UZOEFU (6) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 2 Aprili 2021

UZOEFU (6)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
"Naomba niusikilize moyo wako!" Nilimuomba naye alifikiri kwa kitambo kabla ya kuniruhusu labda alihofia ningeshika ziwa lake hadharani.
SASA ENDELEA...
"Enhee umesikia unasemaje!?" Naye aliniuliza vile vile kama mimi nilivyomuuliza yeye.
"Wako umeongea kifaransa naomba unitafsirie please (tafadhali)" Nilimjibu Lisa kisiasa naye akacheka kidogo nazani alitambua nilichotaka.nilitaka anithibitishie kwa mdomo wake mwenyewe kuwa ananipenda au la!.
"Poa ntakwambia lakini sio sahivi!...ntakwambia badae!"
"Je baadae tusipoonana!?" Nilihoji kwa huzuni huku hofu ikiwa imeshaanza kutanda moyoni mwangu,nikafikiri kuwa anaona haya kunitamkia kuwa hanipendi.
"Naomba simu yako!?" Lisa aliniomba simu kwa namna ya kutaka kuziweka namba zake na mimi nikampitia.
"Jina nisave (nihiifadhi) nani?.....nasave nyau sawa eenh!"
"Aaasnh Lisa utasave vipi Nyau bhana?" Niling'aka kidogo kwa namna ya kughafilika na Nilifurahi kidogo nikaona binti mrembo kama Lisa kajishusha hadhi kiasi cha kujiita Nyau mbele yangu.Nikapata tumaini fulani.
"Sasa kumbe nisave nani?" Lisa aliendelea kuhoji baada ya mimi kupingana vikali na jina la nyau!.

"Save jina lolote zuri lakini lisiwe la kwako (Lisa)"
Baada ya kusema hivyo Lisa alisave na kunirudishia simu kisha tukaagana na yeye kuondoka.
Baadaye nilipokuja kuona jina alilolisave ndipo nilipo taharuki na kushikwa na butwaa.
Nikajizuia mdomo kwa mkono wangu wa kushoto kuzuia kelele za furaha zisitoke na muda huo kijasho chembamba kilinitoka shauri ya mwili kuchemka kwa furaha.

Lisa alikuwa amesave namba yake (ma luv) mpenzi wangu kwenye simu yangu.

Furaha niliyokuwa nayo muda huo isingeweza kufikiwa hata na mtu aliyepewa dunia nzima aitawale.Ma luv!? Ingawa neno hilo lililomaanisha mpenzi halikuwa geni machoni mwangu lakini ndani ya dakika moja nilirudia kulisoma zaidi ya mara kumi.Kama muda huo angetafutwa mtu mwenye raha kuliko wote duniani basi ni mimi pekee ningepatikana.

Inamana Lisa bado ananipenda eenh!? Niliuulizamoyo wangu kutafuta ushahidi nao ukanijibu ndio.
Japo Lisa bado hakuwa amethibitisha kuwa ananipenda kwa mdomo wake mwenyewe lakini hakuna siku niliyomshukuru Mungu kama siku hiyo.

Lisa alikuwa anamaanisha maisha kwangu hivyo kuwa naye kulimaanisha kuwa na maisha mazuri katika kipindi chote ntakachoishi kwenye hii dunia.

Licha ya kumpenda kwa dhati toka uvungu wa moyo wangu Lisa alikuwa anavigezo vyote vya kuitwa msichana mrembo ambapo hata angekabiziwa taji la miss world (mrembo wa dunia) hakuna ambaye angejiuliza mara mbili kwa nini kapewa.Kwanini nisimshukuru sana Mungu kwa bahati hii ya mtende.Bahati ya kupewa kiumbe nilichotamani kuwa nacho siku zote za maisha yangu.Naam ndivyo nilivyofanya.

'Lisa baby i really love you!..i will never hurt you...please belive me!'(Lisa mpenzi kweli nakupenda...sitakuumiza tafadhali niamini!".Ama kweli mapenzi hayafananishwi na kitu chochote kile yaani tangu nilipoingiza neno ma luv moyoni mwangu lililohifadhiwa na Lisa kwenye simu yangu hata utendaji wa ubongo wangu ulibadilika.Nilikuwa nikifikiria maneno mazuri ya kumwambia Lisa tena kwa lugha ya kiingereza.

Siku hiyo ingawa sikuweza hata kula kwa furaha niliyokuwa nayo lakini niliweza kujizuia nisimpigie Lisa simu na ilipofika majira ya saa kumi na moja alasiri,Lisa alikuja tena mgahawani kwetu.Kitendo cha kumuona tu mapigo ya moyo yakaongeza kasi,hata moyo wangu ulitambua macho yalipomuona.Pamoja na mapigo ya moyo kwenda kasi lakini sasa nilikuwa na ujasiri.
"Mambo vipi Lisa!?" Nilimsalimu huku nikimuangalia kwa jicho la huba.
"Poa tu!....naingia hapo ndani kwenye maduka ya stend ila naogopa kwenda peke yangu!"
Lisa aliongea kwa sauti ya kuvutia huku akichezea pindo la nguo yake kuashiria alikuwa akiona haya.
"Kwani unaenda kununua nini!?"
"Kuna kitu mama kanituma!"
"Mmmh! Kwenda hapo stand tu ndo umependeza namna hiyo!?" Nilimpa Lisa sifa iliyoambatana na utani kidogo naye hakujibu kitu zaidi ya kucheka tu.

"Stand ntakusindikiza ila tunaweza kuongea dakika mbili kabla hatujaenda au utamchelewesha mother (mama)!" Ingawa sikuwa nimepanga kitu chochote cha kuzungumza na Lisa lakini niliomba nafasi hiyo.

"Tunaweza kuongea tu hata hivyo maa ( mama) akijua nilikuwa na wewe hawezi kumind (hatajali)!" Lisa aliongea kauli hiyo kirahisi bila kujua sentensi yake hiyo ilinifanya nijione shujaa zaidi ya mwanajeshi aliyeshinda vita vya Kagera.

Yani mama mkwe hatojali akijua mwanae alikuwa na mimi!? nilijiuliza tena huku nikitoa viti viwili na kuvizungusha nyuma ya mgahawa sikutaka bughuza ya mtu yeyote yule nikifanya mazungumzo na mpenzi wangu.

"Lisa unajua nataka kukueleza jinsi maisha yangu yalivyokuwa tangu nilipoondoka mji huu na kutengana na wewe!" Nilitoa muhtsari wa mada husika ambayo ningekwenda kuizungumzia na baada ya kumuona Lisa ananisikiliza kwa hamu na shauku kubwa niliianza habari yangu.

Nilimsimulia kwa hisia na msisitizo wa hali ya juu huku nikidiriki kuongeza hata chumvi kwenye baadhi ya maelezo,hiyo yote ni katika kuziteka fikra zake na kumvutia kwangu zaidi kama ilivyo kwa muwamba ngoma huvutia kwake.

Vyote nilimsimulia Lisa ila sikuthubutu hata kidogo kumwambia habari ya wale wasichana wawili niliowahi kujihusisha nao kimapenzi,Nashukuru hata yeye hakuniuliza swali hilo na hiyo ikawa pona yangu.Lisa hakuishia tu kunisikiliza na kukaa kimya bali na yeye mwisho wa mazungumzo yangu alianza kunisimulia hali ya upweke iliyomkabili baada ya mimi kuondoka.

Alinisimulia kwa hisia na masikitiko makubwa na mimi nikaitumia fursa hiyo vyema kumsogelea karibu zaidi na kuanza kumpapasa mgongo wake taratibu kwa namna ya kumliwaza.Hakunizuia kufanya hivyo,Hivyo kadiri habari ilivyozidi kusimulia hali ya upweke ndivyo mkono wangu ulivyozidi kuzunguka maeneo mbalimbali ya mwili wake kumfariji.

"Lisa you know what? (Unajua nini)" Nilimkatiza Lisa kwa swali hilo alipokuwa anaendelea kuongea.
"What? (Nini)" Aliniuliza huku huku akinitazama kwa jicho la mahaba.
"Sijawahi kupenda kama nilivyokupenda wewe!"
"Sure? (Kweli?)" Aliniuliza huku akinitazama kwa jicho lile lile.
"A hundred percent! (Asilimia mia)" Nilimjibu huku nikimaanisha nilichokisema.
"Tom i love you than you did to me" (Tom nakupenda kuliko wewe unavyonipenda mimi)

Lisa alitamka maneno yaliyopenya masikioni mwangu hadi kufika moyoni na kuzalisha hisia zisizoelezeka,taratibu nikashika kidevu chake na kuanza kusogeza mdomo wangu kwenye papi (lips) za midomo yake tayari kabisa kwa kupata busu la kiutu uzima.Tukiwa katika hali hiyo ya mahaba mazito huku wote tukiwa tumefumba macho kwaajili ya kitendo hicho kitakatifu ndipo tuliposhtuliwa ghafla na kukurupuka kabla hata ya kutimiza azma yetu.


Kilichotushtua ilikuwa ni mtetemo mkali wa simu ya Lisa ambayo ilikazana kuita kwa juhudi na alipoitazama kwenye kioo alikuwa ni mama yake ndiye anayepiga.
"Sasa ntamwambia nini!?" Lisa aliniomba ushauri na kabla sijamwambia neno lolote akawa ameipokea simu hiyo.
"Mama nipo njiani nakuja!" Lisa aliongea haraka haraka baada ya kupokea simu hiyo kisha kabla upande wa pili hujajibu kitu akawa ameikata.
"Sasa baby twende haraka haraka basi!" Lisa alinisisitiza mara baada ya kukata simu hiyo na kitendo cha kuitwa baby na mrembo huyo kikayeyusha donge langu lote la hasira lililokuwa limeanza kujikusanya kooni kutokana na kukosa ladha ya ulimi wa Lisa.

Ama kweli mapenzi upofu yaani niliomba dakika mbili tu za kuongea na Mrembo wangu lakini tumekaa hadi giza limetukuta.Nilijiwazia mwenyewe nikipokuwa namsindikiza Lisa madukani.

Kitendo cha kwenda kukaa nyuma ya mgahawa ilikuwa ni kama vile tumeingia kwenye ulimwengu wa kwetu peke yetu,kwani si kujua tu saa ngapi hata giza lilivyoingia hatukuliona.

"Take care my love (Chukua tahadhari mpenzi wangu) kama mama atahoji kuchelewa kwako,mwambie ulienda maduka ya mbali sawa eenh!?"

Nilimwambia Lisa tulipokuwa tunaagana baada ya kutoka kununua alichotumwa na yeye akajibu kuwa ameelewa kwa kutikisa kichwa.Nikampa busu la shavu kisha mie nikaanza safari ya kurudi nyumbani.

Njia nzima nilikuwa nikitembea kwa madaha kwa mwendo wa kurukaruka kama mwana ndama.Nilikuwa nafikiria jinsi siku hiyo ilivyoniwia nzuri.Usiombe kupendwa na unayempenda sana, unaweza ukajifia kwa raha.

Nilipofika mgahawani sikuwa na hamu tena ya kuendeleaa kukaa hapo.Siku hiyo niliruhusu wafanyakazi mapema nami nikaingia ndani kupumzika.

Baada ya chakula cha jioni nikiwa chumbani kwangu kabla ya usingizi kunipitia.Nilipata wasaa wa kutafakari mawili matatu,nilifikitia nilpotoka na Lisa na maisha ya siku za usoni yatakavyokuwa.Nikabakiwa na tabasamu kubwa baada ya kuona mustakabali wa maisha yangu ya kimapenzi jinsi utakavyokuwa mzuri.

Nikiwa katika hali hiyo ya tafakari,simu yangu iliita na kunigutusha katika dimbwi la mawazo na nilipoangalia kioo ni Bite ndiye aliyekuwa akipiga,Nikatahayari hasa baada ya kukumbuka kuwa nilikuwa na deni na mrembo huyo.

"Yes Bite mambo vipi!?" Nilimsalimu mrembo huyo kwa uchangamfu mkubwa lakini sikuweza kumchangamsha.
"Ah jamani mbona umenichunia hivyo!?" Bite badala ya kujibu salaam moja kwa moja alienda kwenye malalamiko yake.Kama ningemjibu nilikuwa bize asingefurahia jibu hilo na kama ningetoa sababu nyingine ningeonekana muongo,nikajikuta namumunya maneno na kukosa la kusema juu ya tuhuma hizo.
"Haya bwana we endelea tu kunifanyia hivyo!"
"Hamna sio hivyo Bite ila najua nikikwambia huwezi kunielewa !" Niliendelea kujigonga gonga mbele ya Bite huku nikikosa point za msingi za kupambana na mashtaka yake.
"Enhee!! Jana uliniambia kuna kitu utaniambia leo
So nimekupigia nikijue kabla sijalala!"

Hatimaye Bite alinifikisha mahala ambapo nilikuwa sitaki kabisa kufika.Ukweli ni kwamba usiku uliopita nilitaka kumtongoza ili nipate uzoefu wa kusimama mbele ya Lisa bila kutetereka lakini kwa bahati mbaya mazingira

Hayakuniruhusu kufanya hivyo kwa usiku wa jana hivyo nikamuacha na kiporo kuwa kuna kitu ntamwambia leo ili nipate mahali pa kuanzia lakini kwa bahati nzuri nyota ikawa imening'aria kwa siku hiyo na kumpata Lisa kirahisi tofauti kabisa na vile nilivyokuwa nikihangaika.Sikuwa na tofauti na mtu aliyebeba mapanga kwa mashoka kwenda kukata mti na matokeo yake akakuta umeangushwa na upepo.

"Enhee!! nimekumbuka Bite nilitaka kukuomba nije kukutembelea weekend (mwisho wa wiki) hii!"
"Kumbe hilo tu!...mi nikafikiria hata sijui unataka kuniambia nini!"
"Ni hilo tu!"
"Poa basi usiku mwema siku ukitaka kuja utaniambia!" 

Bite aliaga haraka haraka kuashiria kuwa hakutaka mazungumzo zaidi na mie,Mimi kwa upande wangu nikafurahi,kwakuwa nilikuwa nimeshampata Lisa nnayemtafuta,hakuna mwingine ambaye angeniumiza kichwa.

Baada ya Bite kukata simu yake nilimuandikia mpenzi wangu Lisa ujumbe mfupi mzuri wa kumtakia usiku mwema huku nikimsisitiza kuwa nampenda sana naye akanijibu kwa ujumbe mzuri ulionifanya nikalala usingizi mzuri ulioambatana na ndoto za kupendeza,Tangu hapo penzi letu jipya mimi na Lisa likachipuka na kupendeza mithili ya bustani nzuri ya maua inayopata maji na mbolea yakutosha.

Sasa Lisa alikuwa ni Tom na Tom alikuwa ni Lisa hadi siku moja jioni lilipotokea janga moja lililotishia kusambaratisha mahusiano yetu kabisa.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni