BIKRA YANGU (68)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Alichukuliwa na kupakiwa ndani ya gari mpaka walipofika umbali wa kilomita tisa mbele, kisha kuegesha gari pembeni ambapo Catherine alishushwa na kuingizwa chumbani.SASA ENDELEA...
Alikitizama chumba hiko kilivyokuwa kidogo chenye kitanda kidogo juu yake, hakuelewa ni kitu gani kinafuata, ilivyofika katikati ya Usiku mtu aliyemleta mahali hapo alitokea na kuanza kuvua nguo zake mwilini mwake.
Kisha kuufunga mlango na kumuendea Catherine aliyekua amekaa kitandani,
Hisia kali za kufanya Ngono na Catherine zilimpanda, baadhi ya maungo yake ya mwili yalisimama baada ya kumuona mwanamke huyu mzuri aliyekamilika kila idara, udenda ulimtoka na kuanza kumvuta asogee upande wake,
Catherine alivyotaka kupiga kelele alipigwa kofi zito na kumfanya atulie kimnya.
“Do you want to fu*** me?”
Aliuliza Catherine kwa sauti ya chini huku akitoa nguo zake za juu na kumfanya mwanaume huyo aliyekuwa na uchu asiweze kutumia nguvu za aina yoyote ile.
Udhaifu wa mwanaume siku zote ni mwanamke Catherine alilijua hilo, ilimbidi atumie akili ya ziadi ili aweze kujinasua katika mdomo wa mamba,
Alimvuta Mwanaume huyo kitandani kisha kuanza kumshika kifua chake akitumia mikono yake laini kabisa.
Mwanaume aliyeitwa Ngodu alikuwa hoi yupo mbali sana kihisia ameyafumba macho yake.
Catherine alimvua mkanda kisha suruali kufuata alivyohakikisha kalegea kabisa alichukua mkanda na kuuzungusha shingoni kwake kwa haraka huku akiwa ameikaza mikono yake.
Lakini alijikuta yupo chini baada ya Ngodu kumtupa pembeni,alikua ni mwenye misuli na nguvu nyingi alimfuata Catherine kwa hasira na kumuinua na kumzaba kofi zito, Catherine alidondoka chini na kujibamiza kwenye stuli kisha kutulia tuli.
Mwanaume Ngodu mwenye misuli mikononi alipiga hatua mpaka alipolala Catherine lakini kabla ya kumfikia, Catherine aliinuka ghafla na kuishika miguu yake miwili na kuivuta na kumfanya adondoke na kubamiza utosi wake nyuma ya kitanda juu ya mbao,hapo Catherine hakutaka kufanya makosa.
Alimfuata na kumkaba shingo yake na kuivunja hapo hapo,alichungulia nje dirishani ili kujua usalama.
Aliinama kidogo na kuangalia ndani ya suruali ya Mwanaume maiti aliyekuwa chini hana kauli huku akivaa nguo zake, na kuchukua simu kisha kuanza kubonyeza bonyeza akijaribu kuikumbuka namba ya Enock mchumba wake ili amwambie kuwa yupo salama salmin,lakini hakuelewa endapo akiulizwa ni wapi alipo atajibu nini.
Alibonyeza bonyeza namba kisha kuweka simu masikioni.
“Halloo Enock mimi Catherine”
Alisema Catherine baada ya simu kupokelewa upande wa pili.
“Catherine yupi?”
Moyo ulimwenda sana kasi Catherine na kuanza kutetemeka hakuamini alichosikia upande wa pili wa simu kuwa ni sauti ya mwanamke tena anaongea kwa kujiamini,wakati mwingine alidhani wenda amekosea namba,lakini namba ilikua sahihi baada ya kutoa simu masikioni mwake na kugundua ilikuwa ndiyo namba za Enock mchumba wake..
“Weeeka biaaa nyingineeee hapo,usinitumbulie macho binti”
“Pesa kwanza kaka”
“pumbaaaavu wewe,Mimi huwa nakunywa kwa biliii hapa niangalie vizuri kwa umakini,”
“Nishakuangalia!”
“Basi!.. Then Go and add me Another bottle now now!, before I call your boss, I know you not gonna like it(sasa nenda na uniongeze chupa moja sasa,kabla sijampigia bosi wako,najua hutopenda)
“Mhh!”
Dada huyo mhudumu aliguna kisha kuondoka zake,Kwa haraka haraka kilikua ni kiingereza cha kimarekani ndiko kilichomchanganya akili yake,
alimuendea mpaka meneja wake na kumueleza kila kitu.
“Umesema kuwa hataki kulipa?”
Aliuliza Meneja aliyeitwa Massatu.
“Ndio hataki kulipa, na ana deni la elfu themanini”
“yuko wapi?”
“yupo kule”
“subiri nikamuoneshe adabu”
Meneja Masatu alifunga mahesabu kisha kumuendea Mteja aliyeambiwa kuwa ni mbishi kulipa deni la vinywaji alivyokunywa.
“oyaa amka amka!”
“Mmeleta Bia?”
Kitendo cha mwanaume huyo mlevi kuinua kichwa chake kilimfanya Massatu ashtuke sana, hakutegemea kuwa aliyekuwa akilewa pombe ni Enock Mwasha.
Alimfahamu vizuri sana tajiri huyo sababu mke wake ni miongoni mwa wafanyakazi wake katika kampuni ya Nissani, hakuelewa ni kitu gani kimemkumba mwanaume huyo mwenye heshima zake,
siku zote alimuheshimu kwa sababu tu ya roho yake nzuri ya kuwasaidia watu, hakuwa na ubaguzi wowote wa rangi, uwe mweusi au mweupe mfupi au Mrefu!
Kwa kumuangalia haraka haraka Massatu aligundua kuwa Enock ana tatizo kubwa tena ana hitaji msaada wa kimawazo na sio pesa sababu pesa alikuwa nazo pengine ni nyingi hata punda asiweze kuzibeba.
“Mr. Enock”
Aliita Massatu na kumfanya Enock amtizame na kucheua.
“Niletee bia kwanza na Red wine kishaaa tuzungumze, I have problems my friend, a lot of problems, wewee ni Masaaaatu kama sijakosea Mume wa Blandina, Yes yes nipo sahihi kumbu kumbu zangu zipo vizuri sana kama jiniasi, sijalewa Ha haaaa haaaaaaaaa!”
Enock alichanganya na kiingerza akijaribu kumueleza Masatu kuwa ana matatizo mengi sana pengine anahitaij msaada.
Pombe ililetwa kisha kumtizama Masatu kwa kitambo.
“I know kwamba it is hard for you to believe lakini wacha nikueleze, tafadhali naomba utunze hii siri na unishauri sababu kitendo cha wewe kwendaa and spread to every one utakuwa umeniweka bila nguo”
“sawa ninakuhaidi sitosema kwa mtu yoyote”
“Ni kuhusu Mchumba wangu unaamfahamu nadhani?”
“Ndio Catherine kama sijakosea”
“Huyo huyo,Yule Mwanamke ni mchafu Malaya sana,kumbee anacheza sinema za Ngono Motherfuck*** nikimkamata lazima nimuuwe kwa mikono yangu kisha namimi nifee,nisikilize siongei kwamba nimelewa NOOO…..
“Ujue Mungu ni wa ajabu sana,kanionesha kila kitu, each and everything alafu mimi ni muhuni, nimeishi Marekani Miami pale nimeishi nimekaa na balck Americans,najua michezo yote ya kimafia”
“Mr. Enock sijakuelewa”
“Hujaelewa nini, pumbavu nawewe.Catherine ni Malaya mchafu ameondoka kurudi kucheza Sinema za Ngono”
“Sio kweli”
Hapo ndipo Enock alipozama mifukoni na kutoa simu kubwa kisha kumkabizi Masatu nayeye aweze kujionea, lakini kwa sharti moja awe msiri juu ya hilo.
Massatu alibaki kinywa wazi hakuamini kama Catherine mwanamke anayejishemu kujiingiza katika maswala hayo,hakuelewa ni kitu gani alikosa kutoka kwa Tajiri Enock.
“Kumbe Dad alikuwa sahihi kabisa,inabidi nikamtoe gerezani ili tuunge nguvu zetu tumsake huyu mwanaharamu, hawezi kuharibu familia yetu!”
Hayo yalimiminika kichwani mwa Enock.
Chuki dhidi ya Catherine ilizidi kujilimbikiza mara dufu ndani ya moyo wa Enock, alijuta sana kuwa na Catherine badala ya kumtafuta sasa ili wapatane na wafunge ndoa aliapia endapo akimtia mikononi atamuuwa kwa mikono yake,japo Anderson Peter alipingana naye vikali juu ya mawazo yake, lakini hakumsikiliza mpaka wakafikia kugombana na kutukanana matusi ya nguoni bila kujali uzito, hakuwa na maelewano tena na Anderson Peter rafiki yake kipenzi,alijua wote ni wale wale, alitamani siku hiyo hiyo Catherine atokeze na amuuwe ampoteze duniani ikiwezekana baada ya hapo nayeye ajitie kitanzi.
Dunia aliiona chungu mwanamke ambaye aliyejitolea kukinga kifua mbele ili apigwe risasi na Baba yake leo hii kagundua kuwa ni Malaya tena Gwiji na mcheza Ngono maarufu.
Hilo alilithibitisha baada ya kuingia mitandaoni na kukutana na picha nyingine chafu sana za Catherine ambazo amepiga na wanaume akiwa uchi wa mnyama hana hata nguo moja tena akiwa katika tendo la ndoa kaingiliwa,
Mtu kama Enock mwenye heshima zake hakupaswa hata kuwa karibu tena na mwanamke huyo.
Ni picha ambazo hakutaka kuziangalia mara mbili juu ya macho yake maana zilimuumiza sana!
Aliamua kunywa pombe na kulewa kabisa kila kukicha,aliona Dunia ya mapenzi imemkataa, moyo wake ulichanika chanika na kuvuja damu nyingi sana,
Starehe yake ilikua pombe, alikuwa habanduki vilabu vya pombe,haikupita hata siku kadhaa akabatizwa jina na kuitwa Chapombe.
Marafiki waliomuheshimu walimtenga na kumtupilia mbali,hawakuweza kukaa na mtu mlevi.
“Hatuwezi kukaa na walevi,mimi ni mtu na heshima zangu Raphael,Enock ni mlevi na anadaiwa na bank million saba,nina uhakika atafilisika tu”
“Hata kama ni mlevi haina maana ya sisi kumtenga yule ni rafiki yetu isitoshe katusaidia sana, haina maana ya sisi kumuacha ateseke, ana matatizo makubwa sana”
“khaaa!..kwani nani hana matatizo,kila binadamu ana matatizo yeye siyo wa kwanza kupata matatizo na wala hatokuwa wa mwisho. Mimi naondoka, wiki ijayo mwambie ile million saba inatakiwa”
Kila mtu alimzungumzia vibaya Enock, wengi walishatabiri kuwa baada ya miezi mitatu tu atakuwa mzigo kwa watu na atafilisika vibaya mno yaani ataangukia pua!
Hiyo ilikuwa kinyume kwa msichana mdogo wa makamo kati ya miaka ishirini na tano mpaka ishirini na saba aliyeitwa Dorothea, huyu aliajiriwa na Enock miaka mitatu iliyopita kama hafsa manunuzi, muda mrefu sana alitamani kujua nini tatizo la Bosi wake Enock,alijua kabisa ni mwanaume anayeteseka na kitu Fulani, alitamani kuuliza lakini hakujua aanzie wapi, Alikua ni mchapakazi sana tangu aingie katika ofisi za NISSAN haikuwahi kupata hata hasara ya shilingi tano kama hapo miaka ya nyuma,
Enock alimpandisha cheo na kuwa Mkurugenzi Msaidizi, aliendelea kuongeza sana juhudi katika kazi yake,
Alilelewa katika misingi imara ya kumjua Mungu na wakati mwingi akimaliza kazi zake basi pembeni yake hushika Biblia na kuanza kusoma habari za Yesu Kristo.
Alijua kabisa Enock anahitaji mshauri, kila hatua aliyopiga Enock basi Dorothea yupo nyuma yake.
Siku hiyo asubuhi na mapema Enock aliingia macho yake yakiwa mekundu huku akiwa anayumba sana amelewa mpaka ofisini kwa Dorothea!
“Nahitaji Laki tisa sasa hivi Dorootheaaa, nina kiu sana ya bia Mama”
Dorothea BADALA ya kumjibu alimtizama bosi wake akimuonea huruma, aliamini kabisa ni pepo mchafu ndiye anamuongoza na wala sio kitu kingine.
“Usinitumbulie Machoo kama mjusi kafiri, nipatie pesa hizo”
“Bosi zipo bank, ndiyo nimepeleka sasa hivi” Alidanganya!
“okay,nipe elfu hamsini yako nitakulipa hapa sina hata dala mfukoni mwangu..changamka basi”
Dorothea alizamisha mkono wake ndani ya mkoba kisha kutoa noti tano za rangi nyekundu na kumkabidhi Enock bosi wake.
Aliondoka kwa kupepesuka na kuingia ndani ya gari lake badala ya kuliwasha alianza kulia mwenyewe,huku akipiga piga usukani, alishaelewa kabisa kuna utofauti mkubwa sana katika maisha yake,alijionea huruma na kupata simanzi ndani ya mtima wake alimchukia sana Catherine, hapo hapo usingizi mzito ulimchukua, aliyemshtua alikuwa ni Dorothea akigonga kioo cha gari!
“Bosi vipi?”
“Safi tu, saa ngapi sasa hivi?”
“saa kumi jioni”
“Hapana sio kweli ina maana nimelala kiasi hiko?”
“Ndio bosi nenda kapumzike tu nyumbani .lakini….”
“Nini Dorothea?”
“kuna jambo nataka kuzungumza nawewe bosi tafadhali naomba uniruhusu”
“Jambo gani hilo?!”
“Ni mambo mengi sana”
“Sawa ingia ndani ya gari”
Dorothea aliingia ndani ya gari!
“Nakusikiliza”
“Ni maongezi marefu sana,naomba tutafute sehemu tuongee”
“sawa twende kwangu”
Enock aliwasha gari mpaka nyumbani kwake.
Kwa mara ya Kwanza Dorothea kufika nyumbani kwa Bosi wake alistaajabu sana kuona jumba kubwa la kifahari mbele yake iliyojengwa kisasa, aliyalinganisha mambo anayofanya bosi wake ya ulevi na hayakuendana kabisa na wadhifa wake.
Walifika nyumbani na kuingia ndani huku Enock akiwa ametangulia mbele na kufungua mlango,
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni