UZOEFU (13) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 6 Aprili 2021

UZOEFU (13)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Lisa ni kama alikuwa ameniloga vile, Mbona sikutamani kupenda mwingine na muda wote nilikuwa nikimuwaza yeye hata zaidi ya awali tulivyokuwa wapenzi.
SASA ENDELEA...
Baada ya muda mrefu kidogo kupita tangu nimeachana na Lisa, Siku moja majira ya jioni nilipokea ujumbe mfupi kutoka kwenye namba isiyo na jina. ' Helow Tom i miss u'.Ingawa namba hiyo haikuwa na jina niliweza kitambua, ilinikaa kichwani mwangu kuliko namba yeyote ile.Ilikuwa ni namba ya Lisa.Ghafla nikashtuka toka nilipokaa na kuisoma kwa mara nyingine tena.Ndio!..ulikuwa ni ujumbe toka kwa Lisa. 

Kama mimi ningekuwa ni mwanajeshi bila shaka Lisa angekuwa kamiss vita,kama mimi ningekuwa ni mchungaji bila shaka angekuwa kamiss ibada lakini mimi ni mtalaka wake sasa kwangu atakuwa kamiss nini zaidi ya mapenzi?, Bila shaka kipenzi Lisa ameyamiss mahaba. Na ukisikia mtu anapunguza sauti ya redio ili asome ujumbe mfupi kwenye simu basi ilikuwa ni siku hiyo.

'I miss u 2 babie! Siku zote nilikuwa naamini wewe bado ni wangu na nilikuwa nasubiri urejee, Nashukuru umerudi Honey!"

Nilikaa kimyackwa muda ili kumpa tumbo joto Lisa kufikiria kuwa ntamjibu vipi kisha baada ya muda nikamtumia ujumbe uliokuwa na dhamira ya kulirudisha penzi letu kitemi.Halafu ikawa ni zamu yangu tena kusubiri kama nimefanikiwa ama laa!!.

"Tom ar u sure on wat ar u talkin abt?" (Tom una uhakika na unachokisema) Lisa alinitumia ujumbe wa king'eng'e kutaka kuthibitisha kuwa hayo niliyosema nimemaanisha ama namchora na sikuwa najibu lingine zaidi ya '100%' .

Lisa alifurahi kuwa moyo wangu hakuwa mgumu na mimi sikuwa mtu wa kinyongo kwake, Akaniomba radhi kwa yale yaliyotokea na kuniahidi hayatotokea tena.

Siku hiyo tulipiga story nyingi huku kila mmoja akionyesha kuwa ana hamu sana na mwenzake na alimkosa kwa siku nyingi. Asikwambie mtu! Mkiachana afu mkarudiana mapenzi hunoga mara mbili ya awali na kila mmoja anakuwa na nidhamu ya uoga 

Kuliko mkizoeana sana, hakuna atakayemuhofu mwenzake. Baada ya kupiga story nyingi na Lisa kwa simu hatimaye nilimuuliza swali ambalo majibu yake yalinipa raha na karaha kwa wakati mmoja.

Niliweza kumuuliza Lisa kuwa yuko wapi saivi naye akanijibu yupo Dar es Salaam.Nikamuhoji tena alikuja lini akajibu kuwa ana muda kidogo.Basi moyoni mwangu nikafurahi sana kuwa mtoto mzuri nnayependa sana yupo karibu na mimi, Sikutaka kupoteza muda papo hapo nikamueleza kile nnachokiwaza.

' Baby plz naomba kesho uje home!' Nilimwambia Lisa kwa njia ya ujumbe mfupi (msg) huku nikitamani ajibu ndio.

'Swtheart mi mwenyewe natamani sana kama ningekuja ila hapa nilipofikia ni geti kali na isitoshe tunachungwa zaidi ya mbuzi' Majibu hayo ya Lisa hayakuweza kueleweka moja kwa moja kichwani mwangu. Japo nilikuwa namwamini nilihisi kama ananibania. 

Nlitamani hata ampigie simu mama yake Tabora na aombe ruhusa kuwa anakuja kunisalimia hivyo hilo geti kali limuachie lakini nikaenda naye taratibu nione kuwa tutaishia wapi.

'Ina maana Hun hata weekend (mwisho wa wiki) huwa hamtoki?'
'Tunatoka lakini tunakuwa na Mamkubwa na Bamkubwa hivyo itakuwa ni vigumu kuonana na wewe'
'Ok Lisa naomba nikwambie kitu kimoja!'
'Tel me bby'
'Siku mkitoka tu plz tel me mnaenda wapi na sangapi!'

'Worry off babie ntakwambia' Lisa alikubaliana na ombi langu na mimi sikuishia na kuridhika hapo, Nilijiona kama mjinga je wasipotoka ama wakitoka na akasahau kuniambia ama akaniambia na mimi nikawa katika mazingira yasiyoniruhusu kufika walipo itakuwaje?, 

Baada ya kujiuliza hayo niliiona kuwa niliongea bila kufikiri sawasawa na nilazima nitafute njia mbadala ya kuonana na mpenzi wangu kuliko hiyo ya kuwinda kama Fisi, eti Simba abakize mzoga ndiye naye aje kula.

'Bby i have another plan!' (Bby nnao mpango mwingine). Baada ya kimya kifupi kupita nilimtumia Lisa ujumbe huo.
'What plan hun?' (Mpango gani asali)
'Naomba kesho nije kukuona hun!'
'Bby situlishapatana lakini!'
'I know it ma luv bt i cant wait 2 c u plz' (Nalijua hilo mpenzi lakini nashindwa kusubiri kukuona Mpenzi tafadhali' Nilimsihi Lisa naye akanielewa.
'Ok kesho njoo basi lakini tutaonana kwa dk tano tu! Cz nafwatiliwa sana hun!'
'Nimekuelewa bby bt nije mda gani!?'
'Njoo jioni jioni hivi!'

Mwanaume ni mwanaume tu huwa hakubali kushindwa kirahisi rahisi tu baada ya mchezo wa maneno nikafanikiwa kupata ushindi wa ahadi ya kuonana na Mpenzi wangu siku inayofuata, japo kwa sharti la dakika tano tu lakini haikujalisha bora chochote kitu kuliko kukosa kitu. 

Usiku huo nikalala usingizi wa amani na furaha nikiisubiri siku mwanana inayofwata nikaonane na mpenzi wangu. Hakuna kinachonoga dunia hii kama mapenzi ya kweli na hakuna kinachiweka roho juu kama ahadi ya mpenzi umpendaye.

Japo saa ilikuwa ikitembea kasi yake ile ile lakini jicho langu liliona kama inatembea na break (Kipunguza mwendo).Nilikuwa na hamu ya kuonana na Lisa kupita kiasi.Yaani tangu mawio yalipojiri nilikuwa nikiiangalia saa yangu ya mkononi kila mara, Japo ahadi ilisema tuonane jioni sana hadi kufikia majira ya saa tisa alasiri 

Nilishakamilika kwa kila kitu na ikibaki kuianza safari tu. Siku hiyo shule nilitoroka majira ya saa tano asubuhi, Ilipogongwa kengele ya kutoka nilitoka kama kawaida lakini ilivyogongwa ya kurudi badala ya kurudi nikapepea hadi nyumbani.

Naelewa mpenzi wangu Lisa anahusudu kuniona katika mtazamo wa aina gani! Hivyo wakati wa kuchagua mavazi sikufanya kosa. Nilivaa fulana safi kabisa (form six) iliyonakshiwa kwa rangi za orange na nyeupe kisha nikavaa na pensi ya rangi ya brown iliyonikaa sawia na chini nikamaliza na raba za old star za rangi nyeusi.

Mkononi saa peke yake haikunitosha nikaongeza uzito kwa kuvaa ruberband tatu moja ikiwa ya orange na nyeupe zilizoendana na rangi ya fulana niliyovaa na moja ilikuwa na rangi ya brown ili pensi isibaki na upweke. Chini nilikuwa na raba nyeusi rangi iliyokosa support (Haikuungwa mkono).

Hivyo nikaisupport kwa kuvaa miwani nyeusi pamoja na kofia nyeusi. Naam! Nilipojiangalia kwenye kioo sikutofautiana na mtu yoyote mashuhuri (celebrity). Nikaridhika na kuianza safari lakini mara tu baada ya kutoka ndani na kupishana na dada nnje kuna kitu nilikumbuka. 

Nikarudi ndani haraka, mimi si mpenzi wa marashi ( unyunyu) lakini nilikumbuka aina ya manukato anayotumia dada kama ningejipulizia kidogo, hakika Lisa hatotamani kuniachia pindi tutakapokumbatiana, hivyo niliingia chumbani mwa dada kwa siri na kujipulizia marashi yake, Sasa kidume nikawa nimekamilika na kuianza safari ya kuelekea kwa huba la roho yangu! 

Macho ya matamanio ya kina dada kwenye daladala yalinifanya nijiamini zaidi kuwa niko vizuri ( Nimependeza ).

Kutoka nyumbani kwetu hadi anapokaa Lisa haikuwa mbali sana, ni mwendo wa takribani lisaa limoja ukijumlisha na foleni.

'Hey bby m so cloz jiandae kutoka' (Hey mpenzi nipo karibu sana jiandae kutoka) nilimtumia Lisa ujumbe huo na yeye kitendo cha kujibu tu ikawa tayari nimeshawasili.

"Aaaaaargh sheeet!!" Niling'aka mwenyewe mara baada ya kukumbuka ya wahenga kuwa mkono mtupu haulambwi.

Ndio nilikuwa nimependeza lakini hiyo haikutosha kumpumbaza Lisa kuhusu zawadi yake aliyoniambia nimletee, Bahati nzuri mtaani kwao nako palichangamka nikaliendea duka moja kubwa ili kuona kama naweza kupata nnachotaka, 

Baada ya kufika dukani muuzaji aliniona kama nashangaa vile lakini hakujua nilitazama lakini sikuona, kichwa kilifikiri kwa upesi kuwa ninunue nini maana mpenzi wangu alikuwa anapenda vitu vikuubvitatu chocolate ya dairy milk, maziwa ya unga ama biscuit za eet sum mor. Baada ya kufikiri kwa muda nikachukua maziwa ya unga na dairy milk, 

Nikiwa bado nipo dukani simu yangu iliita " baby uko wapi jaamani" sauti laini ililalama kimahaba. Sauti hiyo ilitosha kabisa kunisahaulisha hadi chenchi, muuzaji naye akafaidika na mapenzi yangu juu ya Lisa. Nikaondoka chap chap kuwahi tulipo panga kukutana, 

Nilifika kweli na nikamkuta Lisa, kitendo cha kumuona tu ikawa ni sawa na jua lililomulika rohoni mwangu kila kitu kikawa wazi ( mapenzi ya dhati ) taratibu nikamkumbatia Lisa na P.K iliyokuwa mdomoni mwangu ilipata tabu kwani sasa ilitafunwa na watu wawili na kama hiyo haitoshi ikatolewa kabisa na kuziacha ndimi zetu pekee kufanya mchezo ulioleta utamu.

Hakika ndani ya dakika chache tu tulikuwa tumeshapotea kwenye dunia ya kawaida na kuzama kwenye ulimwengu wa peke yetu, ni bahati nzuri tu kilishaanza kuingia kigiza cha usoni hivyo hatukuonekana na wengi na hata kama ingekuwa ni saa saba mchana nisingemuhofu mtu.

"Mmmh ulimi wako haujaacha ukorofi wake tu!" Nilimtania Lisa kimahaba kwa kuninyonya vizuri naye akaachia tabasam na kuzing'ata lips (papi) zangu kwa lips zake akiwa na maana niache utani.

"Bby tukae basi pale tupate walau dinner pamoja!" Nilimshawishi Lisa huku nikimuonyeshea kwa kidole hotel iliyokuwa karibu yetu.

"Baby haiwezekani yaani hapa tu nimeaga naenda dukani na mtaa huu una wambea hatarii!" Alijitetea Lisa huku akiniangalia kwa jicho la upole na mimi sikutaka kumshawishi zaidi tukaachana na swala hilo na kupiga stori zetu. Kikubwa nilimsisitiza Lisa aache kuzingua katika mapenzi kwani moyo wangu nimemkabidhi yeye.Tuliongea mengi kuhusu mapenzi yetu hadi Lisa alipoaga na kutaka kuondoka.
'Naomba mkono wako wa kulia tafadhali!' Nilimwambia Lisa huku nikiwa nimeshaanza kuukamata mkono huo, naye hakunizuia kufanya nilichotaka kukifanya, nilimvua neckless ya silver yenye kidani cha kopa aliyokuwa kaivaa mkononi.
"Bby all i need for you is Love! Just love me!" (Mpenzi vyote nnavyohitaji kutoka kwako ni mapenzi! We nipende tu) Nilimwambia Lisa alipokuwa akinisaidia kunivisha neckless yake.
Ni kama vile aliupenda mchezo huo wa kunyan'ganyana vitu kwani na yeye aliingiza vidole vyake katikati ya vidole vyangu kisha akaanza kuzihamisha ruberband pana toka kwa mkono wangu kwenda kwake!
"Nibakishie hata moja jamani!!" Nilimsihi Lisa alipokuwa anazibeba zote.
"Tulia wewe mii ndo nakupenda zaidi hakibaki kitu hapa!" Lisa aliniambia kiutani lakini akizibeba kweli rubber hizo.

",Bby chukua na moyo wangu basi ukae nao!" Nilimtania Lisa naye akaangua kicheko. Ingawa kikao chetu hicho tulipanga kidumu kwa dakika tano tu,hadi muda huo tayari kilishakula dakika kumi na ushee, kila mmoja hakutaka kuachana na mwenzake lakini ilitubidi Lisa alinipa ulimi wake kwa mara nyingine nami nikaunyonya inavyotakiwa kisha nikamkabidhi zawadi zake na tukawa tumeagana, japo yeye aliondoka lakini mimi nilibaki 

Nimesimama pale pale nikiutazama mwendo wake wa twiga, ama kwa hakika mtoto huyu alipata mibaraka ya pekee sana toka kwa muumbaji na ingawa alikuwa ni mpenzi wangu sikuwahi kumzoea, kila tulipokutana nilimuona ni mpya, sijui uzuri wake ulikuwa unaongezeka kila kukicha au ndio mahaba niue!

Lisa alipofika kwenye kona ya mwisho alinipungia mkono nami nikamtumia busu la upepo kisha akapotea kwenye mboni za macho yangu. Nilikitazama tena kile kidani chake cha silver kilivyong'aa kwa mkono wangu kisha nikakichum na moyo ukatabasam. Nikaianza safari ya kurudi nyumbani huku nafsi ikinisifu kwa kumiliki mtoto mkali.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni