SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
“Na baada ya hapo ikawaje?” aliuliza Gastoni. “Wewe acha tu ulikimbia ukiwa mtupu na watu wakawa wanakuitia mwizi”. “Acha masihara yako mpenzi, mimi nakupenda sana na kamwe siwezi kukusaliti” alidanganya Gastoni.SASA ENDELEA...
Maongezi yale yalimuumiza na kumshtua Mwajabu ambaye alikuwa amejilaza kitandani akiwa uchi wa mnyama.Alijionea huruma yeye na alimwonea huruma Jesca. Kimoyo moyo akawaa anajisemea “kweli hii ni zaidi ya PENZI PENZINI”.Wakati Mwajabu akiendelea kutafakari na kusikiliza jinsi Jesca alivyokuwa akilalamika na kuonesha kuwa hana imani na penzi la Gaston na yeye aliamua kuwasha simu yake ili kujua nini kiliendelea baada ya yeye kukimbia kwenye fumanizi.
Alivyowasha tu alikutana na meseji nyingi sana za rafiki yake Zuwena. Na kwa kuwa zilikuwa za kufurahisha na kusikitisha aliamua kumpigiakabisa. “Helow shostiti, meseji zako zinanivunja mbavu, ebu nambie nini kiliendelea baada ya mimi kuondoka na kumwacha baba Juma pale chumbani kwangu.Zuwena kwa huzuni alijibu “wewe acha tu best yule mke wake ni mkorofi sana kwani aliingia na kumkurupusha kama mwizi”. Kwa hiyo baada ya kumkurupusha nini kilitokea aliuliza Mwajabu.
“Yaani wewe acha tu alitoka uchi wa mnyama watu wakamkimbiza huku mkia wake ukigongagonga mguu wake utafikiri mguuu wa tatu”.Mwajabu ilimbidi acheke kwa sababu kwa kweli yule mbaba alijaliwa kuwa na maumbile marefu sana ambayo siku zote ulimwitaji Mwajabu kutumia akili ya ziada pindi akiwa nae kitandani la sivyo aliambulia maumivu tu. Yeye siku zote alikuwa akijipimia saizi inayomtosha na alikuwa akitumia ile staili ya jipakulie mwenyewe.
Basi Zuena aliendelea kumsimulia rafiki yake Mwajabu ambaye vyumba vyao vimeongozana jinsi mambo yalivyokuwa. “Yaani shosti umemtia kwenye majanga makubwa sana yule baba wa watu” aliongeza Zuena. Majanga gani kwani mimi nilimlazimisha au alitaka mwenyewe kuharibu ndoa yake. Basi ndo hivyo besti mbaba wa watu akaingia kwenye banda la nguruwe na bila kuogopa harufu ya kinyesi cha wanayama hao na bila kuajali kuwa yeye ni ostadhi alikaaa humo kwa zaidi ya robo saa.
Mkewe alitukana sana mpaka watu wakaamua kumwondoa maana alimchamba sana. Watu wenye busara zao walimwondoa mama huyo eneo la tukio na baadaye baba wa watu alitolewa kwenye banda la nguruwe na kusitiriwa.Mwajabu alicheka sana na kumuuliza kwa hiyo ile meseji uliyoniandikia kuwa ya kwangu ni ya dhahabu ulikuwa na maana gani. Zuwena ilibidi achake na kusema “yaani hapo nilikuwa namaanisha yule mama alikuwa anamuuliza mumewe kuwa amekosa nini kwake au wewe uchi wako ni wa dhahabu?”
Hapo ilibidi Mwajabu akate simu na kuendelea kucheka kwa nguvu.Kicheko kilichosababisha Jesca ambaye alikuwa bado anaongea na Gastoni kuuliza “mbona nasikia sauti ya kike hapo pembeni au upo umelala na mwanamke baby wangu?”.Kauli iliyomfanya Gastoni ashuke na kuteremka kitandani na kusogea mbali zaidi.Gastoni aliendelea kummdanganya mpenzi wake huyo kwenye simu mpaka kikaeleweka. Alimwambia kuwa ni sauti ya kwenye Tv japo haikuwa ya Tv.
Gastoni alivyokata simu na kuagana na Jesca alimwangalia Mwajabu kwa jicho baya akimaanisha kuwa hakufurahishwa na kicheko chake ambacho kilitaka kusababisha majanga.Mwajabu nae akaendelea kujitoa ufahamu akamwonesha tabasamu la nguvu na kumkonyeza kitu ambacho kilimshangaza Gastoni na kijisemea she must be crazy(anaweza kuwa chizi) au ni likahaba lililokubuhu.
Mwajabu kuona Gaston anaendelea kuganda kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme akaamua kufanya makusudi akajifunua lile shuka alililojifunika akamfuata Gastoni na kumpa mikono ishara kuwa amkumbatie. “Wote hatuna makucha basi tusiombe upele” alisema Mwajabu.Gaston akamsukuma na kupanda kitandani.
Mwajabu alikuwa na roho ya ajabu sana yeye aliendelea kucheka tu na kumwambia “ujue Gastoni lazima tukubali kilichotokea na kitakachotokea kwani hata Norman Peale alishawahi kusema “Its not what happens to you that matters, its what you think about what has hapened to you.” Kwa tafsiri isiyo rasmi alimaanisha kuwa kitu chochote ambacho kiliwahi kukutokea maishani sio tatizo, bali kama utaendelea kukifikiria ndio tatizo.
Alivyomtaja tu mwandishi huyo maarufu wa vitabu vya positive thinking, Gaston alitabasamu kwani na yeye alikuwa ni mmoja wa watu waliopenda kusoma vitabu vya mwandishi huyo na kwa kuthibitisha hilo alimjibu Mwajabu kwa kumwambia “We become what we think and what we think come to us” Kwa tafsiri isiyo rasmi yaani tunakuwa tunavyofikiri na tunavyovifikiria utujia maishani.Basi walikumbatiana na Mwajabu akamwambia Gastoni “The bird of the same feather flying together” akiwa na maana ndege wafananao huruka pamoja hivyo basi anaomba wafungue ukurasa mpya wa mapenzi baina yao.
Gaston alikuwa kimya huku huku akiendelea kufurahia kumbatio la Mwajabu, kumbatio lillompa joto la huba. Baada ya kimya kirefu huku kila mmoja akitafakari na kupeleka hisia zake za mapenzi mbali, Mwajabu alimuuliza tena kwa kutumia kimombo “if likes attract likes, can we build a home?” akiwa na maana kuwa kama vizuri huvutia vizuri vyenzao je wanaweza kuwa mke na mme. Gaston alijibu kwa kifupi tu “time will tell”(mda utatuambia).
Wote wakapanda kitandani na Gaston akaanza kujieleza. Ujue Mwajabu wewe ni msichana wa ajabu sana kwa sababu nilitegemea usiku huu uwe na hofu na huzuni kutokana na tukio la fumanizi lililotokea lakini nakuona una furaha tu na unataka tuyaache yote na tufungue ukurasa mpya.Hivi unafikiri jamii mimi itanielewaje? Mwajabu akadakia na ndio maana nilikwambia “its not what hapened to you that matter, its what you think about what has hapened to you.”
Mwajabu alionekana kujiamini sana na wala hakushtushwa na meseji za Beatrice na Jesca na alitangaza msimamo wake mbele ya Gaston kitu ambacho huwa ni kigumu kwa watoto wa kike.Kwa maelezo hayo Gastoni alihisi kuwa Mwajabu atakuwa alichanganyikiwa na lile tukio la fumanizi. Akamwambia “naomba tulale tutaongea kesho na tutafikia muafaka kesho maana suala la mimi kuwa na wewe kama wapenzi ni jambo zito hata hichi tulichofanya ni shetani tu alitupitia”.
Please Gastoni usiseme maneno hayo unaniumiza moyo wangu. Mwajabu alilamika sana na kusema “huwezi amini Gastoni mimi sio malaya nina mwanaume mmoja tu niliyemwacha huko Rufiji Pwani lakini ni ugumu wa maisha tu ndo unasababisha yote haya”.Nazani kama wewe ni mzoefu na wanawake ilikupasa kuligundua hilo pale tu ulipofanya mapenzi na mimi. Najua umegundua kitu na ingekuwa ni kahaba kama unavyofikiria wewe basi hata ikulu ya mzinga wangu usingekuwa na utamu huo ulioukuta alijisifia Mwajabu.
Kauli hiyo ilimgusa Gaston na kumwona kuwa alikuwa na ukweli ndani yake.Mwajabu baada ya kuona Gaston amekaaa kimya ilimbidi amuuulize habari zaa Jesca na Beatrice.Gaston hakumficha kitu alimwambia ukweli kuwa Jesca ni mpenzi wake kwa sasa na yupo Dodoma na anampenda sana.Lakini hakusita pia kumweleza habari za Beatrice na kumwambia kuwa huyo alikuwa ni mpenzi wake wa zamani.
Gastoni anamsimulia Mwajabu jinsi tukio la usaliti aliliofanyiwa na Beatrice binti ambaye alipoteza mawasiliano naye miaka mitatu iliyopita. Anakumbuka ilikuwa ni wiki moja kabla hajaanza mitihani yake ya kumaliza elimu yake ya sekondari siku ambayo alionana na Beatrice akapewa kadi ya best wishes na hela kibao na hiyo ni baada ya kulimenya tunda( kufanya mapenzi) wakaagana na yeye kurudi shuleni, siku mbili baadae anapokea simu kutoka kwa binamu yake na Beatrice mtu ambaye alimpa kazi ya kumchunga na kumfuatilia mpenzi wake.
Habari hazikuwa nzuri kwani zilieleza kuwa eti Beatrice alianza tabia mbaya na siku hiyo hakulala nyumbani alidai amekwenda kwenye harusi lakini binamu yake akamwambia yeyeanahisi amekwenda kwa mwanaume. Gaston aliamua kupotezea zile habari kwa kuwa alikuwa kwenye kipindi kigumu cha mitihani. Aliumia sana lakini akasema atajua ukweli pindi atakapomaliza mitihani kwani walikuwa wapo majirani. Tangia siku hiyo aliaamua kuzima simu yake na kuendelea na mitihani.
Siku aliyomaliza pepa aliwasha simu na kila alipompigia Beatrice hakupokea simu, alipofika nyumbani alienda kwao akamkuta wakaongea na alipomuuliza kuhusu kutopokea simu alijibiwa kwa mkato kuwa “mbona wewe ulinizimia wiki nzima sijakuuliza au mimi ndo nina moyo wa chuma”. Swali lile lilimfanya Gaston aendelee kuwa mpole akaomba appointment ya kuonana na mpenzi wake huyo na akaambiwa jumapili.
Jumapili ilipofika mida waliyopanga Beatrice hakuonekana, simu hakupokea na wala meseji hakujibu. Gaston iliumia sana kwani tayari alishachukua room tayari kwa kile alichokiita kureflesh mind baada ya kumaliza shule. Ilipofika saa moja jioni alikata tamaa akaamua kurudi zake nyumbani huku akifikiria atalipaje deni la hela aliyokopa kwa ajili ya siku hiyo. Hatua chache kabla hajafika nyumbani kwao kwa mbele alimuuona mtu kama Beatrice akiwa ameongozana na kijana ambaye alikuwa ni mrefu sana kama Hashim Thabeet akaamua kujificha ili athibitishe kuwa ni yeye au la.
Hakuaamini macho yake alikuwa ni mpenzi wake Beatrice tena akitembea kwa kujiamini kama mtu na mpenziwe. Gaston kwa ujasiri aliamua kuwafuatilia ajue walikuwa wakielekea wapi. Mdogo mdogo kama wimbo wa Dimond ndo mwendo uliokuwa ukitumika, wakaenda na kuenda, kata kulia kata kushoto mara wakatokea sehemu ile ambayo Gaston alipanga wakutane ingawa yeye hakumwambia ni hapo. Sehemu hiyo ilikuwa ni nzuri sana kwani kwa mbele ilikuwa ni restaurant ambapo watu walipata maakuli na kwa nyuma kulikuwa kuna vyumba vya kulala wageni.
Vijana wengi walipapenda hapo hasa kama demu alikuwa bado ajatiki vizurii hii ina maana kwamba watu wataanza kunywa au kula wakikubaliana wanahamia kwa nyuma kuchimba madini (kufanya mapenzi). Basi Beatrice alisimama kwa nje na yule jamaaa mrefu aliingia peke yake na alipitiliza moja kwa moja mpaka kwa nyuma ya restaurant, Gaston hakuelewa nini kinaendelea lakini alihisi jamaa aliamua kulipia room moja kwa moja. Gaston akapiga moyo konde na kuamua kumfuata Beatrice kabla hajamfikia jamaa naye alikuwa akitoka kuja kumchukua..
Gaston anaeleza kuwa alimwona yule kijana akienda kule sehemu ambayo yeye alikuwa amechukua chumba na Kumwacha Beatrice nje. Basi bila kujua chochote kinachoendelea alimfuata Beatrice na kuanza kumwoji maswali. “Hapa ni wapi? Upo na nani? Na kwa nini unataka kunisaliti”. Wewe vipi una maswali mengi kwani wewe ni polisi? alijibu Beatrice. Kitendo hicho au jibu hilo lilimfanya Gaston kukasirika na kuanza kumshushia kipondo kama anapiga mbwa mwizi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA