UZOEFU (7) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 3 Aprili 2021

UZOEFU (7)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Sasa Lisa alikuwa ni Tom na Tom alikuwa ni Lisa hadi siku moja jioni lilipotokea janga moja lililotishia kusambaratisha mahusiano yetu kabisa.
SASA ENDELEA...
Robby alikuwa rafiki yangu mkubwa kipindi cha utotoni,tulicheza,tuliwinda ndege na hata kuoga mtoni pamoja.Urafiki wetu ulianza kuingia mashaka pale nilipogundua kuwa Robby alikuwa akimpenda sana Lisa na mara kadhaa alishawahi kunitamkia wazi wazi kuwa ameshawahi kutembea(kushiriki ngono) na Lisa.

Japo mimi nilipofanya uchunguzi yakinifu kwa Lisa niligundua kuwa Lisa hana na wala hakuwahi kuwa na hisia zozote za kimapenzi juu ya Robby.Kama ungemuuliza Lisa aseme jambo juu ya Robby basi angekwambia ni mtu apendaye sifa kwa kujitangazia vitu ambavyo hana wala hakuwahi kuwanavyo ama kwa lugha rahisi ni mtu muongo muongo.

Kadiri urafiki wangu ulivyoendelea kushamiri na Lisa ndivyo urafiki wangu na Robby ulivyoendelea kuwa wa mashaka kabla ya kuisha Kabisa,hata kupishana bila salaam kwetu ilikuwa ni jambo la kawaida sana.

Na hata tulipojaribu kuurudisha urafiki wetu ulikuwa ni wakinafki tu.Tulikaa pamoja kupiga soga na kucheka vicheko vya mdomoni huku kila mmoja moyoni mwake akiwa na mtazamo tofauti kabisa juu ya mwenzake naam! hayo ndiyo yalikuwa maisha yetu mimi na Robby kabla ya mimi kuondoka mji huu wa Tabora.

Nakumbuka tangu nimerudi mjini hapa niliwahi kukutana na Robby mara moja tu na kusalimiana naye vizuri na kwa mara ya pili nilipokutana naye tena haikuwa na tena kwa amani kama mwanzo ila sasa ilikuwa ni kwa shari.

Tangu tulipo renew(anza upya) penzi letu mimi na Lisa,kushinda pamoja kwetu ilikuwa ni jambo la kawaida sana.Yaani katika masaa kumi na mawili ya mchana tulitumia masaa matano hadi saba siku zingine kuwa pamoja.

Lisa aliona raha kuwa karibu na mimi,na mie sikutaka abanduke kabisa ubavuni mwangu.Mda mwingine aliona uvivu hata kwenda kula kwao na tulikula pamoja mgahawani kama mke na mume.Hata masaa machache ambayo Lisa alikuwa mbali na mie sukuacha kumuwaza na kumpigia simu kila mara.

Siku moja Lisa alikuja mgahawani majira ya saa tisa alasiri na kama ilivyokuwa desturi yetu nilizungusha viti nyuma na huko tulikaa hadi adhana ya saa moja jioni ilipotutenganisha.Nilimsindikiza Lisa kwao na dakika tano tu kupita tangu nilipomsindikiza mpenzi wangu nikiwa hata sijaingia ndani.

Niliona kuna watu wanakuja nilipo,na kadri walivyozidi kusogea ndivyo taa zilizokuwa zimewashwa zilinisaidia kuwatambua watu hao.Naam! mmoja alikuwa ni Robby na aliambatana na wenzake wawili,nadhani walikuwa ni wapambe wake kwenye safari hiyo.

Nikawa nawaangalia kwa makini huku nikiwa sina uhakika sana na ujio wao.Ingawa macho yangu ya kawaida yaliwachukulia kawaida jicho langu la tatu liliona mbali zaidi.naam! liliweza kutabiri shari juu ya watu hawa na ndivyo ilivyokuwa.

"Tom...mbona unanichukulia dame (msichana ) wangu aisee!??" Robby alifika karibu nakuanza kutoa malalamiko yake kwa sauti iliyotetema labda kutokana na hasira za kuchukuliwa dame wake.

"Dame!....dame gani huyo!?" Sikujibu swali lake na mimi nilimuhoji langu likiambatana na dharau kiasi na mshangao wa hali ya juu sana.Sikufikiria hata kidogo kuwa dame anayeongelewa hapo anaweza kuwa Lisa hivyo nikalisubiri jibu lake kwa hamu.

"Si Lisa!" Robby alinijibu huku akionyesha kuwa hajiamini kwa hicho anachozungumza na majibu yake kichwani mwangu yalipiga kama radi,Kuongelea juu ya Lisa ni sawa na alikuwa ameongelea juu ya roho yangu.Nikajikuta taratibu napotea kwenye ulimwengu wa kawaida na kuzama kwenye uwanda wenye fikara nzito.mawazo kede kede yalikuwa yakikishambulia kichwa changu.Inamaana nilivyoondoka 

Robby alitumia muda huo vizuri kumshawishi na kumpata Lisa??,lakini kwanini Lisa amekubali kuwa mpenzi wangu hali yakuwa anajua yupo na Robby?? Hayo yalikuwa ni moja kati ya maswali sabini yaliyokigonga kichwa changu kila ilipotimu sekunde moja.

"Si umeulizwa wewe!...jibu sasa?" Hilo lilikuwa ni
swali la kipuuzi lililoulizwa na mmoja kati ya wapambe nuksi wawili ambao Robby aliambatana nao.

Swali hilo ndilo lilinishtua toka katika dimbwi la mawazo na kunirudisha tena katika ulimwengu wa kawaida.Hasira kali ikaanza kwenda sawa na mapigo yangu ya moyo huku ikisambaa mwili mzima na kuamsha roho ya vita ambayo ilikuwa imelala kwa siku mingi.Taratibu nikaanza kukunja ngumi zangu huku kichwa kikipiga hesabu kuwa nianze na yupi ambaye ntamfanya wa mfano.Ingawa walikuwa watatu sikuhofia kati yao hata mmoja nakumbuka katika kipindi cha utoto 

Robby kila alipojaribu kupimana nguvu (kupigana)na mie mara zote aliangukia pua nakumbuka hata mpambe wake mmoja nishawahi kumtandika ngumi moja tu akazimia.Ingawa sasa muda ulikuwa umeshakwenda sana bado niliamini kwa asilimia mia kuwa Tom wa K.O (knock out) ni yule yule.Na ingawa nina sifa kubwa ya tabia ya upole,mtu akiingia anga zangu huwa natumia mithali moja tu.Heri lawama kuliko fedheha.

Nikiwa katika harakati hizo za kutaka kuwafunza adabu jamaa hao nilishangaa kuona Lisa amekuja ingawa haikuwa kawaida yake kabisa kurudi akishaondoka majira ya usiku.Hali ya kukata tamaa ikaanza kunishambulia nikaamini kuwa ule ni mpango wa kuachana umeandaliwa.

Taratibu nikaiachia ngumi yangu niliyoanza kuikunja vizuri haikuwa na haja tena kumpigania mtu ambaye sijajua yupo upande gani.Nikasimama kwa upole nikisubiri kuona msichana nnayempenda sana atakavyoniaibisha na kunisaliti mbele ya adui zangu.

Je mwisho wa Lisa na Tom ndio umefika??

Taratibu Lisa akasogea kabisa hadi nilipokuwa nimesimama huku utulivu wa hali ya juu ukitawala eneo hilo.Kila mmoja wetu alikuwa akisubiri kuona Lisa atafanya nini.Lisa akasogeza mdomo wake karibu kabisa na shavu langu na wakati huo hakuna kitu akili yangu ilikuwa inaniambia zaidi ya kunikumbusha kuwa Yuda alimsaliti Yesu kwa kumbusu.Nami nikalisubiri busu la usaliti toka kwa Lisa.

"Baby!...maa kantuma stand ndani,naogopa kwenda peke yangu!" Hiyo ni Sauti laini ya Lisa iliyopenya kwa upole sikioni mwangu na kuipoteza kabisa akili ya kusalitiwa,ikairejesha upya nguvu iliyoanza kupotea na kunifanya nijisikie afya mwilini.

"I am here for you love,let's go!" (Nipo hapa kwajili yako mpenzi,twende!) Nilimjibu Lisa kwa sauti iliyosheheni mahaba.Ingawa niliongea taratibu nilihakikisha kuwa Robby anasikia kila neno nililomwambia mpenzi wangu ambaye yeye alikuwa akiishi kwenye ndoto za kumuita dame wake!

Taratibu nikazungusha mkono wangu wa kulia kwenye kiuno chembamba cha Lisa na tukaanza kutembea kuelekea stand ndani huku tukiwaacha Robby na wapambe wake kwenye hali ya pasua kichwa mithili ya Abiria walioachwa na basi linalopita mara moja kwa mwezi.

Ingawa sikuwa na tabia ya kuonyesha mapenzi yangu kwa Lisa tukiwa hadharani ili kukwepa majungu.Lisa alishangaa kuona siku hiyo nikifanya hivyo, nilimpiga busu la shavu mbele ya umati na tukatembea nikiwa nimeng'an'gania kiuno chake.

Ni lazima alikuwa anajiuliza kwanini siku hiyo nimeamua kufanya hivyo ila kitendo hicho mimi nilikiita fimbo kwa wapumbavu wote

Wanaommezea mate mpenzi wangu na kumpigia mahesabu.Nilifanya hivyo makusudi kuhakikisha kuwa Robby anapata maumivu makali sana ambayo angeweza kuyatuliza kwa kusaga chupa na kunywa ama kubembea na shingo kwenye kitanzi cha manila.

Mapenzi siku hiyo yalinifanya nijione niko juu hata zaidi ya Chief (mtemi) Mirambo,kiongozi maarufu wa kimila aliyetawala mkoa huo miaka ya nyuma na kujipatia heshima kubwa.Naam!,siku hiyo mimi nilikuwa ni zaidi yake.

"Honey please(tafadhali)!..tunaweza tukaongea dakika mbili kabla hujaenda home!" Nilimchombeza Lisa tulipokuwa tunatoka stand huku nikimminyaminya vidole vya mkono wake ambao nilikuwa nimeushika.

"Baby lakini unajua sahivi ni usiku!?" Lisa ambaye hakuwa na tabia ya kukataa wito wangu alijaribu kujitetea nimuache.

"Honey nna kitu cha muhimu nataka mikwambie,naona kesho itakuwa mbali saana pia sitaridhika kama tukiongea jambo hilo kwa simu!"

"Una jambo gani?...mbona tulikaa muda mrefu sana hukuniambia!?"

"Unajua honey wewe ni mpya kwangu kila sekunde.hata tuishi wote miaka elfu moja sidhani kama naweza kukuzoea!"

"Acha maneno yako matamu bwana!...unajua huwa unanipa tabu ukiwa mbali!" Lisa alijibu kimahaba kuonyesha kuwa amekubali kikao changu cha dakika mbili huku moyoni mwake akijua kuwa tunaweza kutumia zaidi ya masaa mawili.

Tulipofika mgahawani niliingia ndani kisha nikazima taa ya upande ambao tungekaa alafu nikatoka na kiti kimoja!
"Khaa! Saa mbona umekuja na kiti kimoja!?"

Lisa aliuliza kwa mshangao baada ya kuona nimekuja na kiti kimoja alafu nimekaa mimi.Sikumjibu kitu zaidi ya kupiga piga mapaja yangu kumuashiria kuwa ndio sehemu aliyotakiwa kukaa, Nashukuru alinielewa alikuja kwa furaha na mie nikampakatia na kikao kikaanza rasmi.

Ni vigumu kumficha mpenzi wako unayempenda kwa dhati jambo ambalo linakuhusu wewe na yeye ama wewe na mtu mwingine.Ndivyo ilivyokuwa kwangu.Nilimsimulia Lisa yote yaliyojiri dakika chache zilizopita kabla yeye hajafika na alionekana kukerwa sana na habari hiyo niliyokuwa nikimsimulia.

"Hivi huyu fala ana nini na mimi!?" Lisa alibwata kwa hasira nami nikaamini kweli mpenzi wangu alikuwa amekereka haswa siku hiyo.Tangu nimemjua Lisa sikuwahi kumsikia akitusi hata siku moja.

"Calm down babie! (Tulie mpenzi)" Nilimtuliza Lisa ambaye alikuwa moto sana muda huo na neno langu hilo likawa kama tone la petroli lililodondokea kwenye moto ulioanza kupoa.

"We ngoja tu kesho ntamuonyesha kazi!" Lisa alitamba kwa hasira huku akipigapiga ngumi kwenye kiganja chake kusisitiza jambo hilo.

"Unataka kufanyaje honey!?" Nilimuuliza Lisa kwa upole huku nikiminya minya vidole vya mkono wake niliokuwa nimeushika.Maneno yake yalishaanza kunitia hofu hadi mimi na nikaogopa jambo baya lisije likamkumba mpenzi wangu.

"Nitamchambaaa!!......nitamchambaaaa!!...heenh!?"

"No need honey (haina haja asali) wee niache hiyo kazi mimi tu ntadeal (ntashughulika) nao!...watanyooka tu!"

"Baby nakuomba please usije ukapigana mpenzi wangu!" Ile hofu iliyokuwa kwangu ikaonekana kuhamia kwa Lisa. Kwakuwa nilimsimulia kama angechelewa dakika moja tu angewakuta wakina Robby wakigaa gaa chini kwa maumivu ya kisago kikali.

Neno hilo lilimkaa kichwani na huenda alikuwa anahofia kuwa ningefanya hivyo siku za usoni.Na hiyo ndo sababu ya kunibembeleza kwa maneno matamu huku akiipapasa shingo yangu kwa vidole vyake laini na mie sikuwa mbishi kwake.

Baada ya kumaliza shauri hilo la Robby nikaanzisha mada nyingine mpya kabisa!.

"Honey!..why do you love me? (Asali kwa nini unanipenda mimi) Nilimuuliza Lisa huku mkono wangu wa kuume ukiwa ndani ya sweta alilovaa ukijaribu kufanya sensa ya vinyweleo ( vimalaika) vipya vilivyokuwa vikichipua kwenye tumbo lake.

"Baby i have no reason and that is enough reason why i love you!"(sina sababu na hiyo ni sababu tosha kwa nini nakupenda!) Lisa alijibu kwa sauti tamu huku vidole vyake vikahama toka kwenye shingo hadi kwenye kidevu.

"And how much do you love me!?(Na kwa kiasi gani unanipenda) Nilimtwanga Lisa swali lingine kwa lugha ile ile ya kigeni mara nyingi nikiwa kwenye hisia nzito za kimahΓ ba huwa nashindwa kuitumia lugha adhimu ya kiswahili.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni