MAHABA NIUE (48)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Loydah tayari alifika Moro goro nyumbani kwa Sabrina, bila kuficha chochote kile Sabrina anamiuua kumuelezea kila kitu Loydah, na kuamua kuweka wazi swala lake juu ya mtoto aliyezaa na Ramsey, hakika hakukuwa na sababu ya kubisha kutokana na Loydah tangu awali alimuwekea mashaka Catherine mtoto wa sabrina.
KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII
SASA ENDELEA...
“Naomba unipeleke kwa Ramsey sasa hivi”
“subiri Loydah, jambo hili, linahitaji utulivu sana,”
“kivipi wakati ume niambia tayari ana kumbu kumbu alafu kesho ndo siku ya kesi kusomwa, nataka Yule shetani aumbuke”
“Yule daktaria ana mahusiano naye ya kimapenzi, cha kufanya tumsubiri aende kazini ili sisi twende tumchukue ikiwezekana tuondoke nae kabisa “
Alishauri Loydah na wote kukubaliana na mawazo hayo, walikua wenye furaha sana siku iyo, kujuana hakika lilikua ni jambo la bahati, walimshkuru sana Mungu wao aliye juu mbinguni,
Baadae kabisa walienda nyumbani kwa Dokta Leila na kugonga mlango na kufunguliwa na Ramsey, Loydah alilia machozi kumuona Ramsey alimtazama mara mbili mbili hakuamini kama leo hii amemuona tena mdogo wake huyo ambae alidhani alikufa muda mrefu sana.
“Ramsey”!
“mimi sio Ramsey jamani”
“wewe ni Ramsey mimi ni dada yako Loydah”
Kila alipojaribu kuongea na Ramsey hakuonesha dalili yoyote ya kukumbuka kitu, jambo lilie lina mshangaza sana
Sabrina hakika alijua kuna kitu kimetokea hapo kati kati sio bure, waliweza kumsha wishi ili waweze kuondoka maeneo hayo, kwa bahati nzuri alikubali, bila kujua kuwa anaenda Dar es salaam.
Waliamini kitendo cha kupatikana kwa Ramsey kinge kua usha hidi tosha mahakamani kwaio walikua na kazi moja tu kufanya juu chini kurudisha kumbu kumbu za Ramsey, jambo hilo linakua gumu sana kwao, mpaka usiku unaingia hawa kuweza kufanya lolote lakini hawa kutaka kumruhsu aende kwa Leila,
Kesho yake asubuhi na mapema wali panda nae basi la ABOOD na kurejea jijini Dar es salaam huku bado wakiwa wana mkumbusha matukio mbali mbali yaliyo pita. Mwisho wana amua waende nae mahakamani ivyo ivyo na kuamini wenda ata kumba kitu chochote kile.
“huyu hapa Sophy, humkumbuki, mtoto wa baba mkubwa Molito Yule mwandishi, Ramsey kumbuka, mimi dada yako Loydah, angalia picha zetu hapa tulikua tuna mapengo na huyu MJOMBA HALFANI SUDI”
Kweli Ramsey kila alipojaribu kukumbuka kitu hakuweza hata kidogo,
Muda wa mahakamani ulifika na watu kuanza kukusanyika ndani, Prosper alitamani kukimbia alivyio muona Ramsey , ila hakutaka kuonesha hali yoyote ile ya wasi wasi, Ramsey alikua amekaa akisikiliza kila kitu, taratibu kumbu kumbu zilianza kumrudia baada ya kumuona Prosper akiongea ila bado hakukumbuka alimuona wapi.
Baadae alipanda Sabrina akisimama kama wakili , na kumpa Ramsey uwanja aweze kupanda na kuongea ukweli wote, japo hakuwa na uhakika kama angeweza kuongea lolote lile, mahakama ilikua kimnya sana kila mtu alitaka kusikia kile anacho taka kusema Ramsey ili hukumu itolewe,
Ramsey alipanda kizimbani na kuanza kumwangalia kila mtu, baada ya kuongea alianza kulia jambo amabalo lili mshangza kila mtu,
“Pr,,,,speer, mimi sija wahi kukuuuzia duk….”
Nguvu zilimuishia Ramsey huku akitetemeka sana kama mtu mwenye kifafa na pale pale kupoteza muhimili wa kusimama na kudondoka chini, hakuna mtu aliyeelewa kwa nini Ramsey kadondoka lakini kilicho washangaza ni baada ya kumuona anavuja damu puani huku akiwa chini, haraka haraka walimchukua na kumuwahisha hospitali,
Hakuna hata mmoja wao aliye jua nini kili mpta ramsey walimfikisha Hospitali ila majibu ya daktari yana zidi kuwa changanya akili zao na kushindwa kuelewa nini wafanye.
“mgonjwa wenu tume mkuta ana kansa ya UBONGO, kutokana na kutumia madawa makali sana, na kufanya mshipa wa nyuma ya MEDULA OBLONGAT kupata michubuko na majeraha ndo maana damu zina mtoka puani”
Loydah na Sabrina waliangua vilio hospitalini hapo sababu walijua nini maana na ugonjwa huo wa kansa, kuwa hauna tiba.
Kweli majibu hayo wana shindwa kuyapokea kwa wakati huo, yalikua ni majibu ya kutisha mno! Majibu ambayo yaliwa fanya kila mmoja wao aanze kulia, waliijua fika nini maana ya kansa ya ubongo, furaha waliyokua nayo ya kuwa na Ramsey duniani ilianza kuyeyuka kama barafu liliwekwa kwenye moto!. Waliamini Ramsey ni mtu wa kufa tu, na hato chukua siku nyingi.
“dokta jaribu kupima tena , wenda utakua ume kosea”
“siwezi kukosea, nime jaribu kupima mara mbili, na hayo ndiyo majibu , lakini kuna dawa pia vile vile ata kua ana tumia”
Hayo ndiyo majibu aliyo wapa daktari wakati huo, hakukuwa na namna nyingine yoyote ile ya kufanya majibu hayo yaweze kubadilika ukweli ulibaki kama ulivyo, yote walimuachia Mungu,
Hali ya hewa ina zidi kuwa mbaya sana katika nyumba hiyo iliyo kua magomeni, wengine walisikika wakisema kuwa wenda panya alikuwa amekufa,
kila siku ilivyo zidi kwenda ndivyo hali ya hewa ilizidi kuwa mbaya sana, na kuwaumiza majirani pua zao, taratibu za kuvunja mlango zina pangwa ambapo kabla ya kuvunja mlango huo ambao ndani yake kulisemekana kuwa ndipo harufu hio ina tokea wana amua kumshikirisha mjumbe wa nyumba kumi ili taratibu izo zianze,
kweli baada ya kuvunja mlango ule nyumbani kwa Prosper walikuta akiwa juu ya kitanzi amening’inia akiwa amejinyonga na kufa pale juu ya kitanzi, pembeni ya stuli walikuta barua iliyoandikwa na Prosper.
“KWAKO RAFIKI YANGU KIPENZI RAMSEY,
NATUMAINI UTAKUWA UMESHTUKA SANA KUSIKIA KUWA LEO HII HAUPO NAMI DUNIANI HAPA, UKWELI NI KWAMBA NAONA AIBU, SIONI PA KUFICHA SURA YANGU, NAONA FEDHEA SANA, KISA TAMAA ZANGU, ,LEO HII NIMEAMUA KUJINYONGA,NAJUA HATA NINGE KUOMBA MSAMAHA, BADO NAFSI YANGU INGEINI SUTA KWANI NAKIRI ULINI TOA MBALI SANA, MIMI SIKU STAILI KUFANYA VITU AMBAVYO NILI TAKA KUVIFANYA KWAKO, NAOMBA UNI SAMEHE SANA NDUGU YANGU, ENDAPO BARAU HII IKI KUFIKIA , JUA KUWA LEO HII NIME TOWEKA DUNIANI KISA FEDHEA, NAOMBA PIA UMWAMBIE DADA LOYDAH ANI SAMEHE SANA, RAMSEY NDUGU YANGU, SIKUWAHI HATA SIKU MOJA KUFIKIRIA KUJIUA ILA LEO HII IME NILAZIMU KUFANYA IVYO, KIWANJA CHAKO KIPO, NIME KIRI KWELI PIA NILI TAKA KUKUDHURUMU KWA KUCHONGA HATI BATILI, SINA MENGI YA KUANDIKA.
WAKO NDUGU PROSPER,
Barua hiyo ili somwa na mjumbe huyo wa nyumba kumi na kushusha pumzi ndefu alimtazama Prosper ambae alikua juu ya kitanzi huku ulimi wake ukiwa nje, na kutikisa kichwa akisikitika sana. Haraka haraka simu ili pigwa polisi na mwili ule kuja kuchukuliwa.
Siku mbili nzima zili pita bado Ramsey akiwa ndani ya hospitali hiyo akipatiwa matibabu huku pembeni akiwa Loydah na Sabrina hawa hawa kutaka kucheza mbali wakizidi kumkumbusha vitu mbali mbali ili kumbu kumbu zake ziweze kukaa kama zamani, kweli zilianza kurudi na kuwa furahisha sana wote, baadae analetwa Catherine na kuoneshewa Ramsey,
“Catherin Mwanangu”
“bee Mama”
“huyu ndio baba yako”
Catherine alimuangalia Ramsey ambae wakati huo alikua ameketi juu ya kitanda na kumchukua mwanae Catherine na kumbeba huku akiwa ame mkombatia, hakika ilikua ni furaha sana kwake, kuku tanishwa na mwanae ambae alimuacha akiwa mdogo sana alimuacha akiwa ana wiki moja tangu kuzaliwa leo hiii miaka takribani mitano ime pita, hakika hakuweza kuamini,
“baba”
Catherine aliita huku akimshika Ramsey kidevu.
“naam mwanangu”
“nakupenda baba”
“namimi nakupenda mwanangu”
Japokua alikua mdogo sana ila alijua nini maana ya neno hilo, Sabrina akiwa pembeni yao alishindwa kuji zuia na kuji kuta akilia machozi na kutoka nje sababu alijua vizuri ugonjwa wa Ramsey ambapo muda wowote ule anakufa na furaha yake kumuisha tena, alikua nje na kuegemea ukuta akilia Loydaha alikuja na kuanza kumbembeleleza, ki ukweli aliumia sana hakuelewa angeishi vipi baada ya kukatishwa furaha yake aliyoipata muda mfupi ulio pita.
“sikia wifi yangu, india kuna matibabu, tufanye harakati aende India”
Alishauri Loydah
“ila ni gharama sana Loydah”
“tuta changa au ikiwezekana tutakopa,”
Kweli wazo lile linaanza kuleta matumaini mappya ndani ya mioyo yao tena, na kuwa wenye furaha tena,
Baada ya siku mbili Sabrina aliamua kurudi Moro goro ili aanze kujipanga na kuta futa pesa za kuweza kumsafiriasha Ramsey india jjijini Mumbai akiamini huko ata patiwa matibabu na kupona kabisa, ila baada ya kufika ana kutaka na dokta Leila, ambae alikua ame fura kwa hasira sana.
“Sam yuko wapi”?
Aliuliza Dokta Leila huku akiwa na jazba nyingi sana,
******
“Sabrina nasikia una mimba”?
“nani. Mimi”?
“ndio wewe”
“hapana baba mbona sina”
“Sabrina nani kakupa mimba”?
“baba sina mimba,”
“usini ongopee nita jie sasa hivi”
“baba mi…”
Kabla ya kuongea chochote kitu kingine Sabrina alipokea kofi zito lililotua juu ya mdomo wake kutoka kwa baba yake huyo, ambae alimuhisi kuwa ana ujauzito, baada ya uongozi wa shule aliye kua akisoma kumueleza kila kitu, lili kua ni jambo la aibu sana kwa mzee huyo mwenye wadhiwa wake jeshini.
Alikua ana taka kujua jambo moja tu, muhusika wa mimba ile, Sabrina aliendelea kuchezea kipigo kama mwizi aliye kutwa ameiba kambini, sio kwamba alikua hajui mtu aliye mpa mimba hiyo ila aliogopa sana
kumtaja sababu alihofia kumuweka matatani, hakika hakutaka kufungua mdomo wake kumtaja kuwa ni Ramsey ndiye alimbebesha mimba hiyo, alimpenda sana Ramsey alikua yupo radhi hata apigwe na risasi lakini sio kumtaja Ramsey,
“uwiii baba ,uta niua”
“nita jie mtu aliye kupa hiyo mimba”
“simjui”
Kipigo kiliendelea mpaka mama yake Sabrina kuingilia kati lakini hakuweza kutuliza kipigo kile kikali alichokua akichezea Sabrina amabpo alianza kuvuja damu nyingi mdomoni.
“nawewe mama Sabrina akimaliza huyu mwanao nakuja kwako, msilitee upumbavu hapa”
“utamuua huyo mtoto sasa”
“afe tu, kuliko fedhea nazopata”
Kipigo kiliendelea bila kuwa na mwisho ila bado Sabrina hakuonesha dalili yoyote ile ya kutaja mpaka alipopoteza fahamu zake na kuzirai kutokana na kipigo kile kuzidi kipimo,
Hakika mama ni mama alimchukua mwanae Sabrina huku akiwa analia machozi na kumkokota mpaka hospitalini na huduma za matibabu kuanza , baada ya siku mbili aliendelea kuwa na hali nzuri huku
mama yake akitumia busara na upole ili Sabrina amtaje muhusika wa mimba ile, lakini bado haikuwa rahisi kwa Sabrina kufungua kinywa chake ilo aliapa.
“siwezi mama kumtaja, siwezi”
“kwanini sasa”?
“baba ata muuwa”
“hawezi niambie mimi siwezi kumwambia”
“kweli mama”?
“ndio mwanangu”
“ila hapana hata wewe siwezi kukwambia”
Sabrina aliongea huku akiangalia ukutani akiwa amelala kitandani , hakika hakuwa tayari kuongea lolote lile kuhusiana na mimba ile ambayo tayari ili kua na mwezi mmoja,
Baadae aliruhusiwa kutoka hospitali na kurudi nyumbani, ila bado vita kubwa sana iliendelea baina yake na baba yake
USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni