NIFANYE NAMIMI KAKA (20)

0
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
“Hadithi inaitwa BADO UNAISHI MOYONI MWANGU na inahusu mapenzi.”
“Kuna kitu gani kipya katika hadithi yako?”
“Vipo vingi sana na ndiyo maana nataka kuifanyia filamu?”
“Unajua kwanini nimekuuliza hivyo?”
“Hapana sifahamu.”

SASA ENDELEA...
“Zipo hadithi nyingi sana za mapenzi pamoja na kazi nyingi ambazo wasanii wamekuwa wakiziingiza sokoni lakini zimekuwa hazifanyi vizuri kutokana na kufanana kwa hadithi, unakuta kisa ni kile kile kinarudiwa katika mtindo tofautitofauti.”
“Ni kweli kama unavyosema lakini hadithi hii ni ya kipekee sana.”
“Unauhakika itafanya vizuri?”
“Ndiyo ninauhakika?”
“Unaishi wapi?”
“Tandale.”
“Basi sawa kesho nitakupa maelekezo ili uweze kufika kwenye kampuni yangu na nitakukutanisha na wadau wa filamu ambao wataweza kulisimamia hilo.”
“Sawa nitashukuru sana.”
“Usijali,” alinijibu kisha akakata simu.

Kama nilivyotangulia kukusimulia hapo awali kuwa Irine alikuwa ni muigizaji maarufu sana wa filamu lakini pia alikuwa akimiliki kampuni yake ya uzalishaji filamu ambayo ilikuwa ikijulikana kama Kisoka Film Company. Ilikuwa ni moja kati ya kampuni bora ambayo ilikuwa ikiaminiwa sana katika kutengeneza filamu nzuri ambazo zilikuwa zikipendwa sana hususani filamu za kimapenzi.

Hakukuwa na kitu nilichokuwa nakipenda katika maisha yangu kama umaarufu, nilikuwa nikiupenda sana umaarufu. Niliamini katika umaarufu ningeweza kupata vitu vingi kwa urahisi moja ya vitu hivyo ni wanawake. Hata nilipoamua kuandika machombezo yangu katika mitandao ya kijamii kitu cha kwanza nilichokuwa nikikifikiria ni umaarufu. 

Naam! Katika hilo naweza kusema nilifanikiwa kwa kiasi fulani kwani licha ya kuwa na umaarufu wa mitandaoni niliweza kutembea na wanawake lukuki.

Ngoja nikuambie kitu ndugu yangu katika haya maisha kuna vitu vine vya msingi ambavyo mimi huwa naamini vikikosekana kwa mwanaume basi katika sekta nzima ya mapenzi atanyanyasika sana, vitu venyewe ni Elimu, Pesa, Umaarufu na Muonekano. Sikulazimishi uniamini haya niyasemayo ila najaribu kukuaminisha katika mkasa huu wa maisha yangu uliyonitokea.

Bado nilikuwa siamini kwamba niliweza kuzungumza na Irine ambaye aliniahidi kuhakikisha ndoto yangu ya kutoa filamu inatimia, kwa kweli nilikuwa nikijihisi furaha isiyokuwa na kifani. Niliamua kumpigia simu Evadia nyakati za usiku.
“Nimezungumza na Irine,” nilimwambia Evadia huku furaha ikiwa imenitawala kwa kiasi kikubwa.
“Anasemaje?” aliniuliza Evadia.
“Amekubali kufanya kazi na mimi.”
“Hongera mpenzi naamini utafanikiwa katika hilo.”
“Nakushukuru sana Mpenzi wangu najua bila wewe hili lisingeweza kutimia.”
“Usijali Mume wangu ni wajibu wangu kuhakikisha nafanya kila niwezalo mpaka natimiza kitu katika maisha yako.”
“Upo sahihi mpenzi wewe ndiyo daraja la mafanikio yangu.”
“Hata kwako pia wewe ndiyo kila kitu kwangu.”
“Wakati mwingine siamini kabisa.”
“Huamini nini?”
“Kama nimweza kukupata umekuwa wangu.”
“Amini nimeshakuwa wako.”
“Nakupenda sana Evadia, nakufananisha na ngozi ama damu mwilini ukiondoka mimi si kitu tena.”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Kwasababu nakupenda sana, moyo wangu unauhitaji ukaribu wako, unakupenda Evadia.”
“Nakupenda pia Dick mpaka nimeamua kukutambulisha kwa wazazi wangu hivi bado huamini kuwa nakupenda, nataka kuishi na wewe.”
“Kuna siri inanitesa moyoni mwangu.”
“Siri gani?”
“Naogopa kukupa siri hii utaitangaza.”
“Ina maana huniamini?”
“Nakuamini sana.”
“Basi niambie ni siri gani hiyo?”
“Kabla sijakwambia niahidi kwanza.”
“Nikuahidi nini?”
“Kuwa hutomwambia mtu mwingine zaidi, itabaki kuwa siri yako.”
“Nakuahidi sitamwambia mtu mwingine yule itabaki kuwa siri yangu.”
“Siri yenyewe….”
“Enhe! niambie ni siri gani hiyo?”
“Nakupenda,” nilimwambia neno ambalo lilimfanya acheke sana, hakutegemea kama ningeweza kumwambia neno lile kwa wakati ule.
“Halafu sitaki uchokozi wako.”
“Hahaha!”
“We cheka tu!”
“Ndiyo umenuna?”
“Ndiyo nimenuna.”
“Usinune bhanaa.”
“Niache mimi.”
“Jamani mpenzi we mwenyewe unajua kuwa tabasamu lako limeimiliki furaha yangu sasa ukinuna unafikiri nitaishi vipi?”
“Niache nimenuna.”
“Usinune mpenzi.”
“Sitaki niachee,” aliniambia Evadia huku akijifanya kununa mnuno wa kimapenzi. Nilianza kazi ya kumbembeleza huku nikijitahidi kutumia mashairi mazuri katika kumrudisha katika hali yake ya kawaida, hahaha! Mapenzi bhanaa! Ilifikia wakati akatulia na ule mnuno wote ukamuisha. Siku hiyo iliweza kupita.

Niliamka katika siku nyingine ya kitofauti sana, naweza kusema ilikuwa ni miongoni mwa siku niliyokuwa nikitamani itokee katika maisha yangu. Nilipokea simu kutoka kwa Irine ambapo aliweza akunielekeza mahali nilipotakiwa kwenda kwa lengo la kupeleka Hadithi yangu.
“Kwa hiyo nikifika hapo Mori naelekea wapi sasa?” nilimuuliza.
“Utanijulisha kuna mtu atakufuata hapo,” alinijibu.
“Sawa kwahiyo naruhusiwa kuja mida hii?”
“Ndiyo.”
“Basi sawa nakuja.”
“Oky,” alinijibu na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu.

Sikutaka kupoteza muda niliamka nikaenda kuoga, niliporudi kutoka bafuni nilivaa nguo zangu na sasa nikawa natoka kuelekea Sinza Mori mahali ambapo nilitakiwa kwenda kwa wakati huo. Nilikumbuka kumtumia ujumbe mfupi Evadia lakini hakuweza kunijibu kwa wakati huo. Niliamua kutoka.

Wakati nilipokuwa kwenye daladala simu yangu iliingia ujumbe mfupi, nilipoitoa mfukoni na kuufungua, ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Precious, alikuwa ameniandikia kwa kuniita jina langu
“Dick!”

Nilikumbuka siku chache zilizokuwa zimepita katika ile siku ambayo Precious alikuwa akiniomba nifanye naye mapenzi kwa lengo la kumpa ujauzito. Alikuwa akitamani kuwa na ujauzito kwa kipindi cha muda mrefu, siku ile aliponiomba kisha nikaweza kumkubalia ombi lake hakika aliweza kufurahi sana.

Sikutaka kujiuliza mara mbilimbili kuwa kitendo cha Precious kuamua kunitafuta alimaanisha nini. Nilifahamu bila shaka nilikuwa nakwenda kupewa taarifa za ujauzito wangu aliyokuwa ameubeba. Hata hivyo sikutaka kuwaza sana, nilipozikumbuka ahadi zake alizokuwa ameniahidi nilihisi kufanikiwa katika maisha yangu.

“Precious,” niliamua kumuandikia ujumbe kwa kumuita jina lake kama yeye alivyoweza kuniita, wakati huo daladala ilikuwa imefika kituo cha Sinza Kumekucha.
“Uko wapi?” aliniuliza.
“Naelekea Sinza mara moja kuna dili nafuatilia.”
“Asubuhi hii.”
“Ndiyo.”
“Dili gani hilo?”
“Dili tu.”
“Ndiyo ni dili gani?”
“La hadithi.”
“Sawa utarudi saa ngapi?”
“Sijajua ila nitakuambia wakati nikiwa narudi.”
“Kwani utachelewa sana?”
“Hapana sio sana.”
“Ok basi utakaporudi utaniambia ili nikufuate kuna sehemu nataka nikupeleke?”
“Sehemu gani?”
“Nitakwambia.”
“Wapi?”
“Mbona maswali mwengi Dick wewe usijali muda huo mimi nitakufuata halafu tutaenda wote?”
“Sawa,” nilimjibu kisha nikashangaa mbona hakuweza kunipa taarifa zozote za ujauzito.
“Au nilifunga nje siku ile?” nilijiuliza lakini sikutaka kujipa muda wa maswali mengi ambayo sikuwa na majibu yake. Nilihisi kuukosa utajiri.

Baada ya dakika kadhaa niliweza kufika Sinza Mori, nilikumbuka kumpigia simu Irine ili niweze kumjulisha kuwa tayari nilikuwa nimeshafika lakini nilipoamua kufanya hivyo nilishindwa, simu yangu ilikuwa imeisha salio.

Sikutaka kupoteza muda haraka nikaweza kununua muda wa maongezi kupitia huduma za kifedha, nikajiunga halafu nikaweza kumpigia simu Irine. Hakuwa akipokea simu kwa wakati huo, kila nilipokuwa nikimpigia simu yake ilikuwa ikiita mpaka ikawa inakata yenyewe. Nilihisi kama kudharauliwa sana, yani mbali na kupigia simu kama mara sita bado hakuweza kupokea.

“Huyu boya anajiona mzuri sana au huo umaarufu ndiyo unamchanganya mpaka anashindwa kupokea simu yangu,” nilijiambia huku nikifyonza, nilianza kuingiwa na hasira.
Baada ya dakika kama kumi ndipo alipoweza kunitumia ujumbe mfupi.
“Umefika tayari?”
“Ndiyo nimeshafika muda tu.”
“Ooh! Sorry upo hapo Mori.”
“Ndiyo.”
“Ok kuna mtu namuagiza anakuja kukufuata hapo.”
“Ok.”

Kama alivyoweza kuniambia baada ya dakika kadhaa niliiona gari aina ya NOAH yenye rangi nyeusi iliweza kunifuata. Sikutaka kushangaa sana kwani nilifahamu mtu niliyekuwa nikiwasiliana naye alikuwa ni mtu wa namna gani hivyo kuliona gari kama lile mbele yangu wala waikuweza kunishtua hata kidogo sana sana nilikuwa makini kumuangalia huyo mtu aliyenifuata alikuwa ni nani.
“Wewe ndiyo Dick?” aliniuliza dereva huku akinitazama kwa madharau.

“Ndiyo,” nilimjibu huku nikimtazama kwa kumthaminisha, alionekana kuwa mtu fulani mwenye hadhi yake.

“Panda kwenye gari,” aliniambia kisha nikafanya kama vile alivyosema, nilipopanda tukaweza kuondoka huku nikionekana kuwa mpole sana.

Hatimaye gari lilifunga breki mbele ya jengo moja kubwa ambalo nilipolizama kwa haraka niliweza kufahamu kuwa pale ni wapi. Kulikuwepo na bango moja kubwa lililokuwa limeandikwa kwa maandishi makubwa ambayo yalisomeka ‘KISOKA FILM PRODUCTION’ maneno hayo hayakuweza kunipa wakati mgumu wa kuweza kugundua kuwa pale nilikuwa sehemu gani. Nilifahamu na nilikuwa nikitabasamu muda wote.
“Karibu sana Dickson,” alinikaribisha Irine mara baada ya kuingia ofisini kwake.
“Asante sana.”
“Hivi ulisema unaishi wapi?”
“Tandale.”
“Anha! Maana nilisahau kabisa.”
“Una mambo sana.”
“Yani we acha tu! kichwa changu kinafikiria mambo mengi mpaka basi.”
“Itabidi upunguze.”
“Oooh! Umekumbuka kuja na hadithi?”
“Ndiyo nimekuja nayo.”
“Kwanza hongera unajitahidi sana kuandika.”
“Asante hata wewe nikupongeze kwa uchezaji mzuri wa filamu zako.”
“Hahahaha! asante.”
“Unaweza kuziteka hisia za mtazamaji pindi anapokutizama.”
“Mmmh! Kweli.”
“Sijawahi kumuongopea mtu wewe niamini.”
“Sawa nakuamini.”
“Hadithi ndiyo umesema inaitwa?”
“BADO UNAISHI MOYONI MWANGU.”
“Kwanini BADO UNAISHI MOYONI MWANGU na isiwe jina lingine?”
“Nadhani kisa nilichokizungumzia humo ndiyo kimenifanya niweze kuiita jina hilo.”
“Inaonekana itakuwa nzuri sana.”
“Ndiyo ni nzuri kwa ujumla,” nilimwambia huku nikimtazama usoni, alionekana kunivutia kila kiungo cha mwili wake. Si kwa macho yake, uso wake, rangi yake, midomo yake, dimpozi zake, kifua pamoja na umbo lake vyote hivi viliweza kunifanya nianze kuwaza ngono.

Irine aliweza kunikutanisha na baadhi ya waandaaji wa filamu aliyokuwa amewaajiri katika kampuni yake, alikuwa amedhamiria kufanya kazi na mimi kwa moyo mmoja bila kujali umaarufu aliyokuwa nao.
“Itabidi unikopie hii kazi yako kwenye hii flash ili baadae niipitie halafu nijue kama itafaa kufanyiwa filamu,” aliniambia Christopher Director mkubwa wa na Irine.
“Sawa haina tatizo mkuu,” nilimjibu kisha nikaondoka zangu huku nikiwa nimechukua namba zake za simu.
“Kwani wewe uko wapi?”
“Mimi niko hapa kituoni Mori.”
“Utaweza kunisubiria nikufuate?”
“Uko mbali sana?”
“Hapana.”
“Uko wapi?”
“Shekilango nakuja hapo.”
“Sawa nakusubiri.”
“Sawa honey love you.”
“Love you two.”

Zilikuwa ni chatting kati yangu na Precious ambaye alikuwa ameniahidi kuwa alikuwa anakuja kunichukua. Haikuchukua dakika nyingi aliweza kufika, nikapanda kwenye gari lake, nikambusu kisha safari ikaanzia hapo.
“Kwani tunaenda wapi?”
“Wewe wasiwasi wako ni nini?”
“Hapana ila nimeuliza tu!”
“Usijali tukifika utajua,” 

Alinijibu kisha sikutaka tena kuzungumza, niliamua kukaa kimya.Safari yetu ilikwenda kuishia Mbezi Beach mbele ya nyumba moja ya kifahari sana, niliitazama nyumba hiyo katika macho ya matamanio, Ilionekana kuwa ni nyumba ya kisasa ambayo ilisheheni kila kitu cha kuvutia, kama ungepata bahati ya kuitazama hakika ungeyasahili maneno yangu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)