
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Katika purukushani hizo bausa mmoja alifanikiwa kuudaka ule mkanda hivyo Dulah akawa hana jinsi zaidi ya kukimbia.Alipotoka nje anataka kuvuka barabara maana wale mabausa walikuwa wanakuja kwa kasi akasikiamlio wa defender ya polisi akaona isiwe tabu akaingia chini ya gari moja ambayo lilikuwa karibu nalo. Ile defender ikapita kwa nguvu na ikafanikiwa kuwakamata wasichana wachache ambao walikuwa wakijiuza hapo nje.SASA ENDELEA...
Wale mabausu wakajua na Dulaha atakuwa amesombwa na defender hiyo iliyokuwa doria.Omary rafiki yake na Dulah akang’ang’niwa na walinzi wakati Deo kijana aliyekuja na kina Alice yeye alikuwa akiomba mabinti hao wamtetee kuwa sio yeye aliyoanzisha ugomvi bali alikuwa anaamulia. Siku ikawa imeingia doa Alice akwatetea wote wawili yaani
Omary na Dulah wakachiwa. Hakuna aliyetamani kuendelea kubaki eneo hilo.Rafiki zake na Dulah wakawa kwenye wakati mgumu kwa sababu Dulah ndo alikuwa na ufunguo wa gari.Mbaya zaidi hiyo ilikuwa ni ya kaka yake na Peter. Omary akaamua kumpigia simu Dulah na alipopokea aliwaeleza kuwa yeye tayari amefikagheto.
Walishangaa kwa sababu walitarajiwa kuwa awaambie yupo polisi kwa sababu hata walinzi waliamini hivyo. Ikabidi Peter apande bodaboda akazifuate funguo za gari hilo maana aliona kuacha gari hiyo ya kaka yake kulala hapo ni hatari. Ikabidi amtumie huyo huyo bodaboda kurudi naye lakini Dulah alikataa kulala na kusema waende club ingine wakamalizie starehe zao kwani ndo ilikuwa ni saa 7 usiku.Kwa sababu wote walikuwa wamelewa wakajikuta wanaamua kufanya hivyo. Kumbe mawazo yao hayakutofautina sana na mawazo ya kina Alice.Alice na kampani yake na wao waliaama kutoka club ya mwanzo na kwenda ingine.Kwa bahati mbaya walikwenda club ile ile ambayo walikwenda kina Dullah.
Safari hii wote walikutana nje shemu ya kulipia kiingilio.Wakaaanza tena kurushiana maneno ya kashfa jambo lilomfanya Omary hasilipe kiingilio kwa sababu yeye ndo alikuwa ameshika pesa. Walimisihi Dulah waondoke zao kwa sababu mmiliki wa club hiyo ndo yule yule wa club waliyokimbia mara ya kwanza baada ya kuanzisha fujo. “Pia nimeona wale wadada wanaongea na wale mabausa hivyo hawawezi kuturuhusu tuingie” alisisitiza Peter. Dulaha akampkonya ile hela Omary kisha akaelekea sehemu ya kulipa kiingilio. Wakati huo kina Alice na kampani yake walishaingia mda mrefu tu.
Yule bausa wa malangoni alitumia busara na kumwamba Dulah “broh ni vizutri kama ungeenda kupumzika kwa sababuu taarifa zenu za fujo tunazo”. Hapo Dulaha akaona ishakuwa mbaya hivyo hakuwa na haja ya kuendelea kulazimisha.Akawaambia wenzake waingie kwenye gari na kuondoka eneo hilo. Waliamua wote waende kulala kwa Dulah kwa sababu alikuwa amelewa sana hivyo suala la yeye kulala mwenyewe ilikuwa ni ngumu maana ingeweza kuleta mahafa. Walifika gheto salama na Dulah alianza kutapika kutokana na pombe kumzidi na pia alichanganya pombe nyingi sana ikiwemo pombe kali eti kupunguza stress au mawazo kwa kile kilichotokea.
Wakati wao wakirudi nyumbani na kulala wenzao waliendelea kula bata na Deo mwanaume ambaye aikuwa akicheza na Alice.Deo alitumia nafasi hiyo vizuri kumfariji Alice.Pamoja na mambo mengine Deo alikuwa akitaka Alice tangu siku ya kwanza alipoingia tu chuoni.Kwa maana walifahamina wakiwa kwenye foleni ya kufanya registration(uasili).Deo alishatumia kila mbinu bila mafanikio kwa sababu kizuizi kikubwa ilikuwa ni Dulah mwanaume ambaye Alice alikuwa akimpenda sana. Ilifika mahali ikabidi Deo akubaliane na ukweli kwamba hawezi kuwa na bint huyo kimapenzi zaidi ya kuwa marafiki wa kawaida tu.
Kwa hiyo urafiki wao ulikuwa na nguvu sana maana Deo aliamini ipo siku Alice atakuja kuwa mpenzi wake.Alitumia nafasi hiyo vizuri sana kwa kumnywesha pombe Alice ili eti tu amsahau kabisa Dulaha wake.Alice hakufurahishwa kabisa na kitendo alichofanyiwa na mpenzi wake Dulah.Aliona kupigwa mbele za watu ilikuwa ni uzaliishaji mkubwa sana “mbona yeye alikuja club bila kuniambia, mbonamimi sijamuhukumuu aliwaza Alice”. Walicheza mziki na kunywa vileo mpaka asubuhi ambapo waliamua kurudi zao chuoni. Kuanzia siku hiyo marafiki zake wakawa wanamshauri kuwa aachane na Dulah kwa sababu ni mwanaume mkorofi na hasiye na mapenzi ya kweli. “Kwa nini
anataka kukumiliki, kukutawala na kukupangia sheri kwani amekuona”? hayo yalikuwa ni baadhi ya maswali ambayo alikuwa akiulizwa na marafiki zake.Maisha yaliendelea na kwa upande wa Dula yeye alikuwa mjini kwa sababu walikuwa wamefunga likizo ya mda mfupi. Dulaha alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa asijue nini cha kufanya ingawa ni yeye ndo alifanya makosa makubwa kutokana na hasira za kudanganywa na Alice.Pamoja na hayo Dulah hakuweza kumtafuta kabisa Alice akiamini kuwa yeye ndo alipaswa kutafutwa.Siku zilizidi kwenda wikiendi ilifika lakini hakuna aliyemtafuta mwenziye.Dulah alairudi shule na kuendelea na masomo.
Wiki hiyo moja tu bila mawasiliano na Alice ilitosha kabisa kumkondesha Dulah.Marafiki zake walilitambua hilo wakaona ipo haja ya watu hao kurudiana.Omary ambaye ndiye alikuwa amezoeana sana na Alice ndio aliotumiwa kuomba msamaha.Omary kwa busara alipanda mpaka chuoni kwa kina Alice na kuongea na shemeji yake huyo. Omary aliamua kujishusha na kumuombea msamhaa rafiki yake. “ Kwa nini huo msamaha hasije kuomba yeye mpaka wewe umuombee?” Hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza la Alice kwa Omary. “Unajua shemeji makosa yako ndiyo yaliyopelekea
Dula kufanya makosa na kwa sababu wote ni wakosaji basi unapaswa kumsamehe.Kama Mungu aliye mbinu anassamehe wewe ni nani hasa hata ushindwe kumsamehe.Samehee saba mara sabini hata vitabu vya dini vinakwambia. Ila kama unaona huwezi kumsamehe ni kila mtu aaendelee na maisha yeka ni sawa mimii ni mjumbe na mjumbe siku zote hauwawi” alisema Omary na kuondoka mara baada ya kuona Alice hataki kumuelewa na alikuwa na kiburi.
Alice akamjibu jibu la mwisho ambalo lilimkera zaidi Omary yaani alimwambia “Shemeji wewe nenda tu siku nikijisikia kumtafuta Dulah nitamtafuta”. Basi waliachanakwa staili hiyo na Omary akafikisha ujumbe kama alivyoambiwa.Maneno hayo ya Aice yalimkera kila mtu aliyepata kuyasikia wakajua huo ndo ulikuwa uamuzi wa mwisho na lilibaki tamko la Dulah tu kukatisha safari ya uhusiano uliodumu kwa zaidi ya miaka 3.Dulah hakutoa tamko la moja kwa moja kwa sababu historia yao ya mapenzi ilionesha kuwa wamepitia majanga mengi hata na hata kipindi kile Alice yupo form five ilishatokea tukio kama hilo. Ambapo aliwakuta yeye na marafiki zake kwenye hotel yao wakila bata.
Waliachanakwa mda tu ila baadaye walirudiana.Ilikuwa ni kawaida kwa Alice kuomba msamaha hasa linapotokea tukio la namna hiyo. Kwa hiyo Dulah aliamini ipo siku Alice ataomba msamaha. Siku zilizidi kwenda lakini Alice hakujaribu kabisa kumtafuta Dulah.Siku moja wikiendi ilifika na ilikuwa ni siku ya ijumaa ambapo Dulah alishuka mjini na siku hiyo alitoroka asubuhi kwa sababuu hakuonaumuhimu wa yeye kuendelea kuwa shuleni ili hali akiwa katika stress za mapenzi.Alifika gheto kwake na siku hiyo alipanga kuhakikisha anapata muafaka wa suala hilo.Baada ya kufanya usafi aliamua kumtafuta Alice kupitia kwenye simu.
Simu iliita mara ya kwanza lakini haikupokelewa vivyo hivyo akapiga tena lakini haikupokelewa. Baadaye Alice alituma sms nipo darasani nitakutafuta nikitoka. Dulah aliendelea kuwa mvumilivu na baadaye kabisa akiwa ameshakata tamaa simu yake iliita na kuangalia alikuwa ni Alice akimpigia.Alipokea na kumwambia kata nikupigie.Alice naye akajibu wewe ongea shida yako bwana. Kauli ilimkrea Dulaha lakini akajitahii na kusema “Kwa kifupi ni mustakabali wa penzi letu ndo kilichonifanya nikutafute”. Wewe unatakaje alisema Aice mara baada ya Dulah kujieleza.
“Unajua makosa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu, na hakuna mwanadamu aiyekamilika na ndio maana pia watu wanaenda shule ili wapate uwezo wa kukabilian ana changamoto za maisha ikiwemo mapungufu ya wanadamu”. Alisema Dulah kwa upole. “Hiyo ni misemo tu ya wanadamu baada ya kufany amakosa, cha msingi wewe nenda moja kwa moja kwenye pointi unataka nini kutoka kwangu” alisema Alice kwa ukali. Kwa kifupi nahitaji vitu viwili kutoka kwako, moja ni mazungumzo ya usuluhishi, mbili kama itashindikana uje uchukue vitu vyako kwangu alifafanua Dulah. “Sidhani kama nitakuwa na nafasi ya mazungumzo kutokana na uzalilishaji ulionifanyia, cha msingi kesho jioni nitakuja kuchukua vitu vyangu alisema Alice na kukata simu. “Last never end the world” alisema Dulah mara baada ya Alice kukata simu kwa dharau.
Dulaha Alisema msemo huo wa kizungu akiwa na maana kuwa huo unaweza kuwa mwisho wa mapenzi yao lakini haimaanishi kuwa ndo mwisho wa dunia bado anaamini maisha yataendelea na atampata mwingine ampendaye.Wakati Dulah akiugulia maumivu mazito ya mapenzi kwa upande wa Alice ilikuwa ni tofauti kidogo kwa sababu yeye alishaanza ku enjoy penzi la Deo kwa njia ya simu na malavidavi mengine. Deo tayari aishamnunuli Alice simu kali, akampa na line mpya ilimradi tu kukatisha mawasiliano baina ya Alice na Dulah.
Walikubaliana kuwa Alice abadilishe laini lakini Alice alisema atafanya hivyo baada ya wiki moja yaani ikifika wikiendi akatoe hela zake zote na kuivunjulia mbali maana hata hivyo ilikuwa ikifanana na namba za Dulah ambye hiyo laini alimchongea yeye. Usiku huo Alice alifikiri sana swalala yeye kuachanana Dulah lakini hakupata jibu kwa sababu alikuwa akimpenda sana na hakuelewa kama ataweza kuishi bila yeye. Ingawa Deo alioneshakumjali lakini kwa upande wake hakutokea kabisa kumpenda mwaanaume huyo basi tu alijikuta akimkubalia kwa sababu ya matukio yaliyotokea.Alice akajikuta akieendelea kubaki njia panda hasijue nini cha kufanya.
Kesho yake ilifika na ilikuwa ni mda wa jioni Alice akajiandaa na kuwaaga rafiki zake kuwa anaenda kwa dada yake sehemu moja inayoitwa Boma. Akampigia Dulaha simu na wakapanga wakutane mjini sehemu moja inayoitwa Uhuru Park. Siku hiyo Dulah alikuwa na rafiki yake Omary na alimuomba yeye ndo awe mwenyekiti wa kikao.Omary alikata kwa madai kuwa binti huyo alikuwa na dharau sana.Dulah alimwabia kuwa siku zote matatizo hayakimbiwi bali ukabiliwa. Kwa hiyo wakakutana hapo na Alice alipomuona tu
Omary alisema “kumbe mpo wawili si mngenambi ana mimi nije na rafiki yangu”. Omary akajibu kwa kifupi kuwa hajachelewa bado ana nafasi anaweza kumwambia aje. Alice aliona kikao hicho ni bora na rafiki yake mmoja angekuwepo ili wasije wakamzidi kete na kumpakazia makosa. Alice akaona ni bora akmpigie Stella ambaye siku zote amekuwa upande wake na amekuwa akimkubali sana Dulah.Aliona akimpigia Easther ambaye ndo kowadi wa Deo itakuwa ni majanga tupu. Alimwambia Stela achukue bodaboda fasta aende hiyo sehemu waliyokuwepo.Omary akaenda jikoni akaweka oda ya nyama choma.Aliwaacha makusudi ili waanze kikaao chao wenyewe.
Mpaka anarudi kutoka jikoni hakuna hata mmoja aiyejaribu kuongea neno zaidi ya kujianamia tu kama mabubu. Mara Stella akaingia maana kutoka hapo mpaka chuoni kwao haikuwa mbali. Walianza kuongea mawili matatu jinsi ya uzuri wa sehemu hiyo waliyokaa.Stela kama kawaida yake hakuwa mvivu wa kutoa sifa mara baada ya kufika eneo hilo.Nyama choma ilikuja mezani watu wakaendelea kujichana huku kila mmoja akisindikizwa na kinywaji anachokipenda. Baadaye mzee wa Busara ndugu Omary alifungua kikao. “Alice , Dulah pamoja na mgeni kwanza niwapongeze kwa kukubali kukutana. Hata hivyo nawaheshimu sana ndio maana nikakubali kuharisha mambo yangu yote na kuja hapa.
Ninachotaka kuwaeleza kabla ya maamuzi yeyote hayajafikiwa leo hii labda mkumbuke historia zenu. Mimi mwenyewe binafsi ni mtu pekee niliyebahatika kushuhudia mapenzi yenu tangia mmeanza mpaka mlipofikia.Najua mmepitia mambo mengi sana na kama kuachana mngeshaachana miaka mingi iliyopita.Kwa nilichokionamimi sikuile pale club ni maamizi yaliyotokana na hasira.Ndugu Dulaha ahkufanya kitendo xha uungwana kumpiga makofi shemeji maeneo kama yale na kwa hili inabidi ukiri kosa na umuombe Alice msamaha.Bwana shemeji nawe kuwa upande wako hukufanya uungwana kumjibu shemeji vibaya pale alipokuuliza pale ndo chuoni.
Kwa hiyo na wewe pia una makosa mawili ya kudanganya na kumjibu vibaya. Hivyo na wewe itakubidi uombe msamaha yaishe. Kwa kifupi wote mnamakosa na hakuna haja ya kumtafuta mchawi cha msingi kabla kila mtu hajasema chochote Alice na Dulah naomba mkumbatiane na Stella uwapige picha ya ukumbusho.
Kila mtu ilibidi acheke maana Omary alikuwa akiendesha kikao kidikteta kama mtu vile mwenye madaraka makubwa sana. Stella alivyokuwa na mbwembwe tayari alaishasimama ikabidi wausika wafanye walivyooagizwa.Basi kabla ya kuwaruhusu kila mmoja aseme ya kwake ya moyoni bado nitaomba kila mtu ajibu maswali yangu alisema omary.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA