SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Nikasikia sauti ya kike ikiniita kikitokea dirishani.Nikageuka na kutazama dirishani na kumkuta Regina akiwa ananichekea na kunitazama kwa macho ya dharauSASA ENDELEA...
“Unaona hichi kichupa, ndio dawa utakayo mtibu mke wako la sivyo utampoteza”
Regna alinionyesha kichupa chenye maji ya rangi ya kijani na kunifanya nihairishe safari yakwenda alipo mke wangu na kunifanya nitokee
Dirishani ambalo ni lavioo na halina nondo, ambayo inaweza kunizuia.Ragina akaanza kukimbilia kwenye majengo mengine ya hospitalini na kunifanya nianze kumfukuza kwa haraka, kitu kilicho niacha hoi ni spidi kali anayo kimbilia
Regna na kila ninavyo jitahidi kumkimbiza ndivyo jinsi alivyozidi kuchanganya miguu na kuniacha umbali mrefu kiasi.Nikamshuhudia Regina akiingia kwenye moja ya jengo, ambalo sikulisoma jina lake vizuri, kabla sijaingia ikanilazimu kurusdi nyuma hatau chache kuangalia maandishi makubwa yaliyo andikwa kwa herufi kubwa zilizo kolezwa kwa ramgi nyeusi
(JENGO LA KUHIFADHIA MAITI, MOCHWARY)
Sikutaka kuendele kutazama maandishi mengine kwani yatanipotezea muda, nikaisikia sauti ya Regina ikiniita ndani ya chumba hicho na kunifanya niingie pasipo kuogopa, nikamkuta akiwa amesisima mbali kidogo kwenye kordo na katika pende mbili, hizi kuna mafriji makubwa ya kuhifadhia maiti.
“Njoo ukichukue kichupa, ukamuokoe mke wako mpendwa”
Regina alizungumza kwa ujasiri huku, akiendelea kuniringishia kichupa alicho kishika.Nikaanza kupiga hatua za haraka kwenda alipo sima, Regna akapiga kofi moja na taa zote, zikazima na giza totoro likatawala ndani ya chumba na kuanza kunichanganya, kwani sikumuona sehemu alipo simama
“Eddy”
Nilisikia sauti ikiniita nyuma yangu, nikageuka haraka ila kutokana na giza sikumuona mti yoyoye,
“Eddy”
Nikasikia sauti ukiniita upande wangu wa kulia na kunifanya nigeuke kwa haraka huku nikitazama ni wapi alipo Regina.Akaanza kucheka vicheko vikali, nikasikia mlango ukijifunga kwa nguvu, na kelele za watu kucheka zikazidi kuongezeka ndani ya chumba nilichopo.
“Shiiiiii”
Nikasikia sauti ya Regina ikiwanyamazisha wezake anao cheka nao, na wakanyamaza, gafla taa zikawaka na kumkuta Ragina akiwa amesimama mbali kidogo na nilipo mimi, huku pembeni yake kukiwa na wasichana wengine wawili wakifanana naye kwa kila kitu
“Eddy nani unampenda kati yetu”
“Nisikilize wewe, mwanamke naomba hicho kichupa nikamponye mke wangu”
Nilizungumza kwa ujasiri huku nikiwa nimejikaza, kisabuni
“Ohoooo, Eddy unajua mke wako alicho kifanya kwetu?”
“Najua hujui, ila ukweli ni kwamba mke wetu alikuja kwetu na kutuomba tuweze kukurudisha wewe duniani, tukampa masharti ambayo alishindwa kukuambia, na muda wa mashati hayo umepita, sasa ni kipindi cha yeye kupata shida”
“Ni masharti gani mulimpa?”
“Swali zuri sana, kwanza jitambua kwamba wewe tayari ulisha kufa, pili hiyo pumzi sisi tumekupatia udumu dumu nayo kwa muda tu ila utakufa pia”
Naweza kuwaita maregina kwani, wanazungumza kwa kupokezana akimaliza huyu anazungumza mwengine kwa sauti zinazo fanana
“Niambieni hayo masharti mimi, niyafanye”
“Hhaahaaaa Eddy, acha kutuchekesha, unadhani ytayaweza masharti yetu”
“Niambieni, kwani nahitaji mke wangu apone”
“Hahaaaa, mke wako ni mjinga sana”
Regina mmoja alizungumza huku akinisogelea karibu na kuanza kunizunguka taratibu, huku mkono wake mmoja akikishika kiuno changu.
“Tulimuambia mke wako, baada ya siku thelethini ya wewe kuwa hai, tunataka ule watu watano kama sadaka ya kumshukuru Mungu wetu, ambaye yupo India, na siku ya Thelathini ilikuwa ni jana, ndio maana ukaanza kubadiila kuwa joka, ila mke wako alikuzuia, na ukashindwa kubadilika.Tulitaka uwatafune wale waandishi wa habari waliokuwa mbele yako, ila ndio hivyo tena ikashindika”
Maneno ya Regina yakazidi kunivunja nguvu, nikabaki nikiwa ninamtazama pasipo kumjibu kitu chochote.
“Na mke wako alivyo mjinga akadhubutu kunipiga, ulidhani alikuwa akinipiga kwa kunionea wivu, la hasha, ila alikua akinipiga akihitaji nife ila masharti yavunjike ndio maana na mimi nikaamua kumumpa ungonjwa ambao hata madaktarti wamtibu wakiwa wapo uchi, hawataweza kumponya na tunampa nusu saa, pasipo wewe kutekeleza tutakacho kuambia basi mke wako, ATAKUFA”
Regina alizungumza na kuanza kucheka huku akirudi sehemu walipo simama wezake, mwili mzima ulianza kunivuja kwa jasho , japo ndani ya hili jengo kuna hewe ya baridi ila haikufua dafu katika kulizuia jasho langu kunimwagika sana.
“Nipo tayari kwa masharti yenu”
“Waooooo, powa baby’s tuanzeni kazi”
Regina na wezake wakaanza kufungua friji moja baada ya nyingine na kutoa maiti zilizo pata ajali tofauti tofauti, zipatazo tisa nakuziweka mbele yangu.
“Unadakika kumi na tano kuzili maiti hizi zote uzimalieze”
“Eheee……!!!??”
“Unashangaa, tena tumekupungizia adhabu mbona”
“Naona anataka kumuwekee na vikorombezo ili aweze kuzila vizuri”
Regina mmoja alizungumza na kuanza kuishika maiti moja baada ya nyingine na ndani ya dakika moja zote zikawa zinatoa vunza wengi wakubwa wakubwa, walio nona pamoja na ujiuji mzito
“Hapo kuna mchuzi mzuri wa kukuwezesha kula hizo maiti”
Nikabaki nikizitazama maiti za watu, hawa, kumbukumbu za mke wangu Rahma zikaanza kunijia kichwani kwangu kwa kasi kubwa hadi nikaanz akujishangaa, nikaanza kukumbuka kila aliyokuwa akinifanyia ambayo nimema kwangu.
“Eddy, muda unakwenda”
Regina mmoja alizungumza na kunifanya nipige magoti chini na kuanza kuchukua maiti moja na kuanza kuinyafuafua nyama zake, na kadri nilivyo zidi kuitafuna ndivyo mwili wangu ilivyo anza kubadilika na kuwa katika mfumo wa joka,
kasi ya kuzitafuna ikazidi kuongezeka kwani Regina mmoja alikuwa na kazi ya kuniambia muda uilio badilika.Hadi inafika dakika ya kumi na tano nikawa nimeshamaliza kumla maiti wa tisa, na kurudi katika hali yangu ya kawaida ya kibidanamu huku mdomo wangu mzima ukiwa umejaa damu tupu
“Waoooo kazi nzuri Eddy, ila kuna mmoja wa mwisho wa kumalizia, huyo ni mtamu sana kuliko hao wote”
Regina alizungumza huku akilisogelea friji moja na kulivuta nje, na kwakusaidiana na wezake, wakautoa mwili ambao hadi wanauweka chini nikabaki nikiwa ninashangaa kwani ni mwili wangu wote.
“Huyu ni wewe, halisi baada ya kufa wakakuleta huku ila wamejisahau na kujua wewe upo hai”
Regina alizungumza huku akiugeuza mwili wangu, ambao hauna nguo hata moja, nikaliona jeraha la kisiki kilichokuwa kimenichoma mgongoni, kipindi mkia wa joka kubwa ulivyokuwa limenipiga na kunirusha juu na kukiangukia kisiki hicho
“Jile mwenyewe, sasa au unataka tukuwekee rost kama la wengine ulio wala?”
Nikashusha pumzi nyingi huku nikimtazama, Regina na wezake anao fanana nao.
“Moja, mbili, ta…..”
“Ngoja kwanza Regina”
“Ehee unsemaje?”
“Ninakuomba umsaidie mke wangu, hapa nilipo sijielewi kabisa, tafadhali ninakuomba ndugu yangu”
Regina wote watatu wakaanza kucheka kwa dharau huku wakianza kunizunguka kwa kasi sehemu ambayo ni-mechuchumaa na mwili wangu, ninaoa ambiwa niule.Wakasimama gafla huku macho yao na sura zao zikianza kubadilika, macho yao yamejaa miale ya moto iliyo ambatana na machozi ya damu, huku sura zao zikianza kusi-nyaa na kuwa nyeusi tii kama mkaa.
“KULAAAA”
Regina mmoja alizungumza na kunifanya niitazame maiti ya mwili wangu, nikajikuta nikisimama kiujasiri huku nikiwatazama Regina wote watatu, nikamtazama aliye shika kichupa chenye dawa, wakendelea kunitazama ki-sha nikachuchumaa chuni, na kuishika miguu ya maiti yangu, nikaibana vizuri kwa viganja vyangu, kwa kutumia
Nguvu zangu zote nikainyanyua haraka na kuizungusha, ikawapiga kwenye miguu yao na wote wakaanguka chi-ni, aliye shika kichupa chenye dawa akakiangushia karibu yangu.Nikajirusha kwa haraka na kukiokota kichupa, na kuanza kukimbia kuelekea nje, kabla sijafika mlangoni nikastukia kumuona Regina mmoja akiwa amesimama mbele yangu.
Huku sura yake ikiwa imekasirika sana, akajaribu kunirukia ila nikamkwepa na kunipa nafasi ya kutoka nikiwa ninakimbia kuelekea kwenye jingo alipo mke wangu Rahma.Hata mimi mwenyewe nikaanza kuji-shangaa kwa maana mwendo wangu wa kukimbia upo kasi sana, kuwazidi wao, nikafika kwenye mlango wa kuingilia kwenye
Jengo alipo ingizwa Rahma, Regina na wezake wakasimama na kuninyooshea kidole, huku mmoja akinifanyia ishara ya kunichinja kichwa change.Nikatoa kitambaa mfukoni mwangu na kujifuta damu zi-lizopo mdomoni mwangu
Nikaanza kupiga hatua za haraka kwenda kilipo chumba, kitendo cha kujitokeza kwenye kona nikamkuta dada mmoja ambaye tulifika naye hapa hospitalini kipindi tunamleta Rahma, nikamkuta akiwa amekaaa chini huku analia kwa nguvu, huku baadhi ya rafiki zangu wakiwa, wanajifuta machozi kwa vitambaa vyao.
Wasiwasi mwin-gi ukaanza kunijaa moyoni mwangu, nikaanza kupiga hatua za haraka, na kujikuta zikichanganya na kuzaa mwendo wa kukimbia hadi nikafika kwenye mlamgo wa chumba alichopo Rahma, sikumuuliza mtu zaidi ya ku-shika kitasa, nikafungua mlango na kukuta chumba kikiwa hakina mtu hata mmoja, mapigo ya moyo yakazidi kwenda mbio, nikatoka nje huku machozi yakianza kunilenga lenga
“Y..uuu..po wapi mke wangu?”
Niliuliza kwa kigugumizi kikubwa, na kuwafanya rafiki zangu, kuzidi kulia, hakuna ambaye aliweza kunijibu kitu cha aina yoyote.
“YUPO WAPI MKE WANGU”
Nilizungumza kwa sauti kubwa iliyo changanyikana na hasira kali sana, huku nikimshika rafiki yangu mmoja na kukandamiza ukutani
“Ame…”
Jamaa alichindwa kuimalizia sentesi yake, na kujikuta akimwagikwa na machozi mfululizo, moyo wa uchungu ulio amba-tana na machozi yenye hasira ndani yake, vikautawala mwili wangu.
Nikaanza kupiga hataua za kuelekea ilipo ofisi ya dak-teri aliye niita mara ya kwanza, kabla sijafika ofisini mwake, nikawaona manesi wa ne wakisukuma kitanda kimoja, amba-cho juu yake amelala mtu aliye funikwa kwa shuka la kijani, kuanzia miguuni hadi kichwani mwake.
Nikahairisha safari, na kuanza kukimbilia kwenda walipo manesi.Mmoja wao akaniwahi kunizuia nisikifikie kitanda, ila nikamsukuma na akaan-gukia pembeni na kuwafanya wezake kubaki wakiwa hawana la kufanya
Nikalishika shuka na kulifunua na kukuta maiti ya bibi mmoja mzee akiwa tayari amesha fariki dunia, nikabaki nikiwa ni-nashangaa sana.
“Kwani kaka vipi?”
Nesi mmoja aliniuliza
“Mke wangu yupo wapi?”
“Mke wako, anaitwa nani?”
“Anaitwa mke wangu”
Hata jina la Rahma nililisahau kichwani mwangu kwa jinsi nilivyo changanyikiwa, nikaachana na manesi na kuendelea na safari yangu kwenye ofisi ya madaktari, nikazidi kutembea kwa haraka hadi ninafika nje ya ofisi nikakutana na daktari aki-toka huku akiwa amechoka
“Doktar mke wangu yupo wapi?”
“Tulia kwanza bwana Eddy”
“Doktar hivi unielewi nimekuambia mke wangu yupo wapi, kama amefariki ninaomba munionyeshe maiti yake”
“Bwana Eddy tafadhali ninakuomba utilize jazba kwanz…”
Sikumruhusu daktari kuimalizia sentesi yake, nikalishika koti lake sehemu ya kifua na kumgandamiza ukutani
“Mke wangu yupo wapi?”
Nilizungumza kwa sauti nzito na kumfanya daktari kuanza kutetemeka, mwili mzima, hata miwani aliyo ivaa ikaanguka chini.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA