NIFANYE NAMIMI KAKA (24) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 24 Machi 2021

NIFANYE NAMIMI KAKA (24)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Wakati ule mume wake alikuwa bado hafahamu lolote lile, niliutumia udhaifu wa mume wake katika kujivika vazi la ubaba kwa mwanamke ambaye alikuwa ni mke wa mtu, naweza kusema katika hilo nilikuwa kipofu.

SASA ENDELEA...
“Hongera mpenzi kwa kujifungua salama,” nilimwambia Precious wakati nilipokuwa nimempigia simu kwa lengo la kumpongeza. Wakati huo alikuwa bado yupo hospitalini.
“Asante yani Dick nina furaha,” aliniambia kwa sauti iliyoonyesha kufurahishwa.
“Najua furaha uliyonayo inaletwa na nini,” nilimwambia.
“Hatimaye nimekuzalia dume,” aliniambia.
“Tena Dume haswaa!”
“Dick asante kwa kunifanya nimekuwa mama sasa hivi,” aliniambia.
“Precious asante na mimi kwa kunifanya nimekuwa baba sasa hivi,” nilimwambia maneno ambayo nilimuiga kwa kubalidili neno baba. Alicheka sana.
“Mbona unacheka?” nilimuuliza huku na mimi nikicheka.
“Dick unanifanya nakuwa mwenye furaha sana,” aliniambia kwa sauti ya upole.
“Kwanini?” nilimuuliza.
“Sijui hata kwanini.”
“Nikwambie kwanini?”
“Ndiyo niambie.”
“Ni kwasababu moyo wangu na wako umeendana na laiti kama usingeendana nafikiri leo hii tusingekuwa pamoja.”
“Ni kweli mpenzi wangu yani sio siri nakupenda sana.”
“Hata mimi nakupenda pia?”
“Halafu nilitaka kusahau kitu.”
“Ulitaka kusahau nini tena malkia wangu?”
“Jina la mtoto?”
“Ina maana mpaka kufikia muda huu bado hana jina?”
“Ndiyo.”
“Ulikuwa unasubiri nini sasa?”
“Nilikuwa namsubiria baba yake ili aweze kumpa jina,” aliniambia kisha nikacheka.
“Usicheke embu mpe jina mwanangu tafadhali.”
“Tumuite Mzigo wa kuni Tabu Tupu.”
“Heee! Ndiyo jina gani hilo sitaki Dick, naomba mwanangu umpe jina zuri.”
“Ok basi tumuite Nickson.”
“Hahaha kwanini Nickson?”
“Ili isound sawasawa na jina la Baba yake yani Nickson Dickson.”
“Jamani nimelipenda bure.”
“Basi tumuite hivyo.”
“Unataka mwanao aje afanye kazi gani akiwa mkubwa?”
“Nataka nay eye aje kuwa mwandishi wa hadithi kama Baba yake.”
“Unataka na yeye atoe filamu?”
“Ndiyo wanasema maji yanafuata mkondo.”
“Nitafurahi kama ikiwa hivyo.”
“Usijali kila kitu kinawezekana.”
“Sawa Mume wangu,” aliniambia Precious.

Katika mazungumzo yetu sikutaka kabisa kugusia suala la mume wake wala kuhusu ndugu zake, nilifahamu fika kuwa walikuwa wakizifahamu habari zile za Precious, nilijitoa ufahamu na hakukuwa na mada nyingine ambayo nilitaka kuzungumza zaidi ya mada iliyonihusu mimi na mtoto.

Nilifanya hivyo ni katika harakati za kutomfanya Precious achukie, nilifahamu vyema kuwa alikuwa ni mwanamke wa aina gani, hakupenda pindi tulipokuwa katika mazungumzo neno au jina la mume wake alisikie, hilo nililifahamu na ndiyo sababu sikutaka kumuuliza lolote kuhusu mume wake wala ndugu zake. 

Nilijifanya kuwa jasiri nikiamini kuwa kwa kufanya hivyo nilikuwa natengeneza mazingira ya kusifiwa kuwa hakika nilikuwa kidume haswaa, furaha yangu ilikuwa nikuona nasifiwa kila wakati na Precious hasa katika kitendo kile cha kumfanya kuwa na mtoto.

“PENZI LA DICK MAPENZI LAMTEKA IRINE.”, “IRINE HAONI WALA HASIKII KWA PENZI LA DICK.” , “MWANDISHI WA HADITHI FACEBOOK DICK NA IRINE SASA MAPENZI HADHARANI.”

Hivi vilikuwa ni baadhi ya vichwa vya habari vya magazeti ya udaku ambayo nilikuwa nikiyapekuwa kupitia Application ya simu yangu kwa siku hiyo. Sikutaka kuamini kama kile nilichokuwa nikikisoma kilikuwa ni kweli au lah! macho yangu yalirudiarudia kuvisoma vichwa vile mara mbilimbili kana kwamba nilikuwa sioni vizuri.

Moyo wangu ulikuwa katika furaha isiyokuwa na kifani kwa siku hiyo, kama ilivyokuwa ndoto yangu ya hatimaye iliweza kutimia. Katika hali ya kushangaza siku hiyo Mick aliweza kunitafuta lakini alionekana kuwa tofauti kwa kila kitu.

“Niambie ndugu yangu,” nilimwambia huku nikiachia tabasamu la furaha.
“Naona ndoto yako imetimia,” aliniambia.
“Ndoto ipi tena?” nilimuuliza huku nikijifanya sifahamu lolote lile lililokuwa likiendelea.
“Umefanikiwa kuwa na Irine kimapenzi.”
“Irine?”
“Ina maana unajifanya hujui?”
“Hahaha! Ndugu yangu nilikwambia lakini kuwa lazima nimpate umeona?”
“Dick una hatari ujue.”
“Hatari ipi?”
“Umeanza kuandikwa kwenye magazeti, hivi unafikri Evadia au huyo mke wa mtu akiona itakuwaje?”
“Evadia yupi?”
“Evadia mpenzi wako.”
“Mbona nimeshaachana naye muda tu hata sijui habari zake.”
“Dick.”
“Naam.”
“Evadia umeachana naye?”
“Ndiyo.”
“Mbona mapema sana kwani amefanya nini?”
“Mimi ndiyo nimezingua.”
“Dick ipo siku maamuzi yako utayajutia.”
“Mick kila siku umekuwa ni mtu wa kunipa ngonjera tu hivi kwanini usifurahi rafiki yako tayari nimeshakuwa staa, muda wa kutengeneza pesa umefika halafu nina habari nzuri kwako.”
“Habari gani?”
“Precious amejifungua.”
“Dick unapotea.”
“Wewe baki na maneno yako mimi nazidi kutusua tu.”
“Dick hivi kwanini hutaki kubadilika?”
“Unataka niwe vipi sasa?”
“Dick embu badilika huo uhuni wala hautakupeleka popote.”
“Acha niendelee kutengeneza pesa.”
“Sawa ila utakuja kujuta,” aliniambia Mick.

Katika mafanikio na pesa ambazo nilikuwa nikizipata sikutaka ziwe zangu peke yangu, nilikuwa nikimpatia na Mick kiasi cha pesa ambacho niliamini kiliweza kumsaidia katika kutatua matatizo yaliyokuwa yakimsibu katika maisha yake.

“Asante Dick kwa kunipotezea muda wangu ila pia nashukuru kwa yote uliyonifanyia. Kumbe visa vyote vile ulivyokuwa unanifanyia shida yako ilikuwa utembee na Irine rafiki yangu. Asante sana Mungu akujaalie maisha marefu ya mapenzi yenu.”

Huo ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Evadia aliyokuwa amenitumia, nilipousoma nilitabasamu kisha nikaufuta, sikutaka kumjibu lolote.

Nilikuwa nikimchukia Evadia kuliko kitu chochote kile, Laiti kama ingetokea ukaniuliza kuwa Evadia alinifanya nini na kwanini namchukia kwa kweli sitaweza kukupa jibu sahihi, hakuwahi kunifanyia kitu kibaya katika maisha yangu lakini nilijikuta namchukia tu bila sababu.

Tamaa ya pesa na umarufu ndiyo iliyoweza kuniponza mpaka nikamsahau Evadia pamoja na wema wake wote aliyoweza kunionyesha kwangu. Sikufikiria kuhusu Mama yake wala Baba yake ambao walitokea kunipenda sana na walitamani siku moja niweze kufunga ndoa na mtoto wao. Kila kitu nilichokuwa nikikifanya nilikifanya bila kufikiria mara mbilimbili, naweza kusema nilikurupuka kuchukua maamuzi.

“Dick mbona sielewei?” aliniuliza Precious kwa sauti iliyoonekana kugubwikwa na jazba. Wakati huo alikuwa amenipigia simu.

“Huelewi nini?” nilimuuliza huku kichwani mwangu nikianza kukumbuka kama kulikuwa kuna kosa lolote ambalo nilikuwa nimelifanya kwake, hakukuwa na kosa lolote, hali hiyo ilinifanya niingiwe na shauku ya kutaka kufahamu ni nini kilichokuwa kimetokea. Yalikuwa ni majira ya usiku.
“Hiki nilichokiona hivi ni kweli au macho yangu yananidanganya?” aliniuliza.
“Kitu gani?”
“Unatoka kimapenzi na Irine?”
“Umeona wapi?”

“Nimeona wapi wakati kwenye magazeti wameandika na kwenda mitandao naona zenu zinasambaa kila mtu anasema unatoka kimapenzi na yeye….Hivi Dick ni kitu gani umekosa kwangu eeeeh niambie ni nini umekikosa kwangu mpaka umeamua kutembea na Irine au kisa ni supa staa?” aliniuliza huku sauti yake ikiashiria kukosa uvumilivu katika hilo, alikuwa akilia.

“Embu tulia Mpenzi sawa acha kulia kwanza nikuambie kitu sawa,” nilimwambia huku nikianza kupanga maneno ya kumdanganya, Kila kitu alichokuwa akiniambia kilikuwa kina ukweli ndani yake.
“Uniambie nini Dick unahisi utakuwa ni kitu gani cha kunishawishi mimi mpaka nikakuelewa,” aliniambia huku akiendelea kulia kwa sauti ya kwikwi.

“Precious jaribu kunielewa basi mpenzi wangu,” nilimwambia kwa sauti ya upole.
“Unataka kuniambia nini, unataka kuniambia nini Dick?” aliniuliza kisha akawa kama mtu aliyenyamaza kulia, akawa ananisikiliza kwa umakini.

“Najua umejisikia vibaya baada ya kuona hivyo lakini unatakiwa kunisikiliza Darling kumbuka mimi ndiyo ninayeufahamu ukweli sasa usiponipa nafasi utakuwa hunitendei haki,” nilimwambia.
“Hivi ni nafasi gani ambayo unataka nikupe, 

Dick sema ukweli tu! ni nafasi ipi unataka nikupe? Nimekupa nyumba, nimekupa gari, pesa lakini umeona vyote havitosha bado unaamua kunisaliti,” aliniambia maneno ambayo kimoyomoyo yalinifanya nicheke, nilijichekesha kwasababu Precious alikuwa ni mke wa mtu na kwa maneno ambayo alikuwa akiyazungumza laiti kama mume wake angemsikia sio siri ule ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yake, angeanguka chini kwa presha.

“Unajua mimi ni mwandishi na mpaka sasa tayari nimeshafanya kazi na mtu maarufu,” nilimwambia.
“Kwahiyo ukifanya kazi na mtu maarufu ndiyo?” aliniuliza kwa sauti ya kunikejeli.

“Najua unashindwa kunielewa kwasababu moyo wako tayari umeamini kile ambacho umekiona katika magazeti lakini kama utaweza kuuruhusu moyo wake walau uniamini japo kwa sekunde moja basi huwezi kunifanyia hiyo,” nilimwambia.

“Dick unajua ni jinsi gani ninavyokupenda sana nadhani unautumia udhaifu huo kuniadhibu kwakuwa unajua siwezi kwenda mbali,” aliniambia.

“Precious mbona sasa unakwenda mbali mimi nia yangu ni kukuelezea ukweli na si vinginevyo,” nilimwambia.

“Unataka kunielezea ukweli upi?” aliniuliza.
“Kuhusu hizo habari ulizozisoma katika magazeti pamoja na kwenye mitandao.”
“Kwahiyo hazina ukweli?”

“Precious unapokuwa maarufu lazima utakutana nanyo, skendo ni moja ya adui mkubwa sana kwa watu maarufu na mpaka unaona vitu kama hivyo ujue tayari nimeshakuwa staa.”

“Dick niambie ukweli kama unatoka na Irine,” aliniambia huku sauti yake akiwa ameielegeza.
“Hakuna ukweli katika hilo embu naomba uniamini basi hata kwa kuniigizia,” nilimwambia.
“Sawa nimekuelewa ila mimi sipendi kuona au kusikia habari hizo,” aliniambia.

“Hatuwezi kuwakataza waandishi wa habari waache kufanya kazi yao….acha waendelee kuniandika vibaya lakini kitu ambacho nakihitaji kutoka kwako ni uaminifu, nataka uniamini kutoka moyoni mwako,” nilimwambia.

“Sawa nimekuamini,” alinijibu kisha akaweza kuniaga na kukata simu. Precious alionekana kunipenda sana kuliko kitu chochote kile.

Niliutumia umaarufu niliyozidi kuupata katika kuendelea kuandika hadithi mbalimbali ambazo nilikuwa nikizichapisha katika mitandao ya kijamii. Zilizidi kupendwa sana na kila siku nilizidi kujiongezea mashabiki wengi waliyoonekana kunipenda na kuzipenda kazi zangu.

“Hello Dick Mapenzi.”
“Yes Hello Alice.”
“How are you?” (Habari yako?)
“Fine, how about you?” (Nzuri, vipi kuhusu wewe?)
“Everything is good, where are you? (Kila kitu kipo vizuri, uko wapi?)
“Tanzania and you?” (Tanzania na wewe?)
“Kenya.”
“Tell me?” (Niambie.)
“Ireally like reading your stories is very good.” (Napenda sana kusoma hadithi zako ni nzuri sana.”
“Thank you so much and I am glad to hear that.” (Asante sana na pia nafurahi sana kusikia hivyo.)
“Ok.” (Sawa.)
“What story didi you like?” (Hadithi ipiumeipenda?)
“CHUMBA CHA MASAJI.)
“Ok.” (Sawa.)
“Ok.” (Sawa.)

Nilimaliza kuchat Instagram na Alice shabiki yangu kutoka Kenya msichana ambaye alionekana kuvutiwa na hadithi zangu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni