MAPENZI NA NGONO (17)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
Nikajikuta nikishusha pumzi za furaha na kumkombatia kwa nguvu sana
"Oooooo vipi broo vipi samson upo fresh kaka??"
"Mmmh vipi pablo nipo wapi aaaa kumbe shule nilizimia eee aaaa ulinisukumiza ukutani"
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Samson akawa anauliza maswali huku akiwa anajijibu mwenyewe huku akiwa ananiangalia mimi ambaye nilikuwa bado nikimpepea huku nikimuangalia yeye.
"Samahani sana samson halikuwa kusudi langu samahani sana"
"Daaah kichwa kinauma balaa hivi pablo kwanini umemchukua halimaa"
"Daa mwanangu nyanyuka tuondoke kaka Tutayaongea vizuri"
Hakika samson alikuwa anampenda sana halima alikuwa ni chizi kwake jina la halima lilijaa katika daftari lake kutokana na kumpenda bila ya kupoteza muda nikamsaidia samson kunyanyuka kisha haraka haraka nikaenda darasani tena na kumchukulia samson begi lake kisha nikamshika bega huku nikimsaidia na begi lake na kuanza kushuka ngazi za lile jengo.Nikamsindikiza mpaka kituoni na kuhakikisha Mpaka anapanda gari kisha na mimi nikapanda gari la kuelekea nyumbani.
Hakika mawazo ndio yaliendelea kuniandama sana nikiwa katika gari na nilipokumbuka vuguvugu lilotokea nyuma nilibaki kumshukuru Mungu huku nikiwa siamini kabisa kuwa samson ni mzima kutokana na Kipigo kile nilichompa. Nilifika nyumbani Na breki yangu ya kwanza ilifikia kwenye simu yangu ya mkononi ambayo nilikuwa nimeizima Nikaiwasha kisha nikaiandika namba ya samson iliyokuwa kichwani na kuipiga haikuita sanaa ikapokelewa.
"Nambie Man pablo" nikajikuta nikishusha pumzi ndefu huku nikitabasamu kwa furaha baada ya kusikia sauti ya Samson ambaye mchana wake nilipigana naye kisa Halima.
"poa sam vipi unaendeleaje kaka??"
"Fresh Mwanangu kichwa kilikuwa kinanisumbua mida flani lakini sasa fresh kaka"
"Aaaaaa daa safi sana vipi sam unapiga msulu nini"
"Kama kawaida pablo lakini nini kaka naomba unisamehe kwa yale yote ya mchana yaliyotokea unajua hasira tu za hapa na pale"
"Aaaa nishakusamehe kaka tena kitambo tu halafu vitu vile vya kawaida chakumshuruku mungu tu tumebaki wazima Maana mwanangu Nilijua umekufa kaka"
"Aaaa mimi jembe siwezi kufa kizembe sasa unajua nini pablo nakuomba uendelee kumueleza Halima jinsi gani ninavyompenda nampenda sana nipo radhi kumpa kila kitu atakachokihitaji katika Maisha" samson aliongea kwa hisia na kuniambia na kunifanya nitulie kimya kidogo na kutathimini kwa kuchekecha ubongo wangu.
"Usijali mwanangu nishaweka vocha sasa hivi namsaundisha"
"Poaa kaka" Nikajikuta nikitikisa kichwa baada ya kusikia maneno ya samson aliyeniambia Kuwa bado niendelee kumshauri halima awe naye.Nilimuonea huruma samson kutokana na jinsi anavyompenda halima ambaye eti alikuwa akinitaka mimi.Nikachukua tena simu yangu nakumpigia halima na kumuambia mkasa mzima uliotokea na kumshauri kuwa awe na samson ndiye mwanaume anayemfaa jambo ambalo halikupita kabisa katika masikio mwa halima na alikataa kata kata.
"Jamani tena ndio nimezidi kumchukia yani anadiriki kukupiga wewe mpenzi wangu yani mwambie simtaki simpendi na sitompenda tena na aondoe kuwa na Mimi katika maisha yake Pablo sikia Mimi nakupenda wewe nitakupa chochote utakachotaka Baby hata ukitaka kusikostahili baby i love you nakupenda sana" Maneno yakamtoka halima na kuzidi kuniudhi na Kunikera na kunivunja Nguvu bila ya kumjibu nikakata simu yake kwa hasira kisha nikajibwaga kitandani na kuanza kufikiria Mchezo unavyokwenda ghafla mlio wa messeji ukalia katika simu yangu na nilipochukua kuangalia na nani tena alikuwa si Mwingine bali ni Samson kwa hofu nikaifungua.
"Nambie kaka vipi ushamwambia mwambie Bana Nampenda sana yani hapa nasoma lakini hata haviingii namuanza yeye tu" Messeji ya samson ikazidi kunichanganya na wala sikumjibu nikakata simu nakutuliaa kitandani.
"Mmmh yani rebecca,dada tuse,rukaiya,zureiya na huyu halimaa kweli kazi ninayo....."...
. Asubuhi na mapema bila ya kuchelewa siku ya jumatatu nikahamka na kujitayarisha kwenda shule ilikuwa ni siku muhimu mno kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo kila mwanafunzi wa kidato cha nne alikuwa akiisubiri kwa hamu na hofu kubwa kwa sababu ilikuwa ni siku ya kupanda mazao tuliyoyanunua na kusubiri kuyapanda kwa kipindi cha miaka minne.Mwanaume nilikuwa nishajiandaa vya kutosha tena bila ya kuogopa nikiwa nimeshika compass langu mkononi lilikuwa na dhana zote kama pen,penseli na mambo kibao.
Nikaingia shuleni na moja kwa moja nikaanza kumtafuta Samson rafiki yangu ambaye siku mbili za nyuma tulikwaruzana kisa mwanamke ambaye alikuwa ananitaka mimi lakini mimi nilikuwa simuhitaji lakini mdomo wangu ulikuwa mzito sana kumwambia kutokana na kuogopa kumuumiza.Nilikutana na Samson ambaye alifurahia sana kuniona akiwa na washikaji wengine ambao nao baada ya kuniona wakaishia kunipa hai tu
‘’Inakuaje Samson mambo vipi umejiaandaaje na mtihani mshikaji’’ ‘’daa fresh tu Pablo kazi kazi oya vipi mwanangu uliiongea na Halima roho yangu maana nampenda sana’’samson akinichomekea ya Halima jambo ambalo lilianza kunikera lakini sikutaka kumuonyesha zaidi ya kutabasamu tu na kumpa moyo Samson ambaye alifurahi baada ya kumuambia Halima anamfikiria kwa mara ya pili. Baada ya kuonana na Samson mwanaume nikaanza kuzunguka zunguka tu shuleni nikisubiri muda muafaka ufike ghafla nikiwa katika mizunguko yangu pale pale shuleni nikaasikia naitwa na nilipoangalia nani ananiita alikuwa si mwingine bali ni Halima alikuwa ndani ya tabasamu pana baada ya kuniona mimi sikutaka wala kumfuata mwanaume nikajifanya kama simuoni na kuondoka na kumuacha huku akiwa na mshangao wa hali ya juu.
Kengele ikagongwa kuashiria mtihani ulikuwa tayari kufanya na sikuwa na budi kuelekea katika mistarini tuliyoelekezwa kwa lengo la kwenda kupewa maelekezo ya hapa na pale na kukumbushiwa sharia za mtihani ambayo tayari tulikuwa tunazijua sema mwalimu mkuu msamamizi wa mitihani alikuwa akitukumbushia.Ilipotimia saa mbili kamili tukaingia katika vyumba vyetu vya kufanyia mitihani hali iliyosababisha presha kupanda na kushuka kwa muda huo kila mtu alikuwa kimya kuwaza na kuwazua je mitihani itakuwa migumu kama walimu walivyokuwa wakituhusia kuwa mitihani ya mwisho ya kidato cha nne si lele mama kama wanafunzi wengi wanavyotegemea.
Siku zikasogea kwa kasi sana mitihani ilikuwa migumu hatari na hatimaye tukamaliza yote na kufanya hadi practical kwa sisi tuliokuwa tunachukua sayansi.kila mtu alikuwa na furaha na huzuni katika siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuagana kwa sisi wanafunzi na hata walimu ilikuwa ni siku ya graduation ambayo shuleni hapo tuliamua kufanya baada ya kumaliza mitihani ili tuagane vizuri kila mtu alikuwa na furaha yebye majonzi ya hapa na pale kwa sababu tulikuwa tumezoeana sana sema ilikuwa graduation ambayo ilikuwa ni wanafunzi tu wazazi hawakualikwa kutokana na mambo flani ya kifedha ambayo ilikumba shuleni wakiwa na lengo la kuboresha Maabara yetu ya shule.
Wanafunzi tulikusanyika na kuanza kupewa husia na maelekezo ya kukabiliana na maisha ya mtaani huku kila mwalimu alikuwa akiisisitizia kutokana na vijana wengi wakati huu walikuwa weni wavuta bangi na wakabaji hali iliyosababisha wengi wao kuuliwa na wananchi wenye hasira kali na wengine hata kukamatwa na mapolisi ulikuwa ni wosia uliomgusa kila mwanafunzi aliyekuwa akiisikiliza. Baada ya kuhitimisha graduation hiyo iliyokuwa fupi wanafunzi wote tukaruhusiwa kuondoka huku tukipewa na wosia wengine kwamba tusisahau kwenda kusalimia shule.Siku hiyo Samson alikuwa hajaja shuleni na sikujua sababu ya kutokuja kwake shuleni mwanaume nilikuwa mpweke na kuagana na wengine na kubadilishana namba za simu kama wengine wanavyofanyaga
‘’PABLOOOOOOOOOOOOOOOO’’Ghafla nikasikia jina langu likiitwa na kusababisha nisimame na kugeuka nyuma kuangalia nani aliyekuwa akiniita Macho yangu yakakutana na halima aliyekuwa amependeza sana kwa nguo zake alizokuwa amevaa na kuonyesha umbo lake maridhawa lenye shepu nzuri na nene yenye kumvutia kila mwanaume aliyekuwa akimpitia karibu hakika alionekana mrembo hasa na si kama mwanafunzi alionekana mdada mwenye kazi zake aliponifikia karibu bila ya haya akanikombatia mbele ya wanafunzi wengine waliokuwa nao wanaondoka na kusababisha minong’ono flani kuanza kutokea na kusababisha mimi nimtoe haraka
‘’vipi sasa mbona ulikuwa unataka kuondoka bila hata ya kunishtua jamani au umesahau’’ ‘’hamna nimekutafuta sana sijakuona leo sasa unasemaje’’ ‘’Jamani baby ilo ya kuuliza tena twende gesti tu ukanipe kitu roho inataka roho inapenda baby’’ ‘’oooooooo basi twende me sina maneno’’bila ya uoga nikamshika kiuno Halima na moja kwa moja tukatoka shuleni na kuanza kushaka gesti ya kwenda kubanjuka mimi na halima ambaye alikuwa anamchukia sana rafiki yangu Samson bila ya sababu za msingi.safari yetu ikagota barabarani ambapo tulikuwa tukisubiri gari la kuelekea mitaa ya maeneo ya kwetu ambayo ndio nilimwambia kulikuwa na gesti nyingi zenye utulivu mkubwa na tunaweza kuenjoi kwa raha.
Nikiwa pale barabarani Halima akaona baiskeli ya mtu anayeuza koni na kutokana na kupenda akaniaga anakwenda kununua na mimi nikamruhusu akaenda huku nikiwa na msindikiza kwa macho kisha akanunua na kugeuka nyuma na kuanza kurudi huku akiniangalia kwa furaha iliyojaa kifani.ghafla bila ya hata ya kutegemea nikakumbatiwa na mtu nisiyemfahamu kwanza alinikombatia ghafla bini vuu na kusababisha hofu unitande nilipojaribu kutaka kumtoa akanizidi nguvu na kupeleka mdomo wake kwangu na kuanza kuninyonya denda mbele ya watu pale kituoni barabarani.nikatumia uanaume wangu kumsukumiza kwa nguvu ambapo alisukumizika lakini macho yangu yakatua moja kwa moja kwa rukaiya dada yake zureiya na kusababisha roho ianze kudunda ghafla kwa sababu rukaiya anafahimika vizuri sana na Halima ambaye shoga yake ni zureiya
‘’Vipi wewe unaogopa nini baby??’’ Maneno yakamtoka rukaiya na kuniambia mimi niliyekuwa natetemeka kwa uoga wa halii ya juu ‘’Heeeeee makubwa rukaiya hadi weewee unamzunguka mdogo wako??’’ kwa nguvu Halima akayatamka maneno yaliyomshtua sana rukaiya ambaye alipogeuka naye akashtuka na kupigwa na butwaa baada ya kumuona Halima aliyekuwa ameshika koni ambazo akazidondosha kutokana na kitu alichokiona machozi yakaanza kumtiririka na bila ya kuangalia Halima akaingia barabarani akiwa na hasira na majonzi ya hali ya juu
‘’PAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!????’’……
‘’Maaaaamaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!’’ ukulele wa nguvu ukasikika pale barabarani yakiambatana na mlio mkubwa wa gari ambayo iliyokuwa imefunga breki.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni