NIFANYE NAMIMI KAKA (21)
Zephiline F Ezekiel
---
JINA: NIFANYE NAMIMI KAKA
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Alinijibu kisha sikutaka tena kuzungumza, niliamua kukaa kimya.Safari yetu ilikwenda kuishia Mbezi Beach mbele ya nyumba moja ya kifahari sana, niliitazama nyumba hiyo katika macho ya matamanio, Ilionekana kuwa ni nyumba ya kisasa ambayo ilisheheni kila kitu cha kuvutia, kama ungepata bahati ya kuitazama hakika ungeyasahili maneno yangu.SASA ENDELEA...
“Hapa ni wapi?” nilimuuliza Precious kisha akatabasamu, hakunijibu lolote badala yake alipiga honi kuashiria kuwa alikuwa nje na baada ya dakika chache geti liliweza kufunguliwa na kijana mmoja ambaye kwa macho ya harakaharaka alionekana kuwa mlinzi.
Hatimaye tukaingia ndani ya nyumba ile ya kifahari kisha Precious akaenda moja kwa moja mpaka eneo maalumu la kuegesha gari, akaliegesha vyema kisha tukashuka.
Macho yangu yalikumbana na gari la kifahari aina ya BMW 545 yenye thamani ya shilingi milioni hamsini na sita lililokuwa limeegeshwa pembeni na pale ambapo Precious alikuwa ameegesha gari lake. Sio siri nilizidi kujionea maajabu tu! kwani mpaka kufikia wakati huo Precious hakuwa ameniambia lolote lile.
“Vipi mpenzi,” aliniambia Precious kisha akanisogelea na kunishika mkono, tukaingia ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa imekamilika kila kitu ndani, hakukuwa na kasoro yoyote.
“Unaionaje hii nyumba?” aliniuliza swali nililoliona kuwa kama la kunikejeli kwani ukweli nyumba ilikuwa ikionekana kuwa nzuri hata bila kuulizwa lolote.
“Mbaya tu!” nilimjibu huku nikijifanya kama sielewi. Alicheka kisha akajizuia.
“Baby embu acha masihara ujue mimi nakuuliza kwa kumaanisha.”
“Kiukweli nyumba ni nzuri sana inaonekana kukamilika kwa kila kitu kasoro kitu kimoja tu!”
“Kitu gani?”
“Hakuna watu,” nilijibu kisha akacheka tena.
Alionekana kuwa na furaha sana, uso wake ulitawaliwa na tabasamu mwanana lililozidi kumfanya aonekane kuwa wa aina yake.
“Dick,” aliniita baada ya ukimya mfupi kutawala.
“Niambie malkia wangu,” nilimjibu huku nikimshika kiuno chake laini kilichogawanyika mithili ya mdudu nyigu.
“Asante sana kwa zawaidi uliyoweza kunipa katika maisha yangu, siwezi kukusahau.”
“Zawadi?”
“Ndiyo.”
“Zawadi gani?”
“Mimba.”
“Unasema?”
“Nina mimba yako Dick,” aliniambia kisha nikajifanya kama nimeshtushwa na taarifa hizo ambazo sikuzitegemea.
“Nini mbona umekuwa hivyo?”
“Hamna, siamini kama nimeweza kukupa ujauzito.”
“Amini Dick, wewe ndiyo mwanaume pekee ambaye umeweza kunibadilisha jina, naamini hivi karibuni na mimi nitakwenda kuitwa mama wa mwanao, nimebeba kiumbe chako Dick,” aliniambia.
“Ujue siamini kabisa.”
“Amini Dick nina kiumbe chako tumboni.”
“Dah!”
“Ila baby usijali unakumbuka nilikuahidi nini?”
“Nini?”
“Nilikuahidi vitu vingi sana ila kubwa ni kukununulia nyumba, usafiri pamoja na kukupa mtaji utakaoanzia katika biashara yako ya vitabu.”
“Ndiyo nakumbuka.”
“Basi hivi vyote unavyoviona mbele yako kuanzia sasa vipo chini yako,” aliniambia Precious maneno ambayo nilihisi wenda alikuwa katika utani, alikuwa akinitania lakini haikuwa hivyo bali kila ambacho alichokuwa akikizungumza alikuwa akikimaanisha.
“Ina maana ile BMW na hii nyumba unataka kuniambia vyote kuanzia sasa ni mali yangu?” nilimuuliza.
“Ndiyo baby,” alinijibu Precious huku akionekana kutojali lolote lile.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa mimi kumiliki nyumba nzuri, gari la kifahari na pia kukabidhiwa kiasi cha pesa ambacho nilikitumia kama mtaji wa kutoa vitabu vyangu. Niliamua kuhama Tandale na sasa maisha yangu yakahamia Mbezi Beach.
Sikutaka kufikiria lolote kuhusu mume wa Precious pamoja na taarifa zile za ujauzito. Nilichokuwa nakiangalia kwa wakati ule ni ule utajiri wa ghafla! niliyoweza kuupata katika maisha yangu, ulikuwa ni utajiri ambao kwa kweli kama ingetokea ukaniuliza niliupata katika njia zipi, jibu pekee ambalo ningeweza kukujibu ni kuwa nilitembea na mke wa mtu kisha akaweza kunihonga wala hakukuwa na njia nyingine.
Siyasemi haya ili nikushinikize na wewe unayeyasoma maandishi haya uende ukafanye kama mimi nilivyofanya lahasha! isipokuwa ipo sababu ya msingi ya kukuandikia haya kwani naamini mwisho wa siku utaweza kujifunza kitu kupitia mimi Mr. Chombezo au ukipenda unaweza kuniita Dick Mapenzi. Majina haya ndiyo yaliyoweza kuniponza Dick mimi ambaye leo naishia kusimulia tu!.
Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kipekee sana kwangu, kwanza nakumbuka nilimtafuta Mick simuni kisha nikamuelezea kila kitu kichokuwa kimetokea, aliweza kunishangaa sana.
“Dick ujue una michezo hatari sana,” aliniambia.
“Kwanini unasema hivyo?”
“Unajisifia kabisa umempa mke wa mtu mimba halafu kakupa nyumba unafurahi kabisa.”
“Sasa wewe ulitaka ninune au? Kwanza yeye mwenyewe ndiyo kaniletea shobo mimi nifanye nini sasa?”
“Ndugu yangu unapotea.”
“Acha uzoba wewe hapa ni mjini na mjibu kuishi ni mipango hivi unafikiri kwa maisha haya yalivyo magumu halafu anatokea mtu anakupa pesa utaanzaje kuzikataa.”
“Dick mke wa mtu sumu.”
“Hayo ni maneno tu! siku hizi tunakula mpaka vya nyongeza.”
“Unajua unafanya masihara lakini ipo siku hivyo vitu vitakutokea puani.”
“Ndugu yangu sasa naona unafika mbali kama vipi baadae ngoja leo nitafute kahaba nilale naye huku maana tayari nimeshakuwa Don,” nilimwambia kisha nikakata simu.
Kitendo cha kuhamia Mbezi Beach kilikwenda kuufungua ukurasa mpya hata katika upande wa wasichana niliyokuwa nikitembea nao, sikutaka kuendelea kutembea na wasichana kama akina Helena ambao walionekana kuwa na shida, niliamini kama ningeweza kuwa nao basi hakukuwa na kitu cha ziada ambacho kingeweza kubadilika sanasana ndiyo kwanza wangezidi kunipa mawazo ya kuwahudumia wakati mimi mwenyewe nilikuwa nikihudumiwa.
Nilianza kubadilika kimavazi, kila siku nilionekana kupendeza sana hata wale wasichana waliyokuwa wakiziona picha zangu Instagram nilizokuwa nimezipost huku nikiwa nimeegemea gari langu la BMW hakika ziliwachanganya sana.
“Mbona umehama bila kuniambia?” aliniuliza Evadia usiku mmoja nilipoamua kumpigia simu.
“Nisamehe mpenzi nilisahau kukuambia,” nilimjibu.
“Umehamia wapi?”
“Sasa hivi nimehamia Mbezi ila usijali kesho lazima nikuone na utakuja kupafahamu.”
“Sawa Mume wangu nitafurahi.”
“Ukitoa wewe hakuna mapenzi tena, wewe ndiyo maana ya mapenzi yangu.”
“Umeanza na vijimaneno vyako.”
“Huo ndiyo ukweli.”
“Halafu nimekumis baby.”
“Nimekumis pia.”
“Njoo basi sasa hivi mpenzi, nauhitaji ukaribu wako.”
“Nikija siunajua nini kitatokea?”
“Haya nakuja.”
“Njoo tu! babyyy nitakupa ondoa shakaa.”
“Hodi.”
“Karibu.”
“Asante, mbona sasa hujachojoa nguo?”
“Tayari baby.”
“Sawa, sogea basi.” “Tayari baby nipeee,” aliniambia kwa sauti ya kimahaba ambayo ilinifanya akili yangu ibadilike na kuanza kufikiria ngono na kila ambacho nilikuwa nikikizungumza kwa wakati huo hakikuwa na maana nyingine zaidi ya ngono.
Kilichoendelea kusikika kwa upande wa pili ni miguno pamoja na sauti za kimahaba alizokuwa akizitoa Evadia, alikuwa akilalamika kana kwamba nilikuwa nikifanya naye mapenzi kumbe yalikuwa ni mapenzi yaliyofanyika simuni. Kutokana na uhodari wangu katika kucheza na michezo hii nilizidi kumpagawisha kwa kumpa muwashawasha uliyozidi kumuacha mpaka akawa analia kwa kuomba utamu wangu.
“Ooooooh, babbyyyyyyy nipe nipeeee ooooohhh chukuaaaa yoteeee yakoooo aaaasssshhhh ooooohhh aaaaaaah,” alitokwa na miguno wakati huo nilikuwa nikifanya naye mapenzi kwenye simu.
Sauti pamoja na miguno ile ya kimapenzi aliyokuwa akiitoa haikukoma, aliendelea kulalamika huku akidai kuwa alikuwa akiumia. Nilifahamu fika ni maumivu gani aliyokuwa akiyapata, yalikuwa ni maumivu ya utamu aliyokuwa akiutamani kupata kutoka kwangu.
“Dick naumiaaaaaa,” aliniambia kwa sauti la kulalamika. Sikutaka kumjibu lolote, niliendelea na mchezo wangu wa kumpandisha nyege.
“Aaaahhh Dick acha bhnaaa mwenzio naumiaaaa,” alizidi kulalamika.
Nakumbuka siku hiyo niliutumia muda mwingi sana katika kufanya mapenzi na Evadia kwa njia ya simu, yalikuwa ni mapenzi fulani hivi ya kimzaha yaliyotukutanisha kihisia na kuhisi kama tulikuwa tukifanya mapenzi kiuhalisi. Naam! kama uliwahi kuucheza mchezo huu hakika utakuwa umefahamu ni nini ninachokimaanisha.
Mchezo huo uliniweka katika wakati mgumu sana, hali ya mtarimbo wangu haikuwa shwari, alikuwa katika midadi ya kuukamata utamu wa mwanadada Evadia kwa wakati huo.
“Dick…”
“Niambie Mpenzi wangu.”
“Umefanya mpaka nimechafua nguo.”
“Hahaha! Pole.”
“Sitaki.”
“Hutaki nini sasa kwani hujafurahia tendo?”
“Nimefurahia.”
“Sasa mbona usemi asante?”
“Asante Dick.”
“Mmh! Mpaka nikuombe?”
“Hapana Darling.”
“Nikuulize?”
“Ndiyo niulize.”
“Unanipenda?”
“Ndiyo nakupenda, mbona unaniuliza swali hilo?”
“Nilitaka kufahamu.”
“Dick nakupenda sana wala hakuna Mwanaume ambaye nimewahi kumpenda zaidi yako hata Ex-boyfriend wangu sijawahi kumpenda kiasi hiki.”
“Nitaamini vipi kuwa unanipenda?”
“Baby kitendo cha kukutambulisha kwa wazazi wangu nahisi ni sababu tosha ya wewe kuniamini.”
“Unaonekana kuwa mwanamke ambaye niliwahi kumuona sehemu.”
“Mwanamke yupi na ni sehemu gani ulimuona?”
“Nimekuwa nikiiamini ndoto kwa muda mrefu, niliishi maisha hayo ya kumuota msichana mrembo ambaye niliamini huyo ndiyo mwanamke wa maisha yangu, sikuwa nafahamu anafananaje sura yake, umbo lake au hata tabia yake lakini kupitia wewe nimeweza kuiamini ile ndoto. Wewe ndiyo huyo mwanamke niliyekuwa namuota kila siku.”
“Nafurahi kusikia hivyo mpenzi wangu, kila siku namuomba Mungu atujaalie kila tulilolipanga liweze kutimia.”
“Hata mimi nafanya hivyo,” nilimwambia Evadia maneno ambayo kuna kipindi nafsi yangu ilikuwa inanisuta. Sikuwa nikimaanisha kila neno nililokuwa nikilisema, kuna wakati nilikuwa nikizungumza kuwa kama sehemu moja wapo ya sanaa ya utunzi niliyokuwa nao. Maneno yangu mazuri, matamu yenye kumsisimua msichana pindi anisikiapo yaliweza kumuingia vyema Evadia.
Alikuwa akiniamini kupitiliza na hili ndiyo kosa kubwa ambalo alilokuwa amelifanya bila kujua. Nilikuwa nikizungumza na wanawake wengi sana, si kwa kuzungumza nao simuni tu lahasha! bali wengine nilikuwa nikichat nao muda mrefu kitendo ambacho kilinifanya niwe mvivu kujibu jumbe za Evadia pamoja na kupokea simu zake kwa wakati, hilo lilikuwa ni tatizo kubwa ambalo liliweza kuzua ugomvi kati yetu lakini nilipojaribu kumpigia simu yake na kuitumia fursa hiyo kumdanganya kwa mpangilio wa maneno yangu mazuri hakika aliweza kunielewa na kunisamehe.
Siku iliyofuata niliweza kumleta Evadia katika nyumba niliyokuwa nimehamia maeneo ya Mbezi Beach. Alionekana kushangaa kila kitu kilichokuwa mbele yake. Nilifahamu siku hiyo ningeweza kukumbana na maswali lukuki kutoka kwa Evadia ambaye asingeweza kuamini kirahisi mabadiliko yangu ya kimaisha hasa katika kipindi kama kile.
“Hii ni nyumba yako?” aliniuliza wakati nilipokuwa nikimzungusha sehemu mbalimbali za ile nyumba.
“Ndiyo,” nilimjibu huku nikitabasamu kumuonyesha kuwa hakukuwa na tatizo lolote bali kila kitu alichokuwa akikishuhudia kilikuwa ni mali yangu.
“Na lile gari je?”
“Baby vyote ni mali yangu.”
“Umewezaje kumiliki vitu hivi Dick, umefanya kazi gani mpaka uweze kumiliki mali zote hizi.”
“Evadia mjini ni mipango, kila mtu unayemuona anaishi katika mji huu basi fahamu kuwa anaishi kwa mipango. Nilifahamu kuwa utaweza kushangaa hasa kwa mali hizi ambazo nimeweza kuzimiliki lakini nikuondoe wasiwasi mimi ni mtafutaji na siku zote ulizokuwa unaniona nyuma ya pazia kulikuwa kuna mishe nazifanya na ndizo zimeweza kuzaa matunda haya.”
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni