MAPENZI NA NGONO (16)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
Haaaamadi ile natoka tu nikakutana uso kwa uso na Rafiki yangu samson ambaye alikuwa katika sura ya hasira kali akiwa ananiangalia mimi kwa shauku nakujikuta nikisita kunyanyua mguu na kubaki nikiganda bado tena nikiwa nimemshika mkono halima ambaye naye kumuona samson kwake kulimfanya naye ashtuke flani na hata kusita kutembea naye akaganda kumuangalia samson.TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Nilitaka kumtoa mkono alionishika lakini halima akakaza mkono na mimi nikashindwa kumtoa.
"Mmmmhhh s...aaa..mson vipi broo".......
Nilijitutumua kumuuliza Samson swali ambalo wala hakulijibu aliniangalia kwa Macho ya hasira sana yenye dalili ya machozi jambo ambalo lilinitia wasiwasi na moyo wangu kuanza kuchukua nafasi yake na kuanza kudunda kama saa dalili ya ugomvi kutokea ilionekana dhahiri kutokana na samson jinsi Alivyo.
"Pablo jumatatu basi si ndio Mtihani tutawasiliana vizuri Leo usiku love you mwaaah"Halima akaniambia na yale Maneno yakazidi kunishtua na Bila ya aibu palepale halima akaniachia busu zito la mdomo mbele ya samson ambaye aliishia kuangalia kisha kwa mwendo wa Maringo halima akaanza kuondoka na Alipomfikia karibu samson akaachia msonyo wa nguvu kisha akaendelea na safari yake kwa mwendo wa haraka haraka bila ya kugeuka nyuma.Samson akabaki ananiangalia mimi macho yakiwa yamemtoka na Machozi yakaanza kumtoka na kutiririka katika Mashavu yake na mimi aibu ikanishika na kujikuta Mwanaume nainamia Chini kutokana na Aibu ambayo kwa kiasi kikubwa nilitaka kujaribu kuificha lakini nikajikuta nikigonga mwamba.
"Sasa Mwanangu huu ndio ushikaji au usnitch si ungesema kama huyu demu unamtaka na sio kunidanganya kama Unakaribia kumaliza kila kitu??" samson akafungua mazungumzo na kusababisha mimi niinue kichwa kimtizama kwa Macho ya huruma kutokana na kumuonea huruma kwa sababu alikuwa analia sio kwa sauti lakini machozi yalikuwa yanamtiririka.
"Hamna Mshikaji samson mimi mbona natengeneza na mule aliniita tuongee kuhusu we..."
"Nyamaza mwanangu pablo nitakuzingua sasa hivi yani mwanangu mimi nilikuwa nakutumiaga vocha ili ongee naye unionganishie kumbe demu unamtaka wewe kwa hiyo unanichukulia mimi boya sio??"
Ghafla hali ikabadilika samson taratibu akaanza kunisogelea mikono yake ikiwa imekunja ngumi tayari kabisa kupigana jambo lililosababisha mwanaume nianze kurudi nyuma taratibu kutokana nilikuwa sipendi ugomvi kabisa hasa kupigana na mtu ambaye alikuwa ni rafiki yangu.
"si nakuuliza unanichukulia poa sio mwanangu pablo yani mimi nilikuwa nakuamini kumbe daah hivi unajua jinsi gani ninavyompenda halima hivi unajua jinsi ninavyotesekaa aaa sikubali" Bila ya kutegemea samson akanisogelea na kunikunja shingoni kwa hasira huku ngumi akiwa kaikunja na kuninyooshea tayari kabisa kutaka kunitandika nayo.
"Oyaa jamaa kausha bwana mwanangu sio fair ngumu za nini sasa subiri nikueleweshi ilivyokuwa sasa ngumi za nini mwanangu d....." kabla hata sijamaliza kuongea ngumi ikamtoka samson na kunipiga mdomoni na kuniachia nikidondoka huku nikitoa miguno ya maumivu.haraka haraka nikashika mdomoni kwa mikono yangu vitu kama mate yaliokuwa mdomoni mwangu na kuleta ladha ya chumvi nikayasikia na nilipotema yalikuwa ni damu zilizokuwa nyingi mdomoni mwangu kutokana na ngumi ile kunichana.
"Daa Mwanangu ndio umenipiga kweli??" Nikamuuliza samson aliyekuwa akiniangalia kwa hasira kali huku mimi nikiwa bado naendelea kutema damu zilizokuwa zinatoka mdomoni.
"Ndio una hamua nini sasa fala wewe au nije Nikuongeze" Maneno ya samson yakanitia hasira na kujikuta nikinyanyuka na kuanza kumsogelea na nilipomfikia karibu nikamrushia kibao cha nguvu kilichompata vyema katika shavu lake la kulia na kusababisha agune kidogo na kuinama chini na alipoinuka aliinuka na ngumi kali niliyoikwepa.
Nikamrukia na kumkaba shingoni kwa hasira lakini roba yangu ikatolewa na samson na kwa hasira akafanikiwa kunitia mtama ulionipeleka chini kisha akanikalia juu nakuanza kunitandika ngumi za pua kama mbili zilizonitoa damu lakini nikatumia nguvu zangu na kufanikiwa na mimi kumbidua na kumkalia juu na kuanza kumshindilia ngumi lakini pia samson akafanikiwa kunitoa na wote tukasimama huku tukiwa tumekunja ngumi. Damu zilikuwa zinanitoka nyingi mdomoni na puani huku samson akiwa naye anatokwa na damu nyingi mdomoni na kichwani zilizokuwa zikichafua Shati lake la shule.
Shule nzima tulikuwa wawili tu hakukuwa na mwanafunzi mwingine yoyote hata walinzi wa shule sijui walikuwa wapi na sisi ndio tulikuwa tupo juu kabisa la jengo la ghorofa katika madarasa ya floor ya juu tukizichapa mimi na rafiki yangu kipenzi samson ambaye wala sikuwai kutegemea kwamba kuna siku itakuja kutokea.tukiwa tumesimama huku bado kila mtu akiwa amekunja ngumi kwa hasira na kumuangalia mwenzake samson kwa kasi akanivamia mpaka katika ukuta na nikukandamiza na kuanza kunitandika ngumi mfululizo za tumbo ambazo ziliingia barabara na kuleta maumivu makali lakini nguvu za ghafla zikanijia na kujikuta nikimtandika kichwa kikali cha pua samson kilichomrudisha nyuma kisha nikakunjuka teke kali likakwepwa vizuri na samson aliyebonyea chini kisha akanidondosha chini kwa kunipaga tena mtama mkali ambalo ulisababisha nifikie kiuno na kuniletea maumivu mengine makali ya kiuno kwa kujishika na bila ya huruma samson akanikalia tena juu nakuanza kunipiga tena ngumi kadhaa.
"Weee mtoto lazima nikuue leo lazima nikupasue ukome"samson aliniambia kwa hasira huku akinipiga ngumi mfululizo zingine za masikio kwa Lengo la kutaka niachie ili anipige usoni ambapo nilikuwa nimeziba kwa mikono yangu miwili ili ngumi zake zisinipige usoni.Samson baada ya kuniona naanza kuishiwa nguvu haraka haraka akaninyanyua na kunigeuza nyuma kisha akanipiga robo kali na kunipeleka tena chini huku akiwa amenikaba shingoni kwa kutumia mkono wake ukisaidiwa na mwingine ambayo ilitosha kabisa kuninyong'onyesha kwa maumivu.Ukali wa roba ile ulipelekea nianze kukohoa huku macho yakinianza kunitoka hata nilipotaka kujaribu kumng'ata sikufikia mkono wake uliokuwa shingoni mwangu.
"Aaa...aaa....aaaa....u..na..niuaa mw..anaanguu unan..niumizaa b..anaaa yalaaa unaniumizaaa.." Nililamika kwa tabu huku nikiendelea kurusha rusha miguu yangu huku mikono yangu ikiwa juu ya mikono yake shingoni nikijaribu kuitoa hapo shingoni mwangu ambao ndio samson alikuwa kanishikilia kwa nguvu akanikaba na wala hakutaka hata kuniachia.
"Eeeewe utakoma...Nakuuuliza utakoma yani mpaka nikufundishe Adabu f**** wewe" Samson akaongezea huku akiwa amezidisha kabisa kunikaba hakika alionekana kabisa kudhamiria kuniua nilipaparika kama kuku kuitoa mikono yake udenda ulikuwa unanitoka na kumwagikia yeye mikononi mwake lakini wala hakushtuka yeye aliendelea kunishikilia na kukaza mikono yake kwa nguvu za hali ya juu.Ghafla nguvu zikanijia nikaangaika mpaka mdomo wangu ukakaribia karibu na Mkono wangu ambapo bila ya kuchelewa nikamng'ata kwa nguvu na kusababisha samson atoe ukelele wa nguvu wa maumivu na kuniachia kutokana na jinsi nilivyong'ata kwa nguvu na kusababisha Maumivu makali.
"Aaaaa Mjinga wee yani unaning'ata" samson akalalama na mimi nikanyanyuka Haraka haraka samson akanivaa tena lakini safari nilimkwepa kwa ufundi kisha nikamkamata na kumsukumiza kwa nguvu ambapo yeye moja kwa moja akaenda kuvaa ukuta na kujigonga kwa Nguvu kichwani na Papo hapo akatulia kimya.
"Heeee nimeuaaaaa!!!"...
Jasho jembamba likaanza kunitiririka mwili mzima baada ya kumuona samson amelala chali hata nilipojaribu kumuita alikuwa kimyaa haongei wala kutingishika uoga ulionivaa ulinifanya nishindwe hata kumsogelea kumtingisha niliaanza kutetemka kama mtu anayesikia baridi hakika lilikuwa baridi ambalo na Majasho yalikuwa yanachuruzika mwili mzima.
" Sa...aa..mson br..oo a.mka.." kwa sauti ya chini kama mtu ananisikia vile nikalalama machozi nayo yakaanza kunitiririka hakika nilitamani ile ingekuwa ndoto lakini nilipokuja kuona sio ndoto bali ni kweli hakika nilichoka ndipo nilipozidi kulia na machozi yakanitoka kwa wingi zaidi kilio ambacho hakikuwa na sauti kubwa kilikuwa ni cha kawaida chenye simanzi nzito hakika usifanye masihara kuua bila ya kudhania au kukusudia ni kitu kingine na usiombee hali kama hiyo ikutokee
"Weee kimbiaaa" sauti ya ghafla ikanijia katika kichwa changu ikiniambia nikimbie na hata sikutaka kukataa na kupinga licha ya kuwa nilipotaka kunyanyua mguu kukimbia miguu yangu kukimbia ilikuwa mizito si kawaida ilikuwa kama imewekwa sumaku flani hivi ambayo ilikuwa ikinivuta pale nilipotaka kujaribu kukimbia.Nilimuangalia samson aliyekuwa amelala kwa huzuni kubwa na bila ya kujiuliza nikaanza kukimbia kushuka chini ya jengo lile ya shule ambalo ni ghorofa mbili ndefu zilizojengwa vizuri.
Kwa mwendo wa haraka nikaanza kuzishuka ngazi kwa spidi ya hali ya juu lakini ghafla nikajikuta nikiganda kama mtu aliyepigwa shoti ya umeme au sindano ya ghafla hamadi!!!
"Begi langu!!" Nikalikumbuka begi langu nililoliacha darasani wakati na jisomea mimi na samson na lilikuwa kulekule juu ya ghorofa shauri yakutaka kuliacha lilikuwa ngumu kwa sababu atakapokuja kuchukuliwa samson na kutakapofanyiwa uchunguzi na kukutwa begi langu lingekuwa kosa na kukamatwa kwangu.
Nikakata shauri ya kurudi juu kwa kasi tena kwa mwendo wa kusua sua mara nijikwae mara nigongane miguu nikafanikiwa kufika na Moja kwa moja nikaelekea katika darasa tulilokuwa tunajisomea Mimi na samson na kuchukua begi langu kisha nikatoka tena haraka haraka kushuka tena huku safari nikiwa siuangalii tena Mwili wa samson aliyekuwa chali pale.
"Kohooo!!!,kohoooo......!!!" kabla hata sijaanza kuzishuka ngazi sauti za mtu kukohoa nikazisikia kabisa kwenye tundu za masikio yangu nakunifanya nigande nigeuke nyuma kwa hofu kuangalia anayekohoa ni nani tena.Macho yakatua kwa samson ambaye alikuwa akikohoa na kuanza kutingishika Jambo ambalo lilinifanya nidondoshe begi langu kwa Mshangao wa furaha ya hali ya juu furaha ambayo ilikuwa imepotea ghafla nakuingia dosari ya hatari.
Nikajikuta nikirudi mpaka pale kwa samson nakumuangalia alikuwa akikohoa huku akihema kwa nguvu majasho yakiwa yanamtiririka kama Maji huku akiwa anahema haraka haraka nikavua shati langu la shule na kubaki na vest kisha nikaanza kumpepea kwa kutumia shati langu huku nikiwa siamini kilichotokea Niliona kama miujiza mingine kwa sababu nilihisi samson atakuwa amekufa kutokana na kumsukumiza vibaya ukutani.
Nikajikuta nikishusha pumzi za furaha na kumkombatia kwa nguvu sana
"Oooooo vipi broo vipi samson upo fresh kaka??"
"Mmmh vipi pablo nipo wapi aaaa kumbe shule nilizimia eee aaaa ulinisukumiza ukutani"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni