UZOEFU (4) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 1 Aprili 2021

UZOEFU (4)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
"Safi!...Mzee nimemkuta!?" Huwa sinaga nidhamu ya uoga mbele ya watu wenye wasiwasi kama yeye.Nilijibu salam yake kwa kujiamini ni sikutaka aniulize shida yangu moja kwa moja nikamuulizia baba mwenye nyumba kama vile nilikuwa namtafuta kwa udi na uvumba lakini rohoni mwangu nilipiga dua ya kimya kimya asiwepo.

SASA ENDELEA...
Mungu alikuwa upande wangu na kweli mzee huyo hakuwepo.alikuwepo tu mama na nikaomba kuonana naye,bila hiyana dada yule akanikaribisha ndani.

"Ooooh! Tom jamani umekuja lini!?" Baada ya kuingia tu ndani mama yake Lisa alinipokea kwa furaha.Ingawa alikuwa amekaa kwa mtindo wa kulala kwenye sofa alitaka kunyanyuka ili anisalimie vizuri.Nililitambua hilo nikamuwahi na kumpa mkono.

"Shikamoo mama!" Nilimsalimu huku nikiona haya kiasi flani kwasababu alikuwa akiniangalia saana.Moyoni mwangu nilifurahi sana mama Lisa kunipokea kwa mikono miwili kwani alikuwa ameniongezea sifa (credit) toka kwa yule binti aliyenifungulia mlango nilifahamu fika kama angeniona siku nyingine hata kama ndani pasinge kuwako na mtu basi angenifungulia kwa heshima na taadhima bila kuuliza swali hata moja.

Baada ya kusalimiana na mama Lisa (mama mkwe) Nilikaa kitako na tukaanza kupiga hadithi (story) mbili tatu.Aliniuliza maswali mengi kuhusu Shule,wazazi na habari za Dar es salaam,maswali yake yote niliyajibu vizuri na kwa ufasaha mithili ya mnadi sera anayewania jimbo asilotaka kulikosa hata kidogo.

Na mara kadhaa mama mkwe wangu huyo alikuwa akinisifia kuwa nimekua na kurefuka saana.Hata mimi nilimpa hongera zake kwa kuonekana kijana kila uchwao.Sifa zangu kede kede juu yake pamoja na mazungumzo yangu ya busara yalionyesha wazi kuwa amefurahia sana uwepo wangu chini ya dari ya nyumba yake.

Hadi maji ya matunda (juice) niliyowekewa kwenye glasi yangu inaisha na mimi maswali yangu yote kichwani yalikuwa yameisha.Kitendo cha kukaa na mama mkwe wangu huyo nusu saa tu kilitosha kujua habari zote za Lisa,halikazalika na yeye alizijua za kwangu.

Hivyo hapakuwa na la ziada zaidi ya kuaga na kuondoka,japo mama mkwe alinisihi sana kuwa niendelee kusalia kwake muda huo lakini sikulegeza msimamo wangu kabisa wa kutaka kuondoka. 

Ingawa nilipenda kupendwa na mama mkwe wangu huyo lakini sikutaka anizoee na kitendo cha kukaa naye muda mrefu huenda kingefanya hilo kutokea.Siku zote ni muhimu kuondoka mahali wakiwa bado wana hamu na wewe hiyo husababisha wasikukinai siku nyingine wanapokuona tena na ndivyo nilivyofanya.

Usiku wa siku hiyo baada ya kupata chakula cha jioni bamdogo alisema ana mazungumzo na mimi,Sikuwaza sana juu ya anachotaka kuniambia bamdogo na mamdogo pamoja na watoto walipokwenda kulala,Ilikuwa ni wasaa wa Bamdogo na mimi kufanya mazungumzo hayo."Mwanangu unajua hapo nnje tuna cafe (mgahawa) nzuri sana.

Sema mama yako mdogo alipopata ujauzito tukaamua tuifunge ili awe na muda mzuri wa mapumziko pamoja na kuhudhuria kliniki inavyotakiwa kwasababu yeye ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu.Si unajua tenashughuli zangu mimi si mtu wa kutulia sehem moja,Sasa unaonaje kama tukiufungua tena ili wewe usiwe idle (huna kazi).

Uwe unausimamia? Hili ni wazo langu lakini kama haupo huru wee sema tu ila nakupa muda wa kufikiri hadi kesho alafu utaniambia!"

Bamdogo akawa ameleta mada mpya kabisa kwangu ambayo sikuitarajia kwa muda.Huwa siwazi kitu bila kushirikisha uwepo wa Lisa maishani mwangu.

Haraka haraka nikawaza na kuwazua kama ntakuwa msimamizi (Menager) katika mgahawa huo si nnaweza kukosa muda wa kuenjoy (kufurhia) na Lisa kweli atakaporudi.Lakini kama pia ntakuwa na muda alafu sina pesa (mwanaume suruali) si ntakuwa sina furaha kweli,Japo mapenzi sio pesa lakini pesa ni chachu ya mapenzi na mkono mtupu siku zote haulambwi.

Nilishayajaribu mapenzi na kuliona hilo.Ingawa nilikuwa nimekuja na akiba ya pesa nilizojitahidi kuzitunza toka kipindi nipo shule,lakini niliamini pesa hizo zisingetosheleza mahitaji hasa ukizingatia zingekuwa za kutoka tu bila kuingia.

"Hayaa mi nakwenda kulala asubuhi utaniambia umefikiria nini!" Bamdogo baada ya kuona nipo kimya muda mrefu akaamua kuniaga akalale lakini hakujua mimi sikunyamaza bure,ukiona kobe kainama jua anatunga sheria na ndivyo ilivyokuwa kwangu nilikuwa nikichanganua maisha yangu ya mapenzi na kazi na hadi muda huo nilikuwa nimeshapata jibu.

"Baba mimi nipo tayari kuanza kazi hata usiku huu ila nilikuwa nataka kujua mambo kadhaa kuhusiana na cafe (mgahawa) hiyo!" Maneno hayo toka kwangu yalimfurahisha sana Bamdogo akafuta wazo la kwenda kulala na mazungumzo yakaanza upya.

Nilimuhoji kuhusu mambo mengi sana ikiwamo jinsi walivyokuwa wanaendesha mgahawa huo.mapato yanavyopatikana,aina ya wafanyakazi waliokuwepo,bei za bidhaa na mengineyo mengi,maswali yote bamdogo alijibu 

Vizuri pia mimi sikumwambia nimefikiria kufanya nini kutokana na majibu yake hata hivyo bamdogo alishangaa sana jinsi nilivyokuwa nikimuuliza maswali kama vile mjasiriamali mkongwe aliyebobea katika fani hiyo.

Bamdogo alinizoea kuwa mimi ni mtu mwenye story nyingi za mizaha kila wakati hakujua kuwa kuna busara kubwa na maarifa ya hali ya juu yaliyojificha ndani yangu.

Hadi kufikia majira ya saa sitta unusu za usiku tulikuwa tumemaliza kikao chetu. Na nilienda kulala nikiwa na deni la mchanganuo mpya wa uendeshaji wa mgahawa mimi kama menager (Msimamizi) mpya.Mchanganuo ambao nilitakiwa kuuwasilisha mapema asubuhi.

Usiku wa deni haukawii kucha.Hatimaye mapambazuko yakalifukuza giza na jogoo wa jirani akawika kuthitibisha pamekucha.

Naam,ilikuwa ni siku ambayo natakakiwa kuwasilisha mchanganuo wangu kwa bamdogo.Haikuwa kazi ngumu sana kwani mchanganuo tayari ulikuwepo kichwani na nilichofanya asubuhi hiyo ni kuuhamishia tuu kwenye karatasi ili wakati wa kuuwasilisha nisije nikasahau jambo.

Mara baada ya bamdogo naye kuamka tulielekea mbele ya nyumba ambapo ndipo ulipo mgahawa.

"Hongera bamdogo umejitahidi kutengeneza kitu cha kisasa kabisa!" Nilimsifia bamdogo mara tu baada ya kuingia ndani ya mgahawa huo uliokuwa una manthari ya kuvutia macho!.

"Sema kama hizi kuta tutaziwekea picha nzuri za matunda na vyakula patavutia maradufu!" Nilianza kutoa ushauri wa hapa na pale huku bamdogo akiwa kachanua tabasam kubwa kuashiria kuwa alikuwa ananielewa sana.

Baada ya kuuona mgahawa huo nilianza kutoa mchanganuo wangu rasmi.

"Sasa bamdogo kwanza kabisa pindi tutakapoanza kazi tunatakiwa tuachane na ule mfumo wa kwnza wa kununua vitu reja reja sasa kama ni mchele tununue gunia zima kama ni unga tununue kwa viroba halikadhalika kwenye sukari na maharage tufanye vivyo hivyo.Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunapata faida kamili sio nusu nusu ya kugawana na watu pia kuna faida kuu tatu za kufanya hivyo Kwanza kabisa gharama itapungua kwa kuwa tutakuwa tumenunua kwa bei ya jumla.Pili hatutapoteza muda kila siku kuzunguka maduka kwajili ya kununua vitu hivyo na badala yake muda huo tutautumia vizuri katika kuongeza ufanisi wa kazi na kuboresha huduma na mwisho kabisa hatutokusumbua mara kwa mara eti vitu vimeisha!" 

Niliendelea kutoa mchanganuo wangu kama mjasiriamali mkongwe aliyebobea katika fani hiyo na muda wote nilimuacha bamdogo mdomo wazi kwa mshangao hakuweza kujua nimetoa wapi akili hiyo ya kibiashara wakati sijawahi kuuza hata pipi.

"Swala lingine ni upande wa wahudumu.Jikoni mtamuweka yule yule mpishi wenu aliyekuwa akipika awali lakini kwa upande wa muhudumu hiyo kazi niachie mimi!" Hapa nilipasisitiza sana kwani tayari nilikuwa namjua mtu wa kumuweka.

Yule binti niliyekutana naye jana wakati natoka kwa kina Lisa na kulalamika sana kuwa maisha yamemuwia magumu kutokana na kukosa ajira.

Naam huyo alikuwa ni Sauda mrembo wa haja niliyesoma naye shule ya msingi na akashindwa kuendelea na masomo ya sekondari baada ya kufeli mtihani wa kidato cha pili mara mbili.

Huyu alikuwa na mvuto wa kipekee na asingeshindwa kukaimu nafasi hiyo.

Na kama ningefanikiwa kumuweka mrembo huyo mwenye mvuto wa kipekee basi kungekuwa na mvuto na kwa wateja pia.

"Jambo la tatu bamdogo nataka tuongeze hadhi ya mgahawa kwa kupandisha vitu bei.Chai ya maziwa haitauzwa tena shilingi mia tatu kwa kikombe ila sasa itauzwa mia tano isipokuwa tu tutaiongezea ubora yaani haitakuwa tena nusu lita ya maziwa kwa lita mbili za maji ila sasa itakuwa nusu lita ya maziwa kwa nusu lita ya maji.

Chai ya rangi haitauzwa tena shilingi mia mbili kwa kikombe ila sasa itauzwa mia tatu isipokuwa tu haitakuwa chai ya maji moto na majani ila sasa itaungwa kwa hiliki,mdalasini,tangawizi na mchai chai.

Chapati hazitauzwa tena shilingi mia tatu ila sasa zitauzwa mia tano isipokuwa hazitasukumwa mara moja tu na kukaangwa ila sasa zitasukumwa mara mbili kwa mafuta na kuongezewa ujazo halikadhalika inabidi tuongeze vitafunwa (bites) zingine kama vile vitumbua,bagia na sambusa pia supu nayo ni muhimu kuwepo ili wateja wasiopenda chai nao wasiondoke bila kula kwenye mgahawa wetu.

Kwenye upande wa vyakula napo sahani ya wali haitauzwa tena shilingi elfu moja na mia tano ila sasa itauzwa elfu mbili na mia tano isipokuwa tu sasa hautakuwa wali wa mchele uliochemshwa kwenye maji ila mchele utakaangwa 

Kabla ya kuchemshwa na utachanganywa na njegere ili kuongeza ladha.sahani ya ugali nayo haitauzwa shilingi elfu moja na mia mbili ila sasa itauzwa elfu mbili ila tu sasa haitakuwa na nyama za kuchemshwa,itakuwa ni nyama za kukaanga pia pembeni ya maharage na mchicha tutaongeza kachumbari pamoja na dagaa.

" Niliendelea kumtajia bamdogo bidhaa zote na jinsi ambavyo tungeziongezea thamani na kuzipandisha bei.Ingawa katika ajenda zangu zote alikubaliana na mimi kwa asilimia mia lakini kwa hili la kupandisha bei alilitilia shaka kidogo.

"Sasa mwanangu watu wengi wa hapa ni wa bahili sasa tukipandisha bei situtapoteza wateja kweli!" Bamdogo alidhihirisha mashaka yake katika swali hilo.

"Sasa bamdogo kwanza kabisa unatakiwa ujue kuwa watu wengi wa hapa sio wateja wetu kwasababu wanakula makwao.pili hapaa tupo stand centre ya kibiashara kwahiyo kukosa wateja ni ndoto sababu watu wanashuka na kupanda kutwa mzima na mwisho siri ya mafanikio ipo katika kujaribu.

Na kwa kuwa bidhaa zitaongezwa ubora mara dufu kabla ya kupandishwa bei mi sioni kama kuna tatizo hapo hasa ukizingatia watu wa kileo wanaangalia ubora na sio bei" Baada ya majibu hayo ya kumtoa wasi wasi bamdogo na kumpa moyo hakuwa na swali la ziada hivyo tukafunga mjadala na kufungua utekelezaji.

Wiki chache baada ya kuanza kazi rasmi.matunda yalianza kuonekana bamdogo alifurahi sana na kuniamini mara elfu.Faida iliyokuwa ikipatikana ilikuwa ni mara saba ya ile ya awali.

Mtoto mnyang'anye kisu mpe panga.Bamdogo alifanikiwa kuninyang'anya kisu hicho.Alininyang'anya kisu kilichoitwa mapenzi na kunipa panga ambalo ni kazi.Kazi aliyonipa iliniweka mbali na mapenzi.Na mimi kuniweka mbali na mapenzi ni kunuweka mbali na Lisa kwani ndiye msichana pekee aliyeishi moyoni mwangu kwa kipindi chote.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni