FUPI TAMU (1) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 12 Februari 2023

FUPI TAMU (1)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: FUPI TAMU
Mwandishi: Edgar Mbogo

SEHEMU YA KWANZA
Siku iliyo zaa mambo na kizaa zaa, siku ambayo sito kaa ni isahau, ilikuwa ijumaa, siwezi kuisahau japo nilikuwa mdogo sana, ilikuwa ijumaa ya yapasaka, mwanzoni mwa mwezi wa nne, sikumbuki tarehe, ila nakumbuka sikukuu yapasaka, sababu uwa napenda sana siku kuu, asa kipindi hicho cha utoto, anasimulia shuhuda wetu, bwana Prosper, wacha umsikie mwenye akisimulia mkasa huu.

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI

SASA ENDELEA...
Ilikuwa mwaka tisini nambili, mwezi wan ne, ijumaa ya pasaka, wakatolic wanaiita ijumaa kuu, mwanzoni kabisa mwa mwenzi wanne, yani week ya kwanza ya mwezi huo wa nne, wakati huo nilikuwa na miaka kumi na moja tu! nilikuwa nasoma darasa la tatu, wakati huo tunaishi Mbezi kwa Yusuph, mita kama mia tano toka barabara kuu ya morogoro, kipindi hicho apakuwa na nyumba nyingi kama ilivyo sasa, nyumba zilikuwa moja moja, zikipakana na vichaka na mapori madogo madogo, ilikuwa mida ya mchana, nilikuwa mimi na kaka yangu mkubwa Denis, tunatoka nyumbani, tunaelekea kanisani, siunajuwa mambo ya ijumaa kuu.

Nakumbuka ilikuwa imepita week moja tu! toka kaka amekuja likizo fupi ya pasaka, akitokea songea alikokuwa anasomea udoctor, kwenye chuo cha Pelamiho, kinacho milikiwa na wazungu wakatolic, (kipindi hicho, sijuwi kwa sasa) ukweli nikwamba kaka alikuwa kama mgeni hapa mtaani, sababu muda mwingi akuwa anakaa hapa nyumbani, mimi na kaka tumepishana miaka kumi na mbili, wakati mimi na miaka kumi na moja yeye alikuwa anamiaka ishilini na tatu, hapa katikati kulikuwa na dada zangu wawili na kaka moja, jumla yetu tulikuwa watano, hao wengine kipindi hicho walikuwa mashuleni, sababu walikuwa wanasoma bweni, ata Sophia nilie mfwatia, nae alikuwa anasoma ST Joseph huko hanga monaster songea, kipindi hicho alikuwa darasa la sita.

Nakumbuka asubuhi yake kulinyesha mvua kubwa sana na kutengeneza vidimbwi, na vibwawa vidogo vidogo, baba na mama wao walisha tangulia kanisani na gari lao, walikuwa wanamiliki aina ya volxwagon, watoto wenzangu walikuwa wanaliita mgongo wa chura,

Sasa basi, wakati tunavuka kwenye nyumba moja, ambayo ndio tungeweza kusema jirani zetu, sababu akukuwa na nyumba nyingine kati kati yetu, nika shangaa kumwona kaka Denis akitazama nyumba ya jirani kwa mshangao, nikajuwa anatazama gari la kina Eve, ambalo lilikuwa linatoka pale kwao, lakini aikuwa hivyo nilivyo tazama vizuri, nikagundua kuwa kaka Denis alikuwa anawatazana wakina Eveline na mama yake mdogo, waliokuwa wanakuja kwa miguu, upande huu tuliokuwa sisi, wakiwamevalia vizuri sana, (nikawaida ya mama mdogo kuvaa vizuri) wote walikuwa wanalitazama gari lao, aina ya suzuk pajero, (gari la kifahari kwa kipindi hicho) ambalo lilikuwa linaondoka, pale kwao, taratibu likikwepa vidimbwi vya maji, huku Eveline na mama yake mdogo, wakilipungia mkono, huku kaka akimkodolea macho ya kustaajabu, mama mdogo wake Eveline, nikakumbuka kuwa kaka akuwa anamfahamu mama mdogo, (ndivyo na mimi nilivyo kuwa na mwita mama mdogoeake Eveline) kutokana kuwa mama mdogo, siyo mkaaji sana, wa hapa mbezi, yani kwa kina Eveline, japo nilikuwa ni mdogo kwa umri, lakini na kubari kuwa, mama huyu alikuwa ni mzuri sana, na anavutia kwa kula mwanaume, ata mimi na nautoto wangu alinivutia.

Gari lilipo fika usawa wetu, nika gundua kuwa ndani yake alikuwepo mama na baba Eveline na dada yao wa kazi, awa ndio majirani wetu, wa karibu sana, na awakutupita moja kwa moja, baba Eveline, ambae alikuwandie dereva aka lisimamisha lile gari, karibu yetu, “ujambo bwana Denis” alisalimia baba Eveline, akimlenga kaka yangu, ambae alikuwa amenishika mkono, “sijambo shikamoo mzee” kaka uwa anapenda kuamkia japo baba Eveline, alikuwa nikijana, lakini ata hivyo alikuwa mkubwa kwa kaka, kama ilivyo kuwa kwa mke wake, kwa mkadilio, ningesema wana miaka 34, “marahaba” waliitikia wote kwa pamoja, huku mama Eveline, akiongeza,

“naona doctor umekuja kula pasaka” alisema mama Eveline, nae ni mzuri kiasi flani, lakini siyo kama yule mdogo wake, yani mama mdogo, walio zidiana miaka sita, yani yule alie kuwa anakuja na na Eveline, wakionekana kuulamba kwa mtoko, yeye alikuwa na miaka ishilini na nane, na hapo kati kati yao kulikuwa na kaka yao, alie kuwa na miaka 31, ila kwakipindi hicho alikuwa South Africa, ana endelea na biashara zake, ambazo zilimsaidia sana, pamoja na kuwawezesha ndugu zake wawili, yani mama Eveline na mdogo wao ambae tulikuwa tuna mwita mama dogo, ambae ndie huyu alie kuwa na Eveline, “ndiyo nimekuja toka jumamosi” alijibu kaka Denis, ambae upole ni tabia yake, wakati huo mama mdogo na Eveline, walikuwa wanazidi kutusogelea pale tuliposimama.

Mimi nika mtazama Eveline au Eva, ambae tulikuwa tunalingana umri, na tulikuwa tunasoma wote, nakucheza pamoja, tuka tabasamuliana, kwa furaha, ukihisi kuwa safari yetu itakuwa moja.

Baada ya salam na maswali na majibu, mwisho baba Eveline akasema, “Denis sisi tunaelekea morogoro, kwenye easter conference tunarudi jumatatu, naomba uwe unapita pita hapa nyumbani, kutazama usalama kwa awandugu zako” kaka akuwa na shida, aka kubari na kuahidi kufanya hivyo, kisha wakina baba Eveline wakaondoka zao, huku wakiwa wamejaza mabegi kwenye gari lao, ambalo lilijaa kiasi kwamba wawili awa, wange kosa lift ya kwenda huko waliko kuwa wanaenda.

Naam mala baada ya wakina baba Eveline kuondoka, iliwaona kaka na mama mdogo wana tazamana, kama vile kuna jambo wanataka kuambizana, lakini kila mmoja akasita, na kushindwa kuongea, wakaishia kutabasamuliana, hapo mimi na Eveline tukawa tuna sikilizia, kuona wataanzaje kusemeshana, au wata chuniana, unajuwa kwanini, ebu sikia kwa umakini sababu ambayo ilitufanya tuwe na hamu ya kuwasikia awa wawili wakiongea.

******

Sababu ni kwamba, toka huyu mama mdogo alipo kuja hapa kwakina Eveline, zilikuwa zimepita week mbili, na hii ingekuwa ya tatu, hivyo kaka akuwa anamfahamu, maana safari hii mama mdogo, ndiyo alikuwa amesaana tofauti na zamani ambapo alikuwa anakuja na kuondoka, alikuwa akiongozana na mbaba mmoja hivi, ambae wakina Eveline walikuwa wanamwita baba mdogo, wakitokea kigamboni, walikuwa wana kuja na gari lao, nakumbuka kwa muundo wake na jina la kwanza, tulikuwa tuna liita Toyota Double cabin, sababu lilikuwa na sehemu mbili ya kukaa watu, na nyuma lilikuwa wazi, kwaajili ya kuwekea mizigo, na pengine kubebea abilia, katika hali ya shida.

Nili mfahamu vizuri mama mdogo, ambae jina lake ni Irene, kutokana na kwamba muda mwingi nilikuwa na shinda na Eveline, kama siyo nyumbani kwao, basi nyumbani kwetu, tukicheza michezo mingi tu! ikiwemo ile ya kuitana baba na mama, tukiweka makopo yetu na kuigiza tuna pika na kula kama mume na mke, ilifiki kipindi ata wazazi wetu, ambao ni marafiki sana, wakawa wanatuita wakwe, wakitania kuwa mimi ni mchumba wa Eveline.

Safari hii tokea mama mdogo afike pale mbezi kwa Yusufu, yani nyumbani kwa kina Eve, akiwa peke yake, bila yule mwanaume wake, yani baba mdogo, sikumwona akienda kazini, wakati alikuwa anafanyazia kazi mamlaka ya mapato, na kwafedha alizo kuwa nazo kipindi hicho mama mdogo, siyo wa kukaa kwa dada yake muda wote huu, lakini kwa hali ya utoto, sikuweza kujiuliza sana, ila nilicho kifahamu, nikwamba, kwa uzuri na umalidadi wa ma’mdogo Irene, vidume avikuwa mbali, vilifukuzia kwa udi na uvumba penzi la mwana mke yule, ambae ni mzuri kweli kweli, kila mala vikiwa avipungui nyumbani kwa kina Eveline, basi vingekuja na kuomba kuonana na madogo, na kusimama pale nje wakiongea kwa muda mrefu, na mwisho wasiku wakaondoaka wakiwa awaja ambulia kitu, yani walikuja watu wa aina mbali mbali, wakiambatana na vijizawadi flani flani ambavyo, ni kama vile vinguo vizuri vizuri, mikate na choklet bila kusahau pipi, ambazo mimi na Eve, tulikuwa tuna pewa na kuvi kamua kisawa sawa, ila walitukela mabishoo, wao walimletea mauwa rose na card, lakini hao wote waliishia kupewa karenda za kupewa majibu yao, kipindi hicho kutongoza ilikuwa ni kazi ngumu kidogo.

Tena uwa tulikuwa tuna penda sana kumsindikiza mamdogo, kila sehemu anapoenda, asa mbezi anapoenda kutembea au kununua vitu, maana tulikuwa tuna ambulia offer za pipi nazani wengi amzifahamu, zile za sukari ambazo zilikuwa na rangi rangi, biscuit na vitu vingine vingi, ambavyo mama mdogo Irene alipewa na wanaume au kununua kwa fedha alizo kuwa anapewa na wanaume hao,

Nakumbuka siku tatu zilizo pita, kabla ya leo, (siku ya ijumaa kuu) ma’mdogo alituchukuwa mimi na Eveline, tukaenda mbezi, lakini wakati tuna karibia barabarani, ambapo nyumba na makazi ya watu, zilikuwa nyingi, sambamba na maduka, kuna jamaa mmoja ambae kwa umri anaweza kuwa kama baba yake Eveline, alitufwata na kuanza kuongea na ma’mdogo, tuna mfahamu sababu ni muuza duka, na mala nyingi sana uwa ana mwongelesha ma’mdogo, na kumpatia ela, napengine sisi kuambulia pipi, kutoka kwenye duka lake,

“Irine, mbona jibu langu unanizungusha, yani week ya pili sasa, kama unashindwa kuniambia moja kwa moja, we! niandikie ata kwenye kikaratasi alafu watume awa watoto waniletee” alisema kwa sauti yenye rafudhi ya kipemba na yakubembeleza yule jamaa, ambae na mfahamu vizuri, uwa anauza moja ya duka kubwa, kati ya maduka yaliyopo pale mtaani, kwa Mpemba, “unajuwa sipendi nikupe jibu ambalo litakufanya ujisikie vibaya” alijibu mama mdogo, ambae kwa watoto watukutu kama John bonge, angesha mtamani na kusimamisha dudu, maana alikuwa mnono, kuanzia hips na makalio, tumbo dogo, mguu wabia, zile chupa za zamani, kifua cha wastani tumbo dogo, vilivyo fanya shape yake kuwa ya coca cola, zamani kuna mwanamziki wa Jamaica aliimba coca cola shape, (search you tube unaweza kuupata)

“ok! Irine, sasa chukuwa hii japo kidogo, lakini utatumia siku kuu, mimi nita kuja ijumaa usiku, maana shemeji yako aliniambia anasafiri kwenda morogoro, na kama utaitaji chochote niambaie” alisema yule jamaa, ambae duka lake lilikuwa limeandikwa kwa Mpemba Shop, hivyo watu wengi uwa wanamwita Juma Mpemba, huku akimpa Irine, yani mama mdogo kitita cha fedha noti za shilingi mia mia, sikujuwa ni kiasi gani lakini baadae nika juwa kuwa zilikuwa ni shiringi elfu moja, zilikuwa na thamani kubwa, kipindi hicho, maana anakumbuka, nguo yangu ya sikuku mwaka ule, ilinunuliwa kwa shilingi mia mbili, nilimwona ma’mdogo anashangaa kwa kiasi kukibwa cha fedha alicho patiwa na na Juma Mpemba…

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Usisahau Kunipa Sapoti kwa Kuyabonyeza ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Burudani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni