NIFANYE NAMIMI KAKA (23) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 24 Machi 2021

NIFANYE NAMIMI KAKA (23)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Kila siku alikuwa akiandikwa vibaya magazetini, alikuwa akiandikwa kuwa alikuwa akitembea na wanaume tofautitofauti ambao wengi wao walikuwa ni watu wenye wadhifa fulani, hilo lilizidi kuniogopesha.
“Kuna kitu unataka kuniambia?” aliniuliza.

SASA ENDELEA...
“Hapana,” nilimjibu huku nikiweweseka na jibu langu, nilikuwa nimeshapagawa.
“Niambie usiogope au bado unahisi hujanizoea?” aliniuliza huku akiendelea kula chakula katika mpangilio uliyozidi kupendeza, hakuonekana kuwa na makuu hata kidogo na kila nilipokuwa nikiendelea kumtazama mapigo ya moyo wangu yalizidi kwenda kwa kasi kuhofia uwepo wa Irine. Kwa wakati huo nilikuwa tayari nimeshamsahau Evadia na Precious mwanamke ambaye alikuwa akinihudumia kwa kila kitu.

Nilichoamua kufanya kwa wakati huo ni kuchukua maamuzi, nikayapanga maneno yangu vyema halafu neno moja nikaliunganisha na lingine kisha nikatiririka katika kumpangilia vina, nakumbuka kuna baadhi ya maneno nilikuwa nikiyatoa katika dayaloji ya machombezo yangu ambayo niliamini yangeweza kumvutia kiasi kwamba akawahi kunikubalia na huo ndiyo ungekuwa mwanzo wa umaarufu wa kuandikwa magazetini na kwenye mitandao ya kijamii.

“Hapana Irine unajua kuna vitu vinaniweka katika wakati wa mawazo sana.”
“Vitu gani hivyo?”
“Uzuri wako,” nilimwambia kisha akatabasamu.
“Unajua unavituko Dick sasa uzuri wangu umefanyaje?”
“Irine wewe ni mwanamke mzuri sana una kila sifa za kumvutia mwanaume yoyote yule, ujue mpaka sasa hivi siamini kama zile habari unazoandikwa magazetini ni za kweli au?”
“Dick unajua mimi ni staa na kama unajua maisha yetu sisi mastaa kuchafuliwa na kuandikwa kila aina ya mabaya mitandaoni, magazetini ni sehemu moja wapo ya maisha yetu.”
“Ina maana unataka kuniambia hakuna ukweli wowote kuhusu ile habari niliyoisikia?”
“Habari gani?”
“Kuhusu unatembea na kigogo.”
“Hapana hazina ukweli wowote.”
“Kuna kitu nataka kukuambia ila nahisi nafsi inasita.”
“Kitu gani niambie usiogope.”
“Irine sijui kama utaweza kukubali.”
“Kwanini nisikubali wewe niambie kuwa huru.”
“Irine nakupenda,” nilimwambia.

“Unanipenda?” aliniuliza swali nililolitegemea kwa wakati ule, sikutaka kung’atang’ata maneno, nikaanza kumchombezo.
“Ndiyo nakupenda sana Irine wala siwezi kukuficha hilo,” nilimwambia.
“Unanipenda kwasababu mimi ni maarufu au?”
“Nakupenda jinsi ulivyo wala sijakupendea huo umaarufu wako.”
“Nitaamini vipi hayo unayoyasema kuwa ni kweli?”
“Amini tu! ila labda nikuulize swali?”
“Niulize?”
“Hivi unaweza kumuamini daktari akikuambia kuwa mgonjwa wako anasumbuliwa na ugonjwa fulani?”
“Ndiyo naweza kumuamini.”
“Kwanini?”
“Kwasababu yeye ni daktari na ni kazi yake.”
“Kwanini hutaki kuniamini mimi shuhuda wa hisia zangu.”
“Dick siwezi kukuamini kirahisi hivyo.”
“Kwani uko na mtu?”
“Ofcourse nilikuwa naye ila kwa sasa tumeachana.”
“Ni nani huyo au ni…”
“Huyo huyo.”
“Nani sasa?”
“Juma Hiza.”
“Unaweza kuniambia kwanini mliachana?”
“Unajua katika mapenzi hasa kwa sisi mastaa kuna vitu vingi sana huwa vinatokea ila naweza kusema ilifikia wakati kila mapenzi hayakutakiwa yaendelee.”
“Kwani bado unampenda?”
“Sidhani kama kuna ukweli katika hilo na kama ningekuwa nampenda ungetuona tuko pamoja.”
“Nini kilitokea kati yenu?”
“Hee! Dick mbona maswali mengi kama mwandishi wa habari.”
“Inamaana umesahau kuwa mimi ni mwandishi wa hadithi?”
“Sijasahau.”
“Lakini kumbuka kiu yangu ni kutaka kufahamu ukweli kuhusu wewe.”
“Ukweli gani ambao unataka kuufahamu?”
“Ukweli kuhusu mapenzi yako.”
“Nafikiri ukweli wangu ni ndiyo huo na kuhusu kutoka kimapenzi katika maisha yangu nimewahi kutembea na mwanaume mmoja ambaye ni huyo Juma Hiza na baada ya hapo sijawahi kujihusisha na mapenzi na mwanaume mwingine.”
“Kweli?”
“Ndiyo sioni sababu ya kukudanganya Dick na kama kiu yako ni kutaka kuufahamu ukweli nadhani tayari umeshafahamu.”
“Na yale magazeti yanayoandika habari kuwa unatembea na wanaume tofautitofauti vipi?”
“Dick mimi ni staa na mambo kama hayo ya kuandikwa vibaya ni kawaida.”
“Asante kwa kuwa mkweli kwangu hata hivyo najivunia kukufahamu, unaonekana kuwa tofauti na wanawake wengine.”
“Asante Dick.”
“Usijali.”
“Ila kuna kitu Dick nataka kukuuliza.”
“Kitu gani?”
“Samahani lakini kwa kukuuliza swali hili ila inanibidi nikuulize.”
“Bila samahani niulize tu.”
“Hivi katika maisha yako umewahi kutoka na wanawake wangapi?”
“Nimetembea na mwanamke mmoja tu na tena aliwahi kuniumiza.”
“Kivipi?”
“Sikuwa na pesa hivyo wenye pesa walinipiku.”
“Pole sana.”
“Nishapoa na maumivu nimeshaanza kuyasahau.”
“Unaweza kuniambia ulimpenda kiasi gani?”
“Kwa kweli naweza kusema nilimpenda mithili ya nafsi na mwili kimoja kikikosekana basi hakuna maana ya uzima.”
“Una maneno Dick.”
“Hapana najitahidi kukuweka uwe karibu yangu lakini umekuwa kama ndege naona unakwea matawi tu.”
“Hahaha.”
“Niambie kitu kimoja.”
“Dick tatizo mimi sikuamini.”
“Kwanini huniamini?”
“Sijui hata.”
“Au bado unampenda Juma Hiza?”
“Hapana,” alinijibu Irine huku akiwa ameyaelekezea macho yake chini.
Kwa kweli ilikuwa ni kazi kubwa sana katika kumshawishi Irine msichana maarufu ili aweze kuwa na mimi kimapenzi, niliutumia ulimi wangu vyema katika kupangilia maneno, ndoano niliyokuwa nikiitupa baharini ya kumnasa samaki upendo kuna muda nilikata tamaa nikahisi kukosa kila kitu.

Juma Hiza huyu ndiye mwanaume aliyekiri kutoka naye kimapenzi, alikuwa ni miongoni kati ya wanamitindo wakubwa hapa nchini, kipindi cha nyuma mapenzi yao yalionekana kukolea, kila kona walikuwa wakisikika wao tu. Kwenye magazeti hakukuwa na habari nyingine zilizoandikwa zaidi ya mapenzi yao lakini mwisho wa siku penzi lao liliweza kufa.

Umaarufu wa mwanaume huyo pamoja na nguvu kubwa aliyokuwa nayo ilizidi kuniogopesha lakini nilijivika vazi la ujasiri kisha nikaendelea kuamini kumpata Irine. Nilitofautiana naye kwa vitu vingi sana hivyo sikutaka kukubali kuona mapungufu yoyote.

Niliendelea kubembeleza penzi kila siku, nililia kwa kudanganya, nikafanya kila niwezalo, visa vyote nikafanya mpaka Irine akaweza kunikubalia.

“Dick naomba unipende kweli, usicheze na hisia zangu, nimekukubalia ombi lako,” aliniambia Irine maneno yaliyonifanya nizidi kujiona gwuji wa mchezo huu hatari wa mapenzi na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa penzi jipya na yeye. Lilikuwa ni penzi lililonipa umaarufu ambao sikujua kama mwisho wa siku ungeweza kunipa funzo katika maisha yangu.

Nilianza kubadilika baada ya kufanikiwa kumpata Irine kimapenzi, nilijiojna kuwa zaidi ya kila kitu hata kwa upande wa mapenzi niliyokuwa nayo kwa Evadia nilianza kuyapunguza. Sikuwa tena ni mtu wa kumtafuta kama ilivyokuwa kawaida yangu, nilisubiri mpaka yeye ndiyo anianze kisha mimi niendelee.

Niliamua kufanya hivyo kwasababu nilijua wazi kuwa alikuwa akinipenda sana kuliko kitu chochote kile, alikuwa akinipenda kiasi kwamba kuna kipindi nilivyokuwa nikikaa kimya nilikuwa nikimuumiza.

“Kwanini siku hizi umebadilika hivyo?” aliniuliza siku moja alipokuja nyumbani kwangu ghafla! majira ya mchana, alikuwa ameshindwa kuvumilia ukimya ule ambao ulikuwa umetawala kati yetu siku zote hivyo aliamua kunifuata kwa lengo la kutaka kujua ni nini kilichokuwa kinanifanya mpaka nikae kimya kiasi kile, kwa akili ya harakaharaka alihisi kwa ujio wake ule angeweza labda kunifumania na mwanamke mwingine lakini haikuwa hivyo, alinikuta peke yangu tena kwa wakati huo nilikuwa sebuleni nikiandika hadithi kwenye laptop yangu.

“Nimefanyaje kwani?” nilimuuliza huku nikionekana kuwa bize na kuandika.
“ina maana hujanisikia au?” aliniuliza kwa sauti ya kunifokea kisha nikamtazama, alionekana kuwa na hasira kupitia uso wake aliyokuwa ameukunja mithili ya ngozi ya bibi kizee.
“Evadia kwani kosa langu ni lipi?” nilimuuliza.
“Kosa lako hulifahamu?” aliniuliza
“Kama ningelifahamu hivi ningekuuliza kweli?” nilimuuliza.
“Dick hivi kwanini siku hizi unanidharau sana,” aliniambia.
“Nakudharau kivipi mbona sikuelewi?” nilimuuliza.

Nilijikuta naanza kupoteza mapenzi kwa Evadia, kila nilipokuwa nikimtazama nilihisi kumchukia sana, kila sehemu ya kiungo cha mwili wake nilipokitazama sikuhisi msisimko wowote, nilikuwa nimeshamkinai japo sikumwelieza ukweli wa jambo hilo lakini kupitia visa na mikasa niliyokuwa namfanyia nilihisi wenda angeweza kung’amua lolote kuwa nilikuwa nikimchukia kupita maelezo na hivyo hakutakiwa tena kuishi na mimi. 

Nilijisahaulisha yale yote ambayoaliwahi kunifanyia katika maisha yangu, nilichokuwa nikikitazama kwa wakati huo ni mapenzi niliyokuwa nayo kati yangu na Irine.

“Dick siko hapa kwa ajili ya ugomvi na wewe,” aliniambia huku akinitazama kwa macho ya huba, niliamua kuamka pale kwenye kochi nilipokuwa nimekaa nikasimama kisha nikaanza kumogelea taratibu.
“Kwahiyo kama haupo hapa kwa ajili ya ugomvi umefuata nini sasa?” nilimuuliza swali ambalo niliamini lilikwenda kumuumiza moyoni mwake lakini sikutaka kujali lolote.
“Dick hivi kwanini unanichukia?” aliniuliza.
“Hicho ndiyo ulichokifuata?”
“Hapana ila nataka kufahamu kwanza.”
“Unataka kufahamu nini?”
“Dick au kisa nimekupa moyo wangu wa mapenzi unaumiliki na umegundua kuwa nakupenda kwa dhati ndiyo sababu unanifanyia haya?”
“Mbona sioni tatizo lolote huo ni wasiwasi wako.”
“Hapana Dick naomba uniambie.”
“Evadia unajua sikuelewi.”
“Dick nikuulize?”
“Ndiyo niulize lakini usiniulize maswali ya shule ya msingi.”
“Unanipenda?”
“Aaaggghh! Hivi hatuelewani au? Nimekuambia sitaki uniuliza maswali ya kitoto sasa hilo ni swali gani?”
“Naomba unijibu Dick.”
“Jibu unalo wewe mimi siwezi kukujibu.”
“Dick unasemaje?”
“Swali lingine?”
“Hivi kweli una mpango wa kufunga ndoa na mimi kweli?”
“Sahau kabisa kuhusu ndoa tena futa kabisa katika ufahamu wako. Kwasasa sipo na mipango hiyo.”
“Unasemaje?”
“Sina mpango wa kuoa kabisa kama unaona unaharaka na ndoa nenda kaolewe na wanaume wengine nimekukubalia sawa,” nilimwambia maneno ambayo yalimtoa machozi, hakutaka kuamini kama mimi ndiye ambaye nilikuwa nikimwambia maneno yale yaliyokuwa na mkuki wenye sumu kali uliyokwenda kukika katika kuta za moyo wake. Machozi yalikuwa yakimbubujika mfululizo.

“Hajafa mtu hapa tafadhali usiniletee uchuro sawa wewe kahaba,” nilimwambia kisha nikaanza kumtolea maneno machafu ambayo kiukweli mengine nafsi ilikuwa ikinisuta pindi nilipokuwa nikiyatamka, sikupanga kumfanyia yale ambayo nilikuwa nikimfanyia lakini nilijikuta tu! nikifanya bila kutarajia.
“Dick umenifanya niwachukie waandishi wote wa hadithi mitandaoni,” aliniambia Evadia huku akiyafuta macho yake.
“Sasa ulitumwa unipende embu chukua time ondokaaa.”
“Dick.”
“Sikutaki Evadia naomba tuachane.”
“Unasemaje?”
“Sikutakii.”
‘Dick hivi ni wewe kweli?”
“Sasa kama si mimi utakuwa unaongea na nani?”
“Nini kimekupata?”
“Natumia lugha adhimu kabisa ya Kiswahili, nimesema sikutaki na naomba uondoke nyumbani kwangu sawa,” nilimwambia kisha nikaanza kumfukuza bila huruma. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa penzi langu na Evadia, mwisho ambao niliweza kumpa maumivu ambayo hayakutarajia kuyapata.

Baada ya kupita miezi tisa hatimaye Precious aliweza kujifungua mtoto wa kiume, alikuwa ni mtoto ambaye aliyefanana na mimi kila kitu, Precious hakuacha kuniambia kuwa ilitakiwa kubaki kuwa siri kati yetu kwani mpaka kufikia 

Wakati ule mume wake alikuwa bado hafahamu lolote lile, niliutumia udhaifu wa mume wake katika kujivika vazi la ubaba kwa mwanamke ambaye alikuwa ni mke wa mtu, naweza kusema katika hilo nilikuwa kipofu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni