alihitajika akiwa hai ivyo mtu aliyemuwekea bastola hakuwa na uwezo wa kumdhuru, alikua ni kama nyoka asiyekuwa na meno.

Alizidi kufoka kwa sauti ya juu huku akiyabana meno yake wakianza kulumbana, alimsogelea mpaka karibu ya bastola na kutegesha kichwa chake ili apigwe risasi.
“Pull the triga”

Alifoka Catherine kwa ujasiri na kurudisha kichwa chake nyuma kwa nguvu na kukirudisha kwa kasi mpaka juu ya pua za jambazi huyu aliyekua mbele yake na bastola.

Aliyumba yumba kutokana na maumivu makali mpaka chini chali hapo hapo.

Catherine hakufanya makosa alichukua bastola na kumfyatua na risasi ya utosi,

Alishusha pumzi ndefu baada ya kuiweka bastola kiunoni vizuri akielewa kuwa ndiyo itakayo kuwa msaada kwake huko mbeleni na kuanza kusonga mbele kwa tabu sana ndani ya msitu huo mnene ambapo kulikua kuna giza nene,

Nguvu zilimuishia na kukaa chini tena ya mti mkubwa na usingizi mzito kumchukua,

Kilichomshtua asubuhi ni muungurumo wa simba kwa mbali,alizidi kuyatoa macho yake na kutega sikio kwani sauti hiyo ya mnyama huyu mkali ambaye akiunguruma lazima wanyama wote wakimbie ilikua karibu sana,

Hakuamini baada ya kugeuza shingo yake nyuma na kumuona simba mkubwa akiwa anaunguruma, dalili zilionesha kuwa alikua na njaa sana,

Taratibu alianza kumsogelea, Catherine alijaribu kujiburuza kurudi nyuma kisha kutoa bastola iliyokua kiunoni ili kumuuwa simba aliyekua anakuja kwa kasi mbele yake.

“karakacha karakacha”

Mlio wa bastola ulioashiria kuwa hakuna risasi ndani ya chemba baada ya kutaka kufyatua risasi ulimfanya Catherine azidi kuingiwa na hofu,hakua na matumaini tena ya kupona simba alikua teyari mita chache na kuinua miguu yake ya mbele kisha kumvaa Catherine aliyekua chini amelala

Hakuwa anawaza kitu kingine zaidi ya kusubiri kifo chake alichojihesabia kuwa ataliwa na simba huyo mkali ambaye teyari ameupanua mdomo wake akijaribu kuingiza meno yake ndani ya shingo ya Catherine,

Japokua alikua hana nguvu za kutosha lakini ilimbidi ajaribu kujitetea,aliyakumbuka vizuri mafunzo ya Baba Abushiri jinsi ya kupambana na wanyama wakali wa porini kipindi yupo Demokrasia ya Kongo baaada ya kunusurika na majangili waliodhani kuwa yeye ni Raia wa Rwanda,

Bado alipiga moyo konde na kurudisha fikra zake nyuma haraka haraka kama umeme na kumkamata simba shingo kisha kumkumbatia kwa nguvu zake zote,na kuanza kubiringika naye, alishaelewa kuwa kitendo cha kumuachia mnyama huyu Mkali ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yake kwani alishapandwa na hasira na kuanza kuunguruma kwa sauti sana,

Kucha alizokuwa anarusha simba zilimfanya Catherine apate majeraha mengi na damu kumvuja mwilini kama maji, alihisi maumivu makali sana lakini hakutaka kuiachia shingo ya simba huyo.

Licha ya kujitahidi sana alionekana kuzidiwa nguvu na kuchoka kabisa, hapo ndipo aliposali sala yake ya mwisho na kudondoka chini,

Aliyafumba macho yake baada ya kumuona Mnyama huyo anapanua tena midomo yake na kuiweka usawa wa mbavu zake.

“paa paaaa”

Kilichosikika hapo ilikua ni milio ya gobole hakuelewa ilisababishwa na nini, Damu zilitapakaa alishindwa kumtoa Simba aliyekuwa juu yake amekufa tayari baada ya risasi mbili kupenya ndani ya tumbo lake, Watu wanne walitokea mbio mbio na kumbeba simba huyo kisha harakaharaka kuanza kumchuna ngozi yake,

Walimtizama Catherine na kuanza kuongea Lugha isiyoeleweka.

Catherine hakuwa na nguvu tena, nguvu zake zote alizimaliza kwa Simba aliyekuwa akipambana naye dakika mbili zilizopita,

Alikua akihema kwa shida alichokuwa akihitaji kwa wakati huo sio kitu kingine bali ni msaada wa kutolewa katika pori hilo lenye wanyama wakali.

“He…lp me”(nisaidie)

Alisema Catherine kwa tabu sana.

Sauti ya jitu moja jeusi lilisikika likiongea na wenzake kwa lugha isiyoeleweka kisha kumchukua Catherine na kumbeba mpaka ndani ya gari huku wakiwa wameshika ngozi ya simba,gari lilijaa pembe za Tembo na Ngozi za simba kwa harakaharaka Catherine alishaelewa watu hao ni majangili wanaoiba wanyama, lakini hakutaka kufanya lolote alichohitaji yeye ni kujikwamua na kutoka kabisa msituni.

Landrover iliyokuwa imelemewa na mizigo ilianza kusogea mwendo wa kinyonga likipita pori kwa pori,walisita kidogo baada ya kusikia muungurumo wa gari, haraka waliingiza gari porini ili kujificha walivyohakikisha kuna usalama waliendelea na safari kisha ilivyofika mchana waliegesha gari pembeni ili wasubiri usiku uingie na wasonge mbele.

Kweli walifanikiwa kujificha mpaka giza lilipoingia na kuanza kutembea porini bila ya kuwasha taa za gari lao kwa takribani lisaa lizima baadaye!.

Ghafla walisikia tena muungurumo wa magari unakuja nyuma yao huku likimulika taa zake, walivyotaka kukimbia waliwekwa chini ya ulinzi na jeshi linalolinda msitu.

Kisha kuwatoa wote nje ya gari.

Catherine alitetetemeka sana kuliko maelezo yaliyojitosheleza aliogopa sana, walimchukua na kumlaza chini chali akiwa na kamba zake,

dalili zilionesha kuwa walidhani ni jangili vile vile.

Jeshi la kulinda misitu halikuwa na masihala hata kidogo walishakoki mitutu yao na kuanza 

kuwamiminia watu hao waliokuwa majangili wanaiba wanyama pori.

walimfuata Catherine na kumuwekea bastola utosini ili wamuuwe hapo hapo.

“Msimuuwe”

Alitoa kauli hiyo mkuu wao wa kikosi kwa Lugha ya kwao.

“Kwanini?”

“Nimesema msimuuwe”

“sasa tumfanye nini?”

“tuondoke naye”

Hiyo ndiyo ilikua ponea ya Catherine ambapo tayari alidhani ataenda kufa dakika mbili baadaye,
Walimvuta mpaka ndani ya gari kisha kuondoka naye.

Safari ilidumu kwa masaa mawili tangu walipokuwa ndani ya msitu huo mpaka kwenye kambi ya maaskari hao waliokuwa muda wote wanamtizama Catherine kwa macho ya Matamanio.

Walifika kambini na kumshusha mpaka ndani ya chumba kidogo ili wampe huduma ya kwanza kwani alikuwa na majeraha mengi sana.

Walianza kukitibu kidonda chake cha mguuni kwanza kisha baadaye kumpaka dawa mgongoni mwake uliokuwa na majeraha ya kucha za Simba,

baada ya hapo walimpatia chakula ale kisha baadaye kumpa Maji anywe.

“Do you speak English?”(unaongea kiingereza)

Aliuliza muuguzi wa kike aliyekua anamtibu majeraha yake.

“Yes I do(ndio ninaongea)

“My name is Caroline, what is you are name(jina langu ni Caroline,unaitwa nani?)

“Catherine”

“Where do you come from?”(unatokea wapi)

“Tanzania”

“Ohh Tanzania”

Catherine alijibu kila swali aliloulizwa lakini ghafla alitokea Askari na kumtandika kofi zito muuguzi huyo kisha kumsukumiza pembeni na kuanza kuongea lugha ambayo Catherine hakuielewa hata kidogo!.

Lakini kwa haraka haraka alielewa kuna kosa kubwa alilifanya.

Catherine Alichukuliwa na kufungiwa ndani ya chumba kidogo kilichofanana na gereza, humo alikua akipewa chakula na maji lakini alinyimwa kitu kimoja tu uhuru,
lakini bado mpaka siku hiyo hakuelewa ni kwanini yupo mahali hapo na ni kitu gani wanahitaji kutoka kwake.

Akiwa ndani ya chumba kidogo alifikiria mambo mengi sana hususani juu ya maisha yake,ni kweli alipitia mambo mengi sana yenye historia hapo nyuma kilichomuuma zaidi ni Enock mchumba wake, moyo ulimuuma sana alipomkumbuka Mama yake mzazi pamoja na Mdogo wake Christopher ambao alifunga safari ya kwenda kuwakomboa huko visiwa vya Zanzibar matokeo yake kujikuta mahali asipopajua.

Siku zilizidi kusonga bado akiwa mateka lakini Chakula na Vinywaji kila kitu alipewa.

“Heii,Heiii please help Me(tafadhali naomba msaada)”

Alisema Catherine baada ya muuguzi aliyemsaidia kipindi cha Nyuma kupita nje.

Licha ya kuita Muuguzi huyo alimtizama na kuondoka zake dalili zilionesha kuwa alikuwa akihofia kitu na kuogopa kumsaidia Catherine ambaye alikua akiomba msaada kwake.

“Please don’t leave me(tafadhali usiniache)

“No I can’t(hapana siwezi)

“Please I need help, I know you can(tafadhali naomba msaada najua unaweza)

Catherine alizidi kupiga kelele za msaada bila mafanikio ya aina yoyote ile.

Baadaye walisikia muungurumo wa magari nje,kisha kuingia wanaume nane walioshiba na mwanaume mmoja aliyewekwa mateka, alichukuliwa na kupigwa risasi hapo hapo kisha Catherine kufunguliwa ndani ya chumba kidogo alichofungiwa kilichofanana na selo kisha kuwekewa bastola kichwani tayari kwa kuuliwa.

“Embu subiri kwanza msimuuwe”

Alisema Mkuu wao akiongea kwa Lugha isiyoeleweka.

“kwanini mkuu hapaswi kuishi huyu Binti sasa aishi ili iweje?”

“Nasema asiuliwe kuwa mwelewa, hivi tangu lini umeanza kukiuka amri ninayo toa mimi?,hiko kiburi umekitoa wapi?”

“Samahani Mkuu sikuwa na nia mbaya kuuliza”

“haya nasema tena asiuliwe mleteni hapa”

Majasho yalimtoka Catherine sala ya Mwisho aliyokuwa akisali kwa Mungu wake ili atende miujiza hakika ilifanya kazi kabisa, japokuwa hakuelewa ni kitu gani walikuwa wakizungumza kwa wakati huo!.

Alizidi kumuomba Mungu wake aliye juu mbinguni atende miujiza sababu hakuwa na nguvu nyingine ya kujitetea.

Alichukuliwa na kupakiwa ndani ya gari mpaka walipofika umbali wa kilomita tisa mbele, kisha kuegesha gari pembeni ambapo Catherine alishushwa na kuingizwa chumbani.

KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

15 Bikra Yangu Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni