UZOEFU (12) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 5 Aprili 2021

UZOEFU (12)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Tangu nimeingia kwenye ulimwengu wa mapenzi sikumbuki ni mpenzi wangu gani niliyewahi kumuombea zaidi ya Lisa na labda ndio maana hata nilipotembea huku na kule sikuwahi kumuona wa kufanana na yeye.Ama kweli Lisa kwa maisha yangu alikuwa kama sukari kwa chai.
SASA ENDELEA...
Miezi mingi sana ikapita pasipo kuwasiliana na Lisa lakini nakumbuka moja ya mistari niliyomuandikia kwenye barua niliyomsisitiza awe anaisoma mara kwa mara niliandika hivi ' Muda wowote unaponimiss usipate tabu ingiza mkono wako na shika ziwa lako la kushoto kwani hapo ndipo nitakapokuwa na mimi nitakuwa nafanya vivyo hivyo nnapokukumbuka'Baada ya muda mrefu kupita,

Siku moja majira ya saa mbili za usiku nikiwa najisomea,Simu yangu iliingiza ujumbe mfupi na nilipoiangalia,ujumbe huo ulikuwa unatoka kwa Lisa,Alikuwa ananijulisha kuwa muda huo ndio anafika nyumbani kwao Tabora kutokea shule Moshi,Pia alisisitiza kuwa amenikumbuka sana.

Mwili ukanisisimka baada ya kuusoma ujumbe huo na furaha ya ajabu ikautawala moyo wangu hata nikasau nilichokuwa nakifanya.

"Hebu jaribu kuzuia pumzi yako usiheme....endelea kuzuia kadiri unavyoweza...endelea tafadhali...enhee sasa pumua!...jinsi ulivyoimiss hewa ndivyo nilivyokumiss mpenzi wangu" 

Nilimtumia Lisa ujumbe huo niliouandika kwa lugha ya kiingereza huku nikimaanisha kila neno nililoliandika.wengi huwatumia (huwafowadia) wapenzi wao msg ambazo hazitoki mioyoni mwao lakini mimi nilikuwa tofauti sana na hao.Ukweli ni kuwa nilimmiss Lisa kama mtu aliyeziba pua anavyoweza kuimiss hewa.

Kurudi kwa Lisa kwangu mimi kulileta maana zaidi ya maji kwa kiu.Japo tulitenganishwa kwa mamia ya kilometa lakini hiyo haikuzuia kuuhisi ukaribu wa Lisa kwangu.Chem chem ya messages (jumbe fupi) za Lisa kwa simu yangu hazikukauka kamwe!. 'Bby upo wapi saivi','Hny unafanyaje?' 

,'Nimekumiss my luv!','Nalala kidogo mpenzi naomba uniamshe baada ya dk 10!' Jumbe fupi za namna hiyo toka kwa Lisa mchana kutwa zilitosha kabisa kuuondoa upweke wangu nakuona Lisa ananijali na kunifwatilia kutwa nzima.Muda mwingine nililazimika hata kukirudisha kijiko cha wali kwenye sahani ili nijibu kwanza ujumbe toka kwa 

Lisa kwani ningechelewa zaidi ningezua mengine. ' Uko wapi wewe mbona hunijibu?','bby u make me bored','Nikeep busy basi mpenzi wangu!','Mbona kimya hun?'. Lisa alinifanya kila siku nile na simu mkononi,tabia iliyopingwa vikali na Bi mkubwa (mama) bila ya mafanikio.Heri mama akereke kuliko Lisa achukie,Hata simu ilipokaribia kuisha chaji nilitakiwa kutoa taarifa mapema sana.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yetu mapya yaliyotawaliwa na umbali.Ule msemo yakuwa fimbo ya mbali haiui Nyoka ni kama vile uligonga mwamba katika penzi letu.kila mmoja wetu aliweza kumuendesha mwenzake jinsi atakavyo.

Ngoma ikivuma saana haikawii kupasuka, Nakubali!.Japo niliamini kuwa tunapendana sana lakini hata mimi mwenendo wa penzi letu ulikuwa ukinitisha wakati mwingine kwani ulikuwa na kasi ya ajabu na sikuwahi kutambua break (kipunguza mwendo) ni nini.

Tulizoea kuongea sana kwa simu mimi na Lisa nyakati za usiku.Na mmoja akiishiwa salio mwingine hupiga na mazungumzo huendelea kwa muda mrefu sana, Cha maana tunachoongea hakuna lakini atakayeaga atakiona cha mtema kuni. Mazoea hayo yaliyojenga tabia iliyokuwa kama sheria yaliingiliwa na doa siku niliyoomba tusiongee ili nijisomee kwani siku inayofuata nilitakiwa kuingia chumba cha mtihani. Japo 

Lisa alinikubalia lakini niliamini kuwa hakuridhika,Hata mmbwa anamfahamu Boss wake, vipi mimi nishindwe kumjua mpenzi wangu!. Baada ya kukata simu nilimtumia ujumbe mzuri ambao niliamini angeupenda. 'Enx' (ahsante) hilo ndilo jibu nililolipata toka kwa mpenzi wangu Lisa.Inawezekana vipi kwa bingwa wa kuchat kama 

Lisa anijibu herufi tatu tu tena kavu namna hiyo!.Ingawa mwanzo nilihisi Lisa hakuridhika sasa niliweza kulithibitisha hilo.Lisa asiyeweza kunitumia ujumbe bila kuandika baby,sweetie au honey. Leo alinijibu shorty (mkato) sana.

Sikuweza kuivumilia hali hiyo nikamuandikia Lisa ujumbe mwingine uliosomeka hivi 'Baby chochote nnachofanya ni kwaajili ya mimi,wewe na maisha yetu so nnapokuwa bize plz usichukie mpenzi wangu! Naamini umenielewa vizuri lala unono swthrt!! Luv u!' Nikatuma ujumbe huo huku nikiamini sasa Lisa mpenzi atalala salama,Kama kawaida yake ya kuwa mwepesi kwa kuchat,hakumaliza sekunde mbili akanijibu.

Nikaufungua ujumbe kwa haraka niweze kuusoma,lakini sikuona herufi nyingine zaidi ya ' K '. Niliiangalia ile K zaidi ya dakika tano nzima huku nikiwaza inamaanisha nini japo kichwa kiliniambia ni Ok ama Okay lakini moyo ulikataa kuamini kuwa k hiyo imetoka kwa Lisa.Japo nilimuaga Lisa ili nijisomee lakini si hamu ya kusoma tu iliyokuwa imepotea hata usingizi sidhani kama ningeupata usiku huo. 

Nilitamani kumpigia simu Lisa lakini nikahofia kukatiwa jambo ambalo nisingependa litokee. nikawaza kumtumia ujumbe mwingine lakini roho ikasita,ujumbe wangu wa kwanza ulijibiwa kwa herufi tatu 'enx' wa pili ukajibiwa kwa herufi moja ' K ' je wa tatu utajibiwa vipi? Swali hilo lilinifanya niinamishe kichwa changu juu ya meza ya kusomea na hata sikuelewa usingizi ulinipitia vipi ila niliweza kushtuliwa saa kumi za usiku na mmbu ambao waliugeuza mwili wangu chakula cha karamu, Nikaelekea kitandani kulala.
Tamu imegeuka shubiri.Je yapi yatajiri???

Ambako nako sikudumu kwa muda mrefu,Usiku wa tabu ukawa umepita na kuikaribisha asubuhi ya shida.Lisa ambaye ndiye mara nyingi huniamsha kwa salam ya "Gud morn Hunpie", Leo hii hakujibu salaam yangu.Naam! Hapo ndipo nilipoanza kusikia kichwa kikinigonga kwa mawazo,Na bahati mbaya kichwa kinachouma kwa mawazo huwa hakitibiki kwa 

Hedex wala Panaldo za Kenya, Hupona tu kwa tulizo la moyo!,Je tulizo hilo nitalipata wapi asubuhi hiyo hali mwandani wangu hataki lau japo salaam?. Nilipatwa na upweke wa hali ya juu na kama siku hiyo shule pasingekuwa na mtihani basi hiyo ingekuwa excuse ' sababu' ya kutokwenda.Nikajizoa zoa mithili ya mjeshi aliyenusurika kifo kwenye vita na nikajikongoja kuelekea shule.

Nashukuru Mungu kwa kunipa uwezo wa kubadilika kutokana na mazingira, Nilipofika shule Lisa alibaki moyoni huku kichwa kikiyafanya yanayotakiwa kufanyika kwa muda huo.Siku hiyo sikwenda na simu shuleni ili niweze kujizuia kutomtafuta Lisa.Hata majira ya jioni yalipojiri na muda wa kurudi nyumbani ulipofika, Nilirudi huku nikiamini ntakuta kitu chochote kipya kwenye simu yangu kutoka kwa Lisa.

Tofauti na matarajio yangu sio simu ambazo hazikupokelewa tu ( missed call) sikuweza kukuta hata salam yangu ya asubuhi imejibiwa.Nikajuta hata kuipekua simu hiyo.Nikaitupa pembeni kisha na mimi nikajitupia kitandani katika hali ya kukata tamaa."Why Lisa??"(Kwanini Lisa) Niliropoka peke yangu kwa sauti kubwa kama chizi huku nikiukumbatia mto kwa uchungu. Lisa hakuwa mtu wa kunifanyia hivi.Ni jambo gani baya nililomtendea hata anitende vibaya namna hii.

Nikiwa bado nagaagaa kitandani na mzigo wa mawazo nilikumbuka jambo moja kuwa Lisa ni mtu aliyenijali sana nikiwa katika hali ya kuumwa hivyo nikamuandikia ujumbe mfupi uliosomeka hivi "Baby m so sick!!" (Mpenzi naumwa sana) cha ajabu baada ya kuutuma tu ujumbe huo ulijibiwa papo hapo kana kwamba Lisa alikuwa akiusubiri kwa hamu. "M sick 2!" ( Naumwa pia). Khaa!! Nikajikuta nashangaa mwenyewe.Japo ujumbe wa 

Lisa ulinitia kichefu chefu lakini sikuweza kutapika.Sasa Lisa anaumwa nini? Na kama na yeye ana maumivu kama yangu kwanini hataki tuyamalize sasa ili kila mmoja awe huru.Baada ya kujiuliza maswali hayo ndipo kichwa changu kiliponiambia kuwa nimedhihakiwa na kama hiyo si dhihaka basi ni kijembe, pamoja na kupigwa kijembe hicho sikusita kumpa pole kipenzi changu 

Lisa kwa maradhi yanayomsibu lakini jibu lake likawa lile lile la herufi tatu 'enx'.Jibu hilo likakoroga kichwa changu kama vile brenda inavyoyafanya matunda lakini nikajipa moyo na sikuuacha utawala wa hisia mbaya na hasira kali uchukue mamlaka. ' Lisa ma baby i love u so much' (Lisa mpenzi wangu nakupenda sana) Kwa mara ya kwanza nikamuandikia Lisa ujumbe wa kimapenzi usiotoka moyoni. Naye ni kama vile alilijua hilo akajibu 'K'.K kwangu mimi iliyomaanisha KOSA.
' Lisa una nini wewe?'
'Kwani we unaona nna nini?'
'Kama umenichoka si useme tu!"
'Sema wewe ndo umechoka!'
'Kwa hiyo unaamuaje?'

Baada ya majibizano hayo mazito kwa njia ya ujumbe mfupi hatimaye tulifikia mahala ambapo moyo ulinidunda zaidi ya kitenesi.

'Wee ndo useme unaamuaje!' Lisa alinitupia tena mpira huo na mi sikutaka kumuacha kwani nilikuwa bado nampenda nikaurudisha tena kwake.

'Wee ndo uniambie umeamua nini' Baada ya kumtumia Lisa ujumbe huo akaamua kulipasua jipu.

'Kila mtu afanye yake basi!' Huo ndio ukawa ujumbe wa mwisho kutoka kwa Lisa,Ujumbe ambao ulilivunja daraja la mapenzi lililokuwa likiziunganisha nyoyo zetu.Sikuweza kushangaa hata kidogo 

Lisa kufikia maamuzi hayo hata kidogo kwani panapofuka moshi pana moto na moshi huo ulionekana mapema sana.Japo tulipendana kwa dhati tuliachana kimasihara sana hata mtu angeniuliza kwanini tumeachana nisingekuwa na jibu la kumpa, Sijui labda Lisa yeye alikuwa nalo.Pamoja na urembo wote na mapenzi ya dhati niliyokuwa nayo juu ya 

Lisa lakini sikuwa na budi kuachana naye kwani moyo wangu huwa ni mzito saana kupenda pasipopendwa,kubembeleza asiyebembelezeka na kung'ang'ana na mtu mwenye dalili za kutaka kuondoka, Mambo hayo kwangu ilikuwa ni sumu kabisa ambayo inaweza ikaua huba lote la moyo na nisithubutu kupenda tena.

Hatimaye nikayaanza maisha ya peke yangu.Maisha bila ya Lisa, Maisha yaliyojaa chungu tele niliyopaswa kuivumilia. Kushinda mchana kutwa bila ya ujumbe toka kwa Lisa kuliinyima raha siku yangu na Usiku haukufurahi bila kuwasiliana na Kimwana huyo.Namba yake ndiyo! niliifuta kwenye simu lakini ilileta maana gani iwapo namba hiyo niliishika kichwani, Bila shaka hapakuwa na tofauti na kuziba kule wakati huku pako wazi.

Hata baada ya kuuchana na Lisa nilijua ningepata tabu sana lakini haikuwa hivyo, maisha yalikuwa ni ya kawaida sana. Masikini!! Kumbe sikuweza kuyasikia maumivu yeyote kwa kuwa moyo wangu ulikufa ganzi, Lakini vipi ganzi hiyo ikiisha ntaweza kuyamudu maumivu!?.Jibu la swali hilo lilipaswa kusubiri wakati wake ukifika.

Lisa ni kama alikuwa ameniloga vile, Mbona sikutamani kupenda mwingine na muda wote nilikuwa nikimuwaza yeye hata zaidi ya awali tulivyokuwa wapenzi.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni