SORRY MADAM (91)
Zephiline F Ezekiel
---
SEHEMU YA TISINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
“Vipi?”
Nilimuuluza kwa wasiwasi, huku kitu cha kwanza kukifikiria kichwani mwake ni kaka take, niliye muacha ndani ya buti ya gari lililo shambuliwa vibaya kwa risasi.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Umeyaokoa maisha yangu”
Casey alizungumza huku akiendelea kulia
“Casey tuondoke”
Sauti ya kaka yake ilisikika, na kutufanya sote tutizame mlangoni na kumkuta à kiwa amesima, huku akiwa na nguo ya ndani tu. Akajistukia mwenyewe baada ya watu wote, kumshangaa.
“Naweza kupiga simu?”
Casey alimuuliza mmoja wa wahudumu aliye valia sare kama wahudumu wengine
“Ndio”
Casey akaonyeshwa simu iliyo kwenye moja ya ukuta ndani ya hii baa, akaniachia na kwenda kupiga simu, baada ya kumaliza akarudi nilipo simama
“Nimempigia simu baba, atafika muda si mrefu”
Ving’ora vya gari za polisi vikafika katika eneo la tukio
“Kumbe hawa nao hawana tofauti na wabongo”
Nilijisemea kimoyo moyo, huku nikiwatazama askari hawa wakiingia kwa mbwembwe ndabi ya baa hii huku, wakiwa na bunduki mikoni mwao
“Weka silaha yako chini”
Askari mmoja aliniamrisha huku, wakinielekezea bunduki zao.
Nikashangaa wazee wawili wakisimama mbele yangu huku, mikononi mwao wakiwa wameshika chupa za bia.
“Nyinyi muda wote mulikua wapi? Huyu kijana yeye ndio aliye waua majambazi wotw hawa, bila aibu munakuja sasa hivi”
“Kwanza hamshangai, jinsu tulivyo mzingira huyu kijana, munadhani ni jambazi?”
Wazee hawa walipokezana kuwatandika maswali askari hawa, walio baki wakibabaika wasijue nini chakuwajibu wananchi hawa waliopo ndani ya hii baa. Askari wakaachana na mimi, wakaanza kushuhulika na miili ya majambazi hao. Kundi kubwa la waandishi wa habari walio kuja baada ya askari kufika, wakaanza kunihoji naswali ambayo sikuyajibu hata moja.
“Eddy baba yangu amekuja”
Casey alizungumza huku, akinishika mkono na kutoka ndani ya baa. Nijakuta gari nne , nyeusi zinazo fanana, aina ya GVC, zika zimejipanga pembeni, huku zikiwa na vijibendera vidogo vya marekani. Walimzi wapatao kumi, walio valia suti nyeusi, pamoja na miwani nyeusi, wakashuka kwenye magari hayo. Kaka yake Casey akaongoza zilipo gari hizo, huku mkononi mwake akiwa ameshika kamera ya Casey, akashuka mzee mmoja mwenye mvi kichwani mwake.
“Eddy yule ni baba yangu”
Casey alizungumza huku akiendelea kunishika mkono nielekee zilipo gari hizo.
“Ngoja kwanza, siwezi kwenda kwa baba yako nikiwa kwenye halii hii”
“Wewe twende baba yangu hana tatizo”
Casey alizungumza huku akiendelea kunivuta, tukafika zilipo gari zao, akakumbatiana na baba take.
“Baba, huyu ni shujaa aliye yaokoa maisha yangu. Anaitwa Eddy”
“Eddy huyu ni baba yangu, ni balozi wa Marekani, hapa Afrika kusini”
Nikampa mkono, baba Casey naye akaupokea wa kwangu huku akiachia tabasamu pana.
“Asantw kijana kwa kazi nzuri uliyo ifanya”
“Asante mzee”
Casey akamuomba baba yake niweze kujumuika nao kwenda wanapo ishi, ikawalazimu walunzi kunikagua, mwili wangu kamakuna kitu kinaweza kuwadhuru. Wakachukua bastola yangu, wakaniruhusu kuingia ndani ya gari.
Sikupanda gari moja na Casey na baba yà ke, gari nililo panda likari wawili walio kaa siti ya mbele mmoja akiwa ni dereva. Kwangu ikawa kama bahati kukutana na balozi huyu wa Marekani.
Japo mama yangu ni waziri wa nchini Tanzania, ila sikuweza kubahatika kukutana ni viongozi wa nchi kubwa kama Marekani. Katika siti niliyo kaa, nyuma ya siti ya dereva kuna Tv ndogo inayo onyesha, vipindi mbalimbali. Matangazo ya kituo cha television kinacgo itwa ENEWS, kikaanza kuonyesha tukio la majambazi walio kufa, huku ikisadikika kundi hilo la majambazi lilikuwa likitafutwa na jeshi la polisi la Afrika kusini, zaidi ya miaka mitano sasa, pasipo mafanikio.
‘NI MTU MMOJA TU, AMEWEZA KULISAMBARATISHA KUNDI HILO HARAMU’
Nimaneno ya mtangazaji wa taarifa hiyo, huku picha za video zikinionyesha, walivyo kua wakinihoji.
“Wewe ni askari?”
Mlinzi mmoja aliniuliza, pasipo kugeuka nyuma kunitazama
“Hapana”
“Umewezaje kutumia silaha?”
“Nilifundishwa na baba yangu, yeye alikua ni mwanajeshi”
“Yupo wapi?”
“Amesha kufa”
Nilidanganya, huku nikiangalia saa ndogo iliyopo pembezoni mwa dereva, ikionyesha ni saa sita usiku. Nikageza shingo yangu kutazama pembezoni mwa barabara, ambapo kuna bonde kubwa na endapo dereva akikosea basi tukianguka, huko bondeni tutakua tutasagika sagika bibaya,na isitoshe gari zote zipo kwenye mwendo kasi sawa kwa uzoefu wangu, spidi wanayo tembelea ni zaidi ya spidi mita mia moja.
Matone matone ya mvua yakaanza kutotesha vioo vya gari letu tulilo panda, ambalo ni lapili kutokà mbele, kati ya msafata wa magari manne yaliyo ongozana. Kitu ninacho wasifu madereva hawa, ni utaalamu wao kukunja kona, bila kupunguza mwendo wa magari yao, zilizopo kwenye hii bararaba iliyo chogwa kitaalamu, pembezoni mwa mlima ninao weza kuufanan uliopo mkoani Iriñga ni Tanzania.
Nikiendelea kuitadhimini barabara hii, gafla nikastukia kuliona gari la mbele yetu, nikinyanyuliwa hewani na kitu kama bomu kutegwa, likazunguka hewani mara kadhaa na kutua chini, kitendo kilicho mfanya dereva wetu kufunga breki za gafla, zilizo lifanya gari kuserereka na kuligonga gari lililo anguka na kulisukumia bondeni, kwenye korongo refu, huku matairi ya mbele ya gari letu yakianza kutangulia kwenye korongo, huku ya nyuma yakijitahidi kubaki barabarani.
Macho yangu yote, yakahamia kwenye gari inayo kuka nyuma yetu kwa kasi kubwa, huku dereva wake akijitahidi kufunga breki zake, akitumia juhudi zake zote
Nikajiluta nikiyafunga macho yangu, kwani kitu kinacho fwata sekunde chache, ni dereva huyo, kutusindikiza kwenye korongo kama alivyo fanya dereva wetu, kwenye gari lilil kua mbele yetu.
Dakika kama mbili, hivi niliendelea kusikilizia ni nini kitatokea, kwetubila haikuwa hivyo. Mwanga mkali wa taa za gari lililo kua nyuma yetu, ukaendelea kunipiga machoni, ni sentimita chache sana, toka lilipo simama gari lililopo nyuma yetu, huku gari letu, likianza kunesa taratibu.
“Tutulie hivi hivi”
Dereva alizungumza huku akihema sana, askari walio kwenye magari ya nyuma wakashuka kwa haraka, kwenye magari yao, wakaja nyuma ya gari letu na kuanza kujitahidi kulivuta kwa nyuma. Kutokana na uzito wa gari ikawa ni kazi ngumu sana kwao kulivuta. Ikawalazimu kulishikilia na kutuomba tushuke haraka.
Sikutaka nipoteze muda, nikaufungua mlango wa nyuma katika siti niliyo kaa na kutoka nje haraka iwezekanavyo, huku walinzi nilio kua nao ndani ya gari wakitokea kupitia mlango nilio pitia mimi.
Walinzi wakaliachia gari, likaporomoka kwenye korongo. Nikiwa ninatazama huku na kule, nikawaona watu wakiwa juu kidogo ya mlima wakijipanga kwa ajili ya kufanya shambulizi
“Shitiii”
Bila hata ya kuomba, nikachomoa bastola moja ya mlizi aliyo ichomeka kiunoni mwake. Nikafyatua risasi mbili kwa jamaa aliye shika bunduki aina ya ‘Snaiper’ ambayo ni hatari sana, kutokana na uwezo wake mkubwa.
Mashambulizi yakaanza rasmi, na watu hawa ambao ndio walio tegesha bomu barabarani. Ikawa ni ambushi moja ambayo hakuna aliye itarajia kama inaweza kutokea kwa wakati huu, askari wawili wakapigwa risasi na kufa hapo hapo.
“Gari la balozi ni lipi?”
Nilimuuliza mlinzi mmoja, niliye simama naye karibu, tukiendelea kujibu mashambulizi ya wavamizi hawa, ambao wanapig a risasi kama wendawazimu
“Lile la mwisho”
“Nilinde”
Jamaa akaendelea kuwafyatulia majambazi risasi, huku mimi nikikimbia pembezoni mwa kuta ya mlima huu, jambo lililo gumu kwa majambazi kuweza kuniona. Nikafika lilipo gari la balozi, nikamkuta akiwa ameinama kwenye siti yeye pamoja na wanae, wakimuomba Mungu wao
“Muheshimiwa unaniamini?”
Nilimuuliza balozi mara baada ya kuingia ndani ya gari na kukaa, katika siti ya dereva.
“Ndio nakuamini.”
Kutokana gari halikuzimwa, likanirahisishia wepesi wa kufanya jaribio la kumuokoa balozi pamoja na familia yake. Nikaangalia upenyo ulio achwa na gari, lililo simaba barabarani, nikaamini unanitosha kupita.
Mlinzi akanipa ishara nipite, yeye anaendelea kupambana na wavamizi hawa. Nikafanya kama alivyo agiza, kalilazimisha gari kupita kwenye uwazi wa gari lililopo barabani, chakushukuru Mungu likapita, ikawa kazi ni kwangu kuhakikisha ninasonga mbele.
Japo kuna risasi kadhaa zilipigwa kwenye gari letu, ila hapakuwa na iliyo adhiri matairi zaidi ya kuvunja vioo vya pembeni. Kwa mwendo kasi wa gari hili, ulinifanya niwe makini kwa kila kona ninayo kunja barabarani.
“Ohhh Mungu wangu! tunafwatwa nyuma”
Kaka yake Casey alizumgumza huku, akichungulia kwenye kioo cha nyuma kilicho jaa matundu ya risasi. Sikutaka hata kutazama nyuma kuzihofia kona za papo kwa papo, huku nyengine zikiwa ni kali sana.
“Wapo wangapi?”
”Pikipiki mbili na gari ndogo tatu”
“Muheshimiwa unaweza kutumia, silaha?”
“Eheee?”
Balozi alibabaika kwenye kunijibu swali nililo muuliza. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuongeza mwendo kasi wa gari, ninalo liendesha. Tukafanikiwa kuingia kwenye barabara iliyo nyooka, hapa ndipo nikapata wakati mzuri wa kuwatazama wanao tufwata kupitia kioo changu cha pembeni.
“Hawa vijana ni kina nani?”
“Siwajui muheshimiwa”
Waendesha pikipiki, nikawaona wakilikaribia gari letu, kutokana na mwendo wao mkali. Nikapunguza mwendo taratibu
“Mbona unapunguza mwendo?”
Balozi aliniuliza huku akitetemeka, hata sauti yake haikutoka vizuri
“Najua nini, nafanya”
Nilimjibu kwa kujiamini, huku macho yangu yote yakiwa kwenye kioo cha pembeni nikiwatazama jinsi majambazi hao wakija kwa kasi, Nikakanyaga breki kwa nguvu zangu zote, huku nikilizungusha gari kwa mtindo wa duara, jambo lililo wafanya waendesha pikipiki hawa kulivaa gari letu, na kila mmoja akarushwa vibaya na kuangukia upande wake wa barabara.
Kutokana na uhodari wa gari hili, halikuweza kuyumba wala kuzima. Ila kilicho, niogopesha ni jinsi gari ilivyo geuka na kutazama tulipo tokea ambapo kuna gari mbili ndogo zinatufwata, na mbaya zaidi zipo karibu kutufikia.
Ikanilazimu kulirudisha gari kinyuma nyuma ili nipate, japo nafà si la kuligeuza, nitakavyo jua mimi.
Nikiwa ninaendelea kurudi nyuma kwa mwendo wa kasi japo si sana nikaliona, gari tulili liacha sehemu tuliyo vamiwa likaja kwa kasi nyuma ya gari hizi mbili ndogo, zinazo tukimbiza.
“Ohhh wamelichukua hata hili”
Nilizungumza huku nikijitahidi kupata nafasi ya kuligeuza gari hili, ila kwa bahati mbaya upande nilio kuawepo mimi kuna gari kubwa la mizigo, likija kaa kasi huku dereva wake akijitahidi kunipigia honi, nimpishe upande wake, lasivyo anatugonga.
Nikalirudisha kwa haraka upande wa kushoto ambapo ndipo ninapo stahili kupita, dereva wa gari ambaye alikuwa upande mmoja na mimi, nikastukia akigongana uso kwa uso na gari hilo la mizigo, tukio lililo mstusha mwenzake ambaye nipo naye upande mmoja.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni 2
Chapisha Maoni
-
Mapoizon19 Aprili 2022, 07:10Profile
MapoizonSaid: mpzn.blogspot.comView profilempzn.blogspot.comReplyReply