MUUZA CHIPS (33)
Sehemu ya Thelathini na Tatu, hakuwa na mimba, hofuau kuna kitu, kama una hofuau, kapata wapi pesa, kijana chidi akiwa, kitu umeona kwenye, hana mimba
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA THELATHINI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"haloo boss"
"we… Sitisha hilo swala la kumuua huyo kijana"
"kwanini boss"
"sikiliza we kichaa…. Vijana kama hao waache, kwasababu tunaweza kuwatumia kwenye kazi zetu kwasababu wanafahamu siti zetu"
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
"lakini atatoa siri zetu boss"
"nimesema achaaaaaa"
"ok, ok, ok, ok, sawa boss naacha"
"tena msimfatilie huyo kijana, mana makosa ni yakwenu mnampa mtu mzigo na hamumtaarifu kuwa ni mzigo gani ili awe makini"
"sawa boss nimekuelewa"
Jamaa alikata simu, huku mwenzie anamuuliza
"vp juma kuna nini"
"boss"
"boss,… Boss kafanya nini"
"kasema tuache kumfatilia yule chalii"
"heeee kivipi tena"
"mi sijui jamaa angu ata sijui kawaza nini"
"mmhhhh Haya huna budi kuach sasa"
"ah twenzetu"
Basi watu hao walishuka ghorofani hapo huku wakiwa wanasikitika sana kwa kitendo cha kumuacha kijana chidi,..
Tukija huku kwa Ibrahim na mke wake wakiwa wapo njiani Wakielekea hospitali, kama unakumbuka Ibrahim alimwambia wakapime hio mimba kama ipo ama haipo, na rehema hakuwa na mimba wala nini, sema katumbo kake ni kakubwa kubwa tu lakini hakuwa na mimba wala nini,… Sasa walipofika hospitali, Rehema alimtaka mumewe amsubiri hapo nje,..
"naomba nisubiri hapa mara moja"
Aliongea rehema huku akifunga kanga yake vizuri tena alikuwa akiamka kwa taabu kana kwamba ni kweli alikuwa na mimba,
"unakwenda wapi"
Aliuliza Ibrahim huku akitoa macho kwa vitisho, mana kila akifikiria kile alichoambiwa na mdogo wake chidi
"huyo mwanamke hana mimba anakudanganya tu na kukulia pesa zako,.. Ni mwanamke gani katika maisha haya akamaliza elfu 30 kwa siku kwa matumizi ya nyumbani tu"
Ibrahim Alikumbuka sana sauti ya mdogo wake huku akimuangalia mkewe
"naenda hapo odi ya wazazi"
"ok fanya haraka.. Afu ebu simu yako mara moja nimpigie huyu rafiki yangu anikute hapa"
Rehema alimpa mume wake simu aina ya Samsung, wakati Ibrahim anatumia nokia tochi.. Sasa Ibrahim alipiga hio namba na kuongea nae huyo mtu kisha akampa mkewe simu na kuondoka zake,
Basi kijana Ibrahim alikuwa kaketi pale mapokezi akiwa anamsubiri mkewe ili waende wote kupima uja uzito huo…
Punde sii punde mkewe karudi kisha haoo wakaenda kati chumba husika ambacho ndicho kinachotoa huduma hio,
"karibuni"
Alikuwa ni mama ndie aliewakaribisha, huku Ibrahim akiwa ivi kama atakuwa hana mimba atamfanyeje huyu mwanamke,..
Chidi alikaa huku rehema akilazwa kwenye kakitanda ka kuegemea huku dokta nae akianza kufanya mambo yake,.. Mana wanatumia vipimo vya kisasa zaidi,.. Dokta huyo alichukuwa vipimo vya kwanza vya mtu huyo kiyu ambacho hakiwezi kuchukua muda lakini akamaka rehema amletee mkojo ili kupima na vile vipimo vya mwanzo,… Huu upimani kwangu ni mpya, ila labda ni teknolojia mpya imeanza,..
Punde sii punde majibu yamekuja na yalionyesha dhahiri kuwa rehema ana ujauzito tena wa miezi minne na wiki moja,
"unaona sasa mume wangu,.. Mimi spendi tabia yako iyo"
Ibrahim alibaki mdomo wazi mana alichokidhania sicho,.. Sasa hapo hata rehema akapata kichwa na kujifanya kachukia sana,.. Lakini wakati huo rehema akiwa kacbukia, tulimuona Ibrahim akitabasamu, kana kwamba labda kuna anachokijua…
Tukija huku kwa kijana chidi akiwa yupo katika kijiwe kingine kipya, mana kile kilishanuka,
"kile kijiww kina pesa jamaa angu, yani siamini kama tumekiacha"
Chidi alikuwa akiongea hivyo mbele ya wenzake wasukuma mikokoteni,
"kweli ndugu yangu, kile kijiwe kina hela mno"
Basi walipata vikazi kazi vya hapa na pale ili kukidhi maisha yao, ilipofika mida ya jioni chidi anapeleka mkokoteni wake sehemu ya kuupaki kisha akawa anarudi zake nyumbani kama kawaida,…
Alipofika nyumbani kwake ambako amepangisha,… Majirani walianza kunong'ona kwa maneno ya hapa na pale,
"kijana kachoka ghafla, sijui kapatwa na nini yaani ule uhensamu wote kwisha"
Walikiwa wakiongea wadada waliokuwepo vibarazani kwao
"Heheeee haaalooooooo,… Alafu jamani, huyu kijana kapata wapi pesa ya kuweza kupangisha nyumba kama hii"
"we acha tu shosti hata mimi najiulizaga kila siku,.. Kwa hali hii alionayo kapata wapi pesa ya kulipa kodi ya nyumba hii"
"Enheee,.. Tumuulize mama mwenye nyumba"
Wakati mama mwenye nyumba alikuwa anaingia kuja kudai kodi ya nyumba zake,
"mama kubwa karibuni mama eti"
Alikuwa ni mschana mmoja aliomkaribisha mama huyo kwa mbwembwe nyingi,..
"ahsante"
Mama alikaa katika kiti, wakati huo chidi alikuwa akifua fua baadhi ya kuo zake ambazo zilikuwa zimechafuka sana, mana anavaa nguo wiki nzima ndio abadilishe nguo,… Maisha yalimpiga sana na hapo hana hata wiki mbili, na ashukiru kwakua nyumba hio kalipa mwaka, lakini kama sio hivyo hio nyumba asingeweza kuilipia kama ilivyo kwa wengine,..
"mama nina swali juu yako,"
"swali gani tena"
"mama… Sisi tunadhalilika kwa kumpangishia mtu kama kichaa, hebu ona nguo zake zile chafuu, ataanika kwenye kamba ya nani sasa"
"kwahio we watakaje"
"mpe notes, anakudhalilishia nyumba yako,.. Au kama kabakiza mqezi mmoja, hakikisha asipangishe tena ahame, wageni wetu hawali kwa kunukiwa na kikwapa cha huyu mtu"
"kwani we inakuuma nini kwa kijana wa watu"
"anatudhalilisha sisi, nyumba ya kishua lakini unampangisha mtu kama lichaaa, hebu muone alivyo chafuka, kapurwa sio kapurwa, yaani yupo yupo tuuu"
Yule dada kweli alionekana sana kumchukia lijana chidi, lakini mama huyo hakupendezwa na maneno ya huyo dada
"ivi… Unajua kuwa huyu ndiye mlipa kodi viziri kuliko wote himu ndani"
"kivipi yani, sjakuelewa mama etu"
"kuna mtu alishawahi kunipa hata kodi ya miezi 6 humu ndani"
"hhhhh mi sidhani,.. Mana mi mwenyewe natoa mwezi mmoja mmoja au miwili"
"sasa, katika wasumbufu wa kulipa kodi, wewe ni mheshimiwa raisi,… Na katika watu wanolipa kodi vizuri, yeye ndie mheshimiwa Rais,.. Huyo kijana amelipa mwaka mzima"
"yesu wangu na maria,…. Uuuuuuuuwwiiiiiiii.. Kalipa mwaka mzima"
"na sasa ndio kwanzaa anaendea mwezi wa pili huu"
Tukija huki kwa Ibrahim aliokiwa akitabasamu kwa mbali, lakini tabasamu lake lilikiwa likija huku likipotea kana kwamba anachokitabasamia hakina uhakika sana,…
Wakati mkewe kakimbia mpaka nje, huku akijifanya kanuna kwa kitendo cha mume wake kuhisi kuwa huenda asiwe na ujauzito,…
"taxi… Taxi"
Rehema aliita tax, huku Ibrahim akimwambia
"acha kuita taxi.. Tutembee kwa mgu ule mazoezi mke wangi"
"jamani baba king"
"ndio, kula mazoezi kidogo mke wangu"
Aliongea Ibrahim huku akicheka,
"lakini mtoto tutampa shida,.. "
"usijali, mtoto si wangu bwana"
Ibrahim alikuwa haeleweki hata kidogo,
"hebu kwanza naomba simu yako"
"simu yangu yanini tena jamani baba king"
"nataka nimpigie huyu jamaa angu aje hapa mana haji toka saa ile"
Sasa kumbe Ibrahim muda ule alipomuomba mkewe simu, sio kuwa alipiga bali, alibofya sehemu ya kurekodia sauti, kisha akamrudishia mkewe ili aende kule wodi ya wazazi,.. Hivyo mke kaenda na simu lakini ilikuwa ikirekodi sauti… Kwahio kama kuna litu aliongea huko wodini basi kitakuwa kimerekodiwa,..
"lakini mume wangu,.. Si nilikupa saa ile ukaongea nae"
"jamani mke wangu, ina maana hutaki mimi kuitumia simu yako"
"ok.. Sawa chukuwa"
Ibrahim aliipokea ile simu na kukimbilia sehemu ya rekodi, mana aliitegesha irekodi dakika kumi,.. Kweli akaikuta rekodi hii hapa,.. Tena ilikuwa imejaa maneno vizuri,… Yaani ilimfanya mpaka Ibrahim aogope kuisikiliza, mana kama ina ukweli, basi itakuwa ni mwisho wa yeye na rehema,… Hivyo hata kutetemeka alikuwa anatetemeka, kwa kuhofia ukweli ulioluwepo humo japo hana uhakika kama imerekodi jambo gani wakati alipoenda huko wodi ya wazazi…
"mume wangu, mbona kama una hofu…au kuna kitu umeona kwenye simu yangu?… Hebu hio simu"
Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, na kila marefu hayakosi kuwa na ncha,… Kijana chidi siku wanafukuzana na kaka yake, alimchana kaka yake kiwa mke alienae sio mke kama anavyodhani, yaani ni kheri kuwa na shetani kuliko mke kama rehema, Ibrahim aliyapuuzia yale maneno ya mdogo wake, ila kadri siku zilivyozidi kwenda nae akapanuka akili, na kumwambia mkewe waende wakapime kama kweli hio mimba imo ama ni swaga za kumlia pesa, Rehema alipoambiwa akapime alishtuka sana lakini haikuwa na budi ya kukubali,… Kumbe rehema alikuwa na akili yake tofauti…
Ibrahim na rehema walifika hospitalini hapo na kufanya vipimo vyote,
Rehema baada ya kujua kuwa mumewe anamshakia kuwa huenda hana mimba, hivyo kaanza kununa lakini Ibrahim alikuwa akitabasamu muda wote,… Sasa hatukujua kwanini alikuwa akitabasamu kiasi hicho,….
Ibrahim alimwomba simu mkewe na kuanza kuikagua mana kuna kitu alifanya wakati mkewe alipoondoka kwenda wodi ya Wazazi,…. Sasa Ibrahim kuona kuwa ile rekodi ipo na imejaa milis nyingi, akajua hapa kuna maongezi yaliongelewa,.. Ibrahim alikuwa na hofu hata kutetemeka alishaanza kutetemeka huku akiitolea macho simu hio..
"mume wangu, mbona kama una hofu…au kuna kitu umeona kwenye simu yangu?… Hebu hio simu"
Aliongea rehema huku akinyoosha mkono wake ili kuchukuwa simu yake,
"subiri kidogo nitakupa"
Aliongea Ibrahim huku akiibonyeza ile rekodi kana kwamba iplay pale pale wote wasikie,….
Kweli rekodi ikaanza kuzungumza
"habari yako dokta"
Hio ni rekodi nayosikika rehema akianza kumsalimia dokta,..
"salama tu karibu"
"ahsante"
"nikusaidie nini"
"nimekuja kupima… Lakini kuna kitu naomba uniseidie"
Sasa wakati rekodi inaendelea, Rehema alikuwa anatoa macho yaani haamini kama Ibrahim alifanya utundu kama huo ambao hata yeye hakuutarajia kama unaweza kufanyika…
"sema tu"
"nimekuja na mume wangu,.. Ila sina mimba Kiukweli ila nataka tukija…"
Kabla hajamalizia maneno yake, rehema aliinyakuwa ile simu yake na kuizima huku akimwambia Ibrahim
"kama hunipendi niambie kuliko kunifanyia hivi"
"rehema mke wangu,… Hata kama huna mimba lakini mi bado nakupenda"
Rehema kuskia hivyo akajiuliza
"ooohhh kumbe pesa bado naendelea kuzila, ahsante mungu"
Alijiongelea mwenyewe kimoyomoyo huku akiomba msamaha kwa mumewe,..
"mume wangu, nisamehe kwa kukudanganya, nilijua nikikuambia ukweli ungeniacha"
"usijali mke wangu, tupo pamoja"
BAADA YA MIEZI SITA KUPITA
AFTER SIX MONTHS LATER
Baada ya miezi sita kupita tunakutana kijana chidi akiwa bado na hali yake ya kusukuma mikokoteni, yaani mpaka sasa bado hali yake ni mbaya mno,….
Akiwa kijiweni kwake tena kakaa juu ya mkokoteni wake, ghafla kasimu kake kanaita,.. Kuangalia jina alikuwa ni mke wake wa kijijini ndio alikuwa akimpigia simu
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni