MUUZA CHIPS (28)
Sehemu ya Ishirini na Nane, kijana chidi huku, na kaka yangu, wa kijana chidi, achana na kaka, akikaa vizuri kwa, baada ya kujua, chidi huku akikaa
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"we jaribu tu utajua"
"mmmhhh nitajaribu siku nikipata nafasi"
Basi sarah na miriam waliendelea kupiga stori nyingi sana hususan za wapenzi wao jinsi wanavyowaona,…
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Wakati huo kijana chidi kafika M-pesa na yupo tayari kwa kutuma pesa, lakini kabla hajatuma alikumbuka hata jana kaja kutuma pesa, juzi pia alituma… Karibia kila siku lazima atume elfu 30 kila siku iendayo kwa mungu
"broo, hivi ukizituma zile pesa unatuma kwenye namba tofauti tofauti au ni mtu mmoja tu"
Aliuliza kijana chidi huku akionyesha msistizo wa hali ya juu sana
"kwani vipi"
"amna, nilitaka kujua tu broo"
"natumaga kwenye namba moja tu"
"samahani sana kaka… Naweza kuipata hio namba"
"aaahhhh hapana, siwezi kukupata"
"kakaaaa…. "
"siwezi kukupa"
Chidi aliona bila lushwa hapa hapati kitu, chidi aliingia mfukoni na kutoa kiasi cha shilingi elfu kumi, ili tu apewe hio namba inayotumiwa pesa hizo,…
"fanya hio namba bwana"
Chidi alimpa yule wakala elfu 10.. Na kweli wakala kapokea pesa hio huku akifungua kitabu chake cha kuhefadhia namba za watumaji wa kila siku,…
"afu huyo ni mwanaume au mwanamke"
"ni mwanamke"
"eeehhh ni nani uyo mwanamke"
Aliuliza chidi huku akijifikiria sana, mana anajua ana shemeji lakini hajawahi kuonyeshwa, na aliambiwa shemeji huyo ana mimba kubwa tu,…
"ni mke wa Ibrahim"
"wacha bwana…. Kumbe anahudumia eee"
"ndio, ila we namba waitaka yanini"
"no we nipe tu"
"ok… Chukuwa"
Alipewa namba hio ikiwa imeandikwa kwenye kikaratasi kisha akaiinguza kwenye simu yake na kumpigia mtu huyo.. Chidi alisogea pembeni kidogo na kuongea nae
"eee haloo mamy habari yako"
"salama nani mwenzangu"
Rehema aliuliza huku akisikiliza kwa makini sana
"aahhh mimi ni wakala… Sasa leo mtandao unasumbua na kuna pesa nataka nikutumie"
"wewe umebadilisha namba"
"hapana, ila nimeomba simu hapa jirani"
"ok basi ngoja nije niichukue hapo"
"sawa fanya haraka"
"sawa kaka"
Chidi alikata simu, huku akivuta kiti pale kwa wakala
Wakati huo rehema ndio anachukiwa toyo na kuja huku pembezoni mwa mji ambako ndio karibu na ofisi ya zamani ya mume wake Ibrahim, na sasa kamuachia mdogo wake chidi…
Chidi katulia hapo kwa wakala, akiwa anaangaza macho huku na kule kana kwamba huenda akamuona mtu huyo akija,.. Na ni kweli rehema alikuwa anakaribia kufika hapo kwa wakala, na chidi kakaa wazi wazi ili amuone shemela wake, tena akiwa ana mimba mana hajawahi kutambulishwa sasa wacha amuone leo,….
Na shemeji wa chidi alikuwa spidi kweli kuja kuchukuwa pesa alioambiwa mtandao unasumbua mno… Tena chidi alikaa kipesa hapo nje ili… Na rehema na e keshafika yupo nyumba ya pili kutoka hio ya wakala….
"aahhh huyo shemeji mbona haji sasa"
Aliongea kijana chidi huku akikaa vizuri kwa kumsubiria shemeji yake huyoo
Kweli usilolijua ni usiku wa giza, uamuzi wa kijana chidi kumsubiria huyo mschana anaesemekana ni mke wa kaka yake, na sio kuwa chidi hamjui, anamjua vizuri sana ila anamjua kama changudoa tu na hamjui kama shemeji yake, chidi alifanikiwa kupewe namba za mwanamke huyo na kuanza kuzifanyia kazi, alizipiga na hatmae zikapatikana, baada ya kuongea nae aliamua kumsubiria hapo nje ya wakala wa m-pesa ambapo ndipo panapotuma pesa kwenda kwa mwanamke huyo…
"aahh huyo shemeji mbona haji sasa"
Aliongea kijana chidi huku akikaa vizuri kwa kumsubiria shemeji yake huyoo
Na shemela mwenyewe hakuwa mbali yaani alikuwa jengo la pili kutoka hilo alilokuwepo kijana chid,
"aaaahhh nikikaa hapa akinikuta itakuwa sio ishu"
Chidi aliona ni bora atoke eneo hilo ili asikutane nae uso kwa uso,…. Sasa ile anatoka tu na rehema nae ndio anaingia, yaani wamepishana dakika moja tu,.. Na chidi hajamuona huyo mdada kama keshafika eneo hilo, chidi alirudi pale kibandani kwake anapouzia chipsi,.. Akakaa kwa nje pale, sasa akawa anaangalia kwa umakini wa hali ya juu,
"mbona hatokei sasa"
Chidi aliongea hivyo huku akiona mschana mwenye umbo zuri akiwa kasimama pale kwenye dirisha la wakala,. Ila alipomwangalia vizuri alimkumbuka yule mschana
"khaaa yule mdada mbona ana umbo kama la yule changudoa"
Alijisemea kijana chidi huku akiamka ili kwenda kumuangalia,…
Chidi alifika pale dirishani kwa wakala, sasa kabla hajauliza kuhusu kuja kwa mke wa ibra,
"aliokupigia simu ni huyo hapo"
Aliongea yule wakala huku akimnyooshea kijana chidi kidole, na yule dada akageuka na kumuangalia kijana chidi,…
"heeeeee chidiiiii jamani ulipotelea wapi, jamani toka siku ile"
Aliongea rehema huku akitaka kumhag, chidi alikwepa na kumuangalia kwa dharau, mana kama huyu ndio huyo mke wa kaka yake basi hafai hata kidogo, yaani hata kwa dawa,…
"ebu ngoja kwanza… Ivi wewe na Ibrahim mpoje"
Aliuliza kijana chidi huku akimtolea macho rehema, wakati huo rehema yeye hajui kama huyu ndio ndugu wa Ibrahim ambae ni mume wake,…
"we kaka huyu kijana kwani ni nani"
Rehema alimuuliza wakala na wakala hakutaka kumficha, ila sema wakala pia hajui kama mimi na Ibrahim ni ndugu,
"huyu ni muuza chipsi wa pale… Badala ya Ibrahim ndio huyu"
Rehema pale pale akakumbuka siku moja ilikuwa hivi
"mke wangu,.. Nina mgonjwa kule ambae ni ndugu yangu hivyo haitakiwi niimalizw hii pesa yote"
"heeeeeeee mimi na ndugu yako nani wa muhimu"
"aahhh wote ni wa muhimu kwangu"
"taja mmoja kama mimi sio wa muhimu niache"
"ok basi wewe ndio wa muhimu"
Alipokumbuka hilo akakumbuka na siku nyingine tena
"sasa mume wangu wewe una kibanda kingine, je? Hicho kingine umemwachia nani"
"ahahahaha yupo ndugu yangu mdogo ndio anasimamia kile kibanda cha zamani pale shule"
"kumbe una ndugu, sasa kwanini hujanitambulisha kwa shemeji yangu jamani"
"usijali ipo siku utamuona"
Rehema alishtuka baada ya kugundua kuwa huyu huenda ndio huyo ndugu yake na Ibrahim,..
"chidi, usinifiche wewe ni ndugu wa Ibrahim"
"sasa je, hajakwambia nini"
Chidi alimjibu rehema kwa nyodo, na hata ule upendo wa rehema kwa chidi uliisha baada ya kujua kuwa huyo ni ndugu yake na mumewe, afu mbaya zaidi keshampa mwili wake siku ile walipoenda disco,…
Rehema baada ya kujua hivyo hakutaka kuendelea kukaa, aliondoka zake bila kudai pesa iliomleta,… Lakini chidi hakutaka kumuacha alimfuata nyuma nyuma na kumzuia kwa mbele,…
"skia we kahaba, kuanzia leo naomba uachane na kaka yangu, kuanzia leo achana na kaka yangu.. Muache Ibrahim afanye maisha yake, kila siku elfu 30 tu, je anaingiza kiasi gani, na mimi ndio natumwa kila siku kuja kutuma pesa,… Achana na Ibrahim, afu unajifanya una mimba, una mimba iko wapi,.. Mbona nimekugeuza geuza kule gest huna cha mimba wala nini…. Achana na kaka yangu mjinga wewe"
Chidi alikuwa akiongea huku anatetemeka midomo kana kwamba kitendo anachomfanyia kaka yake sio kizuri, kumdanganya ana mimba wakati hana hata kichanga,.. Chidi alikasirika sana na hakujali kitu hata kama alishawahi kula uroda wake lakini hakujali, kwasababu Ibrahim alikuwa akiitenga familia yake kwasababu ya huyu malaya asie na kwao,…
"skia endapo utaendelea na kaka yangu, utakiona cha mtema kuni kutoka kwangu"
Chidi aliondoka na kumpiga kibega dada huyo, kana kwamba kamchukia sana, mana yeye ndio chanzo cha familia yao kuteseka kule kijijini,… Kwanini wanawake hamuna hata huruma ukimkuta Zezeta basi wamgandaa mtu mpaka anasahau familia yake,…
Rehema alipanda toyo kisha akaondoka zake,…
Chidi nae alirudi katika kazi yake huku ile pesa akiwa nayo,…
Tukija huku kijijini katika familia ya kijana chidi, kama kawaidia familia ilikuwa ikihitaji pesa, kwani hali yao ilianza kuwa mbaya kichakula mana mvua hazikunyesha muda mrefu hivyo hata mazao hakuna kwahio tegemezi lao mi watoto wao ambao wapo mjini,..
Katika familia hio mtu mwenye nguvu ni salma peke yake,… Hivyo walichukuwana na wazazi wa kijana chidi na kwenda kulima kibarua japo hawatolima pakubwa lakini ilimradi wapate pesa kidogo ya kiwakidhi mahitaji yao…
"mama kwanini tusimpigie chidi atutumie hata kidogo tu"
"mwanangu,.. Kila wakati tukimuomba pesa atashindwa kufanya hata maendeleo yake,.. Hivyo tuwe tunampa hata nafasi ilo afanye na mambo yake"
Aliongea mama yake chidi huku wakiwa katika shamba wakilimia misitu, kazi hio ni ngumu sana na ilikuwa yamtaka aifanye kijana chidi, kwakuwa yeye ndiye mwenye nguvu ya kuvunjana na misitu ili wapate pesa,… Mashamba wanayo mengi sana ila hawataki kuyauza na sio wao tu hata chidi pia hataki shamba liuzwe, hilo moja liliouzwa kwa ajili ya kuoa basi liishie hilo hilo shamba moja,.. Ilifika jioni wazazi wa kijana chidi walichoka kufanya kazi hivyo waliamua kutangulia nyumbani…
"salma mwanagu, wacha sisi tutangulie, wewe msubiri huyo baba aje akulipe afu upitie kule bondeni ukachume mboga mboga sawa mama"
"sawa mama"
Salma aliendelea kukata kata baadhi ya miti ili kupunguza hasira ya msitu huo,..
Punde sii pende kuna kijana alitokea ambae ni mtoto wa tajiri, yaani huyo wanaemlimia sasa mtoto wake ndio kaja kulipa kwa wale waliofanya kazi,..
"mambo"
Alisalimia kijana huyo huku akimtabasamia mke wa kijana chidi,..
"poa tu hali yako"
"salama…. Aahhhh wewe ndio uliolima peke yako"
"hapana nilikuwa na wazazi wangu, sema wameniamnia nisubirie hela"
"ok.. Na mimi ndio nimeagizwa na mzee wangu nije kuwalipa"
"sawa"
Kawaida wakilima robo heka, wanalipwa elfu 7 (saba) na wakilima nusu heka, wanalipwa elfu 15, sasa leo wamelima robo heka lakini salma alishangaa kulipwa pesa ya nusu heka na wakati wamelima robo heka,…
"lakini kaka, sisi tumelima robo tu"
"usijali dada angu, hio nyingine nimeongeza mimi tu"
"mmmhhh hapana kaka nilipe pesa nilioifanyia kazi"
Salma alikuwa akikataa pesa hio huku akigeuka na kuangalia pembeni mana kijana huyo alionekana kuna kitu alitaka kwa mschana huyo… Salma aliikataa ile pesa lakini mwisho wa saa aliichukuwa na kuondoka zake, hivyo hapo alipo ana elfu 15 ambayo alipewa tu bila kujua malipo yake,…. Maisha yao yalianza kuwa ya tabu kwa mara nyingine tena..
Tukija huku mjini ikiwa ni mida ya jioni chidi alipigiwa simu na jimama lake lile liliomfadhili kwa kila kitu hapo mjini,..
"haloo chidi jamni"
"sema mamy wangu"
"keshokutwa mi naona mbali, ila leo nina hamu imenizidi Please chidi naomba leo tukutane usiku"
"mmmhhh mamy, si nitakuwa nimechoka sana mamy"
"i know but please my boy… Tukikutana leo, kesho huingii kazini utapumzika Please"
"ok poa basi.. Tukutane wapi"
"hotelini…"
"hoteli gani"
"mount Meru hotel"
"ok.. Poa basi nikimaliza hapa nitakutafuta"
"ok… Now am happy to meet with you"
"usijali mamy"
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni