MUUZA CHIPS (27)
Sehemu ya Ishirini na Saba, huku kwa akina, mama yake na, chidi na saidi, hapo kwenye hio, hotelini kwa akina, huko kwenye hicho, huku hotelini kwa
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"oya side, ebu njoo hapa mara moja"
Alimwita rafiki yake saidi…. Punde si punde saidi alifika na kumuacha pale kibandani kisha chidi wakaenda katika duka la fenicha ili kununua kila kitu cha ndani,… Kiukweli chidi alinunuliwa vitu vya gharama sana, yaani vitu vya bei ghali mno…
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Walinunua kila kitu mpaka tv, yaani hakuna kitu kimeachwa hapo,…. Chidi alitoka kwenda kutafuta gari kwa ajili ya kuvipakia,… Walipata gari na kuvipakia vyote,
Lakini wakati wanataka kuondoka, ghafla mama huyo akapigiwa simu ya kikazi, na nia yake ni kuelekea huko kwenye hicho chumba
"sasa, we peleka tu mi ngoja niwahi kazini sawa"
"sawa mamy"
Basi mama huyo akaondoka na kumwacha chidi akiwa anataka kupeleka vyombo hivyo huko kwenye hicho chumba,…
Chidi alitoka hapo na gari hio yenye fenicha zake zenye gharama kubwa mno,.. Chidi alipitia pale kibandani na kumchukuwa saidi mana chidi hapajui,… Hivyo chidi alimwachia fatuma ofisi kitu ambacho ni cha ujinga mkubwa sana,…
"uyo demu ataqeza kuuza hapo… "
"aahhh mi nataka ukanionyeshe tu hicho chumba kisha urudi mi niendelee huku"
"aahhh mbona ni kitendo cha dakika mbili tu, twenzetu basi"
Basi kijana chidi na saidi walipanda gari hio kisha haooo wakaondoka….
Tukija huku hotelini kwa akina sarah, tunamuona sarah anamuuliza mama yake baada ya kufika hapo,
"mama siku hizi upo bize, una nini afu hunishilikishi, na ulikuwa ukinishilikisha mamy"
"usijali, kuna kazi nilikuwa nafanya"
Mama alimjibu mtoto wake hivyo, mana sio kila kitu ajue
Sarah alibaki kuwa kimya huku mama yake akiendelea kuingia ofisini kwake akiwa kama boss na mtoto wake ndio meneja wa pesa za mauzo kisha zinamfikia mama yake,…
Sarah alishindwa kumuelewa mama yake kwani kwasasa kabadilika sana, amekuwa mtu wa kutoka toka kila mara,
Tukija huku kwa akina rehema ambae ni mke wa Ibrahim, akiwa na rafiki yake jasu, wakati huo walikuwa wakipika chakula cha mchana lakini aliokuwa anapika alikuwa ni jasu, kwani rehema alikuwa anaumwa,
"we rehema jwani tatizo ni nini"
"we acha tu jasu… Viungo vyangu vimetibuliwa na yule mwanaume"
"mmmhhh pole sana ila sema nawe hujalipwa bwana umeniuzi"
"Kiukweli sitomdai na wala simdai… Jasu sijawahi kukunwa eti, yaani toka tumalize shule kipindi kilee, yaani hata alionitoa bikra yenyewe haikuwa hivi jasu"
"mmmhhh pole mwaya"
Rehema alikuwa akiumwa kwa kile kilichofanywa na kijana chidi,..
Tukija huku kwa chidi na saidi wakiwa ndio wamefika hapo kwenye hio nyumba, katika mtaa uitwao sakina, chidi mwenyewe alipiga saluti kwa uzuri wa hio nyumba,..
Basi vitu viliingizwa huku saidi akichukuwa toyo ili arudi kule kibandani,.. Chidi aliendelea kuingiza vitu ndani, na katika nyumba hio kulikuwa na wapangaji wanne na chidi ni watano,… Lakini chifi alikuwa akiona familia za kike tu kana kwamba waliokuja kupangisha hapa kabla ni watu na familia zao.. Punde sii punde chidi anapigiwa simu, kucheki namba anakuta ni kaka yake,…
"ivi umepatapata hapo leo"
Aliuliza bwana Ibrahim, na chidi akamjibu
"yes nina kitu kama elfu 40 hivi"
"ok bado mapema, Hebu fanya mpango ukaitume pale M-pesa"
Ibrahim alitaka pesa hio akatumiwe mke wake,..
"nikaitume yote"
Aliuliza kijana chidi mana kazoea kutuma elfu 30 kila siku sasa leo iweje iwe 40 na ndio hio hio iliotoka
"ndio… We itume yote"
"mmmmhhh sawa broo"
Chidi alikata simu na kumpigia saidi ambae aliondoka dakika moja tu iliopita,..
Saidi alirudi mana alikuwa bado yupo karibu sana, chidi alitoa kiasi cha shilingi elfu 40 na kumpa saidi
"aisee ebu kaitume pale M-pesa"
"naituma kwa nani"
"we ukifika pale kwa wakala wetu wa jirani pale, we mwambie kuwa nimeagiziwa na Ibrahim uitume hii pesa,.. Sasa huyo wakala anajua namba ya kutuma"
"oooke, poa basi we pambana hapo, mi wacha niwahi si unajua tumemwacha demu tu pale"
"yes, fanya hivyo aisee mana leo hali ni mbaya sana"
Saidi aluondoka lakini chidi alikuwa ana wasiwasi sana juu ya kaka yake kama akijua kuwa kule kibandani kamwacha mtu afu yeye hayupo…
Tukirudi huku kwa akina sarah na mama yake, Sarah alikuwa bado anaumiza kichwa sana kuhusiana na mama yake, na hapo ofisini tunamwona mama sarah alikuwa kama anataka kutoka tena,.. Sarah aliona ngoja apande rosheni ya juu kwenda kumpatia pesa iliotoka mchana huo, mana haruusiwi kukaa na pesa muda mrefu,…
Ghafla mama sarah anashtuka baada ya kuona mlango umefunguliwa bila hodi,
"aahhh umenishtua wewe aahhh"
Aliongea mama sarah huku akifunga mtandio wake vizuri,….
Sasa sarah alipoingia pale ndani, kuna lisiti aliiona…
Akawa anaitolea macho sana huku akijiuliza kuhusiana na lisiti hio
Sarah hakutaka kuona kwa macho tu bali aliipelekea mkono na kuichukuwa….
"milioni tatu na laki tano"
Sarah alitaamka hivyo, huku mama yake akigeuka kwa mshtuko wa maneno hayo..
Sarah alikuwa akimfatilia sana mama yake mpaka kufikia hatua ya kuigundua lisiti ambayo ndio ilionunulia vitu vya chidi, yaani zile fenicha ambazo chidi anaziingiza kule ndani, lisiti yake ndio hii, kumbe vitu vile vina gharama ya shilingi milioni tatu na laki tano, yani vilikuwa ni vitu vya thamani sana,..
"si nilienda kununua vitu vya kule nyumba mpya"
Mama aliongea hivyo, tena kwa msistizo wa hali ya juu,
"kwani ile nyumba imeisha"
"hapana, ila nilinunua ili tupeleke mlinzi mana nyumba imefikia hali ya kulindwa sasa"
"ahhhhh lakini mbona umemnunulia vitu vingi hivi"
"yes, kwasababu tukigamia kuna vingine tutavichukuwa"
"aahhhh sawa"
Mama ni mama tu,… Mama ndio wa kwanza kuona jua, hivyo huenzi mdanganya na ishu yeyote ile,.. Na ni kweli wana nyumba mpya ambayo inaendea kuisha, ila vyombo hivyo havikupelekwa huko kama alivyosema mama yake na sarah,
Sarah aliridhika kwa moyo wote kutokana na maneno ya mama yake,… Sarah aliiancha ile lisiti kisha akampa mama yake pesa ya mauzo ya toka asubuhi mpaka mchana huo,..
Tukija huku kwa chidi ambako vyombo vilikuwa vikiisha kuingia ndani, hata majirani wenyewe walikuwa midomo wazi kutokana na vyombo hivyo vilivyo vya hali ya juu na vya gharama kubwa,.. Tv yenyewe ni kubwa yenye inchi 40, Dstv decoder, yaani hapo kwenye hio nyumba hakuna aliokuwa anamkuta chidi kuwa na vitu vya gharama kama hivyo,..
Kazi ya kuingiza fenicha iliisha na sasa alikuwa akivipangilia kila kitu sehemu yake,…
Wakati huo huku kwa saidi aliokuwa akiendelea kufanya kazi alioachiwa na kijana chidi ambae ni rafiki yake, na hio ni kwasababu ya kwamba chidi leo yupo katika hali ya kuandaa chumba chake,… Saidi alishatuma ile elfu 40 aliopewa na rafiki yake,..
BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA
AFTER ONE MONTH AGO
BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA
Chidi akiwa yupo katika kazi yake ya uuzaji wa chipsi, tena kwa sasa amekuwa mkali wa kuoika chipsi kuliko hata kipindi cha nyuma,… Chidi alienda disco mwezi uliopita, na kitendo hicho alikilaani sana mana alitumia kiasi cha elfu 40 kule disco, na wakati hio pesa angelituma kwa wazazi wake basi ingewaseidia mno,…. Chidi toka siku ile mpaka kesho hatokaa kupenda kwenda disco,.. Na sasa chidi yupo katika chumba chake ambacho alihamia mwezi mmoja uliopita, hivyo kwa sasa haishi na kaka yake tena…
Ikiwa ni saa saba mchana simu yake ile kubwa ilikuwa ikiita, kucheki alikuwa ni lile jimama lake, ambae ni mama yake na sarah,
"haloo"
"haloo we chidi, mbona unanizungusha jamani we mtoto"
Aliongea mama huyo kwa hali ya kawaida, kana kwamba kumbe chidi hajawahi hata kumpata utamu mama wa watu, hivyo mpaka leo huezi amini hajampa mana kila akimfuata chidi haishi kutoa sababu zinazomfanya mama huyo amuelewe,..
"mamy usijali, bize na kazi kidogo inanibana, yaani ukitaka hivyo inatakiwa siku mbili nzima nisiingie kazini, je nitawezaje kufanya hivyo mamy, na hii ni kazi ya watu nimeajiriwa mimi mamy"
"lakini si nilikuambia nitakulipia siku unayoingiza hapo.. Sawa ok, hata hizo siku mbili mimi nitakulipa"
"ok poa basi tufanye kesho ndio nisiende kazini afu kwshokutwa ndio tunanii"
"sawa mi nakubali… Chidiiii yani niishie kukuangalia tu, afu hata kule kwako hujanipeleka kwanini"
"aahhhh kule kuna waswahili sana, mi spendi iwe hivyo, kuna waswahili sana pale ndani"
"ahahahahaha kwahio hutaki niwe nasemwa semwa"
"ndio spendi, coz huenda kuna mmoja akakujua ikawa tabu tupu"
"ok.. Kwaio kesho ndioooo"
"no keshokutwa, mana kesho nitatakiwa kupumzika ili keshokutwa ukome"
"ahahahaahahahahahahaha… Eti nikome, na mimi ndio nataka hivyo"
"sawa we subiri"
Walikata simu na kila mtu akaendelea na shughuli zake,
Tukija huku kwa rehema akiwa katulia nyumbani kwake, ambako ndiko alikopangishiwa na kijana Ibrahim,..
Rehema alinyanyua simu na kumpigia mpenzi wake huyo huku akijifanya kuwa na huzuni kubwa sana,…
"haloo mume wangu"
Aliongea rehema huku Ibrahim akimsikiliza mke wake kwa umakini sana
"swma mke wangu"
"mbona hujatuma ile pesa"
"aaaahh ooohh sorry sorry ngoja nifanye mchakato"
"sawa mume wangu"
Ibrahim alikata simu kisha akampigia mdogo wake ambae ni chidi
"ww dogo.. "
"sema broo"
"ebu katume elfu 50 haraka haraka sawa"
"yanini tena broo, kumbuka leo hali ngumu eti, kama mpaka saa hizi tuna elfu 60 tu, na sasa ni saa 10"
"ivi nikuulize swali"
"yes uliza tu"
"hio pesa ni yako"
"sawa sio yangu kaka, ila kumbuka biashara kaka"
"nimesema katume hio pesa"
"mmmhhhh sawa"
Basi kijana chidi alikata simu kwa hasira huku akipiga hatua kuelekea kwa wakala wa M-pesa ili aweze kutuma hio pesa…
Tukija huku hotelini kwa akina miriam kumbuka kuna hoteli mbili kubwa na ndogo, ila hio ndogo ni hoteli yenye nyota tatu, na hio kubwa ina nyota tano hivyo ukiambiwa ndogo ndio kuwa ni kibanda, Hapana bali ni ghorofa kubwa haswa…
Sasa hoteli tunayoisemea hapa ni huku kwa akina miriam, Sarah leo alimtembelea rafiki yake huku kazini,
"weee saaaarah jamani, ivi nimekufanya nini ndugu yangu"
"mbona hujanifanya kitu miri"
"sasa kwanini siku hizi huji kulala kwetu"
"ah no sio kuwa spendi, ila ni mama ndio ananiambia nilale pale nyumbani kwasababu, baba sasa hivi anasafiri safiri sana"
"jamani sarah nimekumisije mie"
"ila baba kurudi jana"
"sasa leo si uje jamani sarah"
"ok leo nakuja,… "
"Enhee vp kuhusu yule jambazi lako"
"unaniuzi tena"
"ok basi shost, but i think utakuwa unainjoi nae sana"
"we acha tu miri, yaani sijawahi kumuona hata siku moja shost,.. Yaani toka nimpeleke kwao siku ile mpaka leo sijawahi kumuona na namba yake ninayo ila siikumbuki nimemsevu nani"
"mmmhhh shosti na wewe, hebu fuatilia namba zako zote"
"heeeeeeeeeeee contacts 500 na pointi nitawezaje kufanya hivyo"
"we jaribu tu utajua"
"mmmhhh nitajaribu siku nikipata nafasi"
Basi sarah na miriam waliendelea kupiga stori nyingi sana hususan za wapenzi wao jinsi wanavyowaona,…
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni