NIFANYE NAMIMI KAKA (26) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 25 Machi 2021

NIFANYE NAMIMI KAKA (26)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Juma Hiza

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Tulikuwa katika ugomvi ambao uliletwa na skendo ambayo ilinihusu kwa asilimia kubwa wala hakukuwa na cha kuficha kwani kila kitu kiliwekwa wazi.
SASA ENDELEA...
Nilijitahidi kudanganya kama ilivyokuwa kawaida yangu lakini uwongo wangu uligonga mwamba. Hakukuwa na uwongo niliouzungumza kisha ukaenda kumuingia Irine ambaye alionekana kuwa mwenye hasira sana hasa baada ya kugundua kuwa sikuwa muaminifu katika mapenzi, nilimdanganya vya kutosha.

Kitendo cha kugundua kuwa nilizaa na mwanamke mwingine nje tena mke wa mtu kilimuumiza sana, hakujua ni kwa jinsi gani alitakiwa kunieleza ili niyagundue mamivu aliyokuwa nayo. Kupitia machozi yake pamoja na ukimya alioamua kukaa baada ya kushindwa kuzungumza lolote, nilifahamu alikuwa katika wakati wa hasira, alibaki akinitazama muda wote.

“Nijibu basi mpenzi,”nilimwambia kisha nikamtazama, alionekana kuwa mwenye hasira sana.
“Naomba Dick uende, niache na maisha yangu,” aliniambia maneno ambayo alimaanisha.
Sikutaka kuwa king’ang’anizi sana kwa wakati ule kwani Irine alikuwa tayari ameshagundua ukweli wa kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Niliamua kuondoka nyumbani kwake kisha nikaelekea nyumbani kwangu huku kichwa changu kikiwa na maswali lukuki ambayo yaliniweka katika wakati wa mawazo.

Nilikuwa nikiwaza mambo mengi sana lakini mpaka nafanikiwa kufika nyumbani kwangu sikuwa nimeng’amua lolote lile, nilionekana kuchanganyikiwa kutokana na kile ambacho kilikuwa kimetokea. Sikujua ni nani ambaye alikuwa akinifuatilia undani wa maisha yangu.

Nilianza kupata mashaka na mtu ambaye nilikuwa nikimtilia mashaka alikuwa ni Precious, nilihisi yeye ndiye alikuwa amehusika kwa asilimia kubwa katika kuzisambaza habari zile kwa waandishi wa habari ili aweze kujitengenezea umaarufu.

Niliamua kumpigia simu huku nikiwa mwenye hasira sana, nilitamani kumtukana lakini alipopokea ajabu nilishindwa kufanya hivyo, alikuwa akilia na yale aliyonieleza yalizidi kunichanganya kabisa akili yangu.

“Dick mume wangu, mume wangu Dick,” aliniambia mara baada ya kupokea simu, sauti yake ilinidhihirishia wazi kuwa alikuwa katika kilio kwa wakati huo, kilio chake kikazidi kunichanganya.
“Sasa unalia nini na mume wako amefanyaje?” nilimuuliza.
“Kwanini umeamua kunichafua kwenye magazeti kwanini Dick, mume wangu akijua huoni utaniletea matatizo kwenye ndoa yangu?”
“Precious mbona unanichanganya?”
“Nakuchanganya na nini Dick, umeamua kunichafua magazetini kwanini umenifanyia hivyo?”
“Inamaana unataka kuniambia wewe hauhusiki kabisa na tukio hili?”
“Tukio gani?”
“La kuwaambia waandishi wa habari kuhusu usiri wa jambo hili.”

“Simjui mwandishi hata mmoja hivi nitaanzaje kwenda kutangaza wakati najua kuwa hii ni siri tena tumepanga ibaki kuwa siri kati yetu,” aliniambia Precious maneno ambayo kiukweli yalizidi kuniweka katika wakati wa mawazo, mpaka kufikia wakati huo sikujua ni nani ambaye alihusika katika kuzitangaza habari zangu kwa waandishi wa habari. Nilikuwa katika wakati mgumu sana kwani ni muda mfupi ulikuwa umepita tangu nilipoweza kugombana na Irine kiasi kwamba akaamua kunifukuza nyumbani kwake.

Nilizidi kupagawa baada ya Precious kuniambia kuwa hakuhusika na lolote katika habari zile kwani kwa upande wake alikuwa katika mshangao na muda wote alikuwa akilia kwa kumuhofia mume wake endapo angeweza kuziona au kuzisikia habari zile.

“Kwani mume wako yuko wapi?” nilimuuliza swali ambalo sikumbuki kama niliwahi kumuuliza siku za karibuni, ni muda mrefu ulipita sikutaka kuzisikia habari za mume wake, niliamua kufanya hivyo kutokana na sababu za Precious kutopendelea kusikia habari za mume wake pindi anapokuwa na mimi.
“Yupo,” alinijibu kwa sauti iliyochanganyika na uwoga.
“Sasa unaogopa nini?” nilimuuliza.

“Dick mume wangu namjua na endapo akizisikia habari hizi sijui uso wangu nitauweka wapi?”
“Precious kila kitu nahisi imeharibika na sijui itakuwaje?”
“Dick kwani ni nani ameenda kuwaeleza waandishi wa habari?”
“Mimi sijui yani nimechanganyikiwa Precious.”
“Mungu Wangu.”

Mpaka kufikia hapo nilikuwa nimechanganyikiwa, nilihisi kuwa na nuksi katika siku hiyo, akili yangu haikuwa sawa na kila nilichokuwa nikikifikiria nilihisi kukosea hivyo vyote nilivipuuzia.
Kwa wakati ule nilipokuwa nikizungumza na Precious na kutoambulia lolote nilichoamua ni kukata simu. Sikuwa sawa hata kidogo. 

Nilikumbuka kulitafuta gazeti ambalo lilikuwa limeandika habari iliyonihusu na hapo niliamuakulitafuta jina la mwandishi aliyehusika kuiandika habari ile. Isack Mwakyonya ndiyo jina nililokutana nalo la mwandishi wa habari hiyo, niliamini kwa asilimia kubwa ukweli wa maswali yote yaliyokuwa yakinizonga akilini mwangu majibu yake alikuwa nayo yeye, niliamini kama yeye hakuhusika katika kudadisi ukweli ule basi alikuwepo mtu wa pembeni ambaye alihusika kuzitoa habari hizo kisha nay eye akaweza kuziandika. 

Niliinakili namba yake ya simu kisha sikutaka kupoteza muda niliamua kumpigia, simu yake ilionekana kuwa bize lakini sikukata tama, niliendelea kupiga kila mara mpaka pale nilipobahatika kumpata. Alipopokea niliwahi kujitambulisha kwa jina ambalo haikuwa rahisi kwa yeye kuweza kunifahamu.

“Nazungumza na nani?” aliniuliza kwa sauti iliyoonekana kuwa bize kiasi kwamba hata kitendo cha kupokea simu kilikuwa kikimkwaza.
“Naitwa Akilimali Kazipesa.”
“Akilimali?”
“Ndiyo.”
“Ok Akilimali niambie nikusaidie nini?”
“Bila shaka nazungumza na Isack mwandishi wa habari gazetini?”
“Ndiyo mimi bila shaka hujakosea vipi una dili la habari nini?”
“Ndiyo tena ni zaidi ya dili la habari.”
“Nipe sasa ndugu tupige pesa mjini hapa.”
“Ni kweli lakini kwa habari hii itabidi tuonane ili niweze kukueleza kila kitu.”
“Habari yenyewe inamuhusu Staa au?”
“Ndiyo tena staa wa bongo movie.”
“Ok niambie kwahiyo unataka tukutane wapi?”
“Labda wewe ndiyo uniambie unataka tukutane sehemu gani?”
“Nafikiri maeneo ya Beach itapendeza zaidi.”
“Beach gani?”
“Tukutane Sunrise Beach Resort.”
“Kwa leo itawezekana?”
“No, maybe we do tomorrow.” (Hapana, labda tufanye kesho.)
“Muda gani?”
“Mchana.”
“Sawa,” nilimjibu kisha na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu.

Kwa maongezi ambayo nilizungumza na Isack Mwakyonya alionekana kuwa mtu wa kupiga dili kupitia habari za mastaa, nililifahamu hilo baada ya kugundua kuwa na mimi nilikuwa ni miongoni kati ya wateja ambao walikuwa wakimpelekea habari za udaku jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote. 

Sikutaka kuufikiria ule umbali uliyokuwepo kati ya Mbezi Beach na Mji Mwema, Kigamboni ambapo ndipo ilipokuwa Sunrise Beach Resort bali nilichokuwa nikikifikiria kwa wakati huo ni kukutana na Isack kisha niitumie nafasi hiyo katika kumbaini mtu aliyehusika katika kunichunguza kiasi kwamba akaamua kunichafua magazetini.

Picha zangu pamoja na Precious ziliendelea kusambaa mitandaoni, kila mtu alikuwa na lake la kuandika kwa siku hiyo. Wapo waliyoitumia siku hiyo katika kunitukana na wengine waliitumia kama sehemu moja wapo ya kujiingizia kipato kupitia blog mbalimbali za kijamii.

Nilianza kupigiwa simu na waandishi wa habari kutoka sehemu tofautitofauti ambao walikuwa na lengo la kunifanyia interview kuhusu skendo ile iliyokuwa ikinikabili magazetini. Wote sikutaka kuzungumza nao, niliamini kwa kufanya hivyo nilikuwa naendelea kulilinda jina langu ambalo tayari lilikuwa limeanza kuchafuliwa na magazeti ya udaku.

Laiti kama ingetokea kama ungekutana na mimi kwa wakati ule kisha ukaniuliza kuhusu hadithi au kitu kinachohusu kazi yangu kwa kweli nisingeweza kukujibu jibu fasaha. Akili yangu haikuwa sawa hata kidogo, nilikuwa nikiwaza kitu kimoja tu! ambapo nikukutana na huyo Mwandishi wa habari na niweze kumfahamu huyo mhusika ambaye alikuwa ananifuatilia. 

Kuna muda nilianza kupata mashaka juu ya huyo mwandishi wa habari, nilihisi kuna mchezo alikuwa akiufanya dhidi yangu na kwa maana hiyo nisingeweza kuufahamu ukweli kwani nilikuwa naenda kukutana na mhusika mwenyewe. 

Hilo lilizidi kuniweka katika wakati wa mawazo, nikakumbuka ule mchezo mchafu ambao ulikuwa ukifanywa na waandishi wa habari wenye lengo la kukuchafua halafu baadae wanakuambia ili wasikuchafua inabidi uwalipe kiasi cha pesa ambapo wataweza kuipotezea habari.

Bado sikutaka kuamini kirahisi kuwa nilikuwa katikamhuo mchezo, kila nilichokuwa nikikiwaza nilikiona kuwa na uwongo ndani yake.

“Kama kweli nia yake ni kutafuta pesa kupitia hiyo skendo mbona sasa hajanitafuta?” nilijiuliza swali lililonifanya nipuuzie lile wazo lililokuwa limenijia. Kwa wakati mmoja nilikuwa nikiwaza mambo mengi sana, sikuacha kumuwaza Irine msichana ambaye alihusiika kwa asilimia kubwa katika kunipa umaarufu ambao kwa muda ule ulikuwa ukinitesa, maisha yangu yalibadilika na kuwa kama ya mnyama digidigi. Kuna muda nilijilazimisha tabasamu usoni mwangu, nikataka kutabasamu kinafki lakini tabasamu halikuja, sikuhitaji kutabasamu kwa wakati huo hivyo nilikuwa katika mkunjo wa sura.

Nilimpigia simu Irine, simu yake ilikuwa ikiita tu! bila kupokelewa, niliamini kuwa aliamua kufanya kusudi kunipokelea kutokana na tatizo lililokuwa limetokea. Wakati nikiendelea kumpigia Irine bila mafanikio akili yangu ikaanza kumuwaza Precious, sikujua alikuwa katika wakati wa aina gani wala sikujua kama mume wake alizipata habari hizi au la. 

Hilo sikutaka kujisahaulisha, habari ile ilikuwa ni habari mbaya lakini ilisambaa kila kona ya nchi na niliamini mpaka kufikia wakati ule hakukuwa na mtu ambaye alikuwa hafahamu kile kilichokuwa kikiendelea.

Kitendo cha kuendelea kumuwaza Precious ambaye alikuwa akilia na akimuhofia mume wake kilikuwa kikizidi kuniweka katika wakati wa maumivu, sikutakiwa kuwa katika hali hiyo kwa wakati huo. 

Niliamua kuacha kumuwaza japo ilikuwa ni ngumu kufuta kumbukumbu za mtu ambaye tayari alikuwa akilini mwako, nikajitoa ufahamu kisha nikampigia simu rafiki yangu Mick, alipopokea simu yangu sikutaka akuzungumza lolote zaidi ya kumwambia kuwa nilihitaji kuonana naye.
“Kuna nini?” aliniuliza.
“Nataka tuonane nitakwambia,” nilimwambia.
“Sasa tukutane wapi?” aliniuliza.
“Njoo hapa nyumbani kwangu mida hii kaka,” nilimwambia.
“Sawa nakuja,” alinijibu.

Baada ya kupita dakika kadhaa Mick aliweza kufika nyumbani kwangu, nilimkaribisha kwa kumpa juice hapa ni baada ya kudai kuwa alikuwa ameshiba chakula kisha sikutaka kupoteza muda nikaanza kumwambia kile nilichokuwa nimemuitia.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni