UZOEFU (27) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 13 Aprili 2021

UZOEFU (27)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
ILIPOISHIA...
"Kaa mbali na mie nimeshapenda,kaa mbali na mie nimeshaozaa……" hiyo ni caller tone ya moto band iliyokuwa ikiitumbuiza baada ya kumpiga Sun.
"Hallo!" Nikiwa najaribu kuifikiria mistari ya wimbo huo simu ikapokelewa.
"Mambo vipi Sun!?" Nilimsalimu baada ya kuhakiki sauti yake.
SASA ENDELEA...
"Poa mzima wewe!?" Alijibu Sun kuonyesha kuwa ameshajua anaongea na nani.

Baada ya kumaliza salaam moja kwa moja nilimpeleka Sun kwenye dhumuni langu la kumpigia simu, Sun alionekana kushangazwa sana na mimi ambaye hakutarajia kuwa siku moja ningerudi na alikuwa akijitahidi kuniuliza habari za Lisa ambaye kwa muda huo sikutaka hata kulisikia jina lake, baada ya kuongea kwa muda mrefu kidogo na maongezi kufikia mahali pazuri tuliagana kwa miadi ya kumpigia tena baadaye.

Tofauti kabisa na nilivyofikiria kuwa baadae itakuwa ni kumalizia tu kile nilichokianza mchana lakini sikuamini kile kilichotokea baada ya kumpigia simu majira ya saa nne za usiku.Sun aliniwia mkali mithili ya mzazi wa watoto watukutu na kila mara alikuwa akiyarejea maneno yangu makali niliyomwambia siku ile tunaachana, 

Nikiwa bado najaribu kujitetea kwa sauti ya upole Sun alinitakia usiku mwema haraka haraka na kunikatia simu, ni wazi kwamba hakutaka kuzisikiliza porojo zangu zinazopendeza masikioni pekee, jinsi nilivyo jisikia ni Mola pekee anayejua ama msomaji wangu aliyewahi kufanyiwa mchezo huo.Sikufa moyo kila uchwao niliendelea kumuimbia Sun wimbo ule ule wa kutaka kuwa naye hadi alipoanza kunielewa.
"Kama nilivyokwambia Tom wangu kweli bado nakupenda lakini nimeshapata mwingine na ananipenda sana yaani mie ndio namsumbua na kilichonifanya nimpende anafanana na wewe!" Ni sauti laini ya Sun ikijaribu kunieleza jambo gumu nilipomtembelea mtaani kwao.
"Kama kweli bado unanipenda tatizo ni nini Sun, kwanini usimpige chini huyo jamaa.Niamini Sun kweli nimeshindwa kuishi bila wewe mpenzi wangu!"
" weeh!…weh huo unyama unaweza kuufanya wewe tu! Maumivu niliyoyapata kipindi kile siwezi kumfanyia mtoto wa watu ivyo!"
"Kwaiyo itakuwaje sasa Sipo tayari kukupoteza Sun…nakupenda!"
"Kitu pekee nnachoweza kukwambia Tom nakupa miezi mitano ya kusubiri kama utaweza, huyu jamaa akinizingua tu ntakuwa wako tena lakini akinitendea vizuri basi itakuwa imekula kwako!"
"Ok! Sun haya yote niliyataka mwenyewe na upo sahihi kunipa adhabu yeyote ile uipendayo ila kitu kimoja nnachokusihi naomba unihurumie sababu nateseka juu yako kwaheri naamini tutaonana tena!" Nilimuaga Sun nakuondoka roho yangu ikiwa nyeupe, siku zote nimekuwa mshindi wa michezo ya maneno lakini hakuna marefu yasiyokuwa na nncha leo hii nilizidiwa kete na mtoto wa kike. Niliondoka huku nikijipa moyo kuwa Sunshine atakuwa wangu tena miezi mitano aliyonipa sio mingi.

Baada ya miezi mitano kwisha nilirudi tena kwa Sun kumkumbusha kuwa muda umefika, japo mimi nilikuwa naziona siku hizo kuwa ni nyingi sana nilipomwambia Sun kuwa miezi hiyo imekatika alionekana kushangaa sana imeishaje upesi namna hiyo kwa maana nyingine kwa upande wake mambo yalikuwa ni mazuri bado hivyo hiyo ilimaanisha hakuna tumaini lingine kati yetu na hata kama lingekuwepo nisingeweza kusubiri tena.

Nilichofanya nikumuaga Sun na kumuahidi sitomtafuta kamwe pia moyoni mwangu nilimfuta rasmi na kwa upande mwingine nilimuonea wivu bwana aliyempata kwani alipata mwanamke aliyekamilika haswa.

Sasa Tom mimi niliishi nusu mtu nusu mfu, raha ya maisha haikuwako tena nilipo mimi.Wakati mwingine nilifikiri ni bora kufa tu.Mapenzi hayakunitendea haki, Kweli mapenzi upofu anayependa hayamuoni.

Siku moja majira ya usiku nikiwa nimepumzika chumbani kwangu simu yangu iliita na nilipoangalia ni binamu yangu Dora ndiye aliyekuwa akipiga.Maisha yangu mapya yamenifanya kuwa mpweke kiasi cha kupiga stori na mtu yeyote hata aliye wrong namba.

Baada ya kupokea simu hiyo ya Dora tulipiga porojo nyingi sana hadi ikafikia mahali tukaishiwa vya kuongea na ndipo mada hii ilipozuka sasa.
"Ivi unajua kwanini nilikuwa namchukia sana Lisa?" Dora alianza kwa kuniuliza na nilipomuuliza kwanini alianza kufunguka.
" Nilikuwa simpendi kwasababu alikuwa anamnyima rafiki yangu haki yake ya msingi!'
"Rafiki gani tena!?"
"Tom usitake kujifanya haumjui rafiki yangu Zabibu wakati nilikuwa nakuja naye kwenu mara nyingi tu pindi bado mnakaa tabora"
"Sasa Lisa alikuwa anamkatili vipi!?"
"Tom sidhani kama Dunia hii kuna msichana aliyewahi kukupenda kama alivyokuwa akikupenda Zabibu,Alikuwa anakupenda hadi akikuona anatetemeka na huwezi amini mara zote tulivyokuwa tukija naye kwenu alikuwa anataka kukwambia lakini tukifika anaishia kukutazama tu.Basi tulikuwa hatupendi kweli tukikuona na Lisa!"
"Sasa kwanini ukamsaliti rafiki yako!?"
"Huwezi amini Zabibu alikuwa anakusifia hadi mie mwenyewe nikawa naona wivu na nilipopata fursa ikabidi niuonje huo utamu rafiki yangu aliokuwa anauona kwako!……kwani nilifanya vibaya!" Dora aliniuliza kwa kunitega hali nikijua tulifanya vibaya nilimjibu hatukufanya vibaya.
"Nikuulize kitu!?" Nilimwambia Dora naye alipojibu ndio nikaendea.
"Saivi Zabibu yupo wapi!?"
"Yupo huko huko Dar!"
"Naomba namba yake basi!"
"Sikupi!"Dora alijibu kikorofi.
"Kwanini sasa!?"
"Unafikiri mie sijui unataka kufanya nini, me mwenyewe nakupenda!"
"Lakini Dora sie si ndugu!"
"Aya bhana ulale salaama!" Kabla sijajibu neno akakata simu bila shaka nilimkera japo yeye alinifurahisha sana siku hiyo.

Uongo dhambi kuacha Lisa msichana mwingine aliyekuwa akiutesa moyo wangu alikuwa ni Zabibu na kama nisingekuwa na Lisa basi ningekuwa na mtoto huyo.Uzuri wake wa asili ulioundwa kwa ngozi yake rangi ya chocolate, nywele 

Zake za singa singa, macho yake ya mviringo, umbo lake namba nane, tabia yake ya upole,akili yake iliyotulia vilimfanya mwanaume yeyote apende kuwa naye.Sikuwahi kufikiria kuwa Zabibu alikuwa akinipenda kiasi hicho na jinsi alivyokuwa akionekana kwa nadra kutokana na kusoma bording toka mdogo kulinifanya nimuone kama malkia pindi anaporudi likizo.

"Wooooh! Nakupenda Zabibu!" Nilijisemea kimoyo moyo Nilipokuwa nainuka toka kitandani ingawa nilikuwa nimechoka habari za Zabibu toka kwa Dora zilisababisha usingizi wote kunipaa.Ingawa Dora alininyima namba zake moyoni niliapa kumtafuta kwa udi na uvumba hadi nitakapompata. Usiku huo huo nikaanza kutype jina 

Zabibu kwenye mitandao yote ya kijamii,Twitter,Instagram,Facebook,Skype,Badoo na kwingine koote!,Baada ya kuhangaika kila kona kwa siku kadhaa bila mafanikio ndipo wazo jipya liliponijia, ama kweli penye nia pana njia! Nilijisemea mwenyewe baada ya kumpata Zabibu kwa jina tofauti kabisa nilipokuwa nakagua majina ya rafiki wa Dora Facebook.

Japo alikuwa katumia jina lingine tofauti kabisa lakini sura yake ya kitoto ( baby face) iliniwezesha kumtambua kirahisi.Baada ya kumpata binti huyo kigoli na kumuelezea jinsi nnavyomzimia kisha nayeye kunipokea kwa mikono miwili hatimaye maisha yangu ya kimapenzi yalirejea kwenye ramani tena.
"Baby kwanini unasema tutaishi pamoja hadi kufa!?" Zabibu aliniuliza swali hilo siku moja tulipokuwa tukipata chakula cha jioni kwenye mkahawa mmoja.
"Malkia Wangu nilikupa story ya Lisa na Sunshine nimepitia mengi na sasa nimekuwa MZOEFU!"
"MZOEFU!?" Zabibu aliuliza kwa herufi kubwa!.
"Yes baby mimi ni MZOEFU!"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

MWISHO

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni