ROHO MKONONI (11) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 8 Julai 2022

ROHO MKONONI (11)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Butu mwenyewe binafsi alishangaa kesi yake ilivyopelekwa haraka haraka mpaka kuhukumiwa kwake,hapakuwa na uchunguzi,wala nini,sasa anaelekea gerezani,hakuwa na ndugu wala familia wa kumpigania,hakuwa na rafiki wala hata mpz wa kumfariji,akaingizwa katika karandinga tayari kwa kwenda kuya anza maisha mapya ya gerezani.

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
*'NA AHIDI NITATOKA MR X SITOKUACHA HAI,SAFARI HII UMESHINDA ILA SAFARI NYINGINE UTOSHINDA NASEMA'*.

Huku akiwa kaji inamia,ndani ya karandinga lile Butu alijiwazia safari ikiendelea.
***
SURA YA TANO
LANGO LA JEHANNAMU:
Lango la geti kubwa likafunguliwa na wanajeshi walovaa nguo za magereza,karandinga lile lililobeba wafungwa likapita.

Lango likafungwa!...

Karandinga lile ilitembea kama dakika kumi na tano katika njia ndogo huku pembeni ya njia hiyo pakiwa na miti,ilikuwa ni mfano ya hifadhi ya msitu ndo wameingia.

Hatimaye baada ya mwendo ule wa dakika kumi na tano na ushee hatimaye walifika mwisho wa kale ka njia mnyohofu ,mbele yao palikuwa na jengo kubwa sana ambalo juu kidogo ya mlango palikuwa na maandishi makubwa mekundu yalosomeka

'GEREZA LA SEGEREA'.
Mbele ya jengo lile palikuwa na bustani nzuri ambayo katikati yake iliwekwa bendera ya taifa,palikuwa na uwanja mkubwa!.

Hapa ndipo wafungwa waliposimama mistarini pale ilipowabidi kukutana,na jengo lile ndipo zilipokuwepo ofisi ya mkuu wa magereza na askari wake,.

Gari likapakiwa eneo maalumu la maegesho wafungwa wote ambao walikwepo takribani kumi na mbili wakashushwa na kuswagwa kuingia ofisini!.

Walifikishwa mpaka ofisi ya mkuu wa magereza,wakapewa mavazi mekundu yalokwepo katika mfumo wa ma ovaroli,pamoja na namba za miaka yao watakayoishi gerezani pale!.

Butu akipewa namba 35 ikiwa na maana ni miaka 17 na miezi sita,kwa hesabu za kifungwa!,

Mkuu wa magereza kimuonekano alikuwa ni mzee kichwa chake chote kilijaa mvi,ila ukakamavu ulinyonya uzee wake wote,akaonekana ni mtu katili,asiye na roho ya huruma hata chembe,hakuwa mtu wa kucheka hata na askari wake,kugomba ilikuwa hulka yake!...

"Na sikia kuna polisi hapo ni yupi huyo Mshenzi?!".

Mkuu yule wa polisi akauliza kishari,wala Butu akuangaika kumjibu,mpaka askari mmoja alipo muonesha kwa kumnyo oshea kidole!.

"Huyu anao nekana ni jeuri apelekwe kwanza lango la jehanamu akakae huko masaa 24 kesho ndo tutampangia mahabusu kati ya triple a,b au c sawa?!"

"Sawa mkuu!"

Wafungwa wale wakatolewa sasa kupelekwa katika vyumba vya mahabusu yao!,kesho ndo wangeanza kazi rasmi!.

Baada ya wafungwa wale 12 kutolewa,mkuu yule akashika simu yake na kuipiga!.

"Zidu nishamuona mtu wako,masaa 24 ya awali ataishi na siafu nyoka,na wadudu wote watambahao waumao,hana siku mbili atakufa tu kwa mateso tutakayo mpa hapa ndo segerea!".

"Safi sana ancle,kijana mdogo anataka kupambana na watu wakubwa mwache ajionee".

Zidu aliongea kwa furaha,akakata simu!.

Kwa upande wa Butu si kwamba akulijua lango la kuzimu,yeye ni askari,sifa ya jengo lile alilijua,jengo hilo lilitumika kama adhabu kwa kumuua muhalifu aloshindikana,yeye anapelekwa huko,kwa uhalifu gani aliokuwa nao?,kwa kosa gani alofanya yeye mpaka kustahili kupewa adhabu kubwa kiasi kile?!....

Tumaini sasa la kuishi lilimyeyuka, roho mkononi,ilikuwa ni nadra mtu kuingizwa kule na kutoka,hakukuwa na sakafu,palikuwa na mashimo ya nyoka wakali,siafu wa kutosha,mashimo ya panya wakubwa ambao si wakawaida na juu kabisa kulikuwa na popo walotambulika kwa jina la popo mdonoo.

Unajua kwa nini walipewa jina hilo?!

Butu alijua sababu na mbaya zaidi chumba hicho kilichojengwa kwa umbo la duara,kilikuwa ni giza tupu.

Hatimaye ka mlango ka dogo kama cha kuku ila cha chuma kakafunguliwa akapewa amri aingie, akatii, kakafungwa!.

Ghafla baada ya kuzama ndani likasikika yowe!.....

Kunanini?!

Sekeseke lina ya andama maisha ya Inspekta wa jeshi la polisi John Butu roho mkononi,hatari ya kuyapoteza maisha yake anaiona kabisa,anasekwa ndani ya gereza la Segerea mbaya zaidi anajikuta katika selo ijulikanayokwa jina la lango la jehannamu,selo hiyo uki ingizwa aina stori ya kutolewa ukiwa mzima,kwanza ndani kumetawaliwa na kiza,hewa hafifu,na wadudu waumao,je Butu atasalimika ndani ya hayo masaa 24?!

Baada ya Butu kusukumiwa ndani,kamlango kale kakafungwa,Butu aliachia yowe akijua wazi sasa ndo anaenda kukutana na mateso makali,alipokewa na kiza kikali,nuru ya mwanga aikupata kuwepo ndani ya eneo lile,pua zake zikanusa harufu kali,tena harufu mbaya,ni mizoga ya watu ilooza ghafla akahisi mwili ukianza kumchoma choma,akujua ni saa ngapi alivua lile ovaroli akitoa wadudu wale aina ya siafu waloanza kumtembelea,

Wakati akiwa bado ana angaika ghafla akadonolewa usoni,hakupata tabu kugundua kuwa wale ni popo mdonoo!

Akujua afanye nini,ashike wapi,kati ya mwilini au usoni,ghafla akahisi akidonolewa mguuni,panya nao walisha anza yake.

Ndani ya dakika tano mwili wote ulimvimba,akajikuta akishindwa kuvumilia kuendelea kusimama akaenda chini,hapo ndipo wadudu walipoendelea kumshambulia vizuri,kadri muda ulivyozidi kwenda ndivyo nguvu zilivyozidi kumuisha na hali ilizidi kuwa mbaya!.

Ambacho hakutaka kusahau ni swala la kusali sala zake za mwisho,kumkabidhi Mungu mwili wake!.

Imani kwamba ataendelea kuishi ilishamtoka kabisa.
***

TRIPLE C JAIL
Eneo lingine ndani ya gereza lile la segerea juu kabisa ya lango paliandikwa Triple c,gereza hili la segerea lilijengwa kwa matabaka,na kila tabaka lilijitegemea katika makazi yake,kula kwao,na hata maaskari wake,japo mkuu wa gereza alikuwa ni mmoja,na katika kila tabaka walizungushiwa ukuta mkubwa,lango la kuzimu lilikwepo upande wa triple c,watu walokwepo katika tabaka hili ni wale waloshindikana,majambazi sugu,watu makatili au wenye kesi za kusta ajabisha,kuuana humu ilikuwa kawaida,hata maaskar wao walikuwa nunda vilevile na kila mara walikuwa na mbwa waloijua kazi yao vyema!

Kutoka triple c,kulikuwa na triple B,huku walikwepo watu wa kawaida,wezi wa kuku,wakabaji,wauaji wa kutokukusudia,wezi wa mtandao,na aina nyingine ya wahalifu wadogo wadogo,huku walikwepo askari wakawaida na tabaka la mwisho ni triple A,hawa ni class A,Vip wafungwa walikula chakula kizuri,walilala pazuri waliangalia Tv,walisoma magazeti,hawakupewa kazi ngumu,wengine hawakupewa kazi kabisa,huku walikwepo viongozi wakubwa wa dini,viongozi wa serikali,wasanii,huku ndipo ilipaswa aswekwe Insp Butu naye ndo alijua ivyo ila kitendo cha kupelekwa lango la kuzimu kukamtilia shaka.

Ndani ya ofisi ya mkuu wa magereza Dunga,mbele yake alikwepo askari wake mtihifu,dakika 15 zilishakata askari yule akiwa mbele ya mkuu wake pasina kusemeshwa chochote,dharau ya aina gani hii!,Dunga akijifanya yupo bize na game katika simu yake mguu kauweka mezani,kijana kasimama wima kikakamavu mbele yake,akumjali mpaka alipo kosea na mchezo kuisha ndipo aliposhusha miguu yake chini akaweka simu yake chini na kumwangalia askari aliyekuwa mbele yake!.

"kruta nenda triple c,namuhitaji Manzua haraka ofisini kwangu"

"Sawa mkuu!" Kijana yule akajibu kikakamavu na kujinyanyua kidogo ishara ya kutoa heshima akageuka na kuufata mlango.

Akatoka!.

Alienda mpaka lango la Triple c,akamnong'oneza mlinzi naye akarudi zake,mlinzi akachepuka kuelekea zilipo selo apatikanapo mtu huyo!...
***
Ndani ya selo moja alionekana kijana mmoja alojengeka kimazoezi akiwa kamkamata vyema kijana mwenzake kamnyongea ukutani,kimya kilitawala sauti ya mwamba yule pekee ndo ilokuwa ikisikika.

"Mali ya manzu huwa aipotei, ulinidhulumu uraiani ukajua nimefungwa utanufaika pekee yako wapi sasa leo nakuua kwa mkono wangu sheitwan wewe"

Jamaa yule alomkaba mwenzake aliongea kibabe akizidi kumnyonga mtu yule,punde maaskari wakawasili,ndipo mtu yule alipo muachia yule alo mnyonga hata ivyo hakuwa hata na punje ya uhai tena!"

"Manzu umeua tena?!"

Askari yule alokuja alio ngea kwa ukali,huku akimfata manzu gobole kalishika kwa mbele yani eneo silaha inapo chomokea.

Polisi wengine watano wakiwa nje langoni,silaha wakiziweka tayari!.

Askar yule ambaye ndiye alokuwa langoni na kuambiwa Manzua anahitajika kwa mkuu,alilifikia njemba lile na kuinyanyua gobore lake ile analishusha kichwani kwa sugu,njemba ikapangua na kuudaka ule mkono akauzungusha ukalia kaaa,kilichofatia ni yowe,punde askari wale watano wakazama kumweka kati,ila bila kutegemea jamaa alikuwa mwepesi akafurukuta akimzawadia kila askari teke lake aliye enda kumdondokea mfungwa waliyekuwepo ndani mule,...

Wote wakasimama na kukimbilia gobore zao ila kabla awajafanya kitu ikasikika nje sauti!

"Acheniii!"

Tena ikiwa sauti kali na ya amri maaskari wakasitisha jambo lile, wafungwa wote wakasimama! Kumpa heshima mtu yule,

"Nilituma niitiwe huyu mtu matokeo yake mnampiga ndicho nilicho tuma?!"

Mkuu wa gereza akauliza huku akimwangalia yule mfu alouwawa muda mchache ulopita!

"Lakini mkuu kausika na mauaji tena!"

Askari yule alopigwa wakwanza akajibu huku akishika mkono wake,

"Sicho nilicho tuma mfatilie,chukueni huo mwili mkauzike,jembe langu nifate!"

Mkuu yule akaongea kwa kiburi huku akimwangalia Manzua,aloachia tabasamu,akamfata mkuu wake nyuma,yeye kuwapiga maaskari tena maaskar watukutu ilikuwa kawaida,kuua wafungwa kwake wala akujali...

Maaskari walishindwa kumuua kwa kuwa alipendwa sana na mkuu wao,ivyo kumuua ni kujitafutia kukosa kazi na ikiwezekana kuishia pabaya.icho kikampa uhuru bedui lile kufanya atakalo,hakukuwa na wa kumbambaisha!.

Alifika ofisini kwa mkuu wa magereza akapewa ishara aketi maongezi yakafatia

"Manzu kuna kijana kwa saivi yupo ndani ya lango la kuzimu,sijajua kama atapona,ila akipona kesho atakuwa katika chumba chako mpe mateso uwezavyo hata ukimuua sawa tu!,hii ni kazi ya kwanza nakupa na sitegemei kuniangusha sijawah kukupa kazi kabla,na ukfanikiwa hili ntakupa mwanamke mzuri wa kukidhi haja zako!..."

Dunga akaweka tuo,kwa furaha jamaa yule hakuwa na la kujibu aliishia tu kufurahia,akapewa ruksa aondoke zake,gerezani kupewa mwanamke ilikuwa ni zawadi kubwa alikuwa na miaka zaidi ya mitatu ajawah kukutana na mwanamke,yeye hakuwa na muda mrefu sana gerezani...

Aliomba Mungu huyo maiti wake atoke mzima aje afie mikononi mwake!,japo akujua ni mtu wa aina gani!

Aliyekuwa inspekta wa jeshi la polisi John Butu anaingia katika sekeseke la hatari!

Dalili za kuyapoteza maisha yake zinaonekana dhahiri shahiri!

Anategeshewa madawa ya kulevya anakamatwa anahukumiwa na kuswekwa lupango,mbaya zaidi anaingizwa ndanh ya selo ijulikanayo kama lango la jehannamu,hakuna historia ya kuingia huko na kutoka ukiwa hai naye anajikuta katika mateso makali je atasalimika kweli?! Tusonge kuzidi kuburudika zaidi!

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni