BIKRA YANGU (69)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA SITINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Kwa mara ya Kwanza Dorothea kufika nyumbani kwa Bosi wake alistaajabu sana kuona jumba kubwa la kifahari mbele yake iliyojengwa kisasa, aliyalinganisha mambo anayofanya bosi wake ya ulevi na hayakuendana kabisa na wadhifa wake.
Walifika nyumbani na kuingia ndani huku Enock akiwa ametangulia mbele na kufungua mlango,
SASA ENDELEA...
Nyumba nzima ilinuka pombe kali sana, haikuchukua muda kwa Dorothea kutambua kuwa Bosi wake ndiye aliyekuwa anatumia vilevi ivyo vikali sana.
“Unatumia pombe Dorothea?”
“Hapana Bosi hata siku moja sitoweza”
“okay,ngoja nikuletee juice”
Enock alimkabidhi Dorothea Glass ya Juice huku yeye akiwa na yake ya pombe kali,
alibwia glass ya kwanza na kuisha aliongeza nyingine mpaka mzinga wa pombe kali ya VALUER kuisha yote kisha kuongeza nyingine, Dorothea aliogopa sana.
Enock alianza kuongea maneno ya ajabu yasiyoeleweka huku mara kadhaa akitaja jina Catherine akimlaani sana,kisha kulala papo hapo.
Ghafla simu ya Enock iliita usiku huo na Dorothea kuipokea yeye, alikunja sura yake baada ya kugundua ndiye Catherine aliyepiga simu...-
Moyo ulimuuma sana na kuzidi kusonga mbele hakuelewa ni wapi alipo,
Mvua na jua vyote vilimuishia mwilini mwake alipata mateso zaidi,njaa ilimuuma sana.
Alimchukia sana Enock kwa kumpa msichana wake aongee naye na akamtukana akimwambia kuwa yeye ni changudoa tena anayejiuza na hana thamani, japo hakuisikia sauti ya Enock, Mwanamke aliyeongea naye kwenye simu muda mfupi uliopita ndiye aliyemwambia maneno hayo yote,
alijiona ni mwanamke mwenye mkosi mapenzi.
Aliwakumbuka wanaume wote waliomtenda hapo nyuma alimkumbuka vizuri sana Darlington Shebby mwanaume aliyedhani kuwa atakuja kumsahaulisha kila kitu kilichotokea, kumbe yalikua ni yale yale, alijutia sana kurudiana na Enock ki ujumla alijichukia kupita kiasi.
Aliuona mwili wake hauna thamani tena hasa alipokumbuka jinsi alivyoteseka akichezeshwa filamu za Ngono na kusambazwa mitandaoni, hakuelewa kuwa atakuja kuwa mgeni wa nani.
“Lakini kwanini mimi?” Alijiuliza Catherine huku akitembea barabarani, alikuwa kama mwendawazimu, nywele zake chafu na nguo alizovalia zilitosha kabisa kuonesha kuwa alikuwa mwehu, hakuna aliyemjali walimpita mbali.
Hakuwa Catherine Yule wa miaka ya nyuma iliyopita aliyetishia kwa uzuri wa kipekee na tishio Tanzania Nzima na hata Afrika Mashariki na kati,nchi kama Kenya na Uganda wote walimfahamu na kutuma watu mbali mbali wamtafute ili tu wafanye naye matangazo.
Alisita kidogo alivyoona mbele kuna mama Ntilie akiosha Vyombo, ,bila ya kusema lolote alitembea na kwenda kukaa pembeni yake na kuanza kumsaidia kuosha vyombo, akiamini akimaliza hapo atapewa hata ukoko wa wali ili mradi aweze kupata nguvu na kusonga mbele.
Ni kweli baada ya kumaliza kuosha vyombo aliletewa Ugali mkubwa na mboga mboga kisha kuanza kula haraka haraka kama aliyekuwa vitani.
Alimshukuru sana Mama huyo kisha kutaka kuondoka lakini alishikwa mkono.
“Your name?”(jina lako).
“Elizabeth”.Alidanganya!
Baada ya hapo aliondoka zake.
Enock aliamka akiwa amechoka kichwa kinamuuma sana tena yupo kitandani uchi wa mnyama, hakuelewa ni wakati gani alivua nguo zake na kujilaza kitandani, alijaribu kuvuta kumbukumbu zake nyuma kwa haraka, lakini hakupata picha kamili, jambo alilokumbuka alikuwa na Dorothea wanarudi wote nyumbani kisha kuanza kulewa pombe, kilichotokea hapo hakuweza kuelewa tena mpaka alipozinduka asubuhi.
“Nani kanileta hapa kitandani na kunivua nguo zangu? Tangu nianze kulewa pombe sijawahi kulala kitandani”
Hayo ndiyo yalimiminika kichwani mwa Enock akijaribu kukorofisha kompyuta yake ya ubongoni.
Alitoka Mpaka seblen na kukuta Chai ipo tayari tena mezani imeshaandaliwa,
“NIMEKUANDALIA CHAI BOSI FROM DOROTHEA,”
Ujumbe huo aliusoma Enock uliokua juu ya meza.
Ni Dorothea ndiye aliyeandaa kila kitu hapo mezani kwa Kuwa alikua ana njaa alikula kisha kumtafuta kwenye simu.
“Jana nilikunywa sana eeeh?”
“Ndio Bosi ukaamka ukaniaga kwenda chumbani mwenyewe”
“Mimi?”
“Ndio bosi wewe”
“Haiwezekani, basi maajabu mimi nikadhani wenda wewe ndiye uliyenipeleka mpaka chumbani?”
“Hapana nisingeweza,hata chumba chako sikijui Bosi”
“Lakini Ahsante kwa kila kitu Dorothea japo hukuniambia ulitaka kuzungumza na mimi kuhusu nini”
“Jana nilishindwa muda ulikuwa umekwenda,usiku ulikuwa umeingia bosi nikashindwa, alafu isitoshe haukuwa vizuri, Mungu leo akipenda basi nitatoka mapema nije kukuona Bosi”
“sawa Dorothea,nashukuru sana”
Enock alikua ana hamu sana na kitu gani hasa alitaka kuambiwa na Dorothea,Muda ulisogea mwendo wa kinyonga Mzee.
“Lakiini mimi sindo bosi wake ndiye niliyemuajiri kwanini asije sasa hivi”
Enock aliwaza na kupiga simu kwa Dorothea tena.
“Njoo Nyumbani sasa hivi”
“lakini bosi kuna kazi nyingi leo”
“Achana nazo mpe Blandina”
“sawa Bosi, lakini kwako sipakumbuki vizuri”
Ilikuwa kazi rahisi kumuelekeza Dorothea mpaka nyumbani kwake.
Nusu saa baadaye Dorothea aliwasili ndani ya jumba la Enock kisha mlinzi kumfungulia mlango.
Kama kawaida Enock alimtolea Juice na kumkabidhi nayeye kuchukua pombe kali na kuanza kunywa.
Dorothea hakuelewa ni wapi aanzie kumuuliza bosi wake hakuwa ana uhakika kama anachotaka kumshauri kingewezakana au kuzaa matunda.
“Nakusikiliza Dorothea”
“Bosi”
“Naam nakusikiliza”
“Naelewa una matatizo makubwa sana pia naelewa mambo mengi hayanihusu pengine, lakini nilikuwa naomba unishirikishe ili namimi niweze kukusaidia,Mimi ni Mtumishi wa Mungu kwa Maombi tu nina uhakika utafunguliwa
“Nina amini huyo ni shetani ndiye anayekujaribu na kwa Yesu haya yote yanawezekana”
Enock alimsikiliza kwa umakini badala ya kujibu alibaki kimnya akimtizama huku akiendelea kupiga mafundo ya pombe kali.
“Umechelewa sana”
“Hapana Kwa Yesu hakuna kitu kama hiko, naomba unieleze”
Dorothea alisisitiza.
Enock Alimuamini sana Dorothea kutokana na upole wake hapo ofisini kwake, hapo ndipo alipoanza kumpa historia ya Catherine na mpaka chanzo cha yeye kuwa mlevi kiasi hiko.
“Ni huyu Catherine mchumba wako?”
Dorothea aliuliza kwa mshangao wa waziwazi.
“Ndiyo huyo huyo”
“Pole sana bosi kwa sasa hivi yupo wapi?”
“yupo huko anacheza hizo filamu chafu”
Alijibu Enock na ndivyo alivyoamini.
Dorothea alijaribu kumsihi Enock aweze kumtafuta Catherine na kumwambia kuwa wenda Mungu alimtumia yeye ili ambadili Catherine,lakini kwa Enock ilikua vigumu sana kukubaliana na swala hilo, alimtoa moyoni kabisa Catherine, bado alitamani amuuwe lakini chuki za kumuuwa hakutaka kuziweka wazi kwa Dorothea alibaki nazo moyoni.
Alizidi kupiga mafundo ya pombe huku akimtizama Dorothea kwenye mpasuo wake ulioonyesha sehemu kidogo ya paja lake jeupe tena laini na kwa mwanaume yoyote Yule lijali ilikua ni lazima aibie ibie,ki ufupi Dorothea alikua msichana mzuri tena mwenye umbo dogo ukimuona ungedhani wenda ni binti wa miaka kumi na minane.
Enock bila kusita aliweka mkono wake juu ya paja la Dorothea na kumfanya Dorothea ashtuke sana alimuheshimu sana bosi wake, kwa mara ya kwanza alijua wenda ni bahati mbaya lakini mkono wa Enock ulizidi kupanda mpaka juu karibu kabisa na ikulu, hapo ndipo Dorothea alipotoa mkono wa bosi wake.
“Oooh sorry Dorothea”
Alisema Enock kwa sauti ya kusinzia akiwa tayari yupo bwii!
Kwa pombe kali aliyokuwa anakunywa.
Hapo hapo alianza kumtukana tena Catherine akizidi kumlaani.
Usiku ulikuwa mnene sana macho yake yalimlegea aliona vitu viwili viwili.
“Enock mwanangu unakosea sana”
Sauti hiyo ilimfanya ajaribu kukaza macho yake, kwa mbali sana aliona sura ya Mama yake Mzazi Josephine, akiwa amekasirika sana tena yupo kwenye kochi pembeni yake.
“Mama yaaaangu kipenzi….”
Aliita Adrian na macho yake kuzidi kuwa mazito giza nene lilitawala machoni mwake kisha macho yake taratibu kuzima kama radio mbao iliyokua inaisha mabetri!
Ni saa tatu ya Asubuhi ndipo alipozinduka kitandani baada ya kuangalia saa kubwa ya ukutani,alishtuka tena baada ya kujiangalia na kujikuta yupo uchi wa mnyama hana nguo hata moja,bado hakuelewa mambo yanayotokea.
“Mhhh”
Aliguna baada ya kuona hereni moja ya Dorothea chini.
“Kosa Moja Magoli mia moja”
“Ha! Haa! Haa! Haa! Haaaa! shoga una misemo”
“wahenga walisema Ndondondo si chululu”
“Wacha we, kwanza umefikia wapi mdogo wangu?”
“ukiona maharage yanarukaruka ujue yanakaribia kuiva”
“Embu niambie hatua uliyofikia,maana ni muda mrefu kwelikweli hujanipa michapo Mdogo wangu”
“Mambo yanakaribia sasa wewe usijali”
Maongezi hayo yalifanyika Gerezani huko Segerea siku maalumu ya kuona wafungwa.
Naomi japo alikuwa miongoni mwa wafungwa lakini muda wote alikuwa ni mwenye furaha kuliko mfungwa yoyote yule,furaha yake ilichangiwa na vitu viwili kimoja ni kugundua leo hii Dorothea ni mdogo wake pili ni Dorothea kukubali vile vile kuwa naye bega kwa bega ili wamkomoe Enock na Catherine ikiwezekana wawauwe kabisa.
Baba yao Mzee MASUNGA alikuwa ni tishio la kuogopeka miaka ya tisini iliyopita, alikuwa ni miongoni mwa Wauza madawa ya kulevya akiyasambaza nchi za Israel,china na mpaka Amerika ya Kusini na JAMAICA vile vile, alikua ana mtandao mkubwa sana,aliiishi na mke wake Janeth wote walishirikiana wakiishi Kenya Mombasa japo asili yao ilikuwa Tanzania,hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kuwashtukia kuwa familia hiyo inajihusisha na biashara haramu iliyopigwa vita nchi zote karibu Dunia nzima lakini walijikinga na mwavuli wa Dini ya kilokole, tena Mzee Masunga alikuwa ni mwenyekiti wa kanisa kubwa huko Elidoreti akitangaza Injili,hapo alifanikiwa kuwapumbaza watu wote, aliposimama madhabauni mamia na maelfu walifurika viwanjani na hata viwanja kutapika.
Kizuri zaidi alishirikiana na watu wa serikali walikuwa wakimtuma nchi tofauti kama Israeli kutangaza dini lakini akirudi basi ndani ya begi lake alijaza madawa ya kulevya aina ya Coccaine na Herroin.
Habari nzuri zilizomfurahisha ni baada ya mke wake kujifungua Mtoto mwingine wa kike huyu walimpa jina Dorothea, alikuwa ni mwenye afya alipendwa na kila mtu, kila alipoenda baba yake basi Dorothea yupo mkononi, alimpenda kuliko Naomi ambaye kipindi hiko alionesha kuwa kiburi na sio mtiifu.
Baba yake alimchukia sana.
Mafanikio ya Masunga yalizidi mara mia moja, serikali ilianza kumuhisi vibaya lakini Raisi wa Kenya alimtetea.
“Inawezekana vipi bwana,come on huyu ni mtumishi wa Mungu,amepewa utajiri na Mungu kama Ayubu”
Ivyo ndivyo Raisi Okello alivyomtetea Masunga kila alipotaka kuguswa.
Miaka Mitano baadaye! Raisi Okello alipinduliwa na ndiyo hapo Maisha ya Masunga yaliingia dosari na kukosa muhimili,serikali ilimfuatilia kila kona anayokwenda, ‘Mungu hadhiakiwi’ alikamatwa nchini China mji wa Hongkong akiwa na kete mia tano za madawa makali aina ya Herroin kwenye begi lake la Biblia, hakuna mtu aliyemtetea alipelekwa jela siku hiyo hiyo na kusubiri kunyongwa na ndiyo iyo sheria ya iliyowekwa na Serikali ya China.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni