JINI HUSNAT (2) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 18 Februari 2023

JINI HUSNAT (2)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
hakuweza kujizuia kutetemeka akaziangalia kwenye recevid

kwenye recevd azikwepo!!!

wakati akiwa katika mawazo ya sintofahamu ghafla meseji ikaingia katika simu yake

"usiwaze sana dear utaumwa na kichwa"

namba zilikuwa na jina tu

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
JINA BILA NAMBA?

akazipiga zikakataa!

Azikutambulika na mtandao ule wa simu!

Lakini si ndo hizo zilizomtumia msg,?!

moyo ukaanza kumwenda mbio akaishika simu ya mezani na kumpigia secretary wake MOURINE

"naomba mwambie ZUBERI namwitaji ofisini kwangu" baada ya maneno Yale akakata simu

dakika chache badae ZUBER aliingia

Vergan akamwonesha ishara aketi

alikuwa ni kijana mrefu,alikuwa ndo meneja baada ya yeye ZUBER ndo alikuwa chini yake alimwamini kijana yule alikuwa ndo mshauri wake,siri zake ZUBERI alizijua,siri za ZUBER naye alizijua

Kwa kivipi walikuwa ni zaidi ya marafiki waloshibana,waloshauriana....

Zuberi akupata tabu kugundua bosi wake yule au rafiki yake yule yupo katika matatizo makubwa

Hiyo ni baada ya kuisoma simanzi ilotawaliwa na majonzi pamoja na woga katika uso wake ule

"Nimeitikia wito bosi"

Zuberi akatamka kwa sauti ya upole,akimwangalia kwa mashaka Vergan

VERGAN alimweleza ZUBERI kila kitu!,akimwacha kijana yule katika mshangao wa hali ya juu wa kutokuamini Yale aelezwayo....

Mwisho akatoa ushauri wake akitanguliza pole,

,"dah pole bosi huyo atakuwa ni jini tu! kubali ukatae! kwanza embu nioneshe hizo msg zake! maana siamin kabisa!"

VERGAN akatii na kuchomoa simu yake mfukoni akaanza kutafuta zile meseji inbox

'MESEJI HAZIKWEPO'

na anakumbuka akuzifuta kabisa! bumbuwazi likauvaa uso wake

"kah meseji azipo kak!"

"nini?" ZUBER akaoji kwa mshangao

"sijazifuta lakini nashangaa kutoziona!"

"basi BOSI jibu ndo ilo huyo atakuwa ni jini mahaba!"

"sasa nfanyeje rafiki yangu?"

"kuna mtaalamu namfahamu ntakupeleka"

"hapana best mim ni msomi siamini hao watu wengi wao matapeli....."

Katika vitu ambavyo JOHN VERGAN akuvipenda ni kuamini ushirikina

"mganga wa kienyeji!"

ZUBER alijaribu kumbembeleza lakin VERGAN akuwa tayari,mwisho akakata na tamaa!

Zuberi akaaga akihaidi kurejea baada ya kupata wazo lengine, akamwacha bosi wake katika mawazo Yale....

"ina maana uyu ni mtu au jini?" bado maswali yasiyo na majibu yaliambaa katika kichwa chake.

"sura ya HUSNAT ikamjia kichwani mwake wakati walivyokuwa wakifanya mapenzi"

miguno ya kimapenzi na hata sura yake alivyoikunja,utamu alokuwa nao,HISIA zikampanda,na ghafla tabasamu likamponyoka.

"atakuwa ni binadamu anacheza na akili yangu tu!"

akajifariji upendo moyon mwake ukafumuka kama mvua za masika

ALIANZA KUMPENDA!.

Akashangaa kumpenda ghafla kiasi icho! moyo wake aliujua vyema.

Aukuwa wa mtu aliyeyaendekeza mapenz akupenda kujiumiza kichwa kama kwa MOURINE aliyepanga kumuoa,lakini MOURINE anamzingua,

alipobahatika kumuona HUSNA akajua jibu lake limepatikana lakini vitabia tabia vyake vinamshangaza naye ni jini?

aoe jini?!!

"no siwezi kumpenda HUSNA!"

akapingana kwa nguvu na HISIA zake

ilipofika jioni wakati anajiandaa kuondoka ghafla mlango ukafunguliwa na HUSNAT akaingia na tabasamu pana usoni

Uzuri wake ulikuwa mara mbili ya mwanzo bumbuwazi likauvaa uso wa VERGA akutegemea kama angekuja kweli

mbona secretary wake ajampgia simu?

Na alikuwa kawaida mgeni kuingia bila 'secretary' wake kumpigia naye ndo amruhusu!

Lakini huyu!!!......

Verga alijawa na khofu ulochanganyikana na woga

ilikuwa lazima aogope alikuwa kavaa gauni jekundu refu lililo mkaa vyema, akaenda kuketi kwenye viti vya wageni na kumpa mkono Vergan aliyekuwa bado akitetemeka....

Mbona SECRETARY wake MOURENE ajampigia simu kumwambia juu ya mtu kumuitaji?

au akumwona? au amemdhuru? au naye ameogopa? maswali hayo mfululizo yakakishambulia kichwa chake! akakiri kutoyajua majibu yake akagutuka baada ya kuuona mkono wa JINI yule

"vipi sweet?" sauti tamu imtoaye nyoka pangoni ilipenya katikati ya ngoma ya masikio yake ikawa burudani tosha ndani ya mfumo mzima wa masikio!

lakin burudani hiyo katu aikuwepo katika ubongo wake ubongo wake ulikuwa katika tafakari zito tafakari lililomezwa na woga.

JOHN VERGAN alitaitika! alikuwa akitetemeka na kusogea nyuma mara ghafla kiti kikadondoka!

"unaogopa nini sweet au aunipendi?"

HUSNA kwa mara nyingine tena akauliza! VERGAN akujibu! akabaki kimya

"VERGA TAMBUA NA KUPENDA! NA UKIKUBALI KUWA NA MIMI NITAKUTAJIRISHA UTAMILIKI MALI NYINGI ZAIDI YA HIZI!, MAVIWANDA

,MAKAMPUNI,UTATEMBEA DUNIA NZIMA UNAVYOTAKA UTAPOKEA ZABUNI MPAKA MWENYEWE UTAZIRINGIA

LAKINI UKINI KATAA NTAKUFILISI UTARUDI KIJIJINI MASIKINI MTAOMBA HADI VYAKULA NA UTAISHI MAISHA YA MATESO KATIKA DUNIA HII UTAKUWA UKIZARAULIWA NA KILA MTU CHAGUA MOJA.....

KUMBUKA USINIKATAE KISA MIMI NI JINI!

TAMBUA HATA SISI MAJINI TUNA MIOYO YA KUPENDA KWA DHATI ZAIDI YENU NYINYI BINADAMU HIVYO MOYO WANGU UPO KWAKO WEWE VERGA AU UJAVUTIWA NA MIMI?"

Aliuliza HUSNA huku akiwa anatembea tembea ofisini mule

"hapana! hapan...."

ghafla kitasa cha mlangoni kikawa kina tingishika kuonesha mlango unafunguliwa kutoka nje

JINI HUSNAT AKATOWEKA apo apo

"bosi unaongea na nani? bosi kuna nini? bosi mbona upo chini umefanya nini?!!..."

MOURINE alimuuliza maswali Mfululizo VERGA aliyekuwa kadondokea kwenye pembe ya nyumba

"ulivyo ingia ujamwona mtu?!"

"mtu? mtu gani bosi mbona sikuelewi?"

"HUSNA! ujamwona HUSNAT?"

"Husna ndo nani bosi?"

kabla VERGAN ajajibu swali lile HUSNA akatokea na kumnyooshea VERGAN kidole mdomoni ishara ya kunyamaza,

Verga akatii,akiwa amegwaya....akamwambia MOURINE

"amna kitu MOU kaendelee tu na kaz"

VERGAN alitamka huku akinyanyuka na kujifuta futa

HUSNAT ALISHATOWEKA!

"Bosi kuna wale watu wa idara ya mapato wanasema watakuja kesho ivyo uandae risiti zote"

"sa...w ni.meku..elewa" VERGAN alijibu kwa kubabaika secretary wake akaondoka VERGA akarud kwenye kiti chake na kukaa

"KITI AKIKUKALIKA!"

alinyanyuka na kuchukua koti! lake la suti lililokuwa nyuma ya kiti chake na kulivaa,

akachukua simu na kumpigia MOURINE

"Alooh bosi!"

"Namuitaji ZUBER"

"Sawa bosi"

baada ya muda ZUBER akaingia,

"sasa wewe kijana kaa hapa ofisini mimi naenda kupumzika kidogo kichwa hakipo vizuri"

"sawa bosi"

JOHN VERGAN akachukua brufcase yake na kuondoka!,

aliitaji kupumzika aliisi kichwa kinamuuma,

katu akujua balaa alilokuwa akilifata mbele yake

ZUBER alitafuta ma file na kuendelea kuyajaza taratibu! akujua kinachoendelea yeye alikuwa na yake kichwani katika kudhihirisha ule usemi umdhaniaye ndiye kumbe siye,au rafik yako ndiyo hadui yako,

ZUBER alikuwa ni chui mwenye ngozi ya kondoo ama kweli usilo lijua ni sawa na usiku wa kiza.

na kwa upande wa MOURINE secretary wa VERGAN naye pia kiti akikukalika!

alijua bosi wake ana matatizo tu! japo akuwai kumwambia kuwa anampenda ila moyoni mwake alikiri kumpenda sana bosi wake yule!

" hapa kuna kitu na lazima nifanye kitu kumsaidia bosi wangu "

wakati akiwa anawaza hayo ghafla harufu kali ya manukato ikaanza kusikika, upepo mkali ukaanza kuvuma! vumbi lililotengeneza kimbunga cha wastani kikaanza kuingia ndani na kupeperusha ma file yale pale mezani,

makabati yakaanza kujifunga na kujifungua yenyewe na mara mtoto mzuri mrefu alovaa nguo ndefu akatokea!

Alitokea katikat ya chumba kile MOURINE akataka kukimbia akashindwa, akataka kupiga kelele pia akashindwa akabaki na butwaa

"mimi naitwa ZAIDATU BINT ROUJAT natokea ukoo wa kifalme wa kijini nimekuja kwa ajili ya msaada kwako..."

Msaada?!

"Ndio nimekuja kwa msaada ila lazima ufe"

kabla MOURINE ajafanya kitu JINI ZAIDATU akamvamia na kumnyonya damu yake.

JINI ZAIDATU baada ya kuakikisha amemuangamiza secretary yule MOURINE kwa kumfonza damu yake yote akaachia ukelele mkubwa!

kisha akatoweka!

mara ghafla MOURINE akazinduka ilikuwa kama kazinduka toka usingizini!

ila MOURINE huyu alikuwa tofauti na wa mwanzo!

macho yake yaling'aa!

meno yalichongoka mawili!

ila ghafla vyote vikatoweka akabaki MOURINE wa mwanzo!

ZAIDATU alikuwa kaingia katika mwili wa MOURINE kwa kazi maalumu! ni kazi gani? aliijua moyoni mwake.

aliendelea kufanya kazi zake kama kawaida

machoni alionekana ni MOURINE ila kumbe alikuwa ni jini hatari ilikuwa ni PATASHIKA.

Moyoni mwa ZUBER wazo lililotawala kichwa chake ni kuakikisha mali zote za VERGAN zinakuwa chini yake kwa namna gani?

ilo alikumsumbua akakwapua simu ilokuwa pale mezani na kupiga namba kadhaa akaweka mkonga wa simu yake maskioni

"MOURINE nakwomba uniunganishe na PITER"

"sawa bosi"

MOURINE aliitikia na kuwaunganisha wakaongea machache.

dakika chache zilizofatia PITER au mwanasheria mkuu wa compuny ile alikuw mbele ya bosi wake yule.

"nachotaka kuongea na wewe ni siri kukiwa na makubaliano au hata kama kusipokuwa na makubaliano!"

ZUBERI alifungua kikao kile kwa onyo kali.

"na kama siri hii ikivuja sitokuwa na kingine zaidi ya kukuua!"

"what?" PITER aliamaki

"ndiyo! ni dili litakalo badilisha maisha yetu tutakuwa matajiri wakubwa kama bosi VERGA"

"SAWA nipo tayari weka kazi mezani!"

PITER Alikubaliana na wazo la ZUBER na kuwa tayari kusikia dili lenyewe

"naitaji tutaifishe compuny hii iwe chini yetu! mimi na faida tugawane hamsini kwa hamsini"

"unasema?"

"ndiyo naitaji compuny hii iwe chini yetu"

"sijakuelewa ZUBER ni vipi tutafanikisha ili?"

"swali zuri PITER wewe ni mwanasheria wa compuny una nyaraka hati zote muhimu ni kitendo cha kuzibadilisha tu"

"tatizo itakuwa ni sahii yake"

"atatekwa na kulazimishwa kuweka sahii baada ya hapo tutamuua"

"sawa ZUBER nimekuelewa niachie nianze kazi...

JOHN VERGAN alifika nyumbani kwake na mlinzi akafungua geti VERGAN akaingiza gari taratibu.

mlinzi alimsalimia lakini VERGAN akuitikia, kichwa kilikuwa kikiwaka moto akaenda mpaka chumbani kwake na kujitupa

mara ghafla akapitiwa na usingizi wakati akiwa yupo usingizini akaota yupo na JINI HUSNA akiwa pembezoni mwa jabali palipokuwa pameota majabali makubwa wakiwa wameegemeana kimapenzi HUSNA akasema: kwa sauti ilojaa mahaba....

"dear nna zawadi yako!"

"zawad gan sweet?" VERGAN akaoji akiwa kaushika mkono wa dada yule mrembo

"funga macho yako"

VERGAN akafumba HUSNA akatoa mkufu wa dhahabu na kumvalisha VERGA

"Fungua!"

VERGAN alipofumbua macho yake akuamini akamkumbatia kwa nguvu HUSNA mkufu ule ulikuwa ukimeremeta huku ukiandika jina la VERGAN ulikuwa na picha ya HUSNA na VERGAN wakiwa wamekumbatiana,

Baada ya VERGAN kumkumbatia akamwachia ghafla akashangaa kumuona kabadilika kawa na sura mbaya ya kutisha meno yalochongoka pembe pembeni ya vichwa kucha ndefu VERGA akashindwa kuvumilia na kupiga kelele ghafla akazinduka.

"he! kumbe ilikuwa ni ndoto?"

VERGAN alitahayari alishindwa kuzuia mshangao dhahiri katika macho yake.

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni