SEHEMU YA HAMSINI
ILIPOISHIA...
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kumuona damu zikiwa zinasambaa chini, zikitoea kwenye kichwa cha Regna.Kwa haraka nikavuta Rahma kwa nguvu zangu zote na kumzuia kuendelea kumpigiza Regna kichwa chake chiniSASA ENDELEA...
“Achaa,”
Nilizungumza huku nikimbeba juu juu Rahma na kukandamiza ukutani, tangu nianze kumjua Rahma sikuwahi kumuona akiwa na hasira kiasi hichi, Nikaendelea kumkandamiza Rahma ukutani, tukiwa tunatazama kwa ma-cho makali, kidogo hasira yake ikaanza kumtulia.
Nikageuka nyuma na kumtazama Regna nikakuta akiwa ametu-lia kimya huku damu zikiendelea kusambaa kwenye sakafu, nikamfwata kwa haraka sehemu aliyo lala na kuki-weka kiganja vhangu kifuani mwake na kukuta mapigo yake ya moyo yakiwa yametulia kimya, nikazidi kuchan-ganyikiwa
“Ameshakufa”
Nilizungumza huku nikimtazama Rahma ambaye mwili wake wote unamtetemeka kwa woga
“Rahma umeua”
Niliendelea kuzungumza huku nikimpima mapigo ya moyo Regna ila hapakuwa na msukumo wowote, wa mapi-go ya moyo ulio endelea kwenye kwenye kifua chake, Nikasikia mlango ukigonjwa kwa nje ikiashiria kuna mtu anahitaji kuingia ndani ya chumba hichi
Tukatazamana na Rahma, na hakuna aliye yanyua kinywa chake kusikilizia hodi inayo gongwa, mtu anaye ene-delea kugonga mlango kama dakika tatu hivi kisha akaanza kuita jina
“Regna mke wangu fungua mlango, kuvaa gani masaa kumi”
Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo, ilizidi kuniogopesha, nikapeleka macho yangu kwenye mkono wa kushoto wa Regna na kukuta akiwa amevaa pete ya ndoa akiashiria ni mke halali na huyo anaye gonga mlango
“Wewe mwanamke mimi naondoka zangu, saa utakodi bajaji, nakwenda zangu home kulala muda umesha kwenda”
Jamaa alizungumza na kuzidi kutuchanganya akilia mimi na Rahma, Rahma akataka kuzungumza ila nikawahi kukiweka kidole changu kimoja mdomoni mwangu nikimuashiria kukaa kimya na asizungumze jambo la aina yoyoye.
Nikasimama na kwenda kusimama mlangoni na kuliweka sikio langu kwenye mlango na kusikilizia kama jamaa atakua ameondoka.Nikastushwa na mlango kugongwa, tena kwa nguvu
“Wewe mama Junio, hunisikii humo ndani, au mimi ninaondoka”
Nikameza fumba jingi la mate na kubaki nikimtazama Rahma, ambaye sura yake yote imejaa machozi mengi, akijilaumu kwa kitu alicho kifanya.Nikasikia miguu ya mtu akija, na kusimama kwenye mlango
“Afande Denis mbona hapa?”
“Ahaaa si huyu wifi yeko ameingia humu kutoka, hatoke aliniambia kwamba amekuja kubadilisha nguo”
“Alaa labda ameshatoka, na kama nimepishana naye kule kwenye bustani anakutafuta wewe”
“Ahaaa, atakuwa ametoka saa ngapi?”
“Mpigie simu?”
“Simu yake imezima chaji na ninayo mimi”
“Hembu kamcheki kwenye bustani kule”
“Sawa”
Nikasikia miguu ya watu hao ikiondoka nje ya malango jambo lililo anza kunichanganya na kuhisi kwamba kuna mauza uza yanaendelea kwenye hii nyumba yangu
“Ngoja nakwenda nje mara moja, kaa humu ndani na ufunge mlango kwa nje sawa”
“Unakwenda wapi mume wangu?”
Rahma alizungumza huku akinyanyuka, kutoka sehemu alipokuwa amekaa
“Nimekuambia kaa humu ndani kuna kiitu ninakwenda kukitazama nje sawa”
“Unaniacha peke yangu, humu ndani na hii maiti?”
“Nimekuambia, kaa humu sawa”
Ilinibidi nizungumze kwa ukali kidogo na kumfanya Rahma kustuka na kubaki akiwa amesimama
“Funga mlango kwa ndani na usimfungulie mtu wa aina yoyota zaidi yangu sawa”
Rahma alinijibu huku akitingisha kichwa akionekana kunielewa na kukubaliana na mimi kishingo upande.Nikafungua mlango taratibu na kuchungulia kwenye kordo, sikuona mtu yoyote
“Funga sasa”
Nikatoka haraka, na kumuacha Rahma akifunga kwa ndani, nikapiga hatua za haraka kuelekea nje kwenye bus-tani, nikasimama sehemu ambayo nitaweza kuwaona watu wote waliopo kwenye bustani, ila sikumuona Regna wala mume wake
“Kaka Eddy unatafuta nini?”
Jamaa mmoja aliniuliza baada ya kuniona nikiwa ninapepesa macho yangu kila kona ya bustani yangu
“Kuna dada, hivi ni muandishi wa habari sijui unemuona?”
“Yupoje yupoje”
“Mrefu, kiasi na mwembamba fulani?”
“Huyo atakuwa ni Regna?”
“Eheee huyo huyo”
“Nimemuona akielekea kwenye parking za magari”
“Asante”
Nikaachana na jamaa na kuanza kupiga hatua za kwenda kwenye maegesho ya magari, nikakutana na gari moja aina ya Vitz, ikasimama pembeni yangu na kioo cha gari hilo kikashushwa
“Kaka Eddy, nilikuwa ninakutafuta nikuage”
Sauti ya jamaa ndio sauti ya jamaa aliyekuwa akigonga mlangoni, akimuita mke wake, nikabaki nikishangaa baada ya mlango wa upende wa pili wa dereva ukifunguliwa na akashuka Regna akiwa amevalia kama alivyo kuja kuniomba mara ya kwanza juu ya kuhitaji kuandika story ya kitabu kinacho husu maisha yangu
“Kaka Eddy, niagie kwa wifi yangu, na ile ishu ya story ninakuomba usisahau”
Regna alizungumza na kunifanya nibaki nikiwa nimemtazama kwa mshangao, nikashindwa hata cha kuwajibu
“Eddy, kaka Eddy”
Jamaa aliniita na kunifanya nistuke kwenye bumbuazi ambalo limenikamata gafla
“Yaaaa, sinto sahau”
“Sawa, ngoja sisi tukapumzike”
“Haya usiku mwema jamani”
Regna akanipungia mkono na kuingia ndani ya gari, wakaondoka na mume wake, nikashusha pumzi nyingi na kubaki nikiwa ninaisindikiza gari yao kwa macho hadi inatoka getini, gafla nikasikia kelele kubwa iliyo nistua na kunifanya nigeuke kuangalia walipo watu, nikawashuhudia wageni waalikwa wakikimbilia ndani inapo tokea kelele hiyo
Na mimi nikaanza kuchanganya miguu yangu kwa kasi kwenda kutazama ni kitu gani kinacho endelea ndani ya nyumba yangu.Jinsi ninavyozidi kwenda ndani ndivyo jinsi kelele ilivyozidi kuingia kwenye masikio yangu, nika-zidi kuchanganyikiwa kwani kelele hiyo ni sauti ya Rahma ikitokea kwenye chumba ambacho nimemuacha na maiti, nikakuta watu wakiwa wamekushanyika nje ya mlango wa chumba nilicho muacha Rahma,
Nikawaomba wanipishe njia, na wakafanyahivyo hadi nikafika kwenye mlango, nikaanza kugongwa kwa nguvu ulu nikiliita jina la Rahma, gafla moshi mwingi ukaanza kutoka chini ya mlango, ulio anza kutupalia watu wote tuliopo kwenye eneo hili la mlango
Moshi mwingi ukazidi kutoka ndani ya chumba alichopo mke wangu Rahma, ambaye hadi sasa hivi anapiga kekelele za kuomba msaada, nikajitaidi kuibana pumzi yangu, nisiendelee kuuvuta moshi unaotoka kwenye chumba alichopo Rahma na kuanza kuubamiza mlango kwa kutumia bega langu la mkono wangu wa kushoto, kwa nguvu zangu zote.
Kelele za Rahma zikazidi kunichanganya kiasi cha kujikuta nikizidisha juhudi za kuuvunja mlango kwa kutumia nguvu zangu zote.Wanaume wezangu wakaanza kunisaidia kufanya kitendo ninacho kifanya mimi, cha kumshukuru
Mungu, mlango ukavunjika na sote tukajikuta tukianguka nao baada ya kuurukia kwa nguvu zetu zote, Moshi mwingi tukakumbana nao, ulio ambatana na moto mwingi, nikamshuhudia msichana aliyekuwa amepigwa na Rahma akipotelea kwenye moshi mwingi ndani ya chumba, wezangu hawakumuona zaidi yangu
Nikakimbilia sehemu alipo Rahma na kumkuta akiwa amelala chini, huku hajitambui,
“Rahma, Rahma”
Nilimuita ila hakuitika zaidi ya kuendelea kuyafumba macho yake, tukasaidiana na wezangu kumnyanyua Rahma na kumtoa nje kwa haraka na kuanza kumpa huduma ya kwanza, rahaya ya sherehe ikanipotea kabisa na kuwa ni majanga mengine ambayo sikuyatarajia kama yatatokea katika siku hii ya leo, watu wengine wakaendelea kuuzima moto uiopo ndani ya chumba ambao hadi sasa hivi chanzo chake ni nini.
Hali ya Rahma ikazidi kuwa mbaya kwani mapigo yake moyo yamekuwa ya kuhesabika na ndani ya dakika moja yanaweza kupiga mara tano au saba, ni tofauti na mapigo yamoyo yanavyopaswa kupiga kwa binadamu wa kawaida.Jamaa mmoja akajitolea gari lake, tukamuingiza Rahma ndani ya gari na kumuwahisha katika hospitali ya mkoa ijulikanayo kwa jina la Bombo.
Akili na mwili vyote vimechoka kwa muda mmoja, kila daktari ambaye anatoka kwenye chumba anacho ingizwa mke wangu sikusita kumzuia na kumuuliza hali ya Rahma inaendeleaje ila hawakunipa jibu la kueleweka
“Mungu wangu”
Nilijikuta nikianza kumkumbuka Mungu, kadri muda ulivyo zidi kwenda, ndivyo idadi ya madaktari walivyozidi kuingia na kutoka katika chumba alichopo Rahma.
“Kaka Eddy jikaze atapona tuu shemeji”
Jamaa mmoja alizungumza kunifariji, masaa yakazidi kuyoyoma na saa yangu ya mkononi inaonyesha ni saa tisa usiku na hapakuwa na na jibu lolote la kunipa matumaini juu ya mke wangu.Akatoka daktari mmoja, mzee wa makamo,
Akaniomba tuelekee ofisini kwake, kuna baadhui ya marafiki zangu wakataka kutufwata ila daktari akawazuida.Tukaingia ofisini mwa daktari na kuniomba nikae kwenye moja ya kiti kati ya viti vitatu vilivyomo ndani ya ofosi yake, akafungua ndirisha kuruhusu hewa kuingia ndani
“Dokta usinitumbulie mimacho, niambie ukweli hali ya mke wangu inaendeleaje?”
“Tulia Mr Eddy, kwanza mke wako amepatwa na tatizo gani?”
Haaa dokta unaniuliza tena mimi, wakati nyinyi ndio munapaswa kujua mke wangu amepatwa na tatizo gani?”
“Hapana usinielewe vibaya Mr Eddy, kwa maana, mke wako amepatwa na ugojwa ambao tangu niaanze kufanya kazi huu ni mwaka wa thelethini, ila sijawahi kuuona huo ugonjwa”
Maneno ya daktari yakazidi kunichanganya akili yangu, nikaendelea kumtazama daktari kwa macho makali ambayo
“Labda niende kwe….”
Kabla dokta hajamalizia akaingia nesi akiwa ameshika, bahasha kubwa yenye rangi ya kaki na kumkabithi daktari
“Mumezipiga vizuri?”
“Ndio dokta”
Nesi akanondoka na daktari akachomoa picha, iliyo pigwa na mionzi mikali ijulikanayo y kwa jina la ‘X-RAYS’.Akaitazama na kunikabathi mimi na nikaanza kuiangalia pasipo kuielewa kwani kwa jinsi ilivyo pigwa sikujua imepigwa pigwa vipi
“Ndio nini, hii doktar?”
“Hiyo ni picha niliyo iliyo pigwa kwenye mwili wa mke wako, na chakushangaza hatujaona mfupa hata mmojamwilini mwake, jambo ambalo hata sisi tlimetuchanganya”
“Hamujaona mfupa?”
“Ndio atujaona mfapa kwa maana, hata fuvu la ndani, kwa mke wako hatujaliona, tulihisi ni vifaa vyetu ndivyo vimekosea, ila nikajaribu kupiga tena na majibu ya picha zote zipo kama hivyo”
Doktar alizungumza huku akitoa picha nyingine nne ambazo zinafanana na pica niliyo ishika mkononi mwangu.Kwa kawaida binadamu akipigwa picha ya X-Rays nilazima aonekane na mifupa ndani, ila sivyo ilivyo kwa Rahma, mwili wake mzima umejaa nyama tupu
Gafla mlango ukafunguliwa kwa haraka na kuingia daktari mwengine akivunjwa na damu
“Dokta tunakuhitaji haraka”
Alizungumza na kutoka ndani ya chumba, daktari akasimama na kufungua mlango na kutoka kwa kasi, na mimi nikapiga hatua za haraka kwenda kufungua mlango ila kabla sijaufungua
Nikasikia sauti ya kike ikiniita kikitokea dirishani.Nikageuka na kutazama dirishani na kumkuta Regina akiwa ananichekea na kunitazama kwa macho ya dharau
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA