UTAMU WA FUNDI (10)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Baada ya kuvaa mwanamke yule aliondoka bila ya kunisemesha, nilimuona tu akangahika kujitoa nje ya chumba changu, hivyo kwa upande wangu, nilikuwa nikifikiria hali ile. Kwa maana kilikuwa kitu ambacho sikitegemea kama kingeweza kutokea katika muda hiyo, na hata sikuwaza kama kingeweza kufanyika mule ndani.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Nikiwa nimevalia nguo yangu ya ndani tu, kichwa changu kikapita na tafakari juu ya kile kitendo, nilifikiri sana lakini sikupata majibu ya moja kwa moja, na hata ilipopita kama dakika kumi niliamua kujitoa kuendea bafu kwajili yakutoa mwili uchovu na mmnuko wa jacho ulikuwa ukisababisha na shunguli ile pevu.
Nje kukanipokea na ukimya tu wa hali ya juu, hivyo na hata nilipoelekea bafuni hakuna niliyemkuta akiwa analitumia hivyo, ilinipa wasaa mzuri wa kujisafisha, baada ya kumaliza kuoga , kujitoa kwenye nje ya bafu nikaribishwa na taswira ya mama Husna, sasa sura yake ilionekana imejawaha na bashasha sana, na hata vile tulivyokuwa tunapishana macho yake yalionekana kunena jambo ambalo nilikosa tafsiri ya wazi nikiwa naelekea ndani kwangu.
Kufika ndani nikapokelewa na muito wa simu yangu.
“Hello” ilikuwa sauti ngeni ya kike ilipenya masikioni mwangu nami nikapokea kwa kusema hello, kisha yakafata maongezi.
“ Ni mimi G” .Alijitambulisha.
“G wa wapi? Nikaohoji baada ya kutoaelewa moja kwa moja ile sauti na kuwa namba ile ngeni kwenye kioo cha simu yangu.
“Ulinipatia namba yako jana ulipokuwa clabu hapa Samaki samaki.”
“Laa! Nikumbushe vizuri?
“Nilivalia kinguo chekundu bhana umenisahau mara hii?”
“Anhaa! Nimekupata, samahani wangu, mambo mengi mwenzio”
“Ok sawa hio ndio namba yangu, nitakucheki baadae nikiwa na nafasi.”
“Nashukuru! Baada ya kusema hivyo simu ilikatwa.
Alikuwa G msichana mrembo haswa niliyefahamiana kwenye usikuwa jana nilipokuwa clabu, nakumbuka nilikuwa nimetulia nikipata kinywaji wakati huo, kichwa changu kikienda sambamba kufatisha milindimo ya mziki ulikuwa ukipingwa na DJ manywele ndani ya ukumbi huo, ikiwapagawisha mabinti na mablaza men walikuwa wamejichimbia katikati na pembeni ya clabu, hiyo kubwa maarufu katika Mkoa huo, wakati mimi nikiwa nimejipunzisha nikishanga hili na hili, nikipata kinywaji ndipo nilipokaribishwa na ujio wa binti huyo.
Alivalia kigauni kifupi chekundu kilichoacha wazi sehemu kubwa ya umbo lake, la wastani ambalo lilikuwa limebenuka na kujenga kishepu kilichotengeneza kichura cha wastani kilichokuwa kikileta mvuto kikitazama na kukijengea picha kama upo kwenye eneo la sita kwa sita na msichana huyo, ambaye alikuwa akionekana bado yu mbichi na kama lilikuwa gari basi halikuwa limetembea sana tangu lilipotoka kiwandani.
Nikiwa nimeshikiria chupa ya kinywaji kikali, mara!
Alivalia kigauni kifupi chekundu kilichoacha wazi sehemu kubwa ya umbo lake, la wastani ambalo lilikuwa limebenuka na kujenga kishepu kilichotengeneza kichura cha wastani kilichokuwa kikileta mvuto kikitazama na kukijengea picha kama upo kwenye eneo la sita kwa sita na msichana huyo, ambaye alikuwa akionekana bado yu mbichi na kama lilikuwa gari basi halikuwa limetembea sana tangu lilipotoka kiwandani.
Nikiwa nimeshikiria chupa ya kinywaji kikali, mara sikio langu lilipokea sauti nyororo na ya udekevu wa binti huyo.
“Samahani kaka naweza jumuika nawe’’ alibenjua kidomo, mdomo ulikuwa na vikirombwezo kibao. Kabla hata sijajibu alikuwa tayari amevuta kiti kisha akiwa sambamba name , huku akinivamia na neno lingine.
“ Au kuna mtu upon aye, nisije nikapigwa miye?”
“Haa! Hapana sister karibu tu” nilimjibu huku nikisawili muonekana wake.
“Ooh asante kaka yangu, nimekuona muda mwingi upo pekee yako, nikaona sio mbaya kuja kujumuika nawe au nimekosea?”
“Ahh… ha.. pana haujakosea mrembo” Nilimjibu huku kinywa changu kikionekana kuingiwa na mchecheto mbele ya binti yule.
Basi huo ukawa ndio mwanzo wa kujua na binti yule kwenye usiku wa jana, alinipa kampani sana, wakati huo kichwa changu kilikuwa ndani ya ulevi hatari na hata sikukumbuka ilikuwaje mpaka tukawa tumebadilishana namba bila ya kukumbuka tukio hilo katika siku ya pili, hivyo hata kitendo cha kunitafuta sikukitegemea, lakini niliona ule ulikuwa mwanzo mzuri wa kufahamiana na binti yule aliyejiita jina G. Hivyo kitendo cha kukaa simu yake, haraka vidole vyangu vilikuwa kwenye batani ya simu na kuihifadhi namba ile kwajina la G, kama nilivyokuwa nikifahamu.
Baada ya kuhifadhi namba ile, nilikuwa nikishughulika kuangalia nguo, ambayo ingeendana na siku hiyo, kwa maana kutokana na ule utanashati wangu, nilikuwa nimezipanga nguo kulingana na siku usiku, ilikuleta utofauti na binadamu wengine. Haikuwa dakika nyingi nilizipata, mwili wangu ukapambana nazo, kioo kikawa kinasadifu ule muonekano wangu, hakika nilikuwa nimependeza sana kwenye taswira ya kile kioo kiasi cha kwamba, nilianza kujisifu mwenyewe kabla hata kusiwa na mtu mwingine. Wakati huo, nilipoitwa saa yangu, ilinionesha namna muda ulivyokuwa umekimbia sana. Ilikuwa inatimu saa nane, lisaa limoja kabla ya lile nilikuwa nimeweka miadi ya kuona na ‘Kahawa’, mwanadamu mmoja ambaye tulikuwa tukifanya kazi eneo moja.
Hivyo kitendo kile cha kufahamu kuwa muda umeenda mbio, ilinifanya kuharakisha, ilikujitoa ndani ya chumba changu, kuwahi maeneo ya kihonda Magorofani alipokuwa akiishi bwana huyo.
Laa kitendo cha kutoka nje tu. Hamadi! kwenye mlango wangu, nikakumbana na ujio wa mwanadamu mwingine, ambaye sikuwa namtegemea kabisa kwenye macho yangu, akiwa na kitu kilichonitia shaka na kunijengea hofu kubwa!
ALIKUWA mtoto mdogo wa kike, ambaye nilifahamu kwajina la Husna. Ujio wake ulinishangaza na kilipo chumba changu, hakuwahi kutokea hata siku moja kitoto hicho kuwa na mazoea na mimi. Hivyo kumuona tu, alinisalimia kisha kunikabidhi karatasi ndogo, halafu akatokomea kwenye mboni zangu. Karatasi ile ilikuwa imebeba maandishi kadhaa yaliyokuwa yamebaba nambari ya simu, na yule mmiliki wake ambaye nilifahamu kuwa ni Mama Husna, hivyo mwisho kukitazama kile kikaratasi nilikiweka kwenye mfuko wangu wa suluali, haraka nikijitoa eneo hilo.
Kihonda magorofani, ikanikaribisha punde tu nilipojitoa nyumbani, kwa madaha na umakini mkubwa nilikuwa nikisawili nyumba kadhaa ambazo zilikuwa sambamba na nyumba ya jamaa yangu Kahawa, hivyo baada ya hatua kadhaa, nilikuwa nikitazamana nayo. Ilikuwa nyumba nzuri sana, iliyokuwa imepambwa na maua, huku ikiambatana na uzio ulikuwa ukifanya nyumba hiyo, iyonekana ya hadhi ya juu kati ya nyingi ambazo zilikuwa zimemeza mtaa huo.
Kiukweli Kahawa alikuwa rafiki ambaye kutwa alikuwa akinifanya nami kufikiria kuwa na sehemu ya kuishi nzuri kulingana na ule utanashati wangu.
“hodi!
“karibu!’’ sauti ya kitoto ilinikaribisha, wakati huo nikipambana na kuvua viatu kuingia ndani humo.
“Ahsante, nadhani baba nimemkuta!”
“Ndio baba mdogo, yupo ndani na mama” kile kitoto cha kiume kilinijibu wakati huo akionekana yu bize na mambo yake. Kabla sijatoa neno lingine sauti ya Kahawa ikanisawili.
“Karibu kijana, niende wapi mkuu wakati nilitegemea ujio wako!”
“Laa! Nilidhani utakuwa umetoka bwana, mzima lakini?
“Niko safi, karibu”
“Nishakaribia” nilijibu, mwili wangu huku makalio yangu yakiwa juu ya kochi moja wapo lilikuwa ndani ya sebule ya nyumba hiyo.
“Kinywaji gani kijana unatumia?”
“Anhaa maji ndugu!”
“Maji acha masihara?’’ aliniuliza Kahawa huku akijitoa na kuelekea kwenye jokofu lilikuwa pembezoni mwa sebure, kisha kunipatia maji kama vile nilivyokuwa nikihitaji.
Bilauli ndogo, ilibeba kimininika cha maji, kikawa kinasindikiza maongezi yetu, wakati huo Kahawa akinieleza hali ya shemeji, ya kuwa ilikuwa imebadilika sana, na hapo juzi tu walitoka kugombana kiasi cha kwamba, hakuwepo nyumbani hapo. Hakika ilikuwa taarifa ngeni sana masikioni mwangu, nilifahamu mwanamke wake, japo kwa mara moja, mwanamke ambaye kwa namna nilivyokuwa nikimfahamu bwana yule nilijua wazi lazima angekuwa anapata upinzani mkali sana kwa maana mwanamke alionekana kuwa mjanja mjanja machoni na hata kwa matendo yake. pia na ule uzuri wa mwanamke yule, ijapokuwa sikuwa nimefahamu sana na hata kujua mwenendo wake. Hivyo jambo lile halikunitisha sana.
“Sasa ndugu yangu umeniita hapa, ilinikupe msaada wa nini zaidi?’’ ilinipaswa kukata kauli baada ya kusikiliza maelezo marefu kutoka kwa bwana huyo, maelezo ambayo yaliyokuwa yakionesha wazi alikuwa amechoka vitendo vya mke wake huyo, huku akionesha hakuwa na namna mbele ya mwanamke huyo.
“Ahh! Ndugu yangu, sijui nikwambie nini lakini hakika mwenzio nimeshikwa haswa, tena nimeshikwa pabaya”. Alizungumza, akanyamaza kimywa.
“Niambie hicho hicho braza,” nilimuambia huku nikichombeza kibwagizo cha braza, nilizoe kumuita hivyo, tulizoeana hivyo, urafiki wetu ulijengwa na ile hali ya uchangamfu na ujanja wangu, kwenye maswala mengi. Hivyo kuniita pale alifahamu wazi huenda ningekuwa msaada mkubwa sana kwake.
‘’Siku ya tatu hii unavyoniona shemeji yako, tulivurugana kidogo ametimka, sasa walau ungenipa msaada wa kunibembelezea arudi nyumbani, kwa maana nafahamu kama yupo nyumbani kwao, na hata nilipo jaribu kuwafahamisha wazazi wake wakaniambiwa kuwa amefika nyumbani pale, na unamjua kabisa Mama Abdul, hakuna mzazi wake yoyote ambaye anaweza kupingana na kile alichokuwa amehamu!”
“Enhe nakusikiliza ndugu” nilimuambia huku ni kuvuta umakini wa habari ile kwenye kichwa changu, wakati huo nikitafari ni namna gani ambavyo ningeliweza kumsaidia mbele ya mwanamke huyo, ambaye hatukuwa na mazoea kivile zaidi ya kuonana naye siku moja moja ambapo nilipata kufika nyumbani pale.
“Sasa bwana nakupa hi namba yake ikiwezakana mtafute na umueleze bwana najua hautokosa neno la kumwambia ndugu yangu na akaweza kurudi nyumbani, najua nilikuwa nimemkosea kwa kitendo cha kuchelewa kurudi nyumbani, lakini mwenyewe si unajuaga majukumu ya kazi yanavyotubanaga.”
“Najua basi hilo swala wewe niachie nadhani atarejea tu huyo, siku si nyingi, nitafanya mawasiliano naye na kila hatua nitayokuwa napitia sito sita kukupa taarifa ndugu yangu.’’
Saa kumi na moja ya jioni , ilinikutia nikiwa ndani ya chumba changu nikiwa nimejifungia baada ya kutoka kwa Kahawa, nikiwa na ulevi kidogo umekitawala kichwa changu, ilitokana na kupata vinjwaji vikali viwili vitatu kabla ya kuagana na kumuhidi ningeweza kumuweka sawa mke wake na familia yao kurudi sawa.
Chumba kilikuwa kikubwa kwa wakati, huo, kitanda kikawa kinanibembeleza kutokana na ule ulevi ulikuwa umekichukua kichwa changu, kabla ya kupitiwa na usingizi, usingizi ulikuwa umenitoa pale na kunipeleka sehemu nyingine, ikienda sawa na ulevi wangu.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni