MAHABA NIUE (46)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Asubuhi ya kesho yake aliwasha gari kimnya kimnya na kuelekea Morogoro ambapo baada ya maasaa manne tayari alikua msamvu na kumta futa wakili huyo ambae alienda mpaka nyumbani kwake ila, bahati mbay aaliambiwa kuwa ana umwa, hakutaka kuondoka bila kuonana nae, alicho fanya alimsubiri kwa siku mbili ili aruhusiwe hospitali ambayo haikua mbali na hapo.
KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII
SASA ENDELEA...
Moja kwa moja aliongoza nyumbani kwa wakili huyo, baada ya kusikia tayari kasha ruhusiwa hospitali, kweli aliingia ndani na kuka ribishwa na kuanza kueleza kila kitu,
“ulisema mdogo wako, alifariki akaacha duka kubwa mjini, na shamba ambalo hujui lipo wapi”?
“ndio”!
“huyo ana etaka kumdhulumu ni nani”?
“rafiki yake kipenzi yaani sijui nini kime mpata huyo shetani , “
“dada ninge kusaidia, hiyo kesi ni ndogo sana, ila nita kuelekeza kwa mama mmoja hivi, naamini ata kusaidia sana”
“una sema”?
“nasema hivi, ngoja nibadili nguo nikupeleke kwa mwana mke mmoja hivi, huyo nina amini ata kusaidia, niamini mimi, hali yangu sasa hivi sio nzuri sana nina umwa,”
Mzee huyo alisimama na kuelekea chumbani ambapo baadea alirudi tayari kasha badili nguo na kuondoka na Loydah,
Loyda alioneshwa kuchukizwa sana na kauli ile kutoka kwa Mzee kodende ila haku taka kuji onesha, mwendo wa dakika arobaini walikua teyari wesha fika katika nyumba ndogo ya kawaida ila ili kua ya kisasa sana,
Walishuka na kuingia ndani, kweli wali funguliwa na mtoto mdogo wa kike mlango na kupita ndani,
Wakili Yule aliye fahamika kwa jina la Kodende alimkabidhisha Loyda kwa wakili mwenzake na kuondoka zake ili awaache waongee, ila Loydah alijikuta ana gadisha macho yake juu ya mtoto mdogo aliye kua akiangalia katuni kwenye t,v. alimuangalia sana kana kwamba ana mfananisha.
“dada”
Mwamke yule alimshtua Loydah baada ya kutokea jikoni
“samahani, huyu mtoto ni wako”?
“ndio, kwani vipi”?
“kazuri sana,nime mpenda”
“ naitwa Loydah Felix”
“niite MAMA CATHERINE au jina langu Sabrina. nakusikiliza”!
Loydah alianza kuelezea shida yake kila kitu kuanzia mwanzo mpaka mwisho, bila kuficha chochote, ila kila alipo zidi kuelezea Sabrina alizidi kusikiliza kwa makini sana, na kusogea karibu sababu marehemu aliye kua ana zungumziwa pale alikua akimjua,
“una sema mdogo wako alikua anaitwa nani”?
“Ramsey Felix kidhirwa”
Sabrina alibaki akitoa macho hakika hakutaka kuamini kua anae ongea nae ni dada yake na Ramsey, alihisi mkuki wa moto ume tumbukia ndani ya moyo wake, hakuelewa ni jambo gani afanye alitamani kulia ila alijikaza,
Alimuangalia mwanae ambae alikua hana habari, alirudisha shiingo yake kwa Loydah hususani alimuangalia machoni na kuona ni jinsi gani macho ya Ramsey na dada yake yalivyo fanana, hakutaka kubisha,
Aliji kuta akidondosha chozi na kutoka haraka mahali pale na kumfanya Loydah asielewe nini kime mkimbikiza, hakuelewa kwanini Sabrina kakimbia. Laiti ange jua ndiye mwanamke pekee aliyezaa na Ramsey angeshukuru sana Mungu , ila hakuelewa lolote lile, alibaki kumwangalia Catherine ambae alikua akiangalia katuni ya tom and jerry, alishindwa kuji zuia na kuji kuta ana muita
“una itwa nani”?
“cate”
“cate nani”?
“chijui,”
“baba yuko wapi”?
“Mama ame niambia sina baba. Aliniambia baba yangu hayupo hapa”
“yuko wapi”
“chi…”
“Loydah tuendelee”
Alifika Sabrina na makaratasi huku bado akiwa na kwikwi sababu ilionesha alitoka kulia muda mfupi uliiopita,
“mwanao kafanana na marehemu mdogo wangu Ramsey sana”
Sabrina alimwangalia Loydah na kutamani kumwambia kuwa alimuona Ramsey siku chache zilizo pita ila hakuwa na uhakika na kile anacho taka kukisema, Licha ya kutaka kusema ila nayeye alitambua vizuri kuwa Ramsey alikufa, alikaa kimnya ili ajue mwisho wake, hakutaka kufungua mdomo wake kuongea lolote lile,
Aliandika kila kitu na kumuhaidi Loydah kuwa ata msaidia kwa kila kitu, alimuhaidi kuwa kesi angeenda kushinda na wala si vinginevyo,
*******
TAYARI RAMSEY na dokta Leila walifika jijini Dar es salaam siku hiyo na kupumzika siku moja , na kesho yake kuamua kumta futa Dalali ili akawaoneshe kiwanja hiko alichodai kuwa kipo nje ya mji kidogo,
waliongozana na Dalali huyo, kwa Leila alikua mgeni ndani ya jiji hilo hakuelewa majina ya sehemu mpaka dalali huyo alipo sema kuwa kiwanja kipo BUNJU B,
“Bunju B, nishwahi kufika”
Aliropoka Ramsey na kuonekana akisha ngaa shangaa, baadae wali fika maeneo ya kiwanja hiko kilipo,
Na kuanza kuzunguka
“mhhhh”
Ramsey aliguna na kuki shangaa kiwanja hiko, alionekana kama ana kumbuka kitu sababu aliweka mkono wake mmoja mdomoni,
“nini sam”?
“hapa napajua, hapa napajua, ila siku mbuki nili fika lini”
“Sam acha kuni chekesha. Wewe uli fika lini huku?”
“huku nili fika”
Hakujua kuwa hiko kili kua kiwanja chake, ila alicho kumbuka yeye kuwa Alisha wahi kufika eneo lile, bado aliendelea kukumbuka hasa alipoona nguzo ya umeme na kuisogelea, hakuelewa kwanini yupo katika hali ile, ki ukweli alijua fika kuwa ana tatizo.
“naomba nionane na mwenye hiki kiwanja ili tuandikishiane kwa Mjumbe”
Aliongea Leila na Dalali Yule kupiga simu kwa mwenye kiwanja,
Kweli baada ya dakika hamsini tayari kijana mrefu kidogo mweusi alikua kasha fika kiwanjani hapo , ila alisita kidogo baada ya kumuona Ramsey,mbele yake , alifikicha macho yake sababu alidhani anaota au anauona mzimu. Hakutaka kuamini kuwa aliye kua mbele yake ni Ramsey ambae alitaka kuuza kiwanja chake akidhani kuwa ame kufa,aliogopa sana na kujua anaota,
Kweli hata kwa Ramsey pia alibaki kumuangalia kijana Yule na kuonekana kukumbuka kitu, alivuta kumbu kumbu mtu Yule ali muona wapi na moja kwa moja kukumbuka ndoto aliyoota, siku chache zilizo pita, hakika alishindwa kuelewa na kuji kuta ana rudi nyuma kwa hatua ndogo ndogo, akikumbuka jinsi alivyo chomwa kisu
“Sam njoo uongee na mwenye kiwanja uje kusaini huku, ili twende kwa mjumbe”
“mama nime ghairi kiwanja siuzi tena, nime pata mteja mwingine”
Maneno yale yalitoka mdomoni mwa Prosper na kumfanya hata Dalali Yule ashindwe kumuelewa bosi wake ame kumbwa na nini….
Prosper alitembea mwendo wa haraka haraka na kuonekana dhahiri kabisa kama ni mtu aliye changanyikiwa, alikua akigeuka nyuma mara mbili mbili mpaka aka jikwaa na jiwe na kudondoka chini
alijizoa zoa na kuendelea na mwendo wake, hakika alionekana kuchanganyikiwa hakua na uhakika kama aliye muona mbele yake alikua ni Ramsey mtu aliye jua ame kufa, alijua kivyovyote vile ana chezewa mchezo, licha ya kumuona Ramsey mbele yake ila nafsi nyingine ina mtuma kuwa wenda hakuwa yeye
na duniani kuna watu wanao fanana, aliweka kidole mdomoni huku akizidi kumuangalia Ramsey akiwa kwa mbali, alizidi kumwangalia na kuzani wenda ni mzimu.
“ina maana hapa duniani kuna watu wana fanana kiasi hiki”?!
Aliwaza prosper.
“bosi vipi sasa, mbona ume fanya ivyo?, Yule mama kaja na cash wewe mbona ume kimbia tena”?
“wewe Yule mama ume mtoa wapi”?
“Yule katokea Moro goro”
“na Yule msh kaji”?
“mimi sijui, twende tuka chukue mpunga ule”!
SABRINA AKIWA AMELALA KITANDANI usiku huo hakupata usingizi hata kidogio mawazo yote yalikua kwa Ramsey ambae aliamini ame kufa muda mrefu kidogo, hakika alimpenda sana na mbali na hapo alikua tayari kasha mzalisha na mtoto.
“au ita kua nime mfananisha,? Lakini hapana, mpaka sauti, Yule ni Ramsey, lazima nifanye kitu”
Aliwaza Sabrina huku akiwa amelala chali akitazama juu ya paa!, hakupata hata lepe la usingizi usiku huo, aliji lazimisha lakini ilikua kazi bure, alikumbuka vitu vingi walivyokua waki fanya na Ramsey, kweli alimpenda sana
Ramsey , na kufanya vitu vingi sana vya hatari ili mradi mapenzi yao yaende sawa, kweli alijiapiza kuwa ata fanya juu chini kama Yule ni Ramsey ata jua, na kupitia kesi ya Loydah alijua ndipo hapo ita kua rahisi kumsogeza karibu Ramsey.
KESHO YAKE ASUBUHI Loydah pamoja na Sabrina wali funga safari mpaka Dar es salaama ambapo baada ya siku moja kesi itaanza kusikilizwa, kweli wali fika jijini Dar es salaam salam salmin, na Sabrina kutafuta moja ya hotel nzuri na kupumzika kwa ajili ya kesho ata kavyo kabiliana na kesi hiyo.
Alitoa makaratasi yake, na kuanza kuandika kila kitu kwa ajili ya kesi itakayo somwa kesho, alitamani sana kesho ifike.
Kulikucha asubuhi na Sabrina kuanza kujiaandaa ambapo ana fuatwa na Loydah mpaka mahakamani kwa ajili ya kesi ambayo yeye alisimama upande wa Loydah kama mtetezi,
bila Loydah kujua kuwa Ramsey alishawahi kuwa na mahusiano na mwanamke huyo tena sio ivyo, bali alizaa nae mtoto, kweli Sabrina alibeba siri nyingine ya kumuona Ramsey hakutaka kusema chochote mpka pale uchunguzi wake uta kapo kamilika,
Alipanda wakili Joseph Kabogoza akitetea upande wa Prosper.
“mimi naona hakuna haja ya kusumbuana mpaka huku, kwa sababu gani, kuna usha hidi na vidhibiti vyote kuwa mali ya marehemu tayari ime uzwa muheshimiwa hakimu, kwanza mwenye mali kafariki tayari sidhani kama kuna kesi yoyote hapa”
Aliongea wakili huyo kwa kujiamini sana, aliongea yote na kukaa ambapo baadae na Prosper alipanda kizimbani na kuendelea kukaza kuwa aliuziwa duka kabla ya Ramsey kufariki, bado Loydah hakutaka kuamini kama Prosper
anaendelea kukazia msimamo wake,
haku taka kuamini kama leo hii Prosper ange kuwa vile, ali tamani japo walau Ramsey afufuke na kuongea lakini haikuwezekana, bila kujua Ramsey yupo hai huko alipo kapoteza kumbu kumbu, laity angelijua hilo, ange mtafuta mara moja.
“huyu mteja wangu ni dada yake wa damu,asingeweza kuuza bila kumtaarifu dada yake, isi toshe bado nashaangaa , hata biashara yoyote ile ina kua na masha hidi, je una weza kunionesha mashaidi walioshuhudia duka hilo kuuzwa, bwana wakili”?
“aaah aah masha hidi wa nini, hawa watu wawili walikua waki haminiana sana , hakukuwa na haja ya kuwa na mashahidi”
“sawa. Mbona haku sema kipindi hiko marehemu akiwa hai, naomba nione hayo makaratasi anayo dai kuwa ni kithibitisho, kuwa aliuliza hiyo mali”
Wakili Joseph alifungua begi lake na kumkabidhi sabrina ambaye aliikagua kwa umakini sana.
“muheshimiwa hakimu, naomba kesi hii isogezwe mbele kidogo, bado nina itilia mashaka hii hati anayo dai kuwa aliuziwa duka na marehemu, kuna vitu hapa zivioni, nita muachia, hii orijino yake mimi nitaondoka na copy yake”
Baada ya dakika moja nyundo ili gongwa mezani na kesi ile kuha irishwa na kurushwa .
Leo hii Ramsey alikua njiani ndani ya basi pamoja na Leila wakirudi Morogoro baada ya kukosa kiwanja kile na kuhaidiwa kuwa waende siku nyingine, kweli bila kujua kuwa kiwanja kile alicho taka kukinunuua ni cha Ramsey ambae yeye ali mpachika jina la Sam,
Baada ya masaa manne tayari walikua morogoro na kuta futa taxi ambayo ili ewapeleka mpaka nyumbani hapo wana poishi,
Waliingia ndani na kuoga wote na kula chakula cha usiku, Leila alianza uchokozi wake na kweli kutaka kupewa penzi la Ramsey hakika alimuona Ramsey ni kila kitu kwake, hakuwahi kuwaza kumchoka hata siku moja iliyoenda Mungu! Kweli Ramsey alikua ndiye mwana ume ana ye mkata kiu yake kupita wana ume wote aliowahi kutembea nao huko awali! Hilo alikiri.
USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni