NIFANYE NAMIMI KAKA (17)

0
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
Hata kama ungekuwa hujawahi kupata bahati ya kutazama kwa macho hata mara moja katika maisha yako lakini kwa kupitia sauti pamoja na zile nyimbo zilizokuwa zimetawala pale hakika usingekuwa mgumu wa kutaka kuelewa kuwa kulikuwa na kitu gani cha zaidi kilichokuwa kikiendelea.

SASA ENDELEA...
Kila mtu alikuwa ametawaliwa na tabasamu la furaha ni hapa ambapo nilipata nafasi ya kuishuhudia mechi dhidi ya mabingwa wa kutabasamu, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa katika huzuni.

“Hivi kumbe una ukaribu na Irine huyu muigizaji?” niliamua kumuuliza Evadia.

“Ndiyo ni rafiki yangu niliwahi kusoma naye,” alinijibu huku uso wake ukiachia tabasamu mwanana.
“Duh,” nilijigunia kimoyomoyo na sasa nilizidi kuyapa macho yangu nafasi ya kumtazama Irine.

Alikuwa katika mavazi ya gharama sana, kwa kumtazama harakaharaka alikuwa amevaa gauni pamoja na viatu vya kupanda vyenye gharama kubwa sana. Alionekana kuwa mrembo haswaa! kuanzia lile wigi alilokuwa amevaa, Make-up aliyokuwa ameitumia siku hiyo, pamoja na uzuri wa kila kitu alichokuwa amejaaliwa.

Mbali na maisha yake ya umaarufu katika fani ya uigizaji wa filamu lakini hakuwa ni mtu wa kujisikia sana, kwake kila mtu alimchukulia kuwa kama rafiki, alipenda kuishi na watu vizuri nadhani hii ndiyo sababu iliyomfanya akawa anazidi kupendwa kila siku.

“Kwanza kabisa ningependa nichukue nafasi hii ya kumkaribisa Quuen Irine katika siku yake hii adhimu ya kuzaliwa kwake ili aweze kuzungumza japo kidogo na mashabiki wake kabla zoezi hili dogo halijaendelea,” alisema mshehereshaji kisha akamkabidhi kipaza sauti Irine ili aweze kuzungumza.

Muda wote huo nilikuwa kimya, nimepoa kama maji ya mtungi huku masikio yangu yalikuwa makini kutaka kusikia maneno ambayo alikuwa akitaka kuzungumza Irine kwa wakati ule.

“Aaammh,” alianza kusema kisha kicheko kikachukua nafasi yake, alikuwa akicheka kwa wakati huo kitendo kilichowafanya hata watu waliyokusanyika eneo lile nao waanze kucheka, bila shaka miongoni mwao palikuwa na watu ambao walikuwa wakicheka kwa kufata mkumbo kwani hakukuwa na kitu kilichokuwa kimetokea cha kituko kiasi kwamba kiwafanye wacheke tena kwa sauti kubwa huku wengine wakikaukia.

“Sema Madam tunakusikiaaaa,” zilisikika sauti za kike zikipaza na kumfanya Irine azidi kucheka. Kuna muda alikuwa kama mtu aliyeshindwa kuzungumza kabisa kila alipokuwa akitaka kuzungumza alijikuta akiishia hewani asijue ni wapi alitakiwa kuanzia kuzungumza. Katika hali ya kushangaza machozi yalianza kumdondoka mashavuni mwake, alikuwa akilia kilio cha furaha kwa wakati ule.

“Sijui nianzie wapi kuzungumza…,” alisema Irine kisha akanyamaza kwa muda, ukimya ulikuwa umetawala eneo lile, hata ile bendi ya muziki iliyokuwa ikituburudisha kwa wakati huo ilikuwa imesimama kwa muda, kila mtu alikuwa akimtazama Irine msichana mrembo mwenye mvuto wa kimapenzi akizungumza kwa wakati huo.

“Nawashukuru sana ndugu zangu kwa upendo huu mlionionyesha kwa kweli nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipo washukuru wote mliohudhuria hapa. Namshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyonipa katika maisha yangu, nawashukuru wazazi wangu wawili Baba na Mama kwa kunileta duniani na kwa malezi yao bora, pia nawashukuru sana marafiki zangu wa karibu kwa kuweza kunionyesha upendo huu, niseme tu nawashukuru sana sina neno lingine la kusema isipokuwa nawapenda wote,” alisema Irine kisha akamkabidhi kipaza sauti mshehereshaji wa shughuli ile.

Kila kitu kilikwenda kama kilivyopangwa, kuanzia tukio zima la kulishana keki mpaka vinywaji na mpaka kufikia majira ya saa tatu za usiku hakukuwa na tofauti yoyote iliyoweza kujitokeza katika siku ile ambayo ilikuwa ni maalumu kwa kusherehekea siku ya kuzaliwa Irine Kisoka muigizaji wa filamu maarufu hapa nchini.

Waandishi wa habari hawakuwa mbali katika usiku ule, vyombo mbalimbali vya habari vilikuwa vimetawala huku kila mwandishi akionekana kutafuta habari. Kila mahali kamera zilikuwa zimetawala.
“Mambo mpenzi,” alisema Evadia huku akimtazama Irine kisha wakakumbatiana, wakati huo nilibaki nikiwatazama tu, nilikuwa nikionekana kushangaa kila kitu hasa kitendo cha kumshuhudia muigizaji kama yule mbele ya macho yangu hakika nilikuwa siamini, nilihisi wenda nilikuwepo ndotoni na muda wowote ningeweza kuamka lakini haikuwa hivyo bali kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwa wakati ule kilikuwa ni ukweli mtupu, ukweli wa macho kuona na uhalisia wake, hapo ilikuwa ni baada ya utambulisho kutoka kwa baadhi ya marafiki zake kama Diana, Zulfa, Shamsa na Anitha ambao alikuwa ametoka kunitambulisha muda sio mfupi.
“Safi mamii kumbe na wewe ulikuwepo jamani?” aliuliza Irine huku akiwa amekumbatiana na Evadia na haikuchukua dakika wakaweza kuachana kutoka katika lile kumbato ambalo nilikuwa nikihisi kama kukumbatiwa katika mawazo yangu.
“Sasa nitakosaje kwa mfano kuwepo wakati juzi uliniambia mwenyewe kuwa nisikose,” alisema Evadia huku akimtazama Irine ambaye alikuwa ametawaliwa na tabasamu mwanana, wakati huo waandishi wa habari walikuwa wakiendelea kupiga picha mbalimbali, niliamini katika picha zile lazima na mimi ningeweza kuonekana kwani nilikuwa karibu kabisa na Irine msichana ambaye alikuwa na umaarufu mkubwa sana.
“Mmh! Mambo mengi ndugu yangu enhe! vipi mambo yako yanaendaje lakini?” aliuliza Irine huku akiwa amemshika mkono Evadia tukio ambalo lilizidi kunidhihirishia wazi kuwa walikuwa ni watu wanaojuana kwa ukaribu mkubwa sana.
“Namshukuru Mungu siku zinaenda vizuri,” alijibu Evadia.
“Yani we acha kila siku napanga nije dukani kwako lakini unakuta nasahau, mambo yanakuwa mengi sana.”
“Nafahamu hilo wala usijali,” alijibu Evadia.
Irine alinitazama kwa muda kama mtu anayenitathmini kisha akamgeukia Evadia na kumuuliza kuwa mimi ni nani? kwa kweli kitu nilichokishukuru ni kuwa 

Evadia aliweza kumdanganya Irine, alimwambia kuwa mimi ni rafiki yake na alikuwa ameniomba nimsindikize katika usiku ule katika tukio lile jambo ambalo aliweza kuamini kabisa, akanipa mkono na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuwa karibu na muigizaji huyo maarufu, mwanzo ambao naweza kusema ulikaribisha safari mpya ya maisha yangu.

Usiku wa siku hiyo niliporudi nyumbani kwangu Tandale nilionekana kuwa ni mwingi wa furaha sana, nadhani tukio la kukutana na muigizaji maarufu Irine ndilo lililonifanya kila wakati tabasamu lisinikauke katika uso wangu.

Evadia hakutaka kwenda nyumbani kwao usiku ule, aliamua kujitoa muhanga na kuamua kulala na mimi. Mwanzo nilionekana kuwa mgumu kidogo kwa kuhofia usalama wake kama mtoto wa kike kwani alikuwa bado ni msichana ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake japo alikuwa akifanya biashara zake. 

Hilo halikuonekana kuwa swala gumu sana kwangu baada ya kunilazimisha na kuzidi kuniaminisha kuwa niondoe wasiwasi juu ya yeye kulala nje na nyumbani kwako siku ile niliamua kukubaliana naye kila kitu na ni katika usiku huohuo ambao niliweza kufanya naye mapenzi. 

Mapenzi yalichukua sehemu kubwa sana usiku huo, sauti za miguno iliyofungamana na utamu wa penzi ndizo zilizokuwa zikizikika mule chumbani kwangu tulipokuwa tumelala na mara baada ya kumaliza kufanya tendo lile tulienda kuoga na baada ya hapo tuliamua kulala.

Tuliamka katika asubuhi ya siku ya jumapili tulivu, hali ya hewa ilikuwa shwari kabisa, niliyapepesa macho yangu kutoka katika usingizi mzito ambao uliambatana na uchovu, nilianza zoezi la kujinyoosha viungo vya mwili wangu huku likifuatiwa na miayo mingi iliyoashiria njaa kwa wakati ule, nilihisi mwili mzima ukiwa umechoka sana.

Nilimtazama Evadia kwa wakati ule, alikuwa bado amelala. Sikutaka kumuamsha nilichokifanya ni kuamka na kwenda kuoga. Niliporudi kutoka bafuni nilimkuta akiwa amekaa kitandani, nilipomtazama alikuwa akitabasamu huku viganja vyake vikiwa bize katika kuibofyabofya simu yake aina ya I phone 6 yenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni moja za kitanzania.
“Mbona hujaniamsha jamani baby?” aliniuliza wakati huo nilikuwa nikiliweka sawa taulo langu.
“Nilihisi nitakusumbua ndiyo sababu,” nilimjibu huku na mimi nikijaribu kulitengeza tabasamu mwanana.
“Hapana.”
“Hapana nini sasa?”
“Ungeniamsha tu!”
“Sikujua,” nilimwambia kisha akaonekana kuwa bize kidogo na simu yake.
“Vipi huendi kuoga?” nilimuuliza.
“Naenda,” alinijibu.
“Nenda basi mpenzi maji yanakusubiri.”
“Kwani umeniwekea?”
“Ndiyo nimeshakuwekea tayari.”
“Sawa baby ngoja nikaoge,” 

Aliniambia kisha akaiweka simu yake kitandani, akainuka halafu akaniambia nimuelekeze kuwa bafu lilikuwa lipo sehemu gani, nikamuelekeza kisha akaenda kuoga. Haikuchukua dakika kadhaa aliweza kurudi wakati huo na mimi nilikuwa namalizia kuvaa.

Hakutaka kupoteza muda aliporudi kutoka bafuni alianza kuvaa nguo zake katika utaratibu wa kupendeza, macho yangu hayakukoma kumtazama katika namna ya kumsifia jinsi alivyokuwa mrembo, alikuwa ameumbwa akaumbika kisawasawa.
“Nimeshindwa kuvumilia,” nilimwambia kisha nikajikoholesha kwa makusudi kabisa.
“Umeshindwa kuvumilia nini?” aliniuliza.
“Evadia yani nikikutazama sioni kasoro yoyote ile hivi nimewahi kukuambia ukweli?”
“Ukweli upi jamani?”
“Juu ya uzuri uliyokuwa nao.”
“Jamani Dick kila siku unanisifia inaamana umesahau?”
“Hapana yani nikikutazama nahisi kama hii ndiyo mara yangu ya kwanza kukutana na wewe,” nilimwambia maneno yaliyomfanya akacheka.
“kweli tena yani wewe ni mrembo asikudanganye mtu.”
“Asante mpenzi wangu.”
“Kwani ukitoka hapa unaenda wapi?”
“Dukani.”
“Na nyumbani je?”
“Kumefanyaje?”
“Jana hujalala nyumbani wazazi….” Kabla sijaimalizia sentensi yangu Evadia aliweza kunikata kauli.
“Kwani wewe wasiwasi wako ni nini? mimi ni mtu mzima na nina uhuru wangu pia katika kufanya maamuzi halafu kwanza kuhusu nyumbani pamoja na wazazi wangu ondoa shaka, jana usiku nilimpigia Mama simu na nilimueleza kuwa sitarudi nyumbani na alinikubalia,” aliniambia Evadia.
“Kwahiyo hakuna tatizo.”
“Ndiyo hakuna embu jiamini bhana.”
“Sio kwamba sijiamini ila kumbuka wazazi wako wanakupenda.”
“Sasa kama wananipenda?”
“Umeshakuwa mwandishi wa habari, mimi maswali mengi siyapendi.”
“Jiamini basi.”
“Najiamini,” nilimwambia.

Nilifahamu kuwa mbali na ule uhuru aliyokuwa akiusema lakini bado wazazi wake walikuwa wakimpenda sana, hasa ukizingatia kuwa alikuwa ni mtoto wa kipekee katika familia yao. Alikuwa akipendwa sana na wazazi wake na ndiyo sababu hata baba yake aliamua kumfungulia duka ili aweze kuliongoza.

Baada ya kumaliza kuvaa nguo, Evadia alinitazama kwa macho ya huba bila kusema lolote, alibaki akinitazama huku asiwe na la kuniambia. Wakati huo nilikuwa nimesimama.
“Mbona unanitazama?” nilimuuliza.
“Sitamani kuondoka natamani nibaki na wewe tu siku nzima,” alinijibu kisha akanisogelea na kitendo kilichofuata ni kuanza kubadilishana mate.
“Unaonekana kuwa mtamu kila sehemu,” 

Nilimwambia kwa kumchombeza, wakati huo mikono yangu ilikuwa imekishikilia kiuno chake laini, alikuwa ametulia kana kwamba hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kwa wakati ule, macho yake legevu meupe yaliyorembwa na udoti mweusi wa mviro yalizidi kuniambia nifanye kitu cha utofauti ili kiweze kumshtua kwa wakati ule.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)