KUTI KAVU (9) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 8 Februari 2023

KUTI KAVU (9)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: KUTI KAVU

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Mapunda alisema na maneno yake yalisikika sawia masikioni mwa Zai aliyekuwa pembeni yake. Maneno yale yalimchoma moyo kiasi cha kumfanya aangue kilio cha sauti. Akajiona kama mjinga na mpumbavu wa mwisho chini ya jua, akaliona kuti kavu alilolikalia likidondoka na yeye akiwa juu yake. Alilia sana.

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI

SASA ENDELEA...
Mudi aliiweka helmet yake ubavuni, kisha akachapa mwendo.
*****
SIKU ya Jumapili Domi aliamka asubuhi, aliamka asubuhi na mapema akafaya maandalizi yake kisha akaelekea kanisani. Siku hiyo alipanga kusali misa ya kwanza ambayo huanza saa 12:30 asubuhi. Alipanga hivyo kwa lengo la kurudi mapema nyumbani ili ajiandae na kazi za kesho ofisini kwao.

Baada ya ibada Domi aliwasha gari kurejea nyumbani, kabla hajafika nyumbani alipita kwa muuza magazeti kwa lengo la kununua magazeti ili pindi awapo nyumbani ayasome ili kujua yaliyojiri duniani, ilikuwa ni kawaida yake kutopitwa na gazeti. Alipofika tu pale kwa muuza magazeti, yule muuza magazeti alichukua magazeti manne akampelekea kwenye gari, Domi aliyapokea na kuyatupia magazeti yale kwenye kiti cha abira kilichokua pembeni yake. Akatoa pesa akampa yule muuza magazeti akaondoka.

Domi alifika nyumabani kwake, akaingia ndani, akajitupa kwenye kochi na kuanza kuyapitia magazeti yake moja baada ya jingine.

Aliposhika gazeti la kwanza, Domi alibaki mdomo wazi baada ya kukutana na kichwa cha habari kilichoandikwa; “MREMBO AKAMATWA NA KILO 6 ZA COCAIN UWANJA WA NDEGE” Domi alizidi kupagawa baada ya kuiona picha ya msichana anayedaiwa kukutwa na madawa hayo hatari ya kulevya ikiwa imeipamba habari. Alipoitazama picha ile kwa makini alibaini kuwa picha ile ilikuwa ni ya Doi, “Ooowh nooo… hapana!” Domi alimaka kwa mshangao.

Akalitupa gazeti lile pembeni akachukua jingine. Gazeti alilolichukua pia lilikuwa na habari kama ile aliyokutana nayo kwenye gazeti la kwanza, kichwa cha habri kwenye gazeti hili kiliandikwa, “MREMBO AKALIA KUTI KAVU, AKUTWA NA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE” kama gazeti la kwanza, hili pia lilikuwa na picha ileile ambayo Domi alijiaminisha kuwa ni ya Doi.

Akalitupa na hili kando, akashika jingine ambalo pia lilikuwa na kichwa cha habari kisemacho, “MADAWA YA KULEVYA TISHIO, MREMBO MWINGINE AKAMATWA” Domi hakuchoka, akiwa kwenye taharuki alichukua tena gazeti jingine ambalo lilizidi kumtisha zaidi kwa kichwa chake na picha zilizopamba ukurasa wa mbele gazeti lile, lilikuwa na kichwa kisemacho, “MREMBO MATATANI KWA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA” Domi alipoitazama picha iliyopamba habari hiyo alizidi kuthibitisha kuwa ile picha ni ya Doi, Domi alipagawa!

Ikabidi aanze kuisoma habari yenyewe, na sehemu ya habri hiyo ilisomeka hivi; “……mrembo huyo aliyefahamika kwa jina la Doi Vioja, mwenye umri wa miaka 26 kwa mujibu wa pasi yake ya kusafiria, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere akiwa na kiasi hicho cha madawa hatari ya kulevya akiyasafirisha kuelekea nchini Ufaransa.

Taarifa zaidi zinadai kuwa; kuna wimbi kubwa la wasichana wanaotumiwa kusafirisha madawa haya na mengine kwa kuyaingiza ama kuyatoa nchini Tanzania kuelekea nchi za nje.

Kukamatwa kwa Doi Vioja kumetokana na maboresho ya kiutendaji yaliyofanywa na waziri wa wizara ya usafirishaji na uchukuzi kwa kuwafukuza kazi na kuwabadirisha wengine kutoka idara moja hadi nyingine baada ya mrembo mwingine wa Tanzania kukamatwa katika uwanja wa ndege wa Afrika kusini akiwa na kilo 150 za madawa ya kulevya aina crystal methamphetamine au maarufu kama blue stones….

Mkuu wa kitengo cha kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya katika jeshi la polisi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na amesema kuwa, Doi Vioja amepelekwa mahabusu kusubiri apelekwa mahakani mara baada ya uchunguzi kukamilika….” Domi alichanganyikiwa kabisa na hakujua afanye nini kwa wakati huo. Alisimama kutoka pale kwenye kochi alipokuwa amekaa na kuanza kuzungukazunguka mule sebuleni kama mwendawazimu.

“Oowh.. noo… it can’t be” Sauti ilimtoka Domi. Akarudi pale mezani yalipo magazeti akaichukua simu yake ya mkononi, akaibonyezabonyeza baadhi ya vitufe katika simu ile kisha akaiweka sikioni, “..namba unayopiga kwa sasa haipatikani….” Sauti kutoka upande wa pili wa simu ikajibu na kuzidi kumuweka Domi kwenye wakati mgumu.

Akaitupa simu kwenye kochi kisha akawasha luninga iliyokuwa pale sebuleni.

“….msichana huyo aliyefahamika kwa jina la Doi Vioja, ambaye ni raia wa Tanzania amepelekwa mahabusu kusubiri uchunguzi utakapokamilika ili afikishwe mahakamani kusomewa mashitaka yanayomkabili…” Sauti ya mtangazaji wa kituo cha luninga iliendelea kutangaza huku picha ya Doi ikionekana bayana kwenye kioo cha luninga.

Domi alijibwaga kivivu kwenye kochi huku maneno yakimtoka, “Ooh… Doi kwa nini… kwa nini lakini?” sauti ilimtoka sambamba na machozi yaliyokuwa yakimchuruzika kwenye mashavu yake.

“Ina maana.. umeamua kuniacha ili ukafanye biashara haramu na ya kishenzi… yaani wewe uliyekuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya madawa ya kulevya leo umekamatwa na madawa hayo… kilo sita…kilo sita” Domi alizidi kuwaza.

Domi hakutaka kabisa kusadiki kuwa Doi anaweza kukutwa na madawa ya kulevya. Lakini alipojaribu kulihusisha tukio hilo na zile dola za marekani, Domi alipata tena mkanganyiko.

“Huyu amerubuniwa huyu …. Hii siyo akili yake… siyo akili yake kabisa ina maana hizi dola ni matokeo ya hii biashara?” akiwa mawazoni, Domi alishituliwa na mlio wa simu yake ya kiganjani iliyokuwa kwenye kochi, “Ngriii…ngriii…” Domi akaipokea simu na kuiweka sikioni, “Hallow baba shikamoo” Saut ilimtoka Domi.

Bila hata kujibu salamu, sauti ya upande wa pili ilionesha dhahiri kuwa ilikuwa imetwaliwa na hofu, wasiwasi na mashaka tele ikajibu kwa swali, “Una taarifa gani kuhusiana na mwanangu?”

“Mzee taarifa nilizo nazo kuhusiana na Doi si nzuri,,, magazeti yote ya leo yameandika kuhusu yeye, nimefungua pia luninga habari ni kuhusiana na yeye…Doi amekamatwa na madawa ya kulevya mzee,” Alisema Domi.

“Ina maana hukuwa na taarifa zozote kuhusiana na safari yake?” Sauti ya upande wa pili ilizidi kuhoji.

“Kusema ukweli baba mimi sikuwa na taarifa zozote kuhusiana na Doi kwa zaidi ya wiki tatu sasa” Domi alijibu, na safari hii alijibu kwa utulivu zaidi.

“Yaani huyu mtoto huyu…. Sasa ameleta tabu gani hii,” alisema mzee Vioja na kukata simu “Hallow hallow…” Domi aliita bila mafanikio.

Aliendelea kushikilia simu yake mkononi, aliitazama kama vile anaiuliza kitu kisha akabonyeza vitufe kadhaa kwenye ile simu kabla hajaiweka sikioni, “Hallow bwana Makeke….aliuliza Dominic na sauti ya upande wa pili ikajibu “Ndiyo bwana Masaka…. habari za weekend?”

“Za weekend sio njema hata kidogo bwana Makeke…. kuna tatizo… tena tatizo kubwa sana…..” Domi akaweka pumziko kidogo ili ameze walau funda la mate. Wakati anaweka tu pumziko bwana Makeke akamuwahi kwa kuuliza “ Kuna tatizo gani tena ndugu yangu?”

Dominic akajibu, “Sikuwa nimewahi kukueleza juu ya hili swala ….. ila kwa ufupi nikupe tu dokezo” “Ndiyo bwana Masaka endelea…”

“Nadhani umeipata taarifa kuhusiana na huyu binti aliyekamatwa uwanja wa ndege akiwa na madawa ya kulevya?”

“Ndiyo nimeipa na hapa mkononi nina gazeti la leo ambalo lina habari hiyo,”

“Basi siku chache zilizopita yaani kabla sijaanza kazi KWITALE…. nilikuwa nikiishi na huyo binti kama mke wangu ingawaje hatukuwa tumefunga ndoa. Hata siku niliyosaini mkataba wa kazi KWITALE yeye nilikua nimemuacha nyumbani asubuhi ya siku hiyo… lakini niliporudi nyumbani jioni ya siku hiyo sikumkuta kabisa….. na tangu siku hiyo si mimi wala wazazi wake, hakuna aliyekuwa akijuwa ni wapi alipokuwa Doi mpaka hii leo baada ya kusoma kwenye gazeti na kutazama kwenye luninga,” alimaliza Domi na kuacha uwanja wazi ili asikie au apate neno la bwana Makeke.

“Kwanza kabisa pole…. Pole sana bwana Masaka nimekusikia na nimekuelewa lakini ni vyema endapo mimi na wewe tukaonana leo kwa mazungumzo ya kina ili tujue nini cha kufanya”

“Sawa bwana Makeke mi nafikiri tusipoteze muda… hapa nyumbani kwangu kuna utulivu unaoweza kuturuhusu kuzungumza kwa nafasi, lakini pia nisikubane ….. unaweza kupendekeza mahali popote ambapo unaona panafaa kwa mazungumzo”

“Mi nafikiri uje tu hapa nyumbani kwangu, kuna ofisi ndogo ambayo inaweza kutupa faragha na wakati tunaendelea na mazungumzo shemeji yako atakua anatuandalia chakula cha mchana”

“Hakuna shida bwana Makeke… nipe kama dakika arobaini na tano hivi nitakua hapo nyumbani,” “Sawa karibu sana bwana Masaka,” wakaagana kwenye simu, na bila kupoteza muda Domi alikusanya magazeti yote aliyoyanunua asubuhi akayaweka kwenye gari tayari kwa safari ya mikocheni mahali alipokuwa akiishi bwana Makeke.
****
Doi alikuwa amejikunyata kwenye kona iliyokuwa katika moja ya vyumba vya mahabusu vilivyopo katika gereza la Keko. Macho ya Doi yalikuwa mekundu na yaliyovimba kwa sababu ya kulia kwa muda mrefu. Doi alikuwa amejitenga kabisa na mahabusu wenzake. Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza yeye kuwa eneo kama lile! Kwani tangu azaliwe Doi hakuwa amewahi hata kukamatwa na polisi wachilia mbali kulazwa lupango.

Mwanga hafifu, joto kali pamoja na harufu nzito vilizidisha tabu kwa Doi akapakumbuka nyumbani kwake Buza, mahali ambapo alikuwa amepanga pamoja na mchumba wake Dominic. Chumba alichokuwa akiishi na Domi kilikuwa na joto… lakini ni afadhali mara mia moja kuliko joto analokabiliana nalo sasa. Chumba alichokuwa akiishi na Domi kilikuwa na mbu… lakini ni afadhali mara kumi kuliko mbu hawa wa gerezani. Mbu ambao hawakujua mchana wala usiku…. Wao walichojua ni kufyonza damu ya Doi pamoja na wafungwa wengine.

Hali aliyokuwa akikabiliana nayo ilimfanya Doi ajute kwa uamuzi wake wa kipumbavu, uamuzi ambao umemfungulia milango ya jela ambamo yumo akiwa hajui nani wa kumsaidia!

“Madawa ya kulevya !” hatimaye sauti ilimtoka Doi na kusababisha mahabusu wenzake wamshangae. Doi alishindwa kuelewa jamii ingemtafsiri vipi, taswira ya Damiani ilipomjia akilini machozi yaliongezeka mashavuni mwake. Alimwona Damiani kama adui yake namba mbili baada ya Zai ambaye mpaka wakati huo alimchukulia kama adui yake namba moja.

Doi alijua fika kama asingekuwa Zai basi yeye asingemfahamu Damiani ambaye amemkalisha kwenye kuti kavu, kuti lisilo na matumaini ya uhai isipokuwa kifo tu.

Doi aliendelea kulia mule ndani huku matumaini ya kupona katika kesi ya madawa ya kulevya inayomkabili yakizidi kupungua kadri muda ulivyokwenda. Hakujua nani angekuwa msaada kwake. Alipowafikilia wazazi wake uchungu ulimzidia kabisa, hakujua ni vipi wazazi wake wangeweza kumsaidia kuepukana na balaa ambalo yumo ndani yake. Balaa ambalo kwa jinsi anavyowajua wazazi wake lilikuwa limewazid uwezo mara sabini. Doi alimjua fika baba yake mzee Vioja, mzee aliyeogopa mahakama kuliko njaa! Mtu wa namna hii ni vipi angeweza kumpigania? Alipoyafikilia hayo matumaini yake kuiepa jela yakazidi kupungua nukta baada nukta

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Kama Una Channel Youtube Haupati Watazamaji Karibu Tuzisambaze Video Zako, Utagharamia Tsh 10 kwa Kila View(Mtazamaji) 1
Wasiliana Nami Kwa WhatsApp +255718274413

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni