UZOEFU (5) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 2 Aprili 2021

UZOEFU (5)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Mtoto mnyang'anye kisu mpe panga.Bamdogo alifanikiwa kuninyang'anya kisu hicho.Alininyang'anya kisu kilichoitwa mapenzi na kunipa panga ambalo ni kazi.Kazi aliyonipa iliniweka mbali na mapenzi.Na mimi kuniweka mbali na mapenzi ni kunuweka mbali na Lisa kwani ndiye msichana pekee aliyeishi moyoni mwangu kwa kipindi chote.

SASA ENDELEA...
Siku moja usiku nikiwa nimepumzika kwenye kitanda changu nilimuwaza Lisa.Tangu niwe bize na kazi hata muda wa kumuwaza mpenzi wangu umekuwa adimu.mara nyingi nikipanda kitandani usingizi hunipita haraka kwajili ya uchovu wa pirika za mchana.Ni siku hii ndipo nilipojaribu kuvuta kumbu kumbu ili niikumbuke ile tarehe ambayo mama yake alinitajia kuwa angerudi.Kichwni zilikuwa zikipita tarehe za vitu tofauti tofauti.

Nilikumbuka tarehe ya kulipa wafanyakazi mishahara,nikakumbuka tarehe ya kulipa kodi TRA,nikakumbuka tarehe ya kununua chakula kingine.Nikajikuta nakipiga kichwa changu ngumi ya hasira kwa kugoma kuniltea tarehe hiyo.Nikalala kwa hasira huku nikijua ya kuwa mara nyingi huwa nikimuwaza sana mtu kuna jambo linatokea.

Siku iliyofuata kwenye majira ya saa nne za asubuhi nikiwa nimechafuka kiasi kutokana na kushusha kreti za soda zilizoshushwa na gari kwa mbali niliweza kuwaona walimbwende wawili wakija na njia niliyopo.

Kadrii walivyozidi kusogea ndivyo nilivyozidi kuwatambua,naam huyu mmoja nilikuwa nikimfahamu vizuri alikuwa ni mteja wa kila siku wa vitafunwa katika mgahawa wetu hata jina nilishawahi kumuuliza akaniambia anaitwa Trace.Ingawa niliweza kumtambua Trace lakini hata huyu mrembo mwingine aliyeongozana naye hakuwa mgeni machoni mwangu.Nilishawahi kumuona mahali ila sikumbuki ni lini na wapi.

Nikabaki nimeduwaa kwa muda nikijaribu kulifikiria hilo nishasahau kabisa kuwa jana nilimfikiria sana Lisa na mara nyingi nikimuwaza sana mtu huwa kuna jambo linatokea.

Trace na yule mlimbwende waliyeongozana naye wakazidi kukaribia nilipo na hatimaye wakafika na kusimama mbele yangu.Pamoja na kusimama mbele yangu bado nilitawaliwa na butwaa lile lile,sikuwa na tofauti na mtu aliyepigwa shoti ya umeme na nilikuwa nikipambana kuzirejesha fahamu zangu zilizoenda mbali.

Zinduka wee bwege huyo unayemuona ni Lisa.Nilisikia akili yangu ikininon'goneza kwa mbali ghafla nikashtuka na kusikia ubaridi mkali katika mifupa yangu viungo vikalegea na mwili ukakosa nguvu.

Hali ya mahaba niuwe ikanikabili,nikapepesuka lakini sikuanguka,naam nilipata muhimili,nilimkumbatia Lisa kwa nguvu sana huku nikiwa na furaha kubwa moyoni.Mwili wangu ukasharabu joto lake,Nikapata nguvu na kuwa kiumbe mpya,Nikamuachia na kumuangalia sura yake tena,naam alikuwa ni mwenyewe haswa,nikamkumbatia kwa mara nyingine tena.

Yote hayo niliyafanya kama chizi.Akili haikufanya kazi yake ila iliusikiliza moyo.Nilitamani kumwambia Lisa jambo lakini mdomo ukawa mzito,ulijaa mate nikajikuta tu nimemuuliza swali moja hadi anaondoka.Nilimuuliza umekuja lini naye akajibu jana usiku.Ingawa moyoni yalikuwepo mengi ya kusema mdomo ulinyamaza kimya kama vile ulikuwa haujui chochote.

Lisa na Trace wslipoondoka niliwasindikiza kwa macho hadi wakazamia.Hata vitafunwa Trace alivyobeba sikujua alivinunua muda gani.

Amaa kweli maji ukiyakamia huyanywi na siku ukitembea uchi ndiyo unakutana na mkweo.Sikuamini kama nimeshindwa kufurukuta kwa Lisa na neno lolote la kimapenzi hadi ameondoka yaani hata i miss you (nimekukumbuka) pamoja na hilo siku zote nimekuwa nikijitahidi kuwa smart (nadhifu) muda wote yaani leo nipo rough (mchafu) ndo Lisa anakuja.

Nililalamika na moyo wangu huku nikijiangalia tena muonekano wangu usio wa kupendeza Lisa atakuwa ameuchukulia vipi.

Siku hiyo baada ya kuonana tu na Lisa nilikuwa nusu mzima nusu chizi.Yani nilikuwa hata sielewi elewi dunia inakwendaje.Yule Lisa niliyemjua utotoni hakuwa Lisa huyu mpya niliyemuona siku hiyo,kila kitu kwake kilikuwa kimebadilika.kile kifua chake kilichokuwa flat enzi hizo sasa kilikuwa kimepambwa kwa chuchu nzuri mbili zilizosimama vilivyo.

Chuchu zilizokichoma kifua changu na kusababisha kunipoteza kabisa kwenye dunia hii ya kawaida pindi nilipomkumbatiaa.

Hips zake nazo hazikuwa flat tena,vilichomoza vibastola vya ajabu kiasi cha kutishia amani ya vidume vilivyomtazama.Hata macho yake sasa aliweza kuyatumia vizuri.yalikuwa ya kicheza kutokana na maneno aliyoongea mdomoni.

Hata zile nywele zake nilizozoea kuona akisuka mabutu au tatu kichwa,alikuwa kazichana vizuri na zilikuwa na mng'aro mweusi wa kupendeza.Ngozi yake nyeupe nayo iling'ara maradufu kuashiria kuwa sasa amejua kuoga na kutumia mafuta yanayofaa na walipokuwa wakiondoka niliweza kuona wezere lake lililotikisika kwa mfumo wa kusema bye bye.

Sikuweza kuyaangalia mabadiliko hayo tu na kufurahi peke yake ila nilibaki na swali lililoniumiza kichwa.na swali hilo ndilo lililonifanya niione dunia imeongeza kasi ya kuzunguka.Kama Lisa ameweza kuwa na mabadiliko ya kimwili kwa kiasi kikubwa hivyo Je vipi kuhusu akili!? Je akili yake bado itakuwa kama ile ya utotoni kuwa anampenda sana Tom ama itakuwa imebadilika kulingana na muda na muonekano wake mpya.Swali hili ndilo lililonigonga sana kichwa na kuumiza akili yangu.

Ukweli ni kwamba nilimpenda Lisa kwa dhati toka moyoni na sikutaka kumkosa hata kwa kufikiri tu.Pamoja na kujihusisha kimapenzi na wasichana wawili tofauti kipindi nikiwa shule lakini kati yao hapakuwa na hata mmoja ambaye aliufikia hata robo ya upendo wangu kwa Lisa.Mapenzi ya dhati yasikie kwa mwingine tu ila usiombe kupenda.

Lile swala ambalo nililichukulia poa (rahisi) kwamba ntafika Tabora nitamkuta Lisa,Nampenda naye ananipenda pia afu maisha yataendelea sasa swala hilo lilianza kuingia uzito na halikuwa rahisi tena kama nilivyozani.

Hivi itakuwaje kama nitamwambia Lisa nampenda alafu anijibu ah Tom acha bwana yale yalikuwa mambo ya utoto si ningekufa mimi kwa kushindwa kuvumilia jibu hilo.Jambo hilo sikutaka linitokee hata ndotoni hivyo nilitakiwa nitumie akili ya hali ya juu sana kumrudisha Lisa mikononi mwangu.

Ingawa nilikuwa mtu wa story sana (porojo) mara baada ya chakula cha jioni.Lakini siku hiyo sikutaka story na mtu nilielekea chumbani mapema kukwepa kushtukiwa maana siku hiyo nilikuwa na mawazo tele na si mamdogo pekee hata bamdogo sikutaka ajue hali hiyo.

Nilipanda kitandani na sikuwa na hata lepe la usingizi.Nilipanga na kupangua,kuwaza na kuwazua na yote hayo yalikuwa juu ya mrembo mmoja tu ,naye ni Lisa.Hivi kwanini timu hucheza match (mchezo) wa kirafiki kabla ya kucheza na timu husika na jibu nililolipata katikaswali hilo ni ili wajipime nguvu.Kwa hiyo na mimi natakiwa nijipime uwezo wangu wa kutongoza kabla sijasimama mbele ya Lisa eenh? 

Nilijiuliza swali hilo na nikaridhia kufanya hivyo.Ila nitamtongoza nani sasa!? Hilo lilikuwa ni swali lingine lililonigonga kichwa lakini nilitabasamu kwa furaha mara nilipokumbuka kikaratasi chenye namba za simu niliyepewa na abiria mrembo niliyeketi naye seat moja nikaamka toka kitandani haraka na kuanza kukitafuta kikaratasi cha binti yule ambacho nilikiweka kwenye mfuko wa begi.

Mungu si Athumani! Nikakipata.Nikianza kuvipanga vya kuongea kabla ya kumpigia.Nikapanga kuifanya kazi hiyo kwa umakini na viwango ambavyo ningevitumia kwa Lisa.Huku nikiamini kwamba iwapo nitafanikiwa kukubaliwa na mrembo huyo basi hata Lisa hata kataa.Kwa hiyo nilichokuwa natafuta hapo ni 

Uzoefu,uzoefu ambao ningeutumia kumpata Lisa.Maswali atayonihoji Bite hata Lisa atanihoji hayo hayo kwani ulimwengu wa mapenzi si mmoja tu.Nijipa imani nilipokuwa naingiza namba za Bite kwenye simu yangu.

Hatimaye kwa mara ya kwanza baada ya wiki kadhaa kupita nilinyanyua simu yangu kumpigia Bite,kadri simu ilivyoendelea kuita ndivyo mapigo yangu ya moyo yalivyoongeza kasi.

Simu iliita mda mrefu kidogona hatimaye ilipokelewa.
"Halloo" Hatimaye nikasikia sauti ya Bite iliyogubikwa na uzito wa usingizi.
"Yes Bite manbo vipi!?"
"Poa nani anaongea!?
"Unaongea na Tom hapa!"
"Wow Tom!...mambo vipi?" Baada ya kujua ni mimi alilegeza sauti kidogo na kuchangamka.
"Poa tu ila nimekumiss sana!"
"Aaaah jamani!...ila Tom tabia yako mbaya!...mbona hukunitafuta siku zote hizo?" Bite alitoa malalamiko yake lakini kwa sauti laini sana hali iliyonifanya nijione mkosaji.
"Yaani ungejua yaliyonikuta ungenipa pole kwanza!"
"Ulipatwa na nini tena?"
"Yaani baada ya kunipa tu namba yako hata ilipopotelea sikujua,nimekuwa nikiitafuta kila siku hadi leo ndo nimeipata...yaani huwezi amini nilivyofurahi!" Nilimuhadaa Bite naye akakubali.
"Jaamanii!...poleee enh! Sasa leo umeipata wapi!?" Hatimaye nikasikia swali nilillolitegemea lakini sikutaka kulijibu nami nikalipotezea kisiasa lakini Bite hakuweza kujua,tukaendelea na mazungumzo mengine na hatimaye nikamuingiza kwenye ile mada niliyoitaka.

Siku iliyofuata asubuhi kwenye mishale ya saa tatu hivi nikiwa ndani ya mgahawa Lisa alikuja.

Ingawa mwanzo nilikuwa na hamu sana ya kumuona lakini sasa nilikuwa namuogopa kama mtu anayenidai fedha nisizonazo.Baada ya kumuona Lisa nilishtuka sana kiasi cha hata kusahau nili chokuwa nafanya.Ama kwa hakika kama ningejua Lisa angefika mahali hapo muda huo ningeondoka na nisingemuona.

"Karibu Lisa!..keti hapa!" Nilijitutumua kiume kumkaribisha Lisa huku nikimuwekea kiti vizuri.Ajaabu alikaa.
"Enhee mambo vipi!?" Nilimuuliza baada ya mimi kukaa kiti kilichokuwa upande wa pili wa meza.
"Poa tu za kuamka?" Alinijibu huku akiwa anachezea simu yake pengine kwa kuona haya kuniangalia.
"Karibu chai sijui utakula na nini!?" Niliongea baada ya kufikiria neno lingine la kuongea na kukosa.
"Ahsante mi nimeshakunywa nyumbani!?"
"Sio vizuri ivyo kunywa kidogo na mimi!"
"Hivi mtapata faida gani iwapo kila mtu akija atakula bure!" Lisa aliuliza swali lilinikera kiasi flani.
"Aaah Lisa wewe si kila mtu maishani mwangu bali wewe ni mtu pekee sana na laiti ungelijua umuhimu wako kwangu wala usingesema hayo!" Hatimaye Lisa akanifanya nizungumze mambo ambayo sikutegemea kuyasema asubuhi hiyo.
"Kwani nina umuhimu gani kwako!" Lisa aliniuliza swali ambalo lilinipa tumbo joto.Je nimueleze nnavyompenda!?.upande mmoja ukasema ndio na mwingine hapana nikabaki njia panda.
"Nikikwambia kwa mdomo nahisi ntakudanganya hebu lete mkono wako usikie mwenyewe!" Niliongea huku nikiutwaa mkono wake wa kuume na kuuweka moyoni mwangu.
"Enhee umesikia nini!?" Nilimuuliza mara baada ya kumuacha ausikie moyo kwa kitambo.
"Nimesikia tu moyo wako ukidunda!"
"moyo wangu si kitenesi Lisa kusema unadunda.Kuna jambo umekwambia labda hujaelewa tu!" Nilalama kwa sauti ndogo iliyotulia huku nikimuangalia Lisa kwa jicho la upole.
"Sasa unasemaje!?" Aliniuliza kimitego nami nikaamua kuwa muwazi.
"Nakupenda wewe tu,nakupenda wewe tu!" Nilimjibu kwa kufwata mdundo wa mapigo ya moyo.Akabaki na tabasam dogo bila kusema kitu.
"Lisa!?" Nilimuita baada ya kuona yupo kimya tu ingawa hakuitika kwa mdomo,macho yake yaliniuliza unasemaje.
"Nikuombe kitu?" Niliendelea baada ya macho yake kuniruhusu!
"Yeah sema!'
"Naomba niusikilize moyo wako!" Nilimuomba naye alifikiri kwa kitambo kabla ya kuniruhusu labda alihofia ningeshika ziwa lake hadharani.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni