UZOEFU (26) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 12 Aprili 2021

UZOEFU (26)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Tuliongea mengi na shemeji yangu huyo na mwisho wa siku alinielewa na akakubali kurudi nyumbani kwa roho moja.Hivyo nikawa hakimu mzuri kwenye kesi hiyo hakuna nilichokuwa nimebakiza zaidi ya kurudi nyumbani huku nikimuacha Amani amsindikize mpenzi wake kwao.
SASA ENDELEA...
Baada ya miezi kadhaa kupita kimya kizito kilitawala kati yangu na Sunshine.Kwa upande mwingine nilifurahishwa na kimya hicho kwani kilimaanisha Sunshine amekubaliana na matokeo.Nilifurahi kwa kuwa wakati mwingine mtu akikupenda 

Sana ukimgeuka anaweza kufanya jambo baya, nashukuru kwa kuwa hali hiyo haikutokea.Kimya cha Sunshine kilimaanisha penzi langu na Lisa kupamba moto.Tulikuwa tukipendana sana kama vile hatukuwahi kuchukiana.

Siku moja tukiwa tumechati mno kwa njia ya meseji roho yangu ilinituma kumuuliza Lisa swali ambalo sikujua kwanini roho imenisukuma hivyo.

' Babe bado unanitunzia mali yangu?' Niliuliza swali hilo kwa ujumbe mfupi huku nikiamini Lisa bado atakuwa na bikra yake niliyokuwa niki ilea lea kuitoa.
"Mali gani hny?" Lisa alijibu na kuonyesha kuwa hajanielewa.
" Bikra swtheart!" Nikaweka mambo hadharani.

"Bby m sorry bt tulivyoachana nilikuwa na hasira hivyo nikapata boy mwingine akaitoa then akanisaliti.Tom i luv u so much baby cz ur alwayz there 4 me!" Lisa alijibu maneno mengi lakini jibu likiwa ni moja tu! Ile bikra niliyomuacha nayo hakuwa nayo tena.

Ghafla nakajikuta nakosa hata nguvu ya kushika simu na kuandika neno lingine la ziada.Meseji ya Lisa iliupa moyo wangu tabu zaidi ya mawimbi makali kwa mashua iliyopo katikati ya bahari.Nikashindwa kuamini na kufikiri Lisa ananitania kwa maana kwa kiasi kikubwa nilikuwa nimemrithisha tabia ya masihara.
' Come on baby stop joking!' Baada ya kufikiri inaweza kuwa utani nilipata nguvu ya kumtumia Lisa ujumbe mwingine ili kuthibitisha kama ni kweli.
" Sure bby m nat lie!" Lisa akathibitisha kuwa ni kweli.

Maskini hali yangu ikawa mbaya ghafla nikavuta picha na kumuona kidume alivyokuwa akishughulika kuitoa bikra ya mpenzi wangu, hakika niliumia sana.Mapigo ya moyo yalienda kasi sana kwa wakati huo sikuweza kufahamu mara moja ni nini kimenisibu ila baada ya muda mchache kupita ndipo nilibaini kuwa toka ile asilimia mia niliyokuwa nikimpenda 

Lisa sasa ilisalia asilimia hamsini peke yake hiyo ilimaanisha kuwa penzi limegawanyika kati kwa kati.Bora usikutane na bikra kuliko ukutane naye akiwa bikra afu itolewe na mtu mwingine sidhani kama ningeweza kuvumilia tena aina yeyote ya maudhi toka kwa kimwana huyo niliyewahi kumpenda kwa moyo wote.

Kama ningekuwa na uwezo basi ningelirudisha penzi langu kwa Lisa lau lifike japo asilimia tisini lakini shida moja ya moyo huwa haupangiwi. Japo Lisa alijiamini kunieleza ukweli kwa kuwa aliamini ningeendelea kumpenda sana lakini alijidanganya, kwa wakati huo ni bora hata angenidanganya ilitoka akiwa anaendesha baiskeli kama wadanganyavyo wasichana wengine lakini ndio hivyo tena maji yalishamwagika,Majira na nyakati vikaendelea kusogea huku bendera ya penzi letu ikipepea nusu mlingoti, tayari 

Nilishamshusha Lisa thamani na sasa sikuwa mwepesi tena kwake kama ilivyokuwa mwanzo hata kumuita sweetheart nilihisi naidhulumu nafsi yangu."Lakini na mimi mbona nilimtoa bikra Sun!" Wakati mwingine nijikuta najiuliza hivyo ili kuushawishi moyo wangu uendelee kumpenda Lisa kama awali lakini moyo ulionekana kutodanganyika


Sikuwahi kufikiri hata siku moja kuwa hata mapenzi ya dhati huwa yanafikia tamati lakini jambo hilo sasa lilikuwa dhahiri.Lisa ambaye alikuwa akiuchafya moyo wangu kiasi cha kuninyima hata usingizi leo hii alikuwa hanitishi kwa lolote, Ni ajabu lakini ni kweli kuwa sasa Lisa hakuwa na tofauti yeyote na wasichana wengine mbele ya mboni za moyo wangu.Kama ilivyo ada hakuna anayesalia ukumbini mara baada ya karamu kuisha vivyo ndivyo ingekuwa ngumu kwa mimi kubaki na Lisa hali yakuwa daraja la mapenzi lililokuwa likiziunganisha nyoyo zetu lilishavunjika. 

Ni rahisi sana kuvumilia kifungo cha miaka mia jela kwa kesi ya kusingiziwa lakini si rahisi hata kidogo kubaki na mtu moyo uliomtema.Hali hiyo ndiyo iliyonipelekea siku moja majira ya jioni kuandika waraka mfupi niliomtumia Lisa kumjuza kuwa nimejiuzulu katika penzi lake.Sikuweza kutambua mara moja ni kwajili ya mshtuko, kutoamini ama maumivu lakini Lisa alikaa kimya siku mbili kabla ya kuujibu waraka wangu.

Hadi mara ya mwisho kabla ya kumtumia waraka huo tulikuwa bado tukiishi vizuri na sikuonyesha dalili yeyote ya kumpiga chini, kanuni moja iliyokuwa ndani yangu ni hii, naweza kuchukia jambo baya leo lakini nikalichukulia hatua baada ya wiki mbili hata Lisa niliachana naye wiki kadhaa nyuma lakini nilimjuza baadaye sana.

Katika kimya chake Lisa hakukaa hivi hivi ukiona kobe kainama jua anatunga sheria, alitumia muda huo vizuri kutengeneza meseji ndefu iliyokuwa na maana ya kutoridhika na maamuzi yangu ya kuachia ngazi lakini aliiandika kwa namna ya kukubali niondoke, mfumo huo mie nauita ' staki natataka'.

Tofauti na meseji nyingine Lisa alizokuwa akiniomba turudiane tulipoachana mara kadhaa hapo nyuma, ujumbe huo wa siku hiyo haukuwa na uzito wowote mbele ya macho yangu na nilipokuwa nikiusoma ulinichekesha mithili ya katuni za Madenge.

Baada ya moyo wangu kuridhia kuwa huo ni mwisho ambao hautakuwa na mwendelezo mwingine na Lisa niliamua kumjulisha Antie yangu kipenzi kuwa Lisa si mkwewe tena.Mara moja nilitafuta namba zake na kumpigia.
"Hello!" Baada ya simu kupasua anga na kukanyaga mawingu ya Tabora niliisikia sauti nzuri ya Shangazi yangu.
"Hello Antie za huko!?"
"Mtoto mbaya wewe au Dar umepata Antie mwingine!?" Shangazi badala ya kupokea salaam yangu alikimbilia kwenye lawama na ilikuwa haki yake kunilaumu kwani tangu nimeondoka Tabora tumekuwa tukiwasiliana kwa mbinde.
" Lakini hata wewe umenisusa sana Antie yangu vipi lakini Uncle yuko poa!?"
" Yupo poa vipi mkwe wangu yupo!?" Kwenye salaam tu Antie akawa amepagusa nilipopataka.
"Me mbona single boy kitambo tu hadi nimesahau yaani!"Nilimjibu kimzaha shangazi.
"Hahaha we Tom haukui tu!?" Shangazi alijua nafanya masihara yangu.
" Kweli Auntie! Lisa tushaachana!"
"Weeh! Usiniambie……tatizo nini lakini!"
"Lisa bado ana akili za kitoto Antie!…nasubiri akue kue kidogo tunaweza tukafanya maisha!" Nilimueleza shangazi katika sentensi moja iliyobeba mambo mia huku nikimpa tumaini ambalo halikuwepo kwani sikuwa na mpango tena wa kurudiana na Kimwana yule.

"Jamani nyie!… mmenisikitisha kweli yani jinsi mlivyokuwa mnapendana vile mmeaachana au Lisa kakuacha Tom niambie nikusaidie!" Shangazi alionyesha wazi masikitiko yake huku akizani huenda Lisa ndio kaniacha lakini nilipomueleza kuwa mimi ndo nimembwaga aliishiwa nguvu kabisa.Nadhani shangazi alikuwa akiufikiria uzuri wa sura,umbo na rangi nzuri ya Lisa lakini hakujua noti hata ipambwe vizuri vipi kama haina thamani hakuna atakayeijali.

Tangu nimeyajua mpapenzi sikuwahi kuwa mpweke ( single) kwa muda mrefu.Baada ya kuachana na Lisa nilihisi bado nahitaji mapenzi.Ulimwengu huu umejaa walimbwende wa kila namna vipi kidume aliyekamilika kama mimi niishi peke yangu? Wakati Duniani penyewe naishi mara moja tu. 

Bila shaka haikuwa na haja ya kufanya hivyo.Ni muda mfupi baada ya kujiunga na chuo cha ardhi ili kupata stashahada katika uchoraji wa ramani na hii ni baada ya kuhitimu A level.Katika chuo hichi napata fursa ya kukutana na vimwana wenye uzuri na sifa za kila namna lakini nabaki kuwatizama kwa macho tu, hii ni baada ya moyo kushindwa kuchagua mmojawapo atakayenifaa.

" Khaah! Hata huyu jamani?" Nilijikuta naushangaa moyo wangu baada ya kujenga mazoea na kipusa mmoja ambaye moyo uligoma kumfungulia mlango aingie ndani.Ukigongwa na nyoka nyasi zikikugusa lazima ushtuke niligundua Lisa hakuondoka hivi hivi ila aliniacha nikiwa nimejifunza mengi.

Naam! Sasa nilikuwa muoga wa kupenda hovyo, nilikuwa nikihitaji mtu ambaye atanifaa haswaa si kwajili ya sura yake nzuri wala umbo lake maridadi ila mtu huyo ni yule ambaye atanipenda kwa dhati, Je ni nani huyo!? Kila niliyekuwa nikifikiria huyu ndiye moyo uligoma,sasa ni nani basi! Hapo ndipo nafsi iliposhtuka baada kumkumbuka Sunshine.

Naam! Huyu ni binti pekee aliyekubalika kumoyo,Katika kipindi chote nilichoishi na Sunshine alinifanya nijisikie mwanaume haswaa, lakini kukubalika pekee moyoni ilikuwa haitoshi kizungumkuti kilikuja jinsi ya kumpata tena mrembo huyo. " Nilivyoondoka kwa mbwembwe namna ile naanzaje kurudi tena kwa Sun!?" Nilijikuta najiuliza swali ambalo majibu yake yalinifanya nione haya kwa kiasi flani. 

Nikiwa bado nawaza jinsi ya kumpata tena Sun nilihisi kiu, ila nilipojaribu tu kunyanyuka ili kufwata maji nikapata kizunguzungu cha ghafula, nuru ikapotea nikahisi kama vile nabebwa juu juu na kubwagwa chini baada ya hapo sikujua nini kiliendelea, nilikuja kushtuka dakika chache baadae, Kitu gani kimeniangusha? Swali hilo halikupata jibu la msingi zaidi ya labda hisia nzito nilizokuwa nazo kabla ya kuamka, nikajizoa zoa pale chini nilipokuwa na kukaa vyema kwenye sofa. 

Ni bahati nzuri tu hapakuwa na mtu karibu aliyeshuhudia kitendo hicho, sikutaka kupoteza hata dakika moja, nikaokota simu yangu mezani nakuanza kuandika namba za Lisa nilizozicopy kichwani na kuzipaste kwenye simu lakini baada ya kupiga ikawa holaaa! Namba hazipatikani masikinii nimepoteza dhahabu nikifuata kipande cha chupa kilichong'aa.Kutopatikana kwa namba ya Sun ilikuwa ni pigo kubwa kwangu.

Akili ikachoka, nikaamua kwenda kulala ambapo napo sikupata usingizi bado nilikuwa nikiwaza namna ya kumpata Sun.Ni muda mrefu sasa toka tumeachana na kuifuta namba yake kwa simu, japo niliikariri vizuri kichwani lakini nikahisi huenda nimeisahau, nikainuka toka kitandani na kuelekea katika meza yangu ya kujisomea, 

Naam! Katika kipindi kile najaribu kuikariri namba ya Sun nakumbuka nilikuwa kwenye meza hiyo hiyo pia nilikuwa nikiichora chora kwenye daftari.Kitendo bila kuchelewa nikaanza kushakura huku na kule hadi nilipolipata daftari ambalo nilihisi litakuwa na namba hizo."Asta la vista!" Nilifurahi mwenyewe baada ya kuziona namba hizo.

Kosa lililosababisha namba hizo kutopatikana ni kuwa namba mbili za mwisho niliziweka mwanzo na zile za mwanzo nikaziweka mwisho.Nikaziandika tena kwenye simu kwa ufasaha kisha nikaziangalia mara mbili kuzihakiki kabla ya kupiga tena.
"Kaa mbali na mie nimeshapenda,kaa mbali na mie nimeshaozaa……" hiyo ni caller tone ya moto band iliyokuwa ikiitumbuiza baada ya kumpiga Sun.
"Hallo!" Nikiwa najaribu kuifikiria mistari ya wimbo huo simu ikapokelewa.
"Mambo vipi Sun!?" Nilimsalimu baada ya kuhakiki sauti yake.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni