JINI HUSNAT (1) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 18 Februari 2023

JINI HUSNAT (1)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI
JOHN VERGAN kijana anayemiliki kampuni kubwa na mwenye mafanikio makubwa katika maisha yake anadondokea katika penzi la mtoto mrembo mwenye asili ya kishombeshombe HUSNA ambaye ni jini!

VERGAN akubali kuwa na HUSNA baada ya kugundua si binadamu heka heka,vituko,uzuni vinamuandama je atafanikiwa kuokoka katika kisanga cha jini huyo mpole na mwenye hasira za karibu?

fuatana nami mwanzo mpaka mwisho wa riwaya hii itakayokuburudisha-..,..

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
TUANZE: 1
Ulikuwa ni ukumbi mkubwa ulojaa watu wenye hela zao, kila starehe iliyopo katika dunia hii ilikwepo hapo kasino ilo lilijaa wadachi,waindi,

walokuwa wakijiuza.

mziki mkubwa ulikuwa ukiendelea kuwaburudisha wateja wa club hiyo

kulikuwa kuna walinzi wa kutosha,walokuwa tayari kupambana na kiumbe chochote kitakachotaka kuleta shida

gari aina mbali mbali za kitajiri ziliingia na kutoka na wasichana warembo ni ukumbi ulosifika kwa matanuzi yote uyatakayo

JOHN VERGAN kama mwenyewe alivyopenda kujiita alikuwa counter akitupia pombe yake taratibu!

machangudoa wachache walijipitisha mbele yake lakini ilo wala akulijali wengine awakuishia kujipitisha tu kwani walimfata na kutaka kutoa company

lakin VERGAN hakuwa tayari, mawazo yalitawala kichwa chake aligubia bia kwa fujo aikujulikana kipi kilichomtesa kijana huyo mwenye umbo la wastani

si mrefu sana wala si mfupi sana,maji ya kunde mwenye body sex mwili wa mazoezi alikuwa na kila mvuto wa kimapenzi kwa mwanamke amwangaliaye!

wanawake wengi sana walimmezea mate lakin moyoni mwake alikwepo mwanamke mmoja tu MOURINE

huyu ndo alomfanya VERGAN Agubie ile bia kwa hasira na hisia tele MAPENZI yalimtesa alimpenda mtu asiyempenda tena secretary wake

macho yake makubwa yaliyozungukwa na nyuzi nyembamba nyeusi yalitua mkononi mwake alivaa saa ya dhahabu iliyosomeka ni saa sita na nusu usiku akashusha pumzi taratibu ni wazi alishachoka na usingizi ulishaanza kuyanyemelea macho yake kilevi kilishaanza kumlevya

Akaishika simu yake na kuibonyeza tarakimu kadhaa akaiweka maskioni....

"simu unayopiga haipatikani tafadhali jaribu tena badae"

ndiyo kauli ilojibu upande wa pili JOHN VERGAN akakunja sura kwa hasira,akaachia mguno wa fedheha

Akashika chupa yake na kugubia kile kinywaji alipoishusha chini ilikuwa tupu

Kwa vyovyote muda ule MOURINE asingeweza kuja

Akaamua kujinyanyua zake akiwa anapepesuka taratibu na kuelekea nje kwa hatua fupi aliendea gari yake na kujipakia ndani

toka jioni alikwepo katika hoteli ile mpaka muda ule aliiwasha gari na kuiondoa kwa kasi.

*************

MOURINE msichana mrembo kiumbo na secretary wake VERGAN akiwa ndani ya gari yake jioni hii moyoni mwake alikuwa na raha sana! kitendo cha BOSI wake kumuitaji hotelini kilimpa faraja,ni kweli alimpenda bosi wake yule, na bosi wake alishamwonesha ishara zote za kumpenda,

Hakutaka kumkubali kwa kutopenda kuonekana mrahisi ila siku hii ya leo alijihisi hali flan si ya kawaida alijihisi KUMPENDA na kuitaji kuwa pamoja naye kimapenzi hisia zile zikamfanya aongeze mwendo wa gari lake kumuwai mwanaume yule

Lakini ghafla akiwa katika mwendo mkali akakatisha mwanamke mrembo mbele ya gari,

MOURINE akajaribu kupiga break huku akiachia yowe ns kufumba macho yake ila breki ikakataa na gari likamvaa dada yule

MOURINE akiwa kachanganyikiwa huku alitetemeka baada ya kujiisi kumgonga mtu yule akashuka kwa speed mpaka mbele ya gari lake

AKUKUWA NA MAITI WALA MDADA MOURINE akashtuka!

kwa haraka akarudi garini na kujaribu kuwasha gari GARI LIKAGOMA, akazidi kuchanganyikiwa

Akashika simu yake nayo kwa ajabu ikawa imezima chaji,safari ya MOURINE ikawa imefia hapo.

************

BADO JOHN VERGAN moyo wake ulijaa simanzi ghafla akiwa kwenye mwendo wa wastani mbele yake akamuona msichana mrembo,

msichana alozivuta na kuziamisha HISIA zake akazidi kupunguza mwendo wa gari na alipo mfikia dada yule kabla ajamsemesha dada yule akamuwahi

"kaka naomba lifti"

VERGAN akujibu swali lile kwani akili yake ilikuwa katika umbo zuri la mrembo yule!

umbo namba nane,mwenye asili ya kiindi akika alikuwa na mvuto wa ajabu,

"mimi naita JOHN mwenzangu sijui unaitwa nani?"

dada yule ndani ya gari alikaribishwa na swali

"MIMI NAITWA HUSNAT"....

Macho ya VERGAN yalikuwa katika mapaja mazuri yalokuwa wazi wakati huo,

binti yule aliyejitambulisha kama HUSNAT alivaa kimini kidogo kilicho acha mapaja yake wazi! kutokana na msukumo wa pombe VERGAN alijikuta akishindwa kuzizuhia HISIA zake nzito kwa dada yule!

akamtongoza!

dada yule akuwa na kizuizi VERGAN akimchukulia kama changudoa akaelekea naye katika nyumba yake,

akiwa na mwanamke yule ndani ya gari alipania kulala naye usiku mzima katika jumba lake lile akilifaidi penzi lake!

Akazidi kuongea mwendo kurudi afike haraka!...

LAITI ANGEJUA!?....

**************

Ilikuwa ni nyumba kubwa na ya kifahari gari aliyepanda VERGAN na msichana mrembo HUSNAT iliingia mpaka parking

VERGAN akiwa kamshika mkono binti yule wakatoka na kuelekea sebuleni ambapo awakukaa sana wakaelekea chumbani

wakapanda kitandani kila mmoja akionekana kumuitaji mwenzake zaidi!

VERGAN katu akuziona kwato zilizokuwa katika miguu ya bibie yule!

Pia hakuyaona macho yake ya kung'aa katika giza kwa macho yake ya kawaida aliyaona kawaida!

wakazama penzini!

penzi ambalo katu VERGAN hakuwai kulipata kwa binadamu wa kawaida,

penzi liliyomlevya na kumpa usingizi mzito,baada ya VERGAN kulala jini HUSNAT akuwa na muda wa kupoteza akavaa nguo zake zote akanyoosha mkono wake juu barua ikatokea akaiweka pale kitandani na GHAFLA AKATOWEKA!!!

Ilikuwa ni alfajiri tulivu ilojaa kibaridi VERGAN alipapasa mbele yake hapakuwa na mtu, akafumbua macho yake taratibu kajua cha asubuh kalitokeza kutarifu sasa kumepambazuka,

VERGAN alishtuka na kucheki mlango

"UKUFUNGULIWA"

Akakumbuka juu ya kukutana na HUSNA jana

"au nilikuwa naota?! hapana!"

bado VERGAN alikuwa katika hali za sintofahamu akakurupuka kitandani pale akiita kwa nguvu kama mweu

"HUSNA! HUSNA! HUSNA!" Bado hakukuwa na jibu! akaingia chooni,bafuni ndani kwa ndani bado akukuwa na mtu!,

vergan akiwa kama kachanganyikiwa akafungua mlango na kutoka nje alipomkuta mlinzi wake kipele

"umemuona msichana katoka humu ndani asubuhi hii?" Akauliza kwa wahka

"msichana? msichana yupi bosi?" Kipele akasaili....

"yule nlokuja naye jana usiku!"........

" Jana usiku?!"

Kipele akaoji huku bumbuwazi likimbumbukia usoni pale....

"Ndiyo yule binti nloshuka naye kwenye gari?!"

"No Bo's!,nliona ukishuka mwenyewe hukuja na mtu kaka"

"What?!"

"Ndiyo!,tena ulikuwa full ukipepesuka ukuja na mtu bosi"

"Mfyuuuuu!"

Vergan akaachia msunyo ulosindikizwa na mguno hafifu wa mfadhaiko

Ni wazi alizidi kuchanganyikiwa

!,akaenda sebuleni akajitupa sofani!,mawazo yakaanza kupishana kama mishale ya saa!!!

"uyu binti atakuwa kaenda wapi yarabi?! mbona mlango ukufunguliwa? mlinzi naye anasema sikuingia na mtu jana usiku au nilikuwa naota? hapana hapana hapana nilimpa binti lifti HUSNA alinambia anaitwa HUSNA nikampenda! nkamchukua nkaja naye akanipa penzi tamu ambalo sijawai kulipata alafu! alafu ikawaje? HUSNA! HUSNA! hapana si ndoto kuna kitu"

alijiuliza VERGAN na kujijibu mwenyewe akajinyanyua na kurudi tena chumbani

macho yakadondokea kitandani

Kitanda kilikuwa shaghala baghala kuonesha kwamba usiku kucha kilitumika,hilo likazidi kumpa picha sahihi kwa kile akiwazacho

macho yake yakatua mezani akakuta barua imefungwa vizuri

Akastaajabu!!!...

Kwa hatua fupi fupi akasogea pale kitandani huku mkono ukiwa unatetemeka akaifata barua ile na kuishika ilinukia harufu nzuri!,

harufu ya manukato,alikumbuka manukato hayo ni ya HUSNA

akaichukua ile barua na kuifungua na kuanza kuisoma naaam macho yalimtoka pima

"DEAR SAMAHANI! KWA KUONDOKA BILA KUKUTA HARIFU NILIHITAJIKA HARAKA NYUMBANI NA WAZAZI WANGU WAKWE ZAKO HASUBUHI NJEMA WAKO KIPENZI HUSNA NTARUDI"

VERGAN akashangaa!,ilikuwa lazima ashangae!

"aliitajika nyumbani!?,alipitia wapi?! aliondoka saa ngapi?!!"

bado maswali mfululizo yalizidi kumuandama akairudia tena kuisoma ile barua yenye hati nzuri ila akupata majibu aloyaitaji akaikunja barua yake na kuirudisha pale mezani alitoka akaenda kuoga, kuswaki, kuvaa nguo za kazini dakika chache zilizofatia zilimkuta mezani akinywa chai aloandaliwa na mfanyakazi wake aliyetambulika kwa jina la Jasmin.

alipomaliza alinyanyuka na kuliendea gari lake akapanda na kuelelea kazini alipofika alimpita secretary wake MOURINE bila salamu na kuingia ofisini kwake.

Dakika chache baadaye Mourine akaingia ili kumuuliza kama aliitaji amletee chai tofauti na matarajio yake VERGAN akaanza kushusha lawama

"hivi MOURINE kwa nini unantesa hivi? kwa nini jana ulin'danganya na ukuja? kama ulikuwa utaki si ungenambia kuliko kuniweka mahali namna ile mapenzi ayalazimishwi Mou sotokulazinisha......

MOURINE huku akiwa anatetemeka akamwangalia bosi wake!

"hapana bosi niliaribikiwa na gari"

"comon MOURINE kwa nini ukunambia kwa simu nikajua?"

"simu nayo iliisha chaji bosi...."

Wakati wakiendelea kuongea ghafla simu ya VERGAN ikaita alipoangalia kwenye scrini ilisomeka HUSNAT.

Ubongo wake ukatingishika! akampa ishara MOURINE aondoke

Kabla ajaipokea maswali yakaanza kutiririka katika kichwa chake!

"nani kampa namba zangu?"

aliwaza alikuwa na uhakika akumpa wala akuserv namba zake, ili kupata jibu akaamua kuipokea simu ile....

"alooo!" VERGAN alisema

"vipi sweet za kazi" sauti nyororo kama kinanda iliuliza VERGAN akaipuuza Na kwa hasira akamuuliza

"nani kakupa namba zangu?"

"si wewe sweet umenipa jana?"

"mimi sijakupa namba zangu"

"umenipa beby"

"sijakupa"

"umenipa!"

"ok ulikuwa unasemaje?" VERGAN aliuliza kwa hasira

"nilikuwa naitaji tuonane" HUSNA alisihi

"siwezi kuonana na wewe" VERGAN alijibu kwa jeuri akapokewa na kicheko kitamu kisha sauti laini ikafatia

"basi my love ntakuja hapo kazini jioni tuondoke wote!"

hapo hapo akakata simu ubongo wa VERGAN kwa mara nyingine ukatingishika idadi ya maswali yasiyo na majibu yakatiririka!

"uyu ni binadamu au jini?,anapafahamu hapa kazini?"

bila kujielewa akaanza kusarch namba ya HUSNA kusudi azipige

NO AZIKWEPO!!!

hakuweza kujizuia kutetemeka akaziangalia kwenye recevid

kwenye recevd azikwepo!!!

wakati akiwa katika mawazo ya sintofahamu ghafla meseji ikaingia katika simu yake

"usiwaze sana dear utaumwa na kichwa"

namba zilikuwa na jina tu

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni