MUUZA CHIPS (32)
Sehemu ya Thelathini na Mbili, afandealiongea huyo jamaa, alipanda gari yake, askari policehaloo afandealiongea, atatoa siri nyingi, gari yake kisha
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Mama huyo aliompangishia chidi, alimpenda sana kijana huyo japo kwa sasa hampati tena kwani hata simu yake haipatikani, kwani hata chidi kwa sasa hakuwa na simu…
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Sasa kutokana na maisha ya chidi kuwa magumu chidi anajikita kwenye kazi ya mikokoteni ili kupata chochote katika maisha yake,…
Lakini tukumbuke kuwa wahenga walisema kuwa ng'ombe wa maskini hazai na akizaa atakuwa dume hivyo halitoleta faida yeyote,.. Msemo huo naufananisha na maisha ya kijana chidi aliokuwa akiyapatia tabu za hapa na pale, na leo anakamatwa akiwa kabeba dawa za kulevya,…
"afande kaeni tayari hapa kuna hatari, huu mzigo unalindwa kisiri siri"
Afande mwingine hakuelewa alichoongea afande mwenzie…
"una maana gani afande"
"afandeeeeee, huu mzigo sio pumba ya kuku, huu mzigo ni madawa ya kulevya"
Chidi aligeuka nyuma kwa mshangao huku akiwa katoa macho, kwa hofu ya maisha yake…
"ati unasemaje broo"
"kaa kimya"
Pale pale chidi anafungwa pingu na kuitwa gari mara moja, na kupakiwa yeye na mizigo yake mpaka kituo cha polisi,..
Tukija huku kwa akina sarah na mama yake,…
Mama hakuwa na raha kabisa na hata sarah hakuwa na raha na haijulikani ni kwasababu gani wapo katika huzuni, kubwa
Sarah alitoka ofisini kwake na kumfuata mama yake kule ofisini kwake,…
Sarah alimkuta mama yake akiwa katika hali ya mawazo mengi mno,..
"mama, una nini mbona ni siku ya nne hii huna hata raha mama yangu"
"usijali mama, nina furaha tu sema ni mawazo ya kiutu uzima tu"
"mama niambie naweza kukuseidia"
"usijali sarah, ni mawazo tu"
Mama alishika simu yake na kupiga namba iliyoandikwa Baby Boy,
"Samahani Namba ya mteja unaempigia Hapatika"
Mama aliisikia sauti hio kila mara kwani yapata mara 20 toka aanze kupiga simu hio, lakini kila akipiga haipatikani,…
"sarah, hebu nisubiri nakuja sawa"
"sawa mama"
Mama huyo alipanda gari yake kisha akaondoka, haikujulikana anakwenda wapi
Tukija huku kituoni tunamwona chidi akiwa katika chumba kidogo sana tena akiwa yupo peke yake,… Ghafla mlango unafunguliwa na kuingia watu wawili waliomchukuwa chidi na kumpeleka katika chumba kingine cha mahojiano, chidi alikuwa kafungwa kitambaa cheusi ili asione anapopelekwa,…
Alikalishwa katika kiti kisha mahojiano yalianza kama ifuatavyo,
"sikiliza we kijana,… Kwa kesi uliokutwa nayo, hakika huezi kupona na utapotea kijana, na sisi ni askari wa hali ya juu, mpaka hapo tunajua wewe huhusiki lakini tunataka utuonyeshe wahusika"
"sawa mimi nipo tayari kufanya hivyo, ila nihakikishieni tu usalama wangu na kuniachia kuwa huru, mana mimi niliambiwa ni pumba za kuku"
"kuhusiana na swala la usalama kwako usijali, na kama ni uhuru utaupa, ila tunataka tujue ulipoutoa ule mzigo na ulipokuwa unaupeleka"
"sawa afande, mimi nitawaonyesha"
Chidi alikuwa hajui chochote na hakuona haja ya kuficha mana hakuambiwa kama ni madawa ya kulevya,… Polisi hao baada ya kujua kijana hakuwa mbishi mana waliandaa zana za azabu ili chidi aongee ukweli kama angegoma, ila chidi alikuwa ni kijana asiependa maisha yake yapotee,
Polisi walichukuwa gari ya private na kumpakia kijana chidi,..
Waliondoka na kuingia mjini kati ili kujua mzigo ule ulitolewa wapi na unaenda wapi…
"dereva kata kulia,… Kwenye lile jengo pale"
Chidi aliongea hivyo bila wasiwasi wowote ule wa kuogopa,..
"unajua nini afande, wauzaji wa madawa ya kulevya wamekuwa na mbinu mpya kila siku, wameona wakipakia kwenye gari wanaweza kusachiwa na askari, hivyo wamegundua kuwa dereva wa mkokoteni hawezi kusimamishwa na askari, hivyo mzigo utafika salama"
Aliongea afande mmoja aliokuwa akimwambia afande mwenzie…
"peleee"
Alionyesha kijana chidi, na wakati huo gari ni nyeusi hata kioo chenyewe huoni ndani, ila wa ndani anaona nje,…
"wapi"
"pale panapouzwa pumba pale"
"aaahhh watu wana akili hawa, yaani mteja akija anapewa pumba na madawa ndani ya pumba"
"watu hawa wana akili sana"
"we kijana,.. Pale ndipo unapotoa mzigo"
"hapana, pale ndipo ninapopeleka"
"hebu tupeleke unapoitoa hio mizigo"
Chidi alikubali bila kujali kitu chochote kile,…
Tukija huku kwa mama yake sarah, tunamuona kasimama pale alipokuwa chidi akiuza chipsi.. Kwenye lile banda la shuleni,..
Aliangalia na kugundua kuwa hapa pana siku zaidi ya tano hapapikwi chipsi tena palikuwa pamefungwa,..
"chidi boy wangu, nitakupataje mie"
Aliongea mama huyo huku, akiiangalia sana sehemu hio,
Kwa bahati nzuri alimwona mtu aliokuwa akiuza duka sehemu hio,…
"samahani kaka,.. Eti kuna muuza chipsi alikuwa hapa, ivi kahamia wapi"
"aahhhh Kiukweli sifahamu huyu mdogo kahamia wapi, ila kaka yake anauza chipsi kule mjini kati"
"wapi hapo"
"ile njia ya kutokea stendi unaiacha unaenda hii njia inayoenda mnara wa saa"
"ok ahsante kaka"
Mama huyo alipanda gari halaka ili kuweza kuwahi huko,…
Tukija huku kwa chidi, tunamwona akiwa anaendelea kutoboa siri za watu, huku askari wakiendelea kufurahia ugunduzi huo kwa kupitia kijana chidi,
"paleeeeee,… Pale ndipo ninapozitoa hizo pumba za kuku…. Enhee unamuona yule mwingine wa mkokoteni, nae kabeba pumba kama nilizobeba mimi muda ule"
Pale pale polisi waligeuza gari na kwenda kituoni,..
Kijana chidi aliachiwa huru, huku akirudi katika kijiwe chake ambcho ni cha kufanyia kazi,… Chidi toka aliookamatwa imepira siku moja na alilala sero, hivyo leo akaona aonyeshe sehemu hizo ili asalimike, mana hana kosa na atamficha mtu ambae hamjui,…. Chidi alikuwa keshamiliki mkokoteni wake binafsi ndani ya wiki moja tu, hivyo mkokoteni wake aliupata kisha akaendelea na kazi,.. Lakini kumbe wale matajiri wenye mzigo wao walikuwa wakimfuata chidi kwa nyuma toka alipoachiwa huru…
Tukija huku clock tower ambko ni mitaa kaka yake anauza chipsi hapo, Ibrahim alishangaa kuona gari kalii ikisimama mbele ya kabati lake la chipsi, kisha akashuka mama huyo na kumsalimia kijana Ibrahim
"habari yako kijana"
"salama tu dada yangu, karibu"
"ahsante… Aahhh samahani nilikuwa namuulizia yule kijana wako aliokuwa anauza chipsi pale shuleni"
"nani yule mjinga…"
"mjinga…mjinga kivipi"
"yule kijana ni ndugu yangu, ila kaniletea ujinga nimemrudisha kijijini"
"eee mungu wangu,… Kwenu ni wapi kwani"
Sasa Ibrahim akashangaa mbona mama huyo anamuitaji sana kijana chidi, kunani, na mama yupo tayari kwenda tanga ilimradi tu ampate kijana chidi, lakini ukweli ni kwamba chidi yupo katika jiji hilo hilo, sema kazi zake anazofanya ni ngumu kukutana na huyu mama,.. Na mbaya zaidi chidi hajui hoteli anayoifanyia kazi huyu mama,.. Yaani hata ramani ya kufika hotelini hapo haijui,
"unataka uende tanga"
Aliuliza Ibrahim kwa mshangao mkubwa tu
"nipo tayari ilimradi tu nimpate"
"tanga katika wilaya ya pongwe mtaa wa singiti"
Ibrahim alimpa ramani mama huyo, huku mama akitafakari safari,…
Mama hakutaka kuuliza sababu ya kumfukuza mdogo wake, mama alipanda gari yake kisha akaondoka,….
Unajua hata Ibrahim hajui kama mdogo wake yupo hapa hapa mjini, mana anajua ndugu yake hana ujanja wowote hapo mjini,…
Ghafla simu yake inaita, kuangalia jina ikuwa ni mke wake rehema,
"haloo"
"haloo mume wangu, mbona leo hujantumia chochote"
"sina pesa leo"
Hata rehema alishangaa sana kwa kusikia leo Ibrahim anamwambia hakuwa na hela, wakati toka waanzishe mahusiano hajawahi kukosa elfu 30 kila siku iendayo kwa mungu,..
"unasemaje ibra"
"nimesema hivi sina pesa"
"heeeee mume wangu,.. Sasa mtoto wako je"
"mtoto yupi"
"si huyu nilienae"
"kaitoe"
Neno hilo lilimfanya rehema kupatwa na kikohozi cha ghafla, na kujikuta anakohoa
"ibra umekuwaje lakini"
"kama unataka tuendelee na mahusiano ya mimi na wewe, nataka kesho tukapime hio mimba"
"tobaaaaaaa"
"hakuna cha toba,…. Nataka tukapime"
"sawa… Nipo tayari hata leo"
Rehema sijui alijiamini na nini na wakati hakuwa na mimba wala nini….
Tukija huku kwa kijana chidi aliokuwa kakaa katika mkokoteni wake akisubiri kazi ila sio ile ya kubeba pumba tena, chidi bila kujua kuwa kuna watu waliokuwa wakimfuatilia nyuma na hao watu walionekana kuwa na bunduki ya masafa marefu, hivyo watu hao walipanda juu kabisa ya ghorofa moja hivi, huku wakiwa tayari kumuua mana huenda akatoa na ushahidi wa mabosi wao wakubwa,… Ila hayo ni mawazo yao lakini chidi hajui kitu chochote,..
"we jamaa, ivi ni kweli yale tunayobebaga sio mapumba ya kuku"
Aliuliza jamaa mmoja ambae yupo karibu na chidi,.. Yaani jamaa huyo. Ndio kamuuliza chidi
"ndio,.. Wale afande walisema kuwa ni dawa za kulevya"
"mungu wangu weeee,…. Ndugu yangu tuhame kijiwe,.. Kumbe ndio mana wanatulipa pesa nyingi vile"
"yaani wanaweka dawa za kulevya ndani afu juu pumba"
"chidi Ndugu yangu, naomba tuhame kijiwe"
"ni kweli kaka… Hiki kijiwe kimeshanuka, tena hata mimi naogopa sana jamaa angu"
Sasa wale wenye bunduki kule ghorofani, walikuwa wanampima chidi, mana katoboa siri zao chache hivyo huenda anajua na zingine asije akatoboa siri hizo,
Ghafla wanapokea simu iliotoka kwa askari police,
"haloo afande"
Aliongea huyo jamaa mwenye bunduki
"huyo kijana ni nuksi na pia ni mwoga sana,… Atatoa siri nyingi sana hivyo sisi tumemuachia huru ili mumfanye mnachotaka,… MUUENI ushahidi upoteeeeee"
Maskini ya mungu kijana chidi anaingia kwenye matatizo makubwa ambayo hakuyatarajia, mana kama angelijua kuwa yale hayakuwa mapumba kama alivyoambiwa, basi asingelibeba mzigo huo. Maisha yake ni magumu sana na bado anaingia kwenye balaa zito la kutaka kuuwawa kwa kutoa siti za watu ambazo kumbe hata polisi walikuwa wakizijua, kama unavyojua nchi yetu kuna wale wanaoitumia kwa ubaya, hivyo kijana chidi alihisi yupo salama salimini kwa kuwaonyesha polisi sehemu inayotoka madawa hayo,… Kumbe polisi hao nao walikuwa ni wamoja,
Ghafla wanapokea simu iliotoka kwa askari police,
"haloo afande"
Aliongea huyo jamaa mwenye bunduki
"huyo kijana ni nuksi na pia ni mwoga sana,… Atatoa siri nyingi sana hivyo sisi tumemuachia huru ili mumfanye mnachotaka,… MUUENI ushahidi upoteeeeee"
Iliskika sauti ya polisi huyo ambaye ni mmoja kati ya wale waliomkamata kijana chidi,…
"usijali, na hapa tupo kwenye kazi husika"
"hakikisheni hamumuachi huyo kijana"
"sawa afande"
Jamaa huyo alikata simu huku akiendelea kumueka chidi tageti zake, huku akiifuata kitufe cha kufyatulia ili kumaliza kabisa mpango wa kumuua kijana chidi,…
Lakini kabla hajafanya hivyo, mara simu yake inaita, kucheki alikuwa ni bosi wake,
"haloo boss"
"we… Sitisha hilo swala la kumuua huyo kijana"
"kwanini boss"
"sikiliza we kichaa…. Vijana kama hao waache, kwasababu tunaweza kuwatumia kwenye kazi zetu kwasababu wanafahamu siti zetu"
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni