UZOEFU (8) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 3 Aprili 2021

UZOEFU (8)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
"And how much do you love me!?(Na kwa kiasi gani unanipenda) Nilimtwanga Lisa swali lingine kwa lugha ile ile ya kigeni mara nyingi nikiwa kwenye hisia nzito za kimahàba huwa nashindwa kuitumia lugha adhimu ya kiswahili.
SASA ENDELEA...
"Baby you know how much i love you nashindwa kukufananisha na kitu chochote kile.Tom i love you!" Ingawa Nakupenda ni neno la kawaida sana lakini kila mara nnapoambiwa neno hilo na mpenzi wangu Lisa, masikio yangu husisimka kwa ladha ya neno hilo.

"Ok babie!...naomba nikuulize swali la mwisho!"
"Uliza tu mpenzi!"

"Hivi unafikiri ni nini kinaweza kuvunja penzi letu!?" Ingaawa Lisa maswali yote alikuwa akjibu haraka haraka.Swali hilo alitumia muda mrefu sana kufikiri.

" Baby kiukweli....i dont know....yaani sijui ni nini!" Lisa alijibu kwa sauti iliyokwama kwama kuonyesha kuwa bado alikuwa akilifikiria swali hilo.

IIngawa sikuridhika sana na majibu yake lakini ilibidi kuridhia mi matumaini yangu ni kuwa angejibu hakuna jambo lolote lakini yeye alijibu kuwa hajui ni kitu gani hiyo kwangu ilimaanisha kipo kitu lakini hajakitambua bado.Baada ya Lisa kuona nipo kimya aliitumia fursa hiyo kuniomba kitu.

"Naomba unipromise (uniahidi) kuwa hutanisaliti!" Lisa aliongea baada ya kuona namsikiliza kwa umakini.

"I promise you my love!(nakuahidi mpenzi)" Nilikubali kwa roho nyeupe!!.
"Naomba tena uape kuwa hutakaa unikane maishani mwako!"
"Ok naapa sitakukana maishani mwangu!!

"Sitaki.....sitakiii....sio hivyo!?" Lisa aliongea huku akizungusha zungusha mikono yake mithili ya mtoto aliyezira.

"Sasa baby unataka niape vipi jamani!?"
Nilimlalamikia Lisa kwa sauti ya upole lakini hakunionea huruma.

"Nyosha mkono wako wa kulia juu!" Lisa aliongea huku akinisaidia kuifanya kazi hiyo.Na mimi nikanyosha kama nilivyoamuriwa.

"Haya sema mimi Tom!" Lisa aliendelea na maelekezo yake nami nikawa namfwatisha anavyosema.
"Mimi Tom!"
"Naapa kuwa!"
"Naapa kuwa!"
"Sitakaa nimkane!"
"Sitakaa nimkane!"
"Mpenzi wangu Lisa!"
"Mpenzi wangu Lisa!"
"Kwa hali yoyote ile!'
"Kwa hali yoyote ile!"
"Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie!"
"Eeh mwenyezi Mungu nisaidie!"

"Wow!...hapo ndo umeapa sasa,sasa ole wako uje uthubutu!" Lisa alinichimba mkwara laini baada ya kumaliza kiapo.

"Hata bila kiapo wee wajua siwezi kukusaliti mpenzi wangu!"
"Lazima nikuwekee Pin code sasa ukijaribu tu unakufa siku hiyo hiyo!"
"Ah jamani kumbe unataka kuniua!"

"Ukinikana utaniua alafu na wewe utakufa ha ha ha kwahiyo tutakufa wote!" Lisa aliongea maneno magumu lakini kirahisi sana.
"Lisa nakupenda sana sweetheart!"

"Nakupenda pia Tom wangu!" Lisa alinijibu kwa sauti ya ndani sana kisha akanishika kidevu nakuanza kuzinyonya papi za midomo yangu,Nikamshika kwa nguvu kiuno chake nakuanza kuunyonya ulimi wake,japo kilikuwa ni kitendo cha dakika mbili tu lakini raha yake nazani iliniongezea miaka saba ya kuishi.

Hivyo ndivyo nilivyomaliza kikao chetu cha dharura siku hiyo huku nikifurahi sana kila mmoja wetu alivyo na utayari wa kupigana na kidudu mtu yeyote atakayeingilia penzi hili.

Tulipokuwa njiani nikimsindikiza Lisa kwao kuna wazo likanijia.Huwezi kuimiki nchi bila kusimika bendera ardhini.Sasa mi nawezaje kummiliki Lisa pasipo mtu yeyote kujua,Akinizingua je nani atakuwa shahidi?.Wazo hilo ndilo lililonifanya nitake kuanza kumtambulisha Lisa rasmi kwa baadhi ya ndugu zangu ambao tunapikika chungu kimoja.

"Baby jiandae!..Jumamosi hii tutakuwa na safari kidogo!" Nilimwambia Lisa baada ya kuridhika na mawazo yangu.
"Ya kwenda wapi tena mpenzi!?"
"We jiandae tu siku ikifika utajua!"
"Haya mpenzi nitajiandaa lakini iwapo tu utaniambia tunaenda wapi!"

Lisa alijibu kimasihara lakini alionekana kumaanisha alichokisema hali hiyo ikaanza kunitia hofu kwani mimi sikutaka kumwambia kuwa nampeleka ukweni.Nilihofia kuwa huenda angegoma.

Baada ya kimya cha dakika kadhaa kupita.Lisa alivunja ukimya.

"Tom!?"Aliniita kwa sauti ya deko.
"Yes baby!" Niliitika kumaanisha aniambie anachotaka kusema.
"Naomba unipromise (uniahidi) kuwa hutanisaliti!" Lisa aliongea baada ya kuona namsikiliza kwa umakini.

"I promise you my love!(nakuahidi mpenzi)" Nilikubali kwa roho nyeupe!!.
"Naomba tena uape kuwa hutakaa unikane maishani mwako!"
"Ok naapa sitakukana maishani mwangu!!
"Sitaki.....sitakiii....sio hivyo!?" Lisa aliongea huku akizungusha zungusha mikono yake mithili ya mtoto aliyesusa.

"Sasa baby unataka niape vipi jamani!?"
Nilimlalamikia Lisa kwa sauti ya upole lakini hakunionea huruma.

"Nyosha mkono wako wa kulia juu!" Lisa aliongea huku akinisaidia kuifanya kazi hiyo.Na mimi nikanyosha kama nilivyoamuriwa.
"Haya sema mimi Tom!" Lisa aliendelea na maelekezo yake nami nikawa namfwatisha anavyosema.
"Mimi Tom!"
"Naapa kuwa!"
"Naapa kuwa!"
"Sitakaa nimkane!"
"Sitakaa nimkane!"
"Mpenzi wangu Lisa!"
"Mpenzi wangu Lisa!"
"Kwa hali yoyote ile!'
"Kwa hali yoyote ile!"
"Eeh Mwenyezi Mungu nisaidie!"
"Eeh mwenyezi Mungu nisaidie!"

"Wow!...hapo ndo umeapa sasa,sasa ole wako uje uthubutu!" Lisa alinichimba mkwara laini baada ya kumaliza kiapo hicho.

"Hata bila kiapo wee wajua siwezi kukusaliti mpenzi wangu!"
"Lazima nikuwekee Pin code sasa ukijaribu tu unakufa siku hiyo hiyo!"
"Ah jamani kumbe unataka kuniua!"

"Ukinikana utaniua alafu na wewe utakufa ha ha ha! kwahiyo tutakufa wote!" Lisa aliongea maneno magumu lakini kirahisi sana.
"Lisa nakupenda sana sweetheart!"

"Nakupenda pia Tom wangu!" Lisa alinijibu kwa sauti ya ndani sana kisha akanishika kidevu nakuanza kuzinyonya papi za midomo yangu,Nikamshika kwa nguvu kiuno chake nakuanza kuunyonya ulimi wake,japo kilikuwa ni kitendo cha dakika moja tu lakini raha yake nadhani iliniongezea miaka saba ya kuishi.

Hivyo ndivyo nilivyomaliza kikao chetu cha dharura siku hiyo huku nikifurahi sana kila mmoja wetu alivyo na utayari wa kupigana na kidudu mtu yeyote atakayeingilia penzi hili.

Tulipokuwa njiani nikimsindikiza Lisa kwao kuna wazo likanijia.Huwezi kumiliki nchi bila kusimika bendera ardhini.Sasa mi nawezaje kummiliki Lisa pasipo mtu yeyote kujua,Akinizingua je nani atakuwa shahidi?.Wazo hilo ndilo lililonifanya nitake kuanza kumtambulisha Lisa rasmi kwa baadhi ya ndugu zangu ambao tunapikika chungu kimoja.

"Baby jiandae!..Jumamosi hii tutakuwa na safari kidogo!" Nilimwambia Lisa baada ya kuridhika na mawazo yangu.
"Ya kwenda wapi tena mpenzi!?"
"We jiandae tu siku ikifika utajua!"
"Haya mpenzi nitajiandaa lakini iwapo tu utaniambia tunaenda wapi!"
Lisa alijibu kimasihara lakini alionekana kumaanisha alichokisema hali hiyo ikaanza kunitia hofu kwani mimi sikutaka kumwambia kuwa nampeleka ukweni.Nilihofia kuwa huenda angegoma.

Siku iliyofuata,niliweza kumueleza Lisa tunaenda wapi na kwa nini na kwa kiasi chake aliweza kunielewa.

Hayawi hayawi huwa,hatimaye ikafika Jumamosi,siku niliyokuwa nikiisubiri kwa hamu sana ili nikamtambulishe Lisa kwa Shangazi yangu ninayempenda sana mtaa wa Cheo.

Majira ya saa tisa alasiri Lisa aliwasili nilipokuwa kisha nikaungana naye tayari kwa kuianza safari ya Cheo.

"Baby usiwe unapendeza sana ivyo utakuja kusababisha wanipore buree!" Nilimtania Lisa kwa kumnong'oneza baada ya kuliona jicho la uchu la dereva wa bajaji tuliyemkodi lilivyokuwa likimtazama mpenzi wangu!.

Baada ya kumwambia hayo wote tukaangua kicheko na safari ya kwenda kwa Auntie ikaanza.Kiukweli Lisa alikuwa amependeza haswaa siku hiyo,kigauni cheupe chenye madoa myeusi kilikuwa kimemkaa haswaa.Binti huyu alikuwa ni mrembo kiasi kwamba wakati mwingine sikuwa naamini kuwa nammiliki mimi.

Baada ya dakika kadhaa kupita hatimaye tukawa tumefika mtaa wa Cheo.Mtaa ambao ardhi yake iliibeba nyumba anayoishi Auntie yangu ambaye tunapatana sana.

"Welcome home babie!!" (Karibu nyumbani mpenzi) Nilimkaribisha Lisa baada ya kufika kwa Auntie.

"Mmmmh home wapi?....wee mwenyewe mgeni!" Lisa aliubeza ukarimu wangu,sisi wawili tunapokuwa pamoja basi masihara huwa hayabaki nyuma.

"Ah jamani karibuni wageni wanguu!" Auntie alitukaribisha baada ya kuona mapenzi yanataka kututeka.Tangu tulipowasili nyumba hiyo,Auntie alikuwa akimtazama Lisa kwa jicho la wizi kitu kilichonifanya niamini kwa asilimia mia kuwa Auntie ameshamkubali.

"Enhee! Mtatumia vinywaji gani jamani...kuna juice,soda,wine,ujii!" Auntie alituuliza mara baada ya kujimwaga kwenye sofa la mtu mmoja sisi tulikuwa tumekaa wawili.

"Tuletee juice!" Nilimjibu Auntie kisha nikamtazama Lisa naye akatikisa kichwa kuashiria amekubali.

"Enhee na wewe mrembo wangu!" Auntie alimuuliza na Lisa kutafuta uhakika lakini mi nikamjibia.

"Tuletee tu juice tena glasi moja huwa tunakunywa wote ikiisha utatuongeza!" Nilimuamuru Auntie naye akaonekana kutoniamini kwani anafahamu fika kuwa napenda sana utani.

"Etii!?" Alimuuliza tena na Lisa kutafuta uhakika na Lisa akajibu ndio kwa kutikisa kichwa!

"Ha ha ha!...nyie watoto mna mambo nyiee!" Auntie alicheka huku akitikisa kichwa kuonyesha kuwa ameshangazwa sana na mtindo wetu wa maisha(life style).

Kama utani vile aliileta glasi moja ya juice nami nikawa namnywesha Lisa kidogo nami napiga funda moja alafu porojo zinaendelea.Nadhani mtindo huo ulimfanya hata Auntie mwenyewe atuonee wivu.

"Jamani muda wote unafanya mbwe mbwe zako lakini bado hujanitambulisha mgeni unajua!?" Baada ya kuwa muda umesogea Auntie alichombeza swali ambalo lilinikumbusha kilichonileta nyumba hiyo.Najua yakuwa Auntie alikuwa akimfahamu vizuri Lisa lakini kwa muda huo alitaka kujua nimekuja naye kama nani,kwa kulielewa hilo nikaenda moja kwa moja kwenye point.

"Auntie huyu ndo mkweo yaani ukisikia roho ya Tom basi ujue ndo huyu!"

"Ooh nashukuru kumtambua!....Lisa karibuni ukweni mama!" Shangazi aliongea huku akimtazama Lisa kanakwamba anamlinganisha na mie.

"Enhee Nini mmepanga juu ya maisha katika safari yenu ya mapenzi!?"Auntie alichombeza swali lingine ambalo kila mtu alionekana kumtegea mwenzake alijibu.

"Eti Lisa! Utaolewa na Tom?" Auntie baada ya kuona tunategeana kujibu alilifafanua swali lake na kumdondoshea moja kwa moja Lisa.

"Ndio atanioa!" Ingawa Lisa alijibu kwa kifupi sana lakini alionekana kujiamini sana katika jibu lake.Jambo hilo lilinifanya nifurahie sana moyoni mwangu kwani ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Lisa kulikiri penzi letu hadharani.

"Wee Tom umjali mwenzako na wewe Lisa umpende mwenzako...sitataka kusikia leo na kesho sijuii mmezinguana nini!" Auntie alihitimisha kwa nasaha hiyo nasi tukamuahidi kuwa jambo baya halitotokea katu.

"Niliwaandalizia kitu kizuri kweli ngoja nikawaletee!" Auntie aliongea akiwa anainuka kuonyesha kuwa alikuwa anakifuata kitu hicho.

Kitendo cha Auntie tu kuondoka ikawa kama vile ameiruhusu simu ya Lisa kuita,Simu ya Lisa iliita naye baada ya kuiangalia alikunja ndita na kubetua midomo yake kama mtu anayesikia kichefu chefu.

"Si nilishakwambia sitaki usumbufu mbona husikiagi bhaana aarrrgh!" Lisa aliipokea simu hiyo na bila kungoja aling'aka kwa kiburi hakuruhusu upande wa pili kusema lolote akawa ameikata simu nami nikapata shauku ya kuhoji.

"Nani huyo!?" Niliuliza nikiwa nimemkazia jicho.
"Robby!" Lisa alijibu kwa upole kana kwamba si yeye aliyekuwa akibwata sekunde chache zilizopita,Sikuwa na swali la ziada kwake,tukakaa kimya tukimsubiri Auntie!.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni