NIFANYE NAMIMI KAKA (18)

0
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
Nilimwambia kwa kumchombeza, wakati huo mikono yangu ilikuwa imekishikilia kiuno chake laini, alikuwa ametulia kana kwamba hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kwa wakati ule, macho yake legevu meupe yaliyorembwa na udoti mweusi wa mviro yalizidi kuniambia nifanye kitu cha utofauti ili kiweze kumshtua kwa wakati ule.

SASA ENDELEA...
Sikutaka kupoteza muda niliamua kuvitumia vidole vyangu katika kuzipapasa sehemu za ubavuni mwake katika mtindo wa kumtekenya hali iliyomfanya akashtuka kwa kunikumbatia kwa ghafla!

“Oooh! Jamani nini Dick mbona mchokozi hivyo,” aliniambia huku akijifanya kuwa ameumia sehemu fulani.
“Vipi kwani?” nilimuuliza swali la kizushi.
“Mchokozi muone vile,” aliniambia kisha akajitoa katika kumbato, alionekana kuwa na furaha kupitia uso wake.

Alipoitazama saa yake ilisoma majira ya saa nne za asubuhi, aliniambia kuwa alikuwa anataka kuondoka kuelekea dukani kwake, sikutaka kuweka mlolongo mrefu wa mazungumzo, nilichoamua kukifanya ni kumruhusu lakini kabla hajaondoka aliamua kuniachia kiasi kidogo cha pesa ambacho aliniambia kuwa nikitumie kwa ajili ya kifungua kinywa.

Kwa kweli niliweza kushukuru lakini akili yangu ilikuwa ikiwaza vitu vingine kabisa, kwanza nilikumbuka kuhusu ule usiku wa jana, jinsi ambavyo niliweza kukutana na Irine yule muigizaji wa filamu za kibongo, bado sikutaka kuamini kama kweli niliweza kukutana naye, nakumbuka nilikuwa nikiishia kuzitazama filamu zake, kuziangalia picha zake mitandaoni na cha zaidi kupitia uzuri wake nilikuwa nikiutumia kuandika machombezo.

Kutokana na furaha niliyokuwa nayo niliamua kumtumia ujumbe mfupi Mick wenye lengo la kutaka kuonana naye siku hiyo jioni.
“Tukutane wapi?” aliniuliza kupitia ujumbe mfupi.
“Pale Hongera Bar,” nilimjibu.

Jioni ya siku hiyo tuliweza kukutana maeneo ya Bamaga ilipokuwa bar moja iliyojulikana kwa jina la Hongera Bar, nilionekana kuwa mwingi wa furaha sana, kila nilipokuwa nikimtazama Mick nilizidi kuonyesha tabasamu langu kila wakati. 

Sikuwa mlevi hivyo nilikuwa nimeagiza maji na Mick naye alikuwa ameagiza pombe aina ya Castle Lager, tulipohudumiwa sasa mazungumzo yakaanza rasmi. Wakati huo giza lilikuwa limeshaanza kutanda angani.

“Mbona sikuelewi leo una nini maana si kawaida yako?” aliniuliza Mick huku akiendelea kunishangaa kwa wakati ule.
“Yani we acha tu! ukisikia nimekuwa top in Dar usishangae,” nilimwambia huku nikiendelea kucheka.
“Mbona sikulewi top in Dar kivipi?”
“Irine.”
“Irine!”
“Ndiyo Irine Kisoka.”
“Irine Kisoka?”
“Ndiyo.”
“Irine yupi huyo?”
“Huyo unayemfahamu.”
“Huyu muigizaji?”
“Ndiyo.”
“Kafanyaje?” aliniuliza Mick kisha sikutaka kumficha lolote, niliamua kumsimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea mpaka kukutana naye. Kwa kweli Mick hakutaka kuamini kabisa kama kweli nilikuwa nimekutana na msichana huyo maarufu.
“Hivi unayoniambia ni kweli au?”
“Sasa umesikia nasimulia hadithi hapa.”
“Na vipi kuhusu Evadia.”
“Evadia kumbe anamfahamu ni rafiki yake.”
“Duh!”
“Yani we acha tu! ukisikia siku nimekuwa staa Dunia nzima ushingae.”
“Ina maana umarufu wako wa kuandika hadithi umeona haukutoshi.”
“Umaarufu gani huu mtu unakuwa maarufu mitandaoni halafu unaishi maisha mabovu,” nilimwambia kisha akacheka.
“Huo ndiyo ukweli,” nilimwambia.

Hakukuwa na kitu nilichokuwa nikikifikiria zaidi ya umaarufu kama aliyokuwa nao Irine, niliutamani sana umaarufu wake, kila nilipokuwa nikilitaja jina lake nilikuwa nikiyaona maisha ya kitajiri nay a ustaa aliyokuwa anaishi. 

Kwa kweli nilikuwa nikijisikia furaha sana kila nilipokuwa nikiyawaza hayo. Kuna kipindi nilikuwa nikitamani utokee muujiza kisha Irine anifuate Tandale nilipokuwa nikiishi halafu niweze kutamba pale mtaani kuwa nilikuwa nikitembea na msichana maarufu lakini haikuwa hivyo, yalikuwa ni mawazo ya ndoto ambayo ilikuwa ni vigumu kuweza kutimia.

Sikuwa nauwezo wa kuigiza katika maisha yangu lakini angalau nilibahatika kuwa na kipaji cha uandishi wa riwaya na machombezo. Nilipanga kukitumia kipawa hiki katika kujiletea umaarufu mkubwa ambao ungeweza kuyabadili maisha yangu.
“Sasa tutafanyaje?” aliniuliza Mick huku akiwa ameshikilia glass iliyokuwa na Castle Lager, akainywa taratibu halafu akanitazama.
“Nitamtumia Evadia ili aweze kunisaidia katika hili.”
“Kivipi sasa?”
“Itabidi niandae hadithi ya kuweza kufanyiwa filamu nzuri ambayo naamini itapendwa sana.”
“Kweli embu fanya hivyo,” aliniambia Mick.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mimi kuamua kujitosa katika kuandika hadithi nzuri ya kimapenzi ambayo niliamini pindi itakapofanyiwa filamu ingeweza kunipa umaarufu mkubwa sana na pia ingeweza kuyabadilisha maisha yangu. 

Hata pale ulipoanza kusumbufu wa wale wasichana niliyowahi kutembea nao niliweza kuwaambia kuwa nilikuwa bize, sikutaka kuwasiliana nao kabisa.

Ubize wa kuandika hadithi ya kimapenzi ilinifanya nikae mbali nao kwa muda. Nakumbuka Hadithi niliyokuwa nikiiandika niliipa jina la “BADO UNAISHI MOYONI MWANGU.” Ilikuwa ni hadithi ambayo nilitumia hisia kali mno katika kuiandika. 

Niliamini ilikuwa ni hadithi ambayo ingeweza kumgusa kila mtu ambaye angeweza kuisoma. Ilikuwa imebeba uhalisia wa maisha halisi ya kimahusiano binafsi iliweza kunigusa kwa namna moja ama nyingine.
“Dick unajua sikuelewi kabisa?” aliniuliza Precious siku moja alipokuwa amekuja nyumbani kwangu majira ya mchana.
“Kivipi kwani?”
“Nakupigia simu zangu hupokei, nakutumia meseji hujibu hivi kwanini lakini?”
“Nilikuwa bize ndiyo maana ukaona hivyo.”
“Huo ubize ni wa nini au siku hizi una wanawake wengine ndiyo maana unanifanyia hivyo?”
“Si kweli.”
“Hunipendi?”
“Nafikiri jibu unalo mwenyewe siwezi kurudia kila wakati.”
“Dick usibadilike basi mimi nakupenda.”
“Nakupenda pia,” nilimjibu kisha akaweza kuondoka.

Nilikuwa nimepagawa na umaarufu ambao nilikuwa nikiutamani kutoka kwa Irine, kila nilipokuwa nikizitazama filamu zake zilizidi kunivutia sana. Alikuwa ni msichana mrembo aliyejaaliwa kila sifa ambazo zinaweza zikamshawishi mwanaume rijali mpaka akatamani kuwa naye. 

Macho yangu hayakumtazama katika matamanio ya kimapenzi lahasha! bali nilikuwa nikimtazama katika namna ya kuutamani ustaa ambao niliamini ungeweza kuyabadili maisha yangu. 

Kazi kubwa iliyokuwa imebadikia kwa wakati ule ilikuwa ni kutafuta njia ya ziada ya kuweza kumuingilia Evadia mpaka akubali kunisaidia nia yangu ya kutoa filamu na muigizaji huyo ambaye alikuwa na urafiki naye. Ilikuwa ni kazi ngumu mno lakini niliamini kufanikiwa katika hilo.

Ulikuwa ni mwanzo wangu wa kuonyesha mapenzi ya dhati niliyokuwa nayo kwa Evadia, nilikuwa nikionyesha kumpenda sana kiasi kwamba kuna kipindi alikuwa akishangaa upendo ule ulikuwa unatokea wapi hasa. 

Kila siku sikuacha kumtafuta, nilikuwa nikimtumia ujumbe mfupi na hata pale alipoonekana kuwa kimya kwa kutonijibu ujumbe wangu niliamua kumpigia na hapo tuliweza kuzungumza mambo mengi sana kuhusiana na mapenzi yetu. Alionekana kuniamini kwa kila kitu na hiyo ndiyo ilikuwa ngao yangu kubwa ya kutimiza lengo langu kwa wakati ule.

“Baby halafu kuna kitu nataka kukuambia,” aliniambia Evadia siku moja tulipokuwa dukani kwake.
“Kitu gani?”nilimuuliza.
“Nataka uje ujitambulishe kwa wazazi wangu,” aliniambia kisha nikabaki nimeshikwa na butwaa kwa muda halafu nikajilazimisha kutoa tabasamu, nilikuwa nikitabasamu tabasamu la uwongo, sikuwa nikitegemea kama Evadia angeweza kuniambia maneno yale kwa wakati ule.
“Nini?” aliniuliza mara baada ya kuniona nikitabasamu.
“Hamna kwahiyo unataka twende lini?”
“Hata kesho mpenzi siunajua jinsi ninavyokupenda?”
“Ndiyo nafahamu ila tusifanye kesho unaonaje tukapanga siku nzuri ambayo nitaweza kwenda kujitambulisha kwa wazazi wako?”
“Sawa nimekuelewa mpenzi naamini wewe ndiyo mume wangu mtarajiwa.”
“Hata mimi naamini wewe ndiyo mke wangu wa maisha,” nilimwambia kisha tukakumbatiana.

Mapenzi yangu na Evadia yaliendelea kupamba moto kila siku, nilijitahidi sana kumfanya azidi kuwa karibu yangu kiasi kwamba hata nitakapofikia hatua ya kumueleza nia yangu asiweze kunikatalia, niliamini kulikuwa na ugumu katika kulitimiza hilo na ndiyo sababu iliyonifanya nizidi kuwa mpole.

Penzi la Precious bado halikufutika kichwani mwangu niliendelea kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi lakini mapenzi yetu yalikuwa ni ya kujiiba. Nilifahamu fika kuwa Precious alikuwa ni mke wa mtu, mke wa mwanaume ambaye alikuwa akipambana usiku na mchana kutafuta riziki ili aweze kuihudumia familia yake.

Kwa muda mrefu wa ndoa yake hakuwa amebahatika kupata mtoto na hii ndiyo sababu iliyomfanya apunguze mapenzi kwa mume wake. Alikuwa akiniambia mambo mengi sana na jinsi ambavyo ndugu wa mume wake walivyokuwa wakimuandama kwa maneno yaliyokuwa yakizidi kumuweka katika wakati wa maumivu kila siku, alikuwa akitamani sana kupata mtoto katika ndoa yake lakini hakubahatika.
“Ndoa yangu inanitesa sana, natesekea Dick natamani mpaka kufa,” aliniambia Precious huku machozi yakimdondoka, alikuwa akilia kwa uchungu mno.
“Hapana hutakiwi kusema hivyo unakufuru,” nilimwambia huku nikijaribu kumbembeleza, alikuwa akibubujikwa na machozi kwa wakati huo, sikutaka kuyaacha machozi yake yaendlee kumtoka mbele yangu, niliamua kumfuta.
“Dick ndugu wa mume wangu wananinyanyapaa sana kila siku ugomvi hauishi ndani ya nyumba.”
“Kwani unaishi nao pamoja?”
“Ndiyo baada ya kuona sijampatia kaka yao mtoto wameamua kunifuata na lengo lao kubwa wanataka niachike.”
“Mh! Kweli hilo ni tatizo.”
“Dick naumia sana, naumia sana,” aliniambia kwa sauti iliyogubikwa na wimbi la masikitiko makubwa.

Kila nilipokuwa namtazama alizidi kuonekana kuwa mtu mwenye shida, sura yake ya masikitiko ilizidi kunidhihirishia wazi kuwa kulikuwa na kitu alichokuwa anakihitaji kwa wakati ule, sikutaka kujifanya ajuza wa kufahamu kila kitu, niliamua kuwa mkimya nikimpa nafasi ya kutaka kujielezea na kama yalivyokuwa mawazo yangu aliniita kwa sauti ya chini huku uso wake akiwa ameuelekeza chini kisha nikamuitikia huku nikiyapa wasaa masikio yangu yaweze kumsikiliza.
“Naomba unisaidie kitu kimoja,” aliniambia.
“Kitu gani?” nilimuuliza.

“Naomba unipatie mtoto sina tatizo lolote mimi katika kizazi changu, tatizo lipo kwa mume wangu naomba unipe ujauzito na ninakuahidi ile ahadi yangu ya kukupa nyumba pamoja na mtaji wa kutoa vitabu vyako nitakupa, naomba unisaidie niondokane na fedhea hii inayoniandama katika maisha yangu,” aliniambia Precious.

Kwa kweli nilibaki nikimshangaa Precious nisijue ni nini nimjibu kwa wakati ule, ni kweli nilikuwa katika mahusiano naye na pia nilikuwa nikifanya naye mapenzi sana kiasi kwamba hakukuwa na kitu kigeni ambacho nilikuwa sikifahamu katika mwili wake, nilikuwa nikimfahamukila kitu kama mume wake wa ndoa.

Kwa muda wote huo ambao niliweza kushiriki naye mapenzi nakumbuka nilikuwa makini sana, sikutaka niweze kumpa ujauzito hivyo kila golinililokuwa nikilifunga nilihakikisha nalitoa nje ama kama niliweza kulifungia ndani basi nilihakikisha hakuwa katika siku zake za hatari.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)